Mwalimu achanganyikiwa kwa jibu la swali lake mwenyewe!

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Darasa linaendelea na kipindi, na mara ukafika muda wa maswali, mwalimu wa kiswahili, akitanguliza maelezo akisema "wanafunzi na sasa atasimama kila mmojawenu atakua anataja neno au jina la kitu ambalo liwe na maana ya kimbele na kinyume (yaani ukilisoma kikawaida lilete maana na ukilisoma ukilisoma kutoka mwisho kuja mwanzo pia lilete maana) mf. :
MACHO- CHOMA
PAKA- KAPA
Hivyo maswali yakaanza ikawa mwanafunzi akitaja mwl anageuza
Mwl : Haya Juma unaanza.
Juma : TATU
Mwl : TUTA very good kaa chini anaefata Asha
Asha : BATI
Mwl : TIBA vizuri kaa anaefata John
John : KABA
Mwl : BAKA good anaefata Mussa
Mussa : SHIMO
Mwl : MOSHI welldone kaa, Mary malizia la mwisho
Mary : ROMBO
Mwl : kimyaa
Mary : Mwl mbona kimyaa narudia ROMBO
Mwl : eti ulikua unasemaje? Mmmh unasema?
Mary : una maana mwl nimerudia mara mbili uko kimya ndiyo nijue nimekosa au?
Mwl : kipindi kimeisha
Mwalimu alitoka kasi kama mgonjwa anaewahi kung'oa jino!
 
mitoto ya siku hizi ndo ilivyo inafikiria kuliko uwezo wao wa kawaida badala yafikirie kugundua vitu vizuri yanafikilia utumbo.
 
Back
Top Bottom