Mwalimu Nyerere (RIP): Matukio Muhimu Mpaka Kutuaga Watanzania

NYERERE:- BORA NINGEKUWA MHUBIRI WA DINI KULIKO KUWA RAIS WA NCHI!

Baadhi ya maneno ya hayati Mwalimu, alipofikisha umri wa miaka 50

"..Wakati nikiwa Makerere, niligundua kwamba serikali ya nchi yangu ilikuwa ikinilipia kiasi cha paundi 80 kila mwaka kwa ajili ya elimu yangu. Lakini hio haikuwa na maana kubwa sana kwangu, isitoshe paundi 80 ni chembe ndogo tu ya kiasi cha jumnla ya pesa zinazokusanywa na kutoka kwa walipa kodi wa nchi yangu, yaani wa-Afrika. Leo hii, paundi 80 ziimeongezeka thamani yake na kuwa na maana kubwa kwangu. Siyo kwamba ni zawadi muhimu tu na tunu kwangu, lakini pia ni deni ambalo kamwe sitaweza kulilipa."

"Sina uhakika kama wengi wetu wamepata kufikiria kwamba wakati paundi 80 zilikuwa zinatyumika kunitunza mimi kule Makerere, hela hizo zingeweza kujenga Zahanati angalau mbili katika kijiji changu au chochote kingine Tanzania."

".. Inawezekana kabisa kuwa wananchi walikuwa wanakufa kwa ukosefu wa dawa kwa sababu tu ya kukosa paundi zile 80 zilizokuwa zikilipwa kwa ajili yangu. Kwa hiyo kuwapo kwangu chuoni kuliinyima jamii huduma ya wale wote ambao wangeweza kusomeshwa kwenye shule chini ya miti, na kuwaandaa kina Aggreys na Booker Washingtons, Je nitawezaje kamwe kutolilipa hilo deni kwa jamii yangu hii?."

"Jamii inatumia fedha zote hizo kwa ajili yetu kwa sababu inataka tuwe nyenzo za kuiinua jamii hiyo. Kwa hiyo lazima siku zote tubakie chini ya jamii hiyo na kuhimili uzito wote wa wananchi ambao wanahitaji kuinuliwa, na lazima tusaidie kuifanya hiyo kazi ya kuwainua wananchi wasiojiweza"


Wakati nikisoma matukio yaliyojiri kuelekea kifo cha Babu (Sokoro) kama tulivyozoea kumuita, machozi yamenidondoka sio tu kwa sababu ya kuondokewa na mtu muhimu kwangu na Taifa, bali pia kwa kukosa nafasi ya kutimiza nadhiri yangu ya kumpa shukrani japo ya ahsante kwa mema aliyonitendea mimi pamoja na mafanikio aliyonitabiria tarehe 2.1.1987. Pia nalia kwa sababu baada ya kuonana naye wakati alipotembelea maonesho ya Sabasaba mwaka 1999, sikumuona tena zaidi ya alipokuwa ndani ya jeneza pale Msasani na Butiama.

Lakini nalia zaidi ninapokumbuka kuwa baada ya kifo chake, watu wengi wamikuwa victimized kwa sababu ya misimamo ya kiuadilifu. Wazalendo wamekuwa wakitemewa mate na kupewa majina ya huyo siyo MWENZETU (katika ufisadi) n.k. Waovu katika jamii wamepewa majina ya Huyo mjanja n.k. Nitaendelea......... machozi yamelowanisha Key Board mpaka imestark.
 
zamani kulikua na member wanaochangia kwa staha kwa kiasi kikubwa mno! nimejaribu kufuatilia thried hii nimegundua wengi wa wana jf walio na nasaba za uchadema wameifanya jf ya sasa kua tofauti na ya zamani kwa kiasi kikubwa sana.
 
zamani kulikua na member wanaochangia kwa staha kwa kiasi kikubwa mno! nimejaribu kufuatilia thried hii nimegundua wengi wa wana jf walio na nasaba za uchadema wameifanya jf ya sasa kua tofauti na ya zamani kwa kiasi kikubwa sana.

