Mwalimu alisema....

Katika siku ya wafanyakazi May 1995, raisi mstaafu na mwenyekiti mstaafu wa CCM Mwl. Julius K. Nyerere ndiyo alikuwa mgeni rasmi. Alitoa hotuba ndefu kidogo iliyo jaa maono na muongozo.

Lakini mimi kuna sehemu moja tu ya hiyo hotuba ndiyo ilinikuna kupita zote. Mwl. alisema kwamba wakati yeye anaingia madarakani na wenzake walikua hawana model ya kufuata. Kila kitu kili takiwa kujengwa kuanzia juu kwenda chini yani "trial & era".

Akaendelea kusema kwamba ana kubali serikali yake ilikua na mabaya yake lakini pia ilikua na mazuri yake. Akasema serikali ya Mwinyi ilipaswa kuchukua yale mazuri na kuya acha yale mabaya. Hali kadhalika aka sema nao serikali ya Mkapa ina takiwa kuchukua yale mazuri ya kipindi cha Mwinyi na kuya acha mabaya.

Haya maneno yali nigusa sana kwa sababu ni maneno rahisi lakini magumu kuelewa. Leo hii ina shangaza serikali zetu inafanya kinyume na kuchukua mabaya yote ya serikali zilizo pita na kuya acha mazuri. Ina sikitisha kwamba baada ya miaka hamsini ya uhuru tuna rudi nyuma badala ya kusonga mbele.

Je ni mazuri yapi ya serikali za Nyerere, Mwinyi na Mkapa zili takiwa kuendelezwa?

Mazuri ya Mwl ni siasa ya ujamaa na kujitegemea. It is a threory and some us have dedicated our lives into taking from where Mwl ended and bring into existence what he dreampt to be the future of our country. I will make all it takes to make sure na muenzi baba wa taifa kwa vitendo and have said this tangu naanza kupata akili. Sihitaji kulaumu wengine but I want to show people it is possible and here I am in the very right track to do what I intended. I dont say will come with all answers but will really bring into existence the system which would later on be updated by the coming generations.
 
Last edited by a moderator:
Tumempa sifa nyingi Nyerere. Mimi nampa sifa mbili tu. Aliipenda tz kwa moyo wake wote na pili alikuwa mwaminifu kwa JMT na watu wake. Nyerere alikufa masikini kwa ajili yetu na aliipenda tz kuliko hata familia yake. Nikimwangalia Dr Slaa naiona sura ya nyerere. namwona kama ni nyerere wa kipindi tunachoishi. ni maoni yangu ila inatoka moyoni
 
Mkuu you are seriously comparing Dr. Slaa to Mwl. Nyerere? Anyway bora ume sema ni maoni yako.
 
Mazuri ya Mwl ni siasa ya ujamaa na kujitegemea. It is a threory and some us have dedicated our lives into taking from where Mwl ended and come into existence what he dreampt to be the future of our country. I will make all it takes to make sure na muenzi baba wa taifa kwa vitendo and have said this tangu naanza kupata akili. Sihitaji kulaumu wengine but I want to show people it is possible and here I am in the very right track to do what I intended. I dont say will come with all answers but will really bring into existence the system which would later on be updated by the coming generations.

Ina wezekana falsafa ya Mwl kuhusu ujamaa ilikua ina matatizo ya hapa na pale. Ila labda kwa kuchunguza marekebisho yana weza fanyika. Binafsi I'm not a fan of neither socialism nor capitalism. I sincerely believe Social Democracy is the best system for us.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kuna wakati mzee huyu alizungumzia katiba, alihoji kwanini ccm wanakaa pekeyao kuandaa katiba mpya, vile vile alizungumzia suala la mgombea binafsi......mazuri ni mengi sana
Angeliiruhusu ilo enzi ya utawala wake....! Mbona alikuwa ndio mgombea pekee wa nafasi ya urais!?
 
Huyu mzee mnamtukuza bure lakini ametawala nchi kibabe na kidikteta sana.

Baada ya kuona mambo yanamkalia vibaya na Watanzania wanaanza kuamka ndio akaanza kuzungumza lugha hizi za kujipendekeza kwa wananchi na kuwafanya waliokuja baada yake wabaya.

Chukua huo mfano wa Katiba unayosema Mkuu. Si Nyerere huyu huyu alieteua wajumbe wa CCM na Zanzibar kuandaa Katiba ya Chama

chao na baadae akatumia Kamati hiio hio ya Chama chake kuunda Katiba ya Tanzania?

Si Nyerere huyu huyu aliekiuka Mkataba wa Muungano na kuligeuza Bunge letu la Kawaida na kulifanya kuwa Bunge la Katiba na kuipitisha?

Si Nyerere huyu huyu alievunja Mkataba wa Muungano na kiongezea madaraka SMT kwa kuifisidi Zanzibar?

Huyu Nyerere tutamkumbuka daima kwa chuki zake dhidi ya Zanzibar mpaka kwa kushindwa kujizuia akasema,

"If i could tow that island out into the middle of Indian Ocean, i could do it" - JK Nyerere

Huyu Nyerere ndio tutamkumbuka sana kwa mabaya yake na hakuna jema alotufanyia zaidi ya kutusaidia kumuondoa Mkoloni lakini kumbe kwa yeye kuifanya Zanzibar Koloni la Tanganyika.

Huyu ni mtu mbaya sana na hastahiki kusifiwa ila na wakoloni wenzake.

wewe umetumwa nini?:director:
 
Angeliiruhusu ilo enzi ya utawala wake....! Mbona alikuwa ndio mgombea pekee wa nafasi ya urais!?

Alikua na mapungufu yake mkuu ila ukiangalia viongozi wengi wa Afrika wakati huo tukubali tuli bahatika kumpata Nyerere.
 
support MKUU! HE IS A YARDSTICK AND HE ACCEPTED THAT HE HAD HIS SHORTCOMINGS LIKE WE ALL HAVE WHICH IS A PLUS! ALIIPA ELIMU KIPAUMBELE WA2 KUSOMESHWA MPAKA HAVARD! BUT WHAT ARE THEY PAYING US WITH? MIKATABA AINA YA CHIEF MANGUNGO! MZEE KIBOLA MAKANI ALIWAHI KUNIAMBIA KABLA YA KUANZISHA NIC WALIPELEKWA CANADA 4 2YRS SECONDMENT! HE COULD HAVE PLUNDERED OUR NATCHOR RISOZ
Alikua na mapungufu yake mkuu ila ukiangalia viongozi wengi wa Afrika wakati huo tukubali tuli bahatika kumpata Nyerere.
 
Taifa lipi are you reffering to Dume? Kijitu nadhani ni matusi au tuseme ni dharau na nikimuona mtu badala ya kujadili issue anajadili mtu, huanza kumdharau sana tu.

JF ni ukumbi huru wa mtu kutolea mawazo yake lakini wewe baada ya kujadili hoja, unanijadili mmi.

Wewe unamuona Nyerere hivyo, usinilazimishe na mimi kumuona hivyo.

Hapa si ubinafsi hata kidogo, ni hoja kwa hoja.

Hoja hujibiwa kwa hoja. Dume jibu hoja na uwe tayari kukubali mawazo ya wengine.
 
kwenye black hoja zako zimegonga
kwenye blue mlilazimishwa na nyerer kuingia TANZANIA?
kwenye nyeusi wewe ni mzushi manamzushia mzee wa watu
Huyu mzee mnamtukuza bure lakini ametawala nchi kibabe na kidikteta sana.

Baada ya kuona mambo yanamkalia vibaya na Watanzania wanaanza kuamka ndio akaanza kuzungumza lugha hizi za kujipendekeza kwa wananchi na kuwafanya waliokuja baada yake wabaya.

Chukua huo mfano wa Katiba unayosema Mkuu. Si Nyerere huyu huyu alieteua wajumbe wa CCM na Zanzibar kuandaa Katiba ya Chama chao na baadae akatumia Kamati hiio hio ya Chama chake kuunda Katiba ya Tanzania?

Si Nyerere huyu huyu aliekiuka Mkataba wa Muungano na kuligeuza Bunge letu la Kawaida na kulifanya kuwa Bunge la Katiba na kuipitisha?

Si Nyerere huyu huyu alievunja Mkataba wa Muungano na kiongezea madaraka SMT kwa kuifisidi Zanzibar?

Huyu Nyerere tutamkumbuka daima kwa chuki zake dhidi ya Zanzibar mpaka kwa kushindwa kujizuia akasema,

"If i could tow that island out into the middle of Indian Ocean, i could do it" - JK Nyerere

Huyu Nyerere ndio tutamkumbuka sana kwa mabaya yake na hakuna jema alotufanyia zaidi ya kutusaidia kumuondoa Mkoloni lakini kumbe kwa yeye kuifanya Zanzibar Koloni la Tanganyika.

Huyu ni mtu mbaya sana na hastahiki kusifiwa ila na wakoloni wenzake.
 
Mazuri ya Mwl ni siasa ya ujamaa na kujitegemea. It is a threory and some us have dedicated our lives into taking from where Mwl ended and come into existence what he dreampt to be the future of our country. I will make all it takes to make sure na muenzi baba wa taifa kwa vitendo and have said this tangu naanza kupata akili. Sihitaji kulaumu wengine but I want to show people it is possible and here I am in the very right track to do what I intended. I dont say will come with all answers but will really bring into existence the system which would later on be updated by the coming generations.

Ame;

You are a great personality! You have dedicated your life into something noble and humane! Am sure you will not regret this!!

It inspire to note there some few people like you who cherish and are sereous with noble personality and full of humanity,

Nyerere alitambua thamani ya Uasili wa mwandamu ..ambao ni Utu! Na akasimamia kila mfumo wa kijamii kufuata dhana ya utu, Kwani hakuna mafanikio yeyote kwa kiumbe chochote hai nje ya Uasili wake. Mwanadamu hawezi kufanikiwa na kupata maendeleo yeyote nje ya uasili wake ambao ni utu wake!!!

Wanyama na mimea yote inafuatia asili zake tu na kupata maendeleo yake yote! Mnazi unafuata uasili wake na kuwa mnazi ...na hauwezi kuwa zaidi ya Mnazi..na taarifa zote za mafanikio ya kuwa mnazi kamili ..unapatikana kwnye uasili wake nje ya uasili wake hakuna mnazi

... wanyama wote wanafuatia ..uasili wao..kobe hawezi kuwa chochote zaidi ya kuwa kobe..wala hajadili kuwa kobe ..anafuata uasili wake na kufanya na kuwa kama kobe wote..Hawezi kuwa kobe kama ataukana uasili wake!!

Katika viumbe wote hai..Ni binadamu peke yake anahoji na kusaliti uasili wake... kwa porojo na visingizio vya kijinga kabisa!!

Watu wanapinga utu... watu wanatamani kuwa kile ambacho sio utu wao..

Watu hawataki mifumo yote ya kijamii kufuata dhana ya utu ambayo ni asili yao..

Watu nwanapingana na asili zao... Sasa kama Mtu na akaili timamu anapinga utu wake tumuite nani? Mnyama ?

Nyerere alikwenda mbali hadi kuweka azimo la utu ... lile la pale arusha...

Leo wanasema azimio hilo la utu ..limepitwa na wakati ... what a stupidity!!

Utu wa mtu unapitwa na wakati...Ni uasili gani wa kiumbe chochote hai ulishawahi kupitwa na wakati..

Nyerere ni mtetezi wa utu wa mtu ...na kila alichosema , alichofikiri na kutenda ..it was along those ... Lines..

Ili kujitegema na kujiogoza na kujitwala kama kiumbe lazima uenzi asili yako...KUJITEGEMEA ni hulka ya mwandamu ..na lazima afanye hivyo kutokea au kupitia kwenye utu wake..ndio maana ya azimio la arusha na siasa ya kujitegemea...

Utu haupitwi na wakati ... Hivyo kujitegemea hakupitwi na wakati ...Usijitegemee ..ili ..uwe nini... !!!

Ndio maana nimekuona wewe mtu maalum kwa kujitolea kumuenzi na kufanya kila utakaloweza ...kuona kuwa ndoto za taifa kufikia UTU KAMILI WA TAIFA UNAFIKIWA!!
 
