MWAKYEMBE HAKULISHWA SUMU,report ya police.

Tusubiri Mwakyembe mwenyewe aje na data za ukweli.. inaumiza sana nikikumbuka wakati ule alipokuwa anatoa taarifa za kutishiwa kifo. Zilikuwa so detail kuonyesha kwamba alishajua anawindwa..Na hata kufikia kumpelekea IGP ushahidi lakini hamna taarifa iliyotolewa mpaka walipofanikiwa kumpata Mzee wa watu, ndio tunaanza kupata taarifa za polisi wetu. Kwa nini hawakutoa taarifa za uchunguzi wakati ule Mwakyembe aliporipoti kutishiwa kifo.. Kufanya siasa africa kunahitaji uwe na moyo wa chuma..!

hawezi kutamka hadharani na hata akisema polisi litaishia hukohuko kwa kuwa analinda KUFA KWA CCM!! na yeye mwenyewe mkono uendelee kwenda kinywani!
 
Natabiri baada ya IGP Mwema the next IGP ni Manumba. Kumbukeni mabomu aliyopigwa Mrema kule Kilimanjaro
wakati Mahita ni RPC aliishia kuwa IGP. Manumba upo.
 
Kumbe police wetu ni madaktari? Kwa nini Mh Penda hakuwamwaga Muhimbili wakati ule wa mgomo?
Anyway, Dr Mwakyembe hajalishwa sumu, sasa anasumbuliwa na nini? India anapata matibabu ya maradhi gani?
 
Du inasikitisha ila kama amelishwa then aliyemlisha laaana itamtafuna hata kama anataka kugombe urais au uwaziri
 
Chanzo Radio One? je,Nani katoa taarifa ?IGP/NAHODHA ama Mwakyembe mwenyewe?

Wanasubiri Nchi itulie kwanza ,watatoa taarifa rasmi na sahihi.Kwa sasa ni vigumu kuweka wazi ISSUE inayogusa SERIKALI kwa namna moja au nyingine! Kunavuguvugu kali la kisiasa ndani ya serikali na CHAMA cha MAPINDUZI.....tatizo kubwa hapa wahusika wanayumbisha ukweli kwa gharama yoyote ile ili wasigundulike.Lakini mwenye macho haambiwi tanzama....Jamaa anaumbuka taratibu na atakufa kifo kibaya kama cha mbwa mwizi pamoja na utajiri wake wa kuhujumu uchumi wetu.Mmoja ameshakimbia,bado wawili ambao ni wazawa...........I wish ningekuwa Presider niwafilisi mali zao!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ninachoshangaa kwa nn sumu hii isimpate El au AC? Eti watanzania wenzangu hii ni jitihada za kuwafanya watu midomo yao isiongee mambo yasiyowafurahisha wakubwa
 
Kuna mtu alitegemea ripoti ya ukweli itoke polisi? Ripoti hii wameitoa maksudi kumbipu sitta ili afyatuke.?
Kweli tz wamejaa majuha.
 
Japo hili swala linampa maumivu makali sn mh . Mwakyembe na kuoneshwa uwezekano wa kifo mi binafsi naomba nichukue nafasi hii kumpongeza lowasa kwa kufanikisha mpango wake huu wa hatari huku yeye akipamba harakati kuusaka urais kutoka makanisani hadi misikitini. Km lowasa anamtegemea mungu au shetani tusubiri nani mshindi.
 
Mwakyembe kaingiziwa sumu mwilini (kwa njia yoyote)!Hili halina ubishi,na waliofanya haya ni walinzani wake kisiasa!Lkn tangu alipomaliza kuwasilisha ile report ya kamati iliyoundwa kuchunguza zabuni ya kufua umeme wa dharula nilijua yatafika huku na naamini yataendelea mpaka alambe udongo.Tza bado c nchi ya hivyo!eti useme ukweli?Ona yaliyowakuta Amina Chifupa & Jerry Muro.Na kwa Jerry hilo lilikuwa ni onyo,acje akarufia tena,ataenda kutolea ushuhuda kaburini.
 