Ungemjua huyu memba na mashudu yake aliyonayo saivi. Nina uhakika haya maneno ungeyatengua

Enzi hizo alikua na akili sana
 
ISSN 0856-5775 NO. 0885 Ijumaaa October 1, 1999.

Agosti 1998:-

Mwalimu agundulika ana kansa ya damu, lakini aendelea na shughuli zake za kutafuta suluhu kwa taifa la Burundi.

Agosti 26&27, 1999:-

Media ya Tanzania, kwa mara ya kwanza inasema wazi kwa public kuwa hali ya Mwalimu sio nzuri, lakini wasaidizi wake wanaota kigugumizi kusema ukweli, kwa kusingizia kuwa wao sio madakitari.

Septemba, Mosi 1999:-

Mwalimu, akisindikizwa na mkewe, Mama Maria na daktari wake, David Mwakyusa, wanaondoka nchini kuelekea Uingereza, kuchekiwa afya yake, na familia ya Mwalimu wanawaaambia waandishi wa haabri kuwa angerudi tarehe 28, Septemba, 1999.

Septemba, 22 1999:-

Rasi wetu Mkapa, atangaza rasmi akizungumza na CNN, na kutangaza rasmi kuwa hali ya Mwalimu kule Uingereza "sio nzuri".

Septemba, 24 1999:-

Mwalimu anazidiwa akiwa huko Uingereza, na kukimbizwa hospitali ya Mtakatifu Thomas, ambako analazwa akiwa "Hoi".

Septemba, 25:-

Rais Mkapa, anamtembelea Mwalimu huko hospitalini London na kumpelekea salam za pole kutoka kwa rais Jimmy Carter, na siku hiyo usiku kwa sauti yenye kutetemeka na majonzi, rais Mkapa, anaitangazia rasmi dunia kuwa Mwalimu anaumwa kansa ya damu.


......Itaendelea...........
mkuu utanitoa machozi upya.
 
Wakuu ninaomba kutoa heshima kwa wananchi wote hapa forum, in the wake ya yanayotutokea sasa hivi kisiasa nchini, kwa unyeyekevu mkubwa ninaomba tumkumbuke Rais wetu wa kwanza Baba wa taifa Mwalimu Nyerere(RIP).

Ninaomba kuyafikisha kwenu matukio muhimu yaliyotokea katika kuelekea kwenye kututoka kwake, nilikuwa ninapitia maktaba yangu nikayakuta haya magazeti ya mwaka October, 1999, ya wiki ambazo zilielekeza mwisho wa Mwalimu, baba wa taifa, mwisho ambao wengi wetu tunaamini kuwa ndio uliokuwa mwanzo wa yanayotukuta sasa hivi katika taifa letu kisisasa.

Tumefikia mahali as taifa hatuelewani tena, kuna wanaonekana kuwa ni wamiliki wa nchi yetu, na sisi wananchi kuwa kama wageni, umoja wetu upo mashakani, mshikamano wetu upo njia panda, Mungu atunusuru na hili balaa tunalotaka kuletewa na wenzetu wachache wenye tamaa za utajiri wa haraka na madaraka yasiyokuwa na mipaka.

Reconciliation inaweza kuwa ni pamoja na kumkumbuka Mwalimu
Baba yetu alivyotutoka.

Ahsanteni Wakuu!

Le baharia enzi hizo ulikua upo vizuri.
 
Nilikuwa naangalia kideo ya wazee walioenda London kusimamia mipango ya kusafirisha mwili wakiongozwa na Marehemu Dr. Omar Juma. Walipoenda kuonana na mama Nyerere nakumbuka mama Nyerere alivyokuwa analia "wanafunzi wako wamefika.. uuwi uuwi" Na baadhi ya hao wanafunzi walikiri kuwa "wamefika" Ninachogundua ni kuwa baada ya kuwa katika darasa la Mwalimu kwa miaka yote hiyo ni wachache waliohitimu maana wengi walikuwa ni watoro! na sitashangaa hao ndio walionyanyua glasi za mvinyo!


Mkuu umepotea kama Kigogo wa Twetter? njoo uwanja wa Taifa utupe za leoleo
 
Back
Top Bottom