Very true mkuu. Ninacho mpendea ni kwamba jamaa alikua na uwezo wa kuona mbali si hawa wa leo wanao ona urefu wa pua tu. Japo ali kuwa na mapungufu yake tunge chukua yale mazuri yake tunge kuwa mbali. He was a political genius and he is my political idol.

nakubaliana na kila kitu isipokuwa sarufi zako tu. 'kua' na 'kuwa' ni vitu vi2 tofauti kabisa
 
kwenye black hoja zako zimegonga
kwenye blue mlilazimishwa na nyerer kuingia TANZANIA?
kwenye nyeusi wewe ni mzushi manamzushia mzee wa watu

Kwenye nyeusi hakuna kilichogonga, ni katika kumtukuza tu Saint wenu mtarajiwa
Kwenye blue huyo mzee wenu ndie aliekuja na proposal kwa Karume na baadae kuuchakachua huo unaoitwa muungano.
Kweye nyeusi nyengine, jibu lake kama la kwanza.
 
Kwa hiyo Karume haku weza kuchambua faida na hasara za muungano au?
 
Nakumbuka mwl. alipinga sana mfumo wa ubinafisishaji akida nchi bado ni changa sana hakuna uelewa wowote akakumbusha tizama viwanda aliviacha vingi vya serikali na binafsi lakini duuu vimeshinwa milikiwa na serikali sasa sijui nani alikuwa bora kati ya Mwinyi Mkapa na Mrisho Kikwete, Mwl. Nyerere aliwaacha hawa kwa fikra na kumbukeni was those 1990's lakini hawa maraisi wa majuzi ndio walipaswa kuja na fikra mpya,hali mpya nguvu zaidi matokeo yake ni kudidimiza nchi kwa siasa zao chafu
 
nyerere amekuwa mjanja tu kuwaachia wenzie mchezo ambao tayari alishapoteza. na kukimbilia kwa wananchi wasio waelewa kujisafisha faster faster.

Kosa kubwa la Nyerere alishindwa kujenga system. zoezi lake la kujenga mfumo wa ujamaa na kujitegema ulishindakana ila hakuwa tayari kulikubali hiko.

Kushindikana kwa mfumo huko ndio kumetufikisha hapa tulipo maana alipomwachia mzee mwinyi utawala, alikuwa akimshinikiza auendeleze mfumo ule ule ulioshindwa Mzee Mwinyi kwa uoga wake akawa anaenda nao hivyo hivyo. Kwa kuwa tanzania wengi hatukuwa na uwezo wa kuchambua mambo kama ilivyo sasa hiyo ilikuwa ni nafasi nzuti kwa Nyerere kutupeleka vile alivyokata.

Utakubaliana nami kuwa kila alikuwa kinyume na mawazo ya mwalimu wakati huo alionekana kama haini. na mifano ipo.

kwa kuogopa hizo fimbo za mwalimu kila mtu alikuwa akiburuzwa tu na fikra za mwenyekiti wa CCM.

Nyerere ametukosea mengi wala watu msimtetee hapa.

Kama Nyerere angekubali demokrasia na mapema ungekuta tuko mbali sana sasa.
 
Kwa hiyo Karume haku weza kuchambua faida na hasara za muungano au?

Karume Mkuu Mwanafalsafa alikuwa baharia na hakubahatika kwenda shule.

Nyerere alimzidi ujanja kwa kumtishia kurudi tena kwa Waarabu na kwa woga na hofu akameza ndoana haraka. Alipokuja kushtuka, kilichokuja kumkuta sio siri tena.

Hata hivyo Mkuu mambo yamebadilika sana tena sana na ndio maana majuzi tu wakati wa kujadili mswada, wazee wenzake walisema,

*"Ule wakati wetu na Nyerere tulikuwa tunakubali lakini hawa vijana wa leo hawakubali, Bw. Sitta, ITS OVER*".
Huyu ni Mzee Hassan Nassor Moyo ambae wakati wa kuungana alikuwa ndie Waziri wa Sheria wa Peoples Republic of Zanzibar
 
Si hivyo tu bali pia hotuba zake zinavutia kusikiliza hata siku nzima kwani hazikuwa za kinafiki kama ilivyo kwa hawa wanaojichubua magamba kwa sasa.

Mzee yule alikua zawadi kwa watanzania lakini hatujui mpaka alipotutoka,Ukweli alikua na UTU na Kiongozi ni yule ambae anaacha legacy.kupitia hizi pulukushani kati yetu na mafisadi tunajifunza kuwa kiongozi ni lazima awe na kitu cha ziada tofauti na sisi wengine tunaomchagua kiongozi husika.
 
Back
Top Bottom