Mwalimu Nyerere (RIP): Matukio Muhimu Mpaka Kutuaga Watanzania

Sasa hapa ndio utaona wale waliokua wanafiki kutoa machozi ya mamba na kuvaa ngozi ya kondoo.
 
Kumbukumbu inanionyesha kwamba baada ya Mwl. Kung'atuka urais 1984 aliendelea kua mwenyekiti wa chama hadi mwaka 1999 ndio akaachia Uenyekiti kwa bwana Mwinyi, baada ya hapo ndo kwanza na azimio la Arusha likahifadhiwa katika nyumba ya milele(likazikwa)na hapo matatizo yalipoanzia, Me nadhani kuna haja kabisa ya hawa waumini wenzangu wa CCM kukubali kutenganisha Uenyekiti wa Chama na Urais ili angalau Rais na Watendaji wake wawe na Mtu au sehem ya kuwakemea, nadhani kashfa zinazoendelea sasa hivi ilitakiwa watu wawajibishwe kwani mie naona mambo yako wazi sana na kila mwananchi anona.

Naomba unikosoe mkuu ili nijifunze toka kwako

Nenda kaangalie kumbukumbu zako sawasawa. JKN aling'atuka 1985 na aliachia uwenyekiti wa chama 1987.
 
GAZETI LA MAJIRA, TAREHE 18, OKTOBA 1999:-

Rais Mkapa, amesema leo kuwa serikali yetu itatumia kila senti hadi ya mwisho kuhakikisha kuwa Mwalimu anazikwa kwa heshima kubwa anyostahili kupewa na taifa letu. Rais pia aliatangaza usimamishaji wa matumizi ya pesa za serikali kwa shughuli zozote za nje hadi baada ya mazishi ya Mwalimu.

Pia akizungumza na waandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi, Waziri wa Kazi Paul Kimiti, alisema kuwa maandalizi yote tayari yameshakamilika, na Mwalimu atazikwa karibu na makaburi ya wazazi wake na mahali alipozaliwa. Kaburi limeshakwisha chimbwa, karibu na makaburi ya wazazi wake, chini kidogo kuna picha ya kuchongwa aliiweka Mwalimu akiwa hai, na familia ya Mwalimu inasema aliagiza azikiwe hapo. Mwili wa Mwalimu utakapofika mjini Musoma, iutazungushwa katika mnitaa ya mjini kabla ya kupelekwa kijijini Butiama, ambako utapelekwa kwa Chifu wa Wazanaki Japhet Wazangi, na kisha kwenda nyumbani kwa Mwalimu.

Hapa mjini Dar-es Saalam, Waziri mkuu Bw. Sumaye, alifanya kikao na viongozi mabli mbali wa serikali nyumbani kwake Osterbay, kujaribu kutafuta njia za kupata hela za kugahramia mazishi haya ambayo nchi 61 zimethibitisha kuhudhuria. Walioshiriki kwenye kikao hicho ni pamoja na Mawaziri Daniel Yona, Sir George Kahama, Wilson Masilingi, Ameir, na Meghji, pia alikuwepo Bw. Keeenja.

......Itaendelea.......!
 
Kama Baba angekuwepo Duniani hakika angeyaona mateso yetu haya. Vijana aliowaamini Baba yetu leo wamegeuka Mafisadi wetu. Kila anayekuwa katika "mtandao" lazima aihujumu Tanzania. Eee! Mungu tupe mtu kama Julius Kambarage Nyerere awakemee hawa mafisadi. Hebu ona sasa haya mafisadi yanataka kuishi ulaya kwani hivi sasa kuna mjadala wa uraia wa nchi mbili hii ni kwa ajili ya kwenda kujificha huko walikoficha hela zetu. Ee!!! Mungu utusikie. Amina.
 
