Mwalimu ajifungua watoto wanne

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610

000001ajifungua.jpg


MWALIMU wa Shule ya Msingi Ukombozi, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Buntwa Brown Mwakabengele amejifungua watoto wanne katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

Watoto hao, ambao watatu kati yao ni wasichana na mwanaume mmoja, walizaliwa Machi 12, mwaka huu kwa njia ya upasuaji.

Mama huyo alisema anamshukuru Mungu kwa baraka hizo ingawa anajua zipo changamoto za malezi mbele yake.
"Namshukuru Mungu kwa sababu wanaendelea vizuri, afya zao si mbaya sana ingawa bado wapo chini ya uangalizi wa madaktari," alisema Buntwa.

Awali mama huyo alikuwa na mtoto mmoja, na sasa ana watoto watano. Alisema alipokwenda kwenye vipimo katika kliniki yake iliyopo Mikocheni, aliambiwa wameonekana watoto watatu katika mfuko wa uzazi.

"Siku niliyoshikwa na uchungu, ilibidi niletwe Muhimbili, niliwasikia madaktari wakisema watoto wapo wanne, lakini awali nilijua nina ujauzito wa watoto watatu tu," alisema Buntwa.

Alisema:"Pamoja na kwamba sasa nina watoto watano, awali niliwahi kubeba mimba nyingine, lakini mtoto alifia tumboni."

Naye Daktari anayeshughulika na huduma za mama na mtoto, Dk Edna Majaliwa, alisema, ilibidi Buntwa afanyiwe upasuaji kwa sababu mtoto mmoja alikuwa amekaa vibaya.

Dk Majaliwa alisema, watoto hao wapo chini ya uangalizi wa madaktari kwa sababu walizaliwa na uzito mdogo.
"Kwa uzito waliozaliwa nao, miili yao isingeweza kupigana na maambukizi ya hapa na pale, ndiyo maana tumewaweka katika vyumba maalumu vya joto na hali zao kwa sasa zinendelea vizuri," alisema.

Alisema watoto wanaendelea vizuri kwa sababu sasa uzito umeongezeka na kwamba wana uzito kati ya kilo moja na gramu 400 na kilo moja na gramu 900.

Mkunga katika wodi hiyo, Sista Evelyn Lemba alisema, timu yake ya wakunga na wauguzi walijitahidi kuwapa huduma zote muhimu mama na watoto hao, ambao ni nadra sana kuzaliwa.
 
Hapo ndio wanaposema tumshukuru mungu kwa kila jambo.... alipoteza mmoja na sasa Mungu kampa wa 4 kwa mpigo. Tunawombea afya njema na waweze kupata uzito stahili mapema na kuweza kutoka hospital na kuishi nyumbani kwao
Katika hali kama hii watanzania inabidi tumsaidie kwa vile tutakavyojaaliwa na kuwezesha watoto hawa kupata mahitaji muhimu
natanguliza pongezi kwa wazazi
 
Ilitosha kusema "Ajifungua watoto wanne" badala ya kutanguliza 'mwalimu' mwanzoni. Hakuna ajabu mwalimu akijifungua, na hata akijifungua watoto wanne!
 
Hapo ndio wanaposema tumshukuru mungu kwa kila jambo.... alipoteza mmoja na sasa Mungu kampa wa 4 kwa mpigo. Tunawombea afya njema na waweze kupata uzito stahili mapema na kuweza kutoka hospital na kuishi nyumbani kwao
Katika hali kama hii watanzania inabidi tumsaidie kwa vile tutakavyojaaliwa na kuwezesha watoto hawa kupata mahitaji muhimu
natanguliza pongezi kwa wazazi

Wazo zuri sana mkuu. Kama watanzania wote tungekuwa na moyo wa kusaidia kama wako bila kuambiana nadhani tungekuwa mbali sana.
 
Hapana ni halali kutumia identification yake...hata hvyo anakabiliwa na changamoto nyingi sana na hasa kama baba yake ni mwalimu pia, kwa mishahara yao mhhhh!!!!
 
Hapana ni halali kutumia identification yake...hata hvyo anakabiliwa na changamoto nyingi sana na hasa kama baba yake ni mwalimu pia, kwa mishahara yao mhhhh!!!!

Nawaonea huruma sana mkuu. I wish kama ningewafahamu niwasaidie.
 
Back
Top Bottom