Mwalimu Julius Nyerere Na Picha Za Uhuru Wa Tanzania, Wachina Wanasema Picha Uongee Mara Elfu Moja

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Kwa Watanzania wengi ambao hatukuwepo miaka kumi na tano baada ya uhuru tunaweza kujifunza kupitia picha. 1.JPG
Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere na baadhi ya Wanachama wenzie wa TANU wakiendesha Mikutano Ya Hadhara Ya Kujenga Chama. 2 (2).JPG
Bibi Titi Mohamed akiwa na Mwalimu pamoja na viongozi wa TANU wakijenga TANU kupitia Mikutano ya Hadhara na wananchi
3 (2).JPG
Mwalimu Juius kambarage Nyerere akila Kiapo chake
4 (2).JPG
Mwalimu Nyerere Pamoja na Baadhi ya Viongozi wa TANU kama Bibi Titi Mohamed Wakiwa katika Mkutano.
4.JPG
Mwalim Nyerere akikaribishwa na Bibi Titi Mohamed.
5.JPG
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wanachama na Viongozi wa TANU akiwaaga kuelekea UNO [Marekani] kwa nia ya kudai uhuru wa Tanganyika.
6 (2).JPG
Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere akiludi tioka UNO [Marekani] alikokwenda kudai uhuru Wa Tanganyika
6.JPG
Mwalimu akiwakilisha ripoti ya Taarifa ya Tarehe ya Uhuru
7.JPG
Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere akiwa na wanachama na baadhi ya viongozi kutoa taarifa za uhuru wa Tanaganyika.
8 (2).JPG
Mapokezi na shangwe za matayalisho ya uhuru wa Tanganyika katika ukumbi wa Karimjee Hall.
8.JPG
Mwalimu katika kikao na ujumbe wa serikali ya kikoloni ya ungeleza, iliyotumwa na malkia chini ya mwailishi wake maalumu kwa swala la uhuru wa Tanganyika.
9 (2).JPG
Mwalimu akila kiapo cha uhuru wa Tanganyika
9.JPG
Mwalimu Julius Kamnbarage Nyerere akiwa na taarifa ya makubaliano lasmi ya uhuru wa Tanganyika mbele yake ni Mama Mzazi wa Mwalimu Nyerere Mgaya Nyang'ombe,
10.JPG Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya uhuru lasmi wa Tanganyika akiwa na vazi lasmi la Picha maalumu kwa matumizi ya ofisi kuu.
11 (2).JPG
Baadhi ya viongzoi wa kwanza wa kiaafrika katika Serikali ya Tanganyika.
11.JPG
Mwalimu akiwa na vijana waliotembea kwa mguu kuunga mkono maamuzi ya TANU wakitokea Kilimanjaro
12.JPG
Mwalimu akioongea na Wananchi Baada ya uhuru wa Tanganyika na kuanza kuimiza ujenzi wa TAIFA.
13 (3).JPG Mwalimu Julius Kambarage na Abeid Aman Kalume wakikabidhiana nyaraka watu hawa ndio waasisi wa Muungano wa Tanaganyika na Zanzibar.
13.JPG Mwalimu Julius Kambarage Nyerer akiongea na Umma wa Wanachi Kwenye maeneo ya vijijini Nchini Tanganyika.

14.JPG Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Abeid Amani Karume na Moyo,Viongozi hawa ni moja ya chachu uasisi wa muungano Zanzibar na Tanganyika.
15.JPG Mwalimu Juklius Kamabarage Nyerere akiwa na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar,Kulia kwa Mwalimu anaongea na Mzee Thabit Kombo na kushoto kwa Mwalimu ni Mzee Abeid Aman Kalume ,
16.JPG Mwalimu Katiaka Ujenzi wa Taifa la Tanzania [By then Tanagyika] kwa Vitendo
17.JPG
Mwalimu katika baadhi ya vikao na baadhi ya Mawaziri kama vile Mzee Rashid Kawawa na alie simama ni George Kahama.
 

Attachments

  • 3.JPG
    3.JPG
    59 KB · Views: 306
  • 18.JPG
    18.JPG
    98 KB · Views: 305
Ahsante kwa picha lakini kwa hawa vijana waliosoma shule za kata ungewasaidia sana kama kila picha ingekuwa na caption.; kwa mfano picha ya pili mwalimu alikuwa jukwaani na Mzee John Rupia na Bibi Titi Mohamed. Sasa hapo hawa vijana wanaposoma historia ya nchi wanaweza kuwa na kumbukumbu ya sura za wahusika.
 
Ahsante kwa picha lakini kwa hawa vijana waliosoma shule za kata ungewasaidia sana kama kila picha ingekuwa na caption.; kwa mfano picha ya pili mwalimu alikuwa jukwaani na Mzee John Rupia na Bibi Titi Mohamed. Sasa hapo hawa vijana wanaposoma historia ya nchi wanaweza kuwa na kumbukumbu ya sura za wahusika.

Ni vyema tukapata wanaojua vyema matukio hayo wakatusaida kujua picha hizo kwa kina ni matukio yapi hayo japo kwa kidogo nimeweza kujua kwa kidogo,nin hakika wapo wanaojua kwa undani zaidi.
 
Safi sana, lakini kichwa cha habari cha habari kimenisumbua sana.
.Vipi Mkuu umesumbuka na nini JK mbona iko wazi au kwa kuwa sikutumia Tanganyika,kidogo kwngau mimi nakuwa mzito kuitumia kwa kuwa mimi nimezaliwa na kukua nakukuta jina Tanzania hivyo kisaikolojia naijua Tanzania kuliko Tanganyika si makosa,ila ndio uhalisia.
 
nimeipenda, picha zinaonesha jinsi viongozi we2 walivyokuwa na muonekano wa uzalendo halisi, yaani ni tofauti kbs na sasa, na hata ukilinganisha na picha za sasa utaona sura zimejaa unafiki na tamaa tupu
 
thanks, picha nzuri sana mkuu!

samahani, kuhusu picha no 4, 6 na 9. Je hao waliomzunguka nyerere ndo wale wazee wetu wa kariakoo?
 
Ukiachia magoti na mkeka hata afya za wahusika hazifanani. Labda ni kwenda na wakati.
 
kaalbum katamu...naweza kutumia siku nzima kumsimulia mwanangu asiyejua tulikotoka
 
From these pictures I have learnt that Bibi Titi was instrumental to our independence. What went wrong between her and Nyerere? How many got lost in the same manner? Am glad Bibi Titi was "picked" back though am sure many were made to disappear from our history. That sin is haunting our nation to date.
 
Mimi binafsi huyu mzee simkubali. Ananikumbusha machungu ya udikteta wake kipindi cha kuanzisha vijiji vya ujamaa. Yeye ni muasisi wa haya matatizo yanayotukabili sasa.

Mungu amrehemu huko aliko.
 
Back
Top Bottom