. UTAPELEKWA HADI NYUMBANI KWAKE MSASANI
. KESHOKUTWA KUFANYIWA IBADA ST. JOSEPH


Rais Mkapa anatarajiwa kuongoza maelfu ya wakazi wa Dar, kuupokea mwaili wa Mwalimu Nyerere, utakapowasili kesho saa tatu asubuhi. Mkuu wa mkoa wa Dar, Bw. Makamba, amesema mwili utapitia bara bara za Nyerere, Nleson Mandela hadi Ubungo na Hospitali ya Magomeni, katika bara bara ya Kawawa. aidha utapitishwa pia njia za Ali Hassan Mwinyi hadi Machafu, TPDC Mikocheni na kulekea nyumbani kwa Mwalimu, Msasani.

Mwili huo utaondolewa Jummane saa 2:00 asubuhi na kusindikizwa na Rais Mkapa, kupitia njia za TPDC, Ali Hassan Mwinyi, Ocean Luthuli, Kivukoni Front, Sokoine Drive hadi kanisa la St. Joseph. misa hiyo itamalizika saa 4:30 asubuhi na mwili utapelekwa Uwanja Wa Taifa kupitia Sokoine, Railway Uhuru, Ilala Boma, Buguruni, Mandela hadi Uwanja Wa Taifa.

Alhamis, pia kutakuwa na ibada maalum ya kuuombea mwili huo wa Mwalimu hapo Uwanja Wa Taifa, kuanzia saa 3:00 Asubuhi, Wananchi wote wa Dar wanaombwa kuhudhuria, na baada ya hapo mwili huo utapelekwa uwanja wa ndege wa Dar tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea Butiama, kwenye mazishi yatakayafanyika Jumamosi.

.....Itaendelea.....!
 
Chakaza,
Hakuna cha kushangaza hapo. Hawa walimwona Mwalimu kama mtu aliyewawekea kauzibe ka kula. Si unaona wanavyotafuna nchi? Nasikia hata pale Ikulu watu wali "toast" baada ya kifo chake. Hakuna cha kushangaza. FM ES, good job, good job!
 
Waheshimiwa, heshima mbele.

Kama FM ES lengo lako lilikuwa kunitoa machozi, basi leo umefanikiwa. Mwalimu alikuwa exceptional. huyu ndiye alistahili kuitwa Nabii aliyewahi kuishi nasi.

Hazina yote aliyotutunzie, wezi na maharamia wameivamia. tukimbilie wapi sasa? mwalimu alituacha kungali asubuhi sana na jua bado kuchomoza. Mungu aendelee daima kuitunza ROHO YAKE. AMEN
 
Nasikia hata pale Ikulu watu wali "toast" baada ya kifo chake. Hakuna cha kushangaza.

Coming from you mkuu, na yanayoendelea sasa hivi, I believe it!

thank you kwa hili, now check this out:-



Rais Mkapa, amesema leo kuwa serikali yetu itatumia kila senti hadi ya mwisho kuhakikisha kuwa Mwalimu anazikwa kwa heshima kubwa anyostahili kupewa na taifa letu. Rais pia aliatangaza usimamishaji wa matumizi ya pesa za serikali kwa shughuli zozote za nje hadi baada ya mazishi ya Mwalimu.


What a unafiki, yaani unafiki tu umetujaaa!
 
Nilikuwa naangalia kideo ya wazee walioenda London kusimamia mipango ya kusafirisha mwili wakiongozwa na Marehemu Dr. Omar Juma. Walipoenda kuonana na mama Nyerere nakumbuka mama Nyerere alivyokuwa analia "wanafunzi wako wamefika.. uuwi uuwi" Na baadhi ya hao wanafunzi walikiri kuwa "wamefika" Ninachogundua ni kuwa baada ya kuwa katika darasa la Mwalimu kwa miaka yote hiyo ni wachache waliohitimu maana wengi walikuwa ni watoro! na sitashangaa hao ndio walionyanyua glasi za mvinyo!
 
Rais Muamar Ghadafi wa Libya, Moi wa Kenya, na Museveni wa Uganda, ni miongoni mwa marais wengi wanaotarajiwa kuhudhuria mazishi ya Mwalimu Nyerere.

Wengine ni pamoja na Prince Clans wa Uholanzi, Waziri Bw. Charles Josselin muwakilishi toka Ufaransa, Waziri Bw. Hon Zedhong muwakilishi wa rais wa China, Waziri Bw. Jan Trojborg muwakilishi wa serikali ya Denmark, Bi Grace Machel aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Msumbiji, ambaye sasa ni mke wa Mandela. Pia katibu mkuu wa OAU Dr. Salim, anatrajiwa kuwasili kesho.

Katika hali isiyo ya kawaida, daktari aliyemtibu Mwalimu hadi kuyafikia mauti yake, amesema kusamehe malipo yote ya kazi yake kwa Mwalimu kama ni mchango wake kwa familia ya Mwalimu, na taifa letu kwa ujumla. Hayo yalisemwa jana na msemaji wa familia hiyo ya Mwalimu, Bw. Joseph Butiku.


.....Itaendelea.......!
 
Hapo October 14, 2007 siku ya kuadhimisha miaka minane tangu Mwalimu atutoke, tutawasikia viongozi uchwara watakaopanda kwenye majukwaa bila aibu yoyote na kutwambia

Watanzania "tumuenzi" Mwalimu. Hawa jamaa wanafikiri Watanzania ni wapumbavu wa hali ya juu. Mtamuenzi vipi Mwalimu wakati yale aliyopigania siku zote ya kuhakikisha maslahi ya Tanzania na Watanzania siku zote yanawekwa mbele katika maamuzi mbali mbali ya serikali. Mtamuenzi vipi Mwalimu wakati mna ulafi wa hali ya juu wa kujilimbikizia mali! Mtamuenzi vipi Mwalimu wakati maadili ya uongozi ambayo yeye alikuwa anayasisitiza kila kukicha CCM ya leo imeamua kuyadharau. Mtamuenzi vipi Mwalimu wakati mnasaini mikataba ya madini ambayo haina maslahi yoyote kwa Watanzania na wakati huo huo details za mikataba hiyo mnaifanya siri kwa wenye rasilimali zao.

Kama kweli mnataka kumuenzi Mwalimu mnajua ya kufanya, vinginevyo acheni unafiki na usanii wa hali ya juu kuweni wa kweli wa nafsi zenu.
 
Nipashe Octoba 23, 1999:-

Rais Mkapa, ametabiri kwamba maisha ya wa-Tanzania yatakuwa bora na mazuri zaidi katika karne ijayo ya 21. Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu, kuhusiana na kifo cha Mwalimu Nyerere.

Akifafanua zaidi alisema kuwa Wa-Tanzania tulimpa Mwalimu jina la "Musa", kama vile mtume aliyehadithiwa kwenye Misahafu. Mwalimu alitupa sisi Uhuru na akatuongoza kupita jangwani kuelekea nchi ya ahadi ya maisha bora zaidi, na mimi kama rais wa sasa moja ya kazi yangu ni kuhakikisha kuwa tunamuenzi Mwalimu na matendo yake.

"Tunaamini kuwa katika karne hii inayokuja, Tanzania itakuwa nchi yenye maisha bora na mazuri zaidi". Aliongeza kuwa "Kama ilivyokuwa katika Musa wa Misahafu, maisha ya Mwalimu nayo yamekatwa kabla hatujaingia karne yenye matumaini mema kwetu, lakini tuko njiani na tutafika tu".


......Itaendelea...........!
 
Nasikia hata pale Ikulu watu wali "toast" baada ya kifo chake. Hakuna cha kushangaza.

