Mwakyembe kuanika ripoti ya vigogo TPA

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe kesho anatarajia kuweka hadharani ripoti ya uchunguzi wa vigogo wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).Hatua hiyo inakuja kufuatia kukamilika kwa ripoti ya Tume ya watu saba aliyoiunda kuchunguza tuhuma dhidi ya vigogo hao na kumkabidhi yeye mwenyewe.Ripoti hiyo ndiyo itakayowaokoa ama kuwatia hatiani Mkurugenzi Mtendaji wa (TPA)aliyesimaishwa Ephraem Mgawe na wasaidizi wake.
Mkurugenzi huyo pamoja na watendaji wengine sita waliosimamishwa kazi Agosti 23 mwaka huu kwa tuhuma za kuhujumu uchumi na kukaidi agizo la Ikulu,tuhuma hizo ndizo zilizokuwa zikifanyiwa kazi na kamati ya watu saba iliyoundwa na Waziri huyo.

Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Lisso Ibrahim aliliambia gazeti hili jana kuwa kamati ilishamaliza kazi na kuiwasilisha ripoti hiyo kwa waziti ambaye baada ya kuipitia kesho ataitoa hadharani.
“Kwa sasa Waziri wetu Dk Mwakyembe hayupo nchini amekwenda kwenye ziara ya kikazi Zimbabwe,anatarajia kurejea nchi kesho (leo) na ratiba iliyopo inaonyesha kuwa kesho atakutana na waandishi wa habari na kusoma ripoti nzima ya uchunguzi inayohusu vigogo wa (TPA)”alisema Ibrahim.
Katika hatua nyingine yameibuka madai kuwa kuna kundi la watu wanaojihusisha na hujuma katika utendaji wao wakazi kwa lengo la kushinikiza kurejeshwa kazini kwa watendaji waliosimamishwa.
Watendaji hao wamelalamikiwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango kama sehemu ya kuhakikisha malengo yao yanatimia.
Akizunguzia hilo Rais wa Chama cha Forodha Tanzania (TAFFA) Stephen Ngatunga, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa anaamini ni changamoto zitakazopita.
Alisema kimsongi wapo watu wanaopenda kuendelea na viongozi walioondolewa kwa kuwa walikuwa wakifanya nao kazi, lakini ikiwa uongozi utaamua kufanyia kazi hilo itakuwa rahisi kuwabaini na kuwaondoa kwenye nafasi zao.


Chanzo: Mwananchi
 
Kama wakati wa ripoti ya uchunguzi wa Richmond, Mhe aliweza kuficha baadhi ya mambo ili kunusuru nchi, ni vipi katika ripoti hii ataweza kutoa ukweli wote?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom