Mwalimu: ukiwa mkubwa unapenda kuwa nani. Mwanafunzi- napenda niwe Fisadi

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Sio utani ni kweli mwalimu mwenzangu kamuuliza mtoto wa chekechea ukiwa mkubwa unapenda kuwa nani mf; daktari, mwalimu, mcheza mpira nk cha ajabu mwanafunzi kamjibu anataka kuwa FISADI.

Katika kumhoji vizuri amedai kila siku kasikia fisadi wanahela na wanaishi vzr kwa hiyo nae anasoma ili awe fisadi
 
Yupo pia mtoto wa chakechea anasoma na mwanangu aliwahi kuulizwa akasema anataka kuwa jambazi. Mtoto huyu aliwahi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuiba vitu vidogo vidogo vya wenzake darasani lakini pia kuwapiga wenzake na kuwaumiza. Nilipopata mashitaka ya kupigwa mwanangu nikaenda kujua kulikoni kwa mwalimu wa darasa ndipo akanisimulia kisa cha mtoto huyo kutaka awe jambazi atakapokuwa mkubwa.

Pengine watoto wanavutiwa na vitu vinavyotokea wakati wa zama zao au matukio ya mara kwa mara katika jamii bila kujali kwamba wanaelewa kwa kina kile ambacho wanakitaka katika maisha yao ya baadaye
 
Back
Top Bottom