Mwakyembe: Marufuku abiria Kuchimba dawa njiani

Akihitimisha hoja yake ya Mawasiliano na Uchukuzi amesema hakuna kujisaidia njiani hata kama unaharisha humo humo kwenye basi au chombo cha usafiri unachotumia
Basi wekeni sheria ya wenye mabasi au vyombo vya usafiri waweke vyoo kwa ajili ya abiria kujisaidia maana kuna umuhimu gani wa kupiga marafuku abiria kutochimba dawa njiani huku kuna wakati watu unakuta wengine wamekula matoke na vichuri sasa kwenye vyombo vya usafiri visiposimama ili kutoa fursa kwa yule anaehitaji kuchimba dawa afanye hivyo c wanataka watu/abiria kujisaidia kwenye vyombo hivyo

dah!kwenye kichuri hapo umenikumbusha mzee kurugumbagekorara na mamamsagane,
 
''ABIRIA NI MARUFUKU KUCHIMBA DAWA NJIANI'', Mwakyembe alipuka bungeni.
Waziri wa uchukuzi ametoa agizo bungeni jioni hii kwamba kuanzia tarehe 1 sept 2012,Ni Marufuku kwa mabasi kusimama njiani kwenye vichaka ili abiria wakachimbe dawa,akidai inavunja heshima na utu wa Mtanzania kwa Mama mtu mzima kuchuchumaa hapa akichimba dawa na kijana mdogo naye hapa akichimba dawa.

kwa hali hii hata da irene naye aliambiwa hivi hivi kuhusu ppf na nssf
 
ila kaniboa,
kamponda Wenje kwamba anafuatilia sana JamiiForums kwamba ina habari za uzushi, yeye ndio waziri pekee wa uchukuzi mwenye dhamana hakuna vikao rasmi nje ya wizara yake, asifuatilie sana jamii forums, namnukuu "TATIZO MNAFUATILIA SANA JAMIIFORUMS"
 
Big up Dr kwa uamuzi wako. Ni aibu sana na ni ufinyu wa mawazo baada ya miaka 50 ya Uhuru tunawaza mawazo ya kizamani. Kuna shida gani kila Halmashauri kujenga "rest areas" katika maeneo yao? Hebu tubadilike kifkra. Yeyote anayempinga Dr anadhihirisha uzamani. Kumbukeni sisi siyo mbwa ni wanadamu....... Big up again Dr. Kanyagia hapo hapo mpaka kieleweke.....
 
swala la ajali ya MV skaggit liko mahakamani halitakiwi kujadiliwa litaaribu uchunguzi..
 
wangejenga vyoo huko vichakani au kwanza angewataka wamiliki wa mabasi waweke vyoo kwenye mabasi yao,halafu ndipo apige marufuku kuchimba dawa
 
ila kaniboa,
kamponda Wenje kwamba anafuatilia sana JamiiForums kwamba ina habari za uzushi, yeye ndio waziri pekee wa uchukuzi mwenye dhamana hakuna vikao rasmi nje ya wizara yake, asifuatilie sana jamii forums, namnukuu "TATIZO MNAFUATILIA SANA JAMIIFORUMS"

Nami nimemsikia kwenye hilo!!!!
 
inaelekea ile sumu aliyowekewa imemuathiri kiaina...huwezi kupinga kuchimba dawa wakati hujajenga miundombinu ya kutosha ya kutoa hiyo huduma barabarani...
 
Serikali itengeneze sehemu maalum kwa ajili ya wasafiri kujisadia.
Siyo kikataza kuchimba dawa wakati hakuna vyoo kwenye barabara kuu.

Nakubaliana nawe mkuu. Kabla ya serikali kukataza hili wajenge vyoo njiani katika barabara zote kuu za kwenda mikoani ambako abiria wanaweza kufika na kujisaidi. Kuna wakati inatokea mnakula chakula njiani na mtu anakamatwa na tumbo la kuendesha, hawezi kujizuia vinginevyo atachafua hali ya hewa kwenye Bus na kudhalilika mbele za abiria wenzake.
 
  • Thanks
Reactions: tz1
Safi sana. Ilikuwa kero sana. Wawashauri Halmashauri waimarishe public toilets kwenye miji ambayo mabasi yanapita. Sasa gari likiharibika polini, sijui itakuwaje!
 
Mh. Mwakyembe, hakuna abiria anayefurahia kuchimba dawa kama unavyosema, ni wajibu wa mamlaka husika kujenga maeneo ya kujisaidia wasafiri wa mabasi. Nawapongeza TANROADS kwa kujenga choo ktk mizani mpya ya Chalinze.
 
wamechimba dawa mababu zetu sembuse yeye anasema leo ndio iwe mwisho!, haoni anataka kuondoa "mila na desturi" zetu tulizoziasisi?
itakua ngumu mno, kuchimba dawa kuna raha yake!.
 
''ABIRIA NI MARUFUKU KUCHIMBA DAWA NJIANI'', Mwakyembe alipuka bungeni.
Waziri wa uchukuzi ametoa agizo bungeni jioni hii kwamba kuanzia tarehe 1 sept 2012,Ni Marufuku kwa mabasi kusimama njiani kwenye vichaka ili abiria wakachimbe dawa,akidai inavunja heshima na utu wa Mtanzania kwa Mama mtu mzima kuchuchumaa hapa akichimba dawa na kijana mdogo naye hapa akichimba dawa.

Kwani huyo mama mtu mzima anakula starehe? Bila shaka huwa inamlazimu ajisaidie, hata kumwomba konda asimamishe gari akibanwa na kushukuru baada ya huduma. Sasa kuna ulazima gani wa kupiga marufuku?
Mawaziri wa Tz wachovu wa kufikiri, ni yale yale ya Physics with Chemistry ya Mungai! Kweli tuna mawaziri vilaza.
 
sipati picha pori la ushirombo mpaka nyakanazi bila kujisaidia balaa!hapo ujue kuna biashara ma bus ya mchina
 
Nami nimemsikia kwenye hilo!!!!
mpwa,
mimi binafsi nisipopita hapa JF huwa najiskia mgonjwa!,
hapa JF kuna kila aina ya watu, na ni SHULE isiyo na mipaka.
hapa jamvini kuna taarifa ambayo ukiisoma leo utashangaa baada ya siku mbili iko mitaani kama ilivyo!, kuanzia taarifa za ikulu, wizarani, tiss na sehemu zote hizo.
namshangaa sana Dr. Mwakyembe kuiponda jamiiforums aka the home of great thinkers, where we dare to talk openly!.
kiukweli serikali yote kuanzia mkuu wa kaya HUWA WANAPITIA HUMU JAMVINI, na wengine maamuzi wanayatolea kwa kurefer JF
 
Back
Top Bottom