Coming from you mkuu, na yanayoendelea sasa hivi, I believe it!

thank you kwa hili, now check this out:-



Rais Mkapa, amesema leo kuwa serikali yetu itatumia kila senti hadi ya mwisho kuhakikisha kuwa Mwalimu anazikwa kwa heshima kubwa anyostahili kupewa na taifa letu. Rais pia aliatangaza usimamishaji wa matumizi ya pesa za serikali kwa shughuli zozote za nje hadi baada ya mazishi ya Mwalimu.


What a unafiki, yaani unafiki tu umetujaaa!
FM ES,Sio unafiki pekee bali hata ubazazi na ukosefu wa shukrani wa kiwango cha juu.Katika wote huyu bwana ndio hasaa aliyetakiwa kuonyesha wazi kufuata kwa vitendo aliyoasisi Mwl. Kama wapigakura wengi walidhani kua huyu ni Ken M beki wa Yanga bila mwl kumuuza nani angenunua "hiyo bidhaa?'
 
Naunga mkono kauli ya Nyerererist, kuwa sisiemu wangebadili katiba yao na kuondoa kipengele kinachomwezesha raisi wa nchi kuwa mwenyekiti wake.
 
.VIONGOZI MBALI MBALI WAMMIMINIA SIFA KEM KEM.

Majonzi, simanzi na huzuni vilitawala byuso za viongozi wa mataifa mbali mbali, waliofurika uwanja wa taifa jana kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere. Wengi wao ambao walikuwa wakifahamiana na Mwalimu, walieleza masikitiko yao, kwa kuzingatia mchango mkubwa wa Mwalimu katika maendeleo ya nchi mbali mbali za Afrika, na nyinginezo zinazoendelea duniani.

Maelfu ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar, walifurika kuuaga mwili huo wa Mwalimu, uliohifadhiwa katika nyumba ndogo maalum tangu siku ya Jumanne asubuhi. Wananchi wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho, na jana ilikuwa zamu ya wawakilishi wa kimataifa waliokuja kujumuika nasi.

Baadhi ya viongozi wakuu wa kimataifa waliozungumza, ilikuwa ni pamoja na :-

1. Rais Olusegun Obasanjo, wa Nigeria ambaye alisema:-

"..Mwalimu alikuwa mshauri wangu wa karibu sana katika masuala yenye masilahi kwa walio wengi, na kifo chake ni pigo kubwa kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.."

2. Rais Daniel Moi, wa Kenya aliyesema:-

"..Hatuwezi kumsahau kamwe Mwalimu, ambaye ni shujaaa na kiongozi mkuu wa kizazi hiki, mimi binafsi nipo pamoja nanyi wa-Tanzania mfarijiwe na Mungu.."

3. Rais Jerry Rawlings, wa Ghana alisema:-

"...Kipaji cha Mwalimu hakikuwa tu kwa Tanzania bali kwa dunia nzima, Mwalimu ni miongoni mwa watu wachache sana duniani katika karne hii na katika taifa hili, na ni haki kwake kuwa baba wa taifa hili.."

4. Rais Joachim Chisano, wa Msumbiji alisema:-

"....Mwalimu anakuwa Baba Wa Taifa la Tanzania na Msumbiji pia. Sisi wananchi wa Msumbiji hatuna maneno ya kuwaeleza jinsi tunvyomshukuru Mwalimu na Wa-Tanzania kwa ujumla kwa ukarimu wenu na jinsi mlivyotusaidia..."

5. Bi Madeleine Albright, Waziri wa nje wa US, alisema:-

"....Mwalimu alikuwa na kipaji cha pekee, cha kuweza kuona mbali, mwenye uvumilivu wa hali ya juu, mchaji Mungu, mpenda maendeleo, na mwanamapinduzi halisi wa Afrika...."

6. Rais Martti Ahtisaar, wa Finland na mwenyekiti wa EU alisema:-

"...Mwalimu aliimarisha umoja wa kitaifa na kuwapa heshima wa-Tanzania ya kufahamika na dunia nzima..."


