Mwalimu Joseph KABALIMU is no More

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Kwa Wana JF waliosoma Tabora Boys na UDSM miaka ya 1980's na 1990's

Nasikitika kuwajulisha kuwa Mwalimu wetu JOSEPH MWOMBEKI KABALIMU amefariki dunia huko Karagwe, siku ya jumapili 27/5/2012. Mazishi yake ni Alhamisi 31/5/2012. Mpaka kifo chake alikuwa ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Karagwe (KARASECO).

Mwalimu Kabalimu atakumbukwa kwa mengi na wanafunzi wake. Akiwa ameanzia kazi ya ualimu katika shule za msingi na kujiendeleza hadi kufundisha Chuo Kikuu.

Apumzike kwa amani mwalimu wetu.
 
Kweli ulimwenguni ni safari tu,Namkumbuka Mwl.Kabalimu sana ila leo ndo nimejua majina yake yote.Pale TS Enzi ya Ndeki ,Mushaija,Biamungu,Kimalamashwi,Mwakasonda,Kalyoto,Afande Kisenge,Hiza nk nk.Jamaa alikuwa mwalimu hasa maanake tulimwita Nazi hasa wakati wa zamu zake.Namkumbuka kwa sababu hakuwahi kunifundisha lakini alinichukia sana.Hata wakati mmoja nilikutana naye Bongo pale Potsa mpya akiwa UDSM kitivo cha sanaa,Sijui kama aliupata U Profesa lakini jamaa alikuwa mahiiri sana kwenye taaluma yake.Ningekuwa Karagwe hakika ningeshiriki maziko yake kikamilifu RIP KABALIMU.
 
RIP Mwl. Mwombeki. Lakini pia ningependa kujua kama huyu Mwombeki anayezungumziwa hapa ndo yule niayemfahamu mimi. Bahati mbaya nilikuwa najua jina moja la Mwombeki. Lakini huu ninaye mjua mimi aliuwapo Boys mpaka miaka ya mwanzoni mwa 2000 tofauti na muda aliosema mtoa taarifa wa 1980's to 1990's. Alikuwa anafundisha hesabu A-Level tena alikuwa bingwa wa hesabu maana kwajinsi alivyokuwa anashuka vitu hutamani kukosa kipindi chake. Ningependa kujulishwa na mtoa mada au mwingine mwenye taarifa kama ndiye hoyo anayezungumziwa. Lakini pia hii habari ingepelekwa kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko maana hii si habari ya kisiasa na wala huyo sidhani kama alikuwa mwanasiasa. Once again RIP Mwl. Mwombeki
 
Kimatire
Ni kweli Kabalimu alikuwa Mwalimu haswa. Akishika zamu wote tulijua yuko zamu.
Pale UDSM hakuwahi kupata U-profesa. Alifanya akapata Masters pale UDSM, baadaye akaenda Addis Ababa akapata Masters nyingine. Mwishowe alienda Australia akapata Masters nyingine. Nakumbuka aliporudi UDSM wakamzibia nafasi ya kurudi kufundisha na ndipo akapata kazi Karagwe. Nilikutana naye Wizarani wakati fulani akawa ananiambia kuwa anafanya PhD Ubelgiji ambayo atakuwa ameimaliza kabla ya kifo chake. Pale TS hakuwa askari jeshi lakini aliwashinda maaskari jeshi kwa nidhamu ya kijeshi.
 
RIP Mwl. Mwombeki. Lakini pia ningependa kujua kama huyu Mwombeki anayezungumziwa hapa ndo yule niayemfahamu mimi. Bahati mbaya nilikuwa najua jina moja la Mwombeki. Lakini huu ninaye mjua mimi aliuwapo Boys mpaka miaka ya mwanzoni mwa 2000 tofauti na muda aliosema mtoa taarifa wa 1980's to 1990's. Alikuwa anafundisha hesabu A-Level tena alikuwa bingwa wa hesabu maana kwajinsi alivyokuwa anashuka vitu hutamani kukosa kipindi chake. Ningependa kujulishwa na mtoa mada au mwingine mwenye taarifa kama ndiye hoyo anayezungumziwa. Lakini pia hii habari ingepelekwa kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko maana hii si habari ya kisiasa na wala huyo sidhani kama alikuwa mwanasiasa. Once again RIP Mwl. Mwombeki

Kabalimu pale Boys hakuwepo kwa jina la Mwombeki na wala miaka ya 2000 tayari alikuwa Mlimani yeye alikuwa Mwalimu wa Lugha tena nadhani Kiswahili na sanaa ,Tukiita UFARAGUZI, Yeye aliingia Tabora School akitokea Butimba miaka ya 1983 nadhani alikaa hadi 1992 hivi.Alikuwa na maringo sana huyu Bwana ,Halafu alipenda kwenda Warsaw sana.
 
RIP Mwl. Mwombeki. Lakini pia ningependa kujua kama huyu Mwombeki anayezungumziwa hapa ndo yule niayemfahamu mimi. Bahati mbaya nilikuwa najua jina moja la Mwombeki. Lakini huu ninaye mjua mimi aliuwapo Boys mpaka miaka ya mwanzoni mwa 2000 tofauti na muda aliosema mtoa taarifa wa 1980's to 1990's. Alikuwa anafundisha hesabu A-Level tena alikuwa bingwa wa hesabu maana kwajinsi alivyokuwa anashuka vitu hutamani kukosa kipindi chake. Ningependa kujulishwa na mtoa mada au mwingine mwenye taarifa kama ndiye hoyo anayezungumziwa. Lakini pia hii habari ingepelekwa kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko maana hii si habari ya kisiasa na wala huyo sidhani kama alikuwa mwanasiasa. Once again RIP Mwl. Mwombeki
=======

Bwana Chona,
Huyu siye Mwombeki unayemjua. Jina la Mwombeki ni la kati kwa hayati Kabalimu na halikufahamika Tabora School wala UDSM. Yeye alijulikana kama Joseph Kabalimu au kwa watani wake aliitwa "Kyoma". Hakufundisha mahesabu, bali masomo ya sanaa na lugha.
 
Mazishi yake yanafanyika kijijini kwao Bulambizi,kanyangereko,Maruku Bukoba vijijini.Ningelikuwa na fursa ningelipenda nihudhurie.kama sikosei alijishughulisha pia na mradi w uanzishaji wa University of Karagwe. RIP Mwalimu
 
RIP Mwl. Mwombeki. Lakini pia ningependa kujua kama huyu Mwombeki anayezungumziwa hapa ndo yule niayemfahamu mimi. Bahati mbaya nilikuwa najua jina moja la Mwombeki. Lakini huu ninaye mjua mimi aliuwapo Boys mpaka miaka ya mwanzoni mwa 2000 tofauti na muda aliosema mtoa taarifa wa 1980's to 1990's. Alikuwa anafundisha hesabu A-Level tena alikuwa bingwa wa hesabu maana kwajinsi alivyokuwa anashuka vitu hutamani kukosa kipindi chake. Ningependa kujulishwa na mtoa mada au mwingine mwenye taarifa kama ndiye hoyo anayezungumziwa. Lakini pia hii habari ingepelekwa kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko maana hii si habari ya kisiasa na wala huyo sidhani kama alikuwa mwanasiasa. Once again RIP Mwl. Mwombeki
RIP Kabalimu,

BOYZIA dont confuse huyu sio Mwombeki wa Maths na Physics mzee wa Swali likishindikana tumplekee H/Master wakat huo alikuwa Mrisho miaka ya 98 to 2007 i think, Mwombeki yuko Sengerema ni Headmaster one time nilikutana nae Mwanza akaniambia.
Asante,
 
RIP mwalimu wetu,umetangulia kama ada ya viumbe vyote!Bwana alitoa na sasa ametwaa,jina lake lihimidiwe,AMINA.
 
Nimemkumbuka Head Master wangu Mr. Kabalimu, namkumbuka kwa mengi ila hii sitosahau..Kuna siku nilisafiri nae kwenye gari la shule tukielekea bukoba mjini,tulifika sehemu akaona ng'ombe wanakula mazao basi akatuuliza hivi ''Hivi hawa ngombe wa nani wanayona shambani?'' Tulokuwa ndani ya gari tulishindwa kuvumilia kicheko ikabidi tucheke sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom