Mwalimu Alisema Ujamaa Wa Kiafrika Ndio Falsafa Yake Ya Kuwaongozea Watanzania,Waliofuta!!!!!!

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
DILA ndio njia mwelekeo na mwongozo wa lolote lile tunalolitenda.Hata vijijini walikotoka wazazi wetu,kabla ya utekelezaji wazee wanakaa wanatoa mwelekeo kuwa jambo hilo lifanyike kwa namna hii na ile.

Mwalimu shuleni akitaka kuwapa wanafunzi wake majaribio [Home work] uwa anatoa mwelekeo vile vile kuwa wapitie wapi na hata Mhadhili [Lecturer] chuoni nae upitia njia hizo hizo kutoa assignment, huku akitoa na ziada kwa kukupa mapitio [reference] ili ujue kuwa anachokupatia majibu yako yatoke ndani ya wigo huu ama ule kulingana na mahitaji ya Mhadhili kwenye somo husika.

Nataka kujua Mwalimu wigo wake katika kuwafundisha Watanzania,alichagua Ujamaa wa Kiafarika,yaani alibuni kwa kuangalia Waafrika wanavyoishi kisha kwa tafukuri yake akaibuka na mbinu na maalifa ya jinsi ya kuwaongoza Watanzania kwa kufuata mfumo ule wa Kiafrika, duniani kote naeleweka waafrika wanaishi vipi.

Uwa nacheka sana na kutafakari sana kuwa Waafrika,waliochukuliwa utumwani Amerika,leo hii maalufu kama Waamerika weusi ukiwaangalia mfumo wa maisha yao huko Marekani,wakiwa ni vizazi vya Waafrika Watumwa miaka hiyo,bado familia zile na ustaarabu wote wa Mataifa ya kimagharibi unaowazunguka wanaishi kama familia moja ya kiafrika.

Ndani ya familia zile watu wanaishi na mjomba,shangazi,binamu,bibi na babu ndni ya nyumba moja kama jinsi,Mtanzania wa leo anavyoweza kuishi na familia yake yenye mfumo huo huo hapa nyumbani.Hivyo kwa aiba hiyo waafrika tunafanana.

Waameriaka weusi pamoja a kuzungukwa na wazungu katika mazingira yao bado wanaishi kiafika wakishirikiana kwenye mambo mengi,na hao wako ndani ya mataifa yaliyoendelea.Je Watanzania walio asisiwa mfumo wa kuishi kiafrika na Mwalimu JKN,na ambao ulizaa matunda kwa kuwafanya waishi kwa pamoja na wenye kuheshimiana licha ya tofauti kubwa ya kimakabila mengi waliyo nayo,wamefika wapi baada ya awamu ya mwasisi huyo wa mfumo kungatuka na hatimae bahada ya kifo chake.

Je sisi baada ya utawala wa Mwalimu Julias Kambalage Nyerere alale pema peponi,Watawala waliofuata na wanatuongoza sasa hivi, wanatumia falsafa hipi kama Dila [Vision] yao ya uongozi dhidi yetu sisi kama Watanzania ambao kihaiba tu Waafrika.

Ni falsafa hipi kati ya hizi,inayotumia na Taifa letu kama Dila [Vision] inayotusaidia kuamua,kutenda,kufikilia na kuwazia mazuri juu ya ustawi wa Taifa letu na Watu wake Kama Taifa huru la Kiafrika?
1: Kizungu
2: Kichina
3: Kiasia
4: Kiarabu
5: Kiafrika [Ujamaa wa Kiafrika Mwalimu Falsafa]

6: Kizungu na Kiafrika
7: Kichina na Kiafrika
8: Kiasia na Kiafrika
9: Kiarabu na Kiafrika
10: Kizungu,Kichina,Kiasia,Kiarabu na Kiafrika.

Ebu Tujuzane.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom