Jamani huyu akifukuzwa CCM atabaki mbunge gani tena, au ndiyo YES men and women watabaki???????? Tafakari
SIKU moja baada ya Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta kupata tumaini jipya kwa kuungwa mkono huku akihakikishiwa msaada kurudi kwenye nafasi hiyo na mwanasiasa mkongwe nchini, Bw. John Malecela, hali si shwari kwa Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Vyanzo vyetu vya kuaminika ndani ya CCM vinaeleza kuwa Dkt. Mwakyembe amewekwa pabaya na wabaya wake kisiasa ambao sasa wamehamishia nguvu zao katika vikao vya chama wilayani Kyela kwa lengo la kummaliza kisiasa.
"Wabaya wa Mwakyembe wamehamisha nguvu zao zote jimboni na wilayani kwake Kyela. Ndani ya CCM Kyela kuna mkakati mzito wa kumng'oa Dkt. Mwakyembe si ubunge tu bali hadi uanachama. Vikao vinafanyika, wameapa kwamba kuwepo Mwakyembe ndani ya bunge lijalo ni kikwazo cha urais kwa baadhi ya wanasiasa wanaosaka nafasi hiyo kwa udi na uvumba," kilisema chanzo chetu.
Imeelezwa kwamba kundi linalomshughulikia Dkt. Mwakyembe limesoma alama za nyakati na kubaini kuwa njia pekee ya kummaliza kisiasa ni kitumia vikao vya chini vya chama hususan ngazi ya wilaya.
Hofu kuu ya kundi hilo ni kwamba iwapo Dkt. Mwakyembe atashinda kipindi kijacho ana uwezo mkubwa wa ushawishi na kutumia vifungu kadhaa vya sheria kukwamisha mipango ya urais kwa baadhi ya wanachama wanaosaka nafasi hiyo mwaka 2015.
"Kuna mikakati michafu inafanyika Kyela hata kutumia vyombo vya habari kutoa ujumbe wa 'kummaliza' kabisa kisiasa Dkt. Mwakyembe, lakini uongozi wa juu umekaa kimya,"kilisema chanzo hicho.
Mbinu zingine zinazodaiwa kuandaliwa dhidi ya Dkt. Mwakyembe ni kupewa alama ndogo, kudaiwa kuwa ana kundi linalokigawa chama wilayani na kama atalalamika, vikao hivyo vitatoa mapendekezo ya kumvua uanachama kwa madai ya kukivuruga chama
"Tayari kazi imekamilika kila kata kinachoendelea sasa ni kampeni za matawi, akipona kwenye kura za maoni lazima akwame katika vikao maalum vya ngazi za wilaya na mkoa,lengo ni kumfukuza kabisa ndani ya chama,"kilisema chanzo hicho na kuongeza;
"Taarifa hizi zote zinajulikana ngazi za juu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, sijui kama mbinu hizi zina baraka au mamlaka ya juu inaogopa nini wakati mambo yanaharibika?"alisema Mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Majira lilipomtafuta Dkt. Mwakyembe ili kujua kama ana taarifa juu ya mpango huo na msimamo wake, alikiri kuwa na taarifa hizo huku akikataa kutoa ufafanuzi kwa kile alichodai kwamba wananchi ndio watatoa jibu.
"Ninajua kila kinachoendelea, ninajua akina nani wanahusika, mimi siyo mjinga hata sasa niko huku Kyela, mngetaka kujua kwa undani hayo unayoniuliza ungekuja Kyela,"alisema Dkt. Mwakyembe bila kutoa ufafanuzi wa kina.
Alipoulizwa hatua alizokwishachukua juu ya suala hilo alisema "Nakumbuka niliwahi kusema kwamba taarifa zote nilishatoa sasa ukitaka fuatilia huko mbele, lakini naomba usisahau kitu kimoja, uamuzi wangu wa mwisho utatolewa na wananchi siku ikifika, mafisadi watumie mamilioni au mabilioni, wafanye nini uamuzi wa mwisho utatolewa na wananchi,"alisisitiza.
Majira ilipomtafuta Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Mkoa wa Mbeya Bw. Basiru Madodi, ili kujua ukweli wa suala hilo, alikiri kusikia taarifa hizo mitaani lakini si rasmi.
"Na mimi nimesikia tu hizo taarifa kama ulivyosikia wewe, hivi sasa tunaendelea kufanya uchunguzi ili kujua ukweli maana Jimbo la Mbeya inaonekana kuna makundi tunataka tujiridhishe kwanza kabla ya kusema chochote,"alisema Bw. Madodi.
Alipoulizwa makundi hayo alisema yanatokana na makovu ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Udhibiti ya Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ya CCM, Bw. Pius Msekwa, alikiri kupokea malalamiko mengi kuhusu njama hizo za kuangushwa wabunge.
Alisema malalamiko hayo yanashughulikiwa na kwamba kabla ya Uchaguzi Mkuu kila kitu kitakuwa hadharani huku akikataa kuzungumzia suala la Dkt. Mwakyembe pekee kwa maelezo kwamba ana malalamiko mengi mezani kwake.
"Hatujapuzia malalamiko ya Waheshimiwa wabunge, ni kweli nimepokea malalamiko mengi sana siwezi kusema ni ya fulani na fulani yapo mengi sana na tunaendelea kuyashughulikia, tayari tumetoa taarifa inayoonesha ratiba ya kushughulikia na tutatoa taarifa baada ya kumaliza kazi,"alisema Bw. Msekwa.
source: Mwakyembe kufukuzwa CCM