Wacha alishwe hata angekufa hana msaada wowote na hata taarifa ya Richmond hakuitoa yote yeye ndiye angelikuwa mstari wa mbele kutuonyesha ukweli uko wapi na uongo uko wapi ili hili jambo liwe jepesi limenyamaza tuu kimya kujidai kuimbilia makanisani kumbe wanafiki wakubwa.
 
Invisible!!

Kwa heshima ya wadau naomba uunganishe hii thread na ile nyingine!

Thankx!
 
Nimekumbuka report ya wafanyabiashara wa mahenge waliouwawa wakisingiziwa ni majambazi,desi kanumba aka kayumba umechemka kweli,sasa wewe unatoa taarifa ya kulishwa sumu kwani wewe ni daktari?
 
Jamani wadau ukweli wa jambo hili tuzidi kumuomba mungu aseme na Dr Mwakyembe siku moja aweke mambo hadharani naamini siku moja na si muda mrefu ukweli utajulikana,tuzidi kumuombea aweze kupona kwa mungu yote yanawezekana mungu yuleyule aliyemfufua Lazaro na kuwaokoa Wanaisrael toka Nchi ya Misri ndiye atakayemponya Dr Mwakyembe!
 
source radio one breaking news
Leo walipaswa watoe nyingine kuwa rais Magufuli kathibitisha Mwakyembe alitiliwa sumu.
Mkuu Mchambuzi, nimependa unavyochambua, ki ukweli unazama deep!.
Nimeupitia uchambuzi wako kuna kitu sijakiona ukikizungumza kuhusu sumu.
Kuna sumu za aina tatu,
1. Intentions or delibarate poisoning, hii ndio ile dhana ya mtu kulishwa sumu, kutiliwa, kushikishwa au hata kutumiwa kwa barua kama 'anthrax', hii ni mtu kupewa sumu be it first poisoning or slow poisoning ila mwisho wa siku mhusika hudhurika!.
2. Food poisoning, hii ni aina ya pili ya sumu ambayo hutokana na kula chakula chenye sumu, mfano kuna baadhi ya mihogo ina sumu, uyoga, na baadhi vya vyakula vya proteion in nature kama nyama, samaki, maziwa, mayai etc ambapo aliyekula vinamdhuru ama instantly kwa kupata rushes, kuwashwa au kupata mafindofindo wanaita 'alergy' au slow reaction ambapo inaibuka baada ya kipindi kirefu na ineweza kuibuka kama kansa etc!.
3. Medical Reaction, japo sumu zote ni chemical reaction, hii sumu ya medical reaction ni sumu inayotokana na reaction ya madawa fulani fulani kwenye mwili wa binadamu mostly kutokana na prolonged use!. Hii humpata mtu ambaye kuna kitu ameugua na ni ugonjwa wa muda mrefu, mtu huyo anakuwa anatumia combination ya madawa fulani kwa muda mrefu imefikia muda madawa hayo yamereact from each other na kugeuka sumu na wakati huo huo mwili unakuwa umetengeza 'antigen' za kukabiliana na hiyo reaction na matokeo huwa ndiyo kama hiyo hali ya Mwakiyembe!.

Wanabodi nilishauri huko nyuma na hapa nashauri tena, tupunguze conspiracy theories tusubiri tamko la Mwakiyembe mwenyewe!.

Japo naye ili kumlindia Sitta heshima, anaweza kusema "Nimesha Muachia Mungu, hivyo naomba nisizungumze chochote"! hivyo kutosema anaumwa nini!.
Akiwa Kyela rais Magufuli amethibitisha Dr. Mwakyembe alitiliwa sumu. Tangu kuibuka kwa kadhia ya sumu ya Mwakyembe, hii ndio kauli from the highest authorities kuwa Mwakyembe alitiliwa sumu. Kutiliwa sumu ni criminal offence ya attempted murder, kama rais anathibitisha Waziri wake alitiliwa sumu na wahusika anawajua na hakuna sio aliyekamatwa, bali aliyehojiwa!, what are the chances kwa wasiojulikana wa Shambulio la Lissu ambao hawajulikani kabisa?.

Hivi katika hili sakata la sumu ya Mwakyembe, iliwahi kuthibitishwa na authorities zozote kuwa ni kweli Mwakyembe alitiliwa sumu, au uthibitisho ndio huu wa leo wa rais Magufuli?.

P.
 
Back
Top Bottom