Viongozi wengine walioshirki katika kumuaga Mwalimu, ni pamoja na Sam Nujoma(Namibia), Museveni(Uganda), Bizimungu/Kagame(Rwanda), Muluzi(Malawi), Chiluba(Zambia), Buyoya(Burundi), Afweki(Eritrea), King Wilhem(Holland), Alix Michel(Sheli Sheli), Maria Mina(Canada) na wawakilishi wa nchi zipatazo 61 duniani.

Mwili wa Mwalimu uliondoka jioni kuelekea Butiama,ukiongozwa na Waziri Mkuu Bw. Sumaye.


.....Itaendelea......!
 
.MWILI WA NYERERE WAPOKEWA KWA MVUA NA RADI KALI BUTIAMA

Mwili wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, umewasili hapa na kupokelewa kwa taratibu za kijadi huku kukiwa na mvua kubwa na ngurumo kali za radi. Mwili huo uliwasili majira ya saa 1.45 usiku, ukitokea Musoma ambako ulipokelewa kwa taratibu za kijeshi.

Ulipowasili Butiama, mwili wa Mwalimu ulipokelewa na Chifu wa wa-Zanaki Japhet Wanzangi,ambaye alisema wanakijiji wamefarijika sana na kuwasili kwa mwili huo. Dada mwa marehemu Wambura Nyamageni, alisema mvua kubwa iliyonyesha ni dalili za mtu mkubwa aliyekuwa akipendwa sana na watu wake, na kwa sababu Mwalimu alikuwa akipenda sana kilimo ndio maana mvua hiy kubwa lilinyesha. Mvua hiyo ambayo ilielekea kufuata safari ya Mwili huo, ilianzia kijiji cha Kyabakari, baadaye Nyamisi, Kilimba, Buturu, na kuishia Butiama.

Pia habari zaidi kutoka Butiama zinasema kuwa jana usiku kulikuwa na tetemeko kubwa la ardhi kijijini hapo, hali ambayo wanakijiji wa hapo wanaihusisha na kifo cha Chifu wao Mwalimu Nyerere. Wakati mwili huo ukipitishwa wananchi wengi kwa malefu walikuwa kwenye miti na mapaa ya nyumba wakijaribu angalau kuliona jeneza hilo.

Mwalimu anatarajiwa kuzikwa kesho, na wananchi wanategemea mvua kubwa zaidi wakati wa mazishi.


.....Itaendelea......!
 
usimsahau na mtikila na alioyasema kuhusu mwalimu
Na hapo ndio wakati ambao pamoja na mengi anayofanya kutetea katiba walimuona mwehu,hata kama alikuwa na chuki naye ,haikuwa wakati muafaka kuropoka aliyosema.
 
.TUTADUMISHA UMOJA KWA NGUVU ZOTE-MKAPA

Rais Mkapa, amesema serikali itatumia uwezo wake wote kudumisha amani na umoja wa kitaifa ulioachwa na Mwalimu kama urithi kwetu wananchi wa taifa hili. Pia alisema serikali italinda Muungano wetu kwa nguvu zake zote, alikuwa akihutubia kutoka Uwanja wa Taifa jana, baada ya wageni kutoa heshima zao za mwisho.

Alisema serikali yake itaendelea kupigana na vita dhidi ya umasikini na kuona kwamba wanyonge wanasaidiwa zaidi. "Napenda nimuhakikishie kila mwananchi aliyeko ndani ya Tanzania na nje pia kuwa serikali yangu itahakikisha urithi wa Mwalimu haupotei kamwe, urithi ambao ni umoja wetu, amani, na vita dhidi ya umasikini".

"Wengi wetu tunajiona kuwa ni wanafunzi wake, na tunajihisi tumepata heshima kubwa kumjua na kufanya kazi naye katika uhai wake, ambapo aliwajali sana wanyonge, masikini, na waliodahifu katika jamiii" alisema Rais Mkapa.

.....Itaendelea.......!
 
Back
Top Bottom