MAHAKAMA ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara imemhukumu mwalimu wa Shule ya Sekondari Basstu aitwae Renatus Massy [29] kifungo cha maisha jela kwa kupatikana na kosa la kulawiti mtoto wa miaka nane.
Mahakama hiyo ilimhukumu mwalimu huyo kwa kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na bila kuwa na shaka na ushahidi huo.
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na mwendesha mashitaka, Athumani Mkilindi huku ikisikilizwa na kutolewa hukumu na Hakimu Joseph Kimaro wa Mahakama hiyo.
Hakimu Kimaro kabla ya kutoa hukumu hiyo alimtaka mshitakiwa kujitetea ili asipewe adhabu kali na mshitakiwa alijitetea kuwa: Naomba nipunguziwe adhabu kwa kuwa hili ni kosa langu la kwanza na nina familia kubwa inayonitegemea hakimu naomba nipewe adhabu ndogo sitarudia tena alijitetea hivyo mwalimu huyo mbele ya hakimu Kimaro.
Hakimu Kimaro hakuridhika na utetezi wake na kumuamuru akatumikie adhabu ya kifungo hicho cha maisha ili iwe fundisho kwa wengine wenye tamaa za kijinga kama zake.
Awali ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 25, mwaka jana, majira ya saa 10 jioni, nyumbani kwa shangazi yake mshitakiwa alikokwenda huko Wilayani Hanang.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alipokwenda hapo alimkuta mtoto huyo [jina kapuni] akicheza na wenzake nje ya nyumba hiyo na kumchukua kuingia nae chumbani na kumbana pumzi na kuanza kumlawiti bila hata chembe ya huruma.
Baada ya kutimiza azma yake hiyo mshitakiwa alikimbia na kumuacha mtoto huyo akipiga kelele kali na watu kukimbilia na kumkuta amefanyiwa kitendo hicho cha kinyama.
Mtoto huyo alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu na mshitakiwa alikamatwa siku hiyo hiyo akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake.
Source: nifahamishe.com