Mwalimu Nyerere Foundation: Ujenzi wa ofisi umesitishwa?

Kitwange

Member
Apr 10, 2011
47
46
Jengo la ofisi ya Mwalimu Nyerere Foundation lililokuwa karibu na chuo cha IFM lilibomolewa kwa ajili ya matengenezo/ujenzi wa jengo jipya. Eneo lilizungushiwa hadi mabati, but hivi karibuni mabati yametolewa na makontena yaliyopo pale yamekuwa ofisi ya NPS (watu wa parking). Jengo linajengwa mahali pengine au ndio basi? Wakuu wenye nyeti tujuzeni, isije ikawa foundation ya baba wa taifa ndio inachinjiwa baharini kiaina.
 
Hayo ni matokokeo ya lile Kongamano la Mwalimu ambapo wazee Butiku et al walitoa yaliyo mioyoni kuhusiana na utendaji wa serkali ya JK na mstakabali wa taifa.
 
Yeah Kikwete kakataa Jengo lisijengwe Samora Avenue ambapo Ardhi ilishatolewa; kasema hataki Majengo Marefu kati kati ya JIJI la Dar

Nadhani anataka Jengo Lake Liwe Katikati ya Jiji
 
NPS wenyewe wapo kwa muda kampuni inahela kibao afu ofisi makontena..
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu mbariki mwakilishi wetu Ikulu..
 
Sijui imekuwaje, lakini hilo jengo walipewa uwanja pale mbele ya Avalon ya zamani baada ya Kikwete kukataa lijengwe pahali pake eti kwa usalama wa Ikulu. Ujenzi ulikuwa uanze Februari mwaka huu na mipango ilikuwa karibu imekamilika. Sasa sijui ni jambo gani limechelewesha.
 
Yeah Kikwete kakataa Jengo lisijengwe Samora Avenue ambapo Ardhi ilishatolewa; kasema hataki Majengo Marefu kati kati ya JIJI la Dar

Nadhani anataka Jengo Lake Liwe Katikati ya Jiji
hii kitu ilishaletwa hapa mwaka juzi nadhani

the only problem kwangu au wasiwasi ni kwamba keshoMNF watauza eneo atakuja mwarabu atajenga gorofa aroubaini na serikali itabariki, MNF imeombakibali imenyimwa

if i was MNF ningeuza nikajenge kwingine na kumuachia Mungu, malipo hapahapa bongo, duniani mbali
 
Hayo ni matokokeo ya lile Kongamano la Mwalimu ambapo wazee Butiku et al walitoa yaliyo mioyoni kuhusiana na utendaji wa serkali ya JK na mstakabali wa taifa.

Hapo sasa!! Hivi hata hiyo MNF ipo kweli? Manake baada ya hilo kongamano sijasikia makali yake tena zaidi ya kumsikia Mzee Butiku mara chache chache. SAS amenyamaa kimya, mzee Waryoba naye kimyaa sijui nini kimewasibu.
 
Back
Top Bottom