Mwalimu mkuu Kiluvya sec amezidisha adhabu

acha kabisa... kuna kibinti kingine bana kilipandisha majini kwa lazima, namaanisha kwa kujilazimisha! aisee, halafu baada ya hapo akaingia staff room na kufanya fujo ya haja!!!

waacheni tu wafeli.. tushaongea mno mpaka sasa ishakuwa kero..

ha ha ha ha, Kiongozi nimecheka kwenye kupandisha majini kwa lazima.
 
duh.. aisee Fidel80, huu mfumo ni majanga..! kuangalia tu matokeo inahitaji akili nyingine..

sasa kwa mfano hawa waliopata 49, tuwasaidije aisee?

Umeona hapo juu mtu ana point 41 kapata 0 na aliye pata point 45 kapata IV mwingine hiyo hiyo kapata 0 huu mfumo upo kwa ajili ya kuwafurahisha wanasiasa na wazazi ambao hawana uwezo wa kudadisi
 
Kuna jambo moja huwa linanikera sana, haswa pale napoona siasa au propaganda katika elimu au malezi kwa ujumla. Na kama wewe ni mzazi naomba nikushauri kuwa kamwe usije ingize swala la propaganda katika kumlea mwanao eti ukajidanganya unatimiza haki za watoto. Mlele kama wewe ulivyolelewa na mzazi wako hadi leo umekua mtu wakuheshimika na jamii.
Hakuna mtu alielelewa kizembe alafu leo umkute anamaisha mazuri, hata nyie humu ni mashahidi
 
kumi naona kidogo sana! Kuna shule inaitwa TAQWA sec ya mwanza angalia matokeo yao centre no ni 578, kwa walio soma hapo wanafahamu viboko kumi ni vichache sana watu wanatembelea 15 hadi juu!

Mzazi ukubisha beba mwanao tafutashule ingine! but impact yake inaonekana! nncho pinga ni kutoa adhabu bila sababu, Lakini pia isiwe ya kumuumiza bali kumfunza mtoto, lakini kama mtoto anasumbua mvua imnyeshee tu! hawa watoto wetu wa shule za kata jamani hem fanyeni uchunguzi mtajua tu! Alafu kuiendesha shule ya kata inahitaji moyo mgumu sana! lasiivyo mtamlaumu huyo mkuu wa shule bure tu! namleta mada nahisi wewe ni mwalimu wa iyo shule na unamalengo yako hapa!

Huo ndo ukweli ndugu. Unajua kuna wakati mimi niliona mwanafunzi wa kidato cha tatu amemkunja mwalimu shati, kisa hatati kupiga magoti mbele ya wenzake. Mwengine akamwambia mwalimu acha mambo ya kisenge kisa alikuwa anasumbua darasani, mwalimu akamwambia toka nje.
 
Hapo hakuna .com
ni full p.o.box ila wakati mwingine
mzazi ni lazima uangalie adhabu na kosa
kama vina ulinganisho.

Hiyo div natumaini uwe care kwa wanao isitokee tu
ila kwa upande wangu walishapita huko kote.

Wazazi wa .com mnawalemaza sana watoto ndo maana serikali inahangaika kubadili alama za ufaulu, we endelea kumwona huruma akipata Div. IV ya point 45 usije kulalamika hapa
 
Hapa najua huyo ticha ndo anaweka siasa kwenye eneo lake la kazi;
na sie wengine tunaojulikana ni wa upande gani ndo akaamua kunicharazia binti yangu;
natamani siku nikutane naye uso kwa uso ila nangoja hasira ziniishe kabisa.

Kuna jambo moja huwa linanikera sana, haswa pale napoona siasa au propaganda katika elimu au malezi kwa ujumla. Na kama wewe ni mzazi naomba nikushauri kuwa kamwe usije ingize swala la propaganda katika kumlea mwanao eti ukajidanganya unatimiza haki za watoto. Mlele kama wewe ulivyolelewa na mzazi wako hadi leo umekua mtu wakuheshimika na jamii.
Hakuna mtu alielelewa kizembe alafu leo umkute anamaisha mazuri, hata nyie humu ni mashahidi
 
Hapo hakuna .com
ni full p.o.box ila wakati mwingine
mzazi ni lazima uangalie adhabu na kosa
kama vina ulinganisho.

Hiyo div natumaini uwe care kwa wanao isitokee tu
ila kwa upande wangu walishapita huko kote.

Unaona inavyo onyesha wewe ni mzazi wa remote control sisi wazazi wa S.L.P tunakuangalia tu unavyo walemaza wajukuu zako kimaadili.
 
we ndo mwalimu sasa unaingia darasani unakuta kuna hewa nzito unauliza 'mbona kuna harufu humu ndani' afu ka mwanafunzi bakibencha huko kanajibu 'hata si tumesikia baada ya we kuingia' unafanyaje hapo.

kusema ukweli mimi nikiingia siulizi ili asijeropoka. Shida yangu nitacheka ila kipindi kikiisha natoka naye taratibu halafu atakuja wasimulia wenzake huyu teacher nuksi kweli. Simchapi hata kidogo. Halafu tuone nani atafaidika. Unajua kazi kubwa ya mwalimu ni kulea. Utajisikiaje ukienda ofisini unamkuta kijana anataka umsalimie ndo akusikilize? Wazazi acheni malezi duni. Sisi tunafahamu tunachokifanya. Ila uangalifu mkubwa sana. Ukipayuka namwonea mwanao its ok. Nakuachia umlee. Kuna mchungaji alisema mtoto wake anadhulumiwa na waalimu na wanafunzi wenzake. Aliachiwa amlee mwanaye. Haikuchukuwa miezi 7. Alipatikana na mimba akarudishwa nyumbani. Baadaye akajaribu kuitoa akafariki. UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO. Tena SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI.
 
Wengine niliwakuta wamekumbatiana hata waliponiona walishindwa wafanyeje. Nami sikupayuka. Niliwaacha. Ndani ya dakika tano niliwakuta wamepiga magoti mbele yangu wanaomba msamaha. Sikutaka kuwaabisha. Niliwasamehe lakini walinichimbia shimo. Walikuwa form 1. Walibadilika. Ila wale ambao nikiwashauri hawanisikii nawakabidhi wazazi wao kwa malezi zaidi.
 
kusema ukweli mimi nikiingia siulizi ili asijeropoka. Shida yangu nitacheka ila kipindi kikiisha natoka naye taratibu halafu atakuja wasimulia wenzake huyu teacher nuksi kweli. Simchapi hata kidogo. Halafu tuone nani atafaidika. Unajua kazi kubwa ya mwalimu ni kulea. Utajisikiaje ukienda ofisini unamkuta kijana anataka umsalimie ndo akusikilize? Wazazi acheni malezi duni. Sisi tunafahamu tunachokifanya. Ila uangalifu mkubwa sana. Ukipayuka namwonea mwanao its ok. Nakuachia umlee. Kuna mchungaji alisema mtoto wake anadhulumiwa na waalimu na wanafunzi wenzake. Aliachiwa amlee mwanaye. Haikuchukuwa miezi 7. Alipatikana na mimba akarudishwa nyumbani. Baadaye akajaribu kuitoa akafariki. UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO. Tena SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI.
well, thats good!
 
Back
Top Bottom