Mwakyembe awaliza watu wa Kyela

Utashangaa sana!
Ukitaka kushangaa zaidi na kuacha mdomo wazi hadi inzi wajae mdomoni, nenda Arumeru, utakuta Mawaziri kibao wako huko kwa mwezi mzima na walishaweka makufuli maofisini kwao!

Wasira amepiga kambi tangu wakati wa kura za maoni za awamu ya kwanza na mpaka sasa bado yuko Arumeru .... huyu Mzee huwa hata sijui kazi zake ni nini.
 
Mwisho wa ubaya aibu. Atembee zake. Hana jipya. JK kamuambia akiendelea kuchonga kwamba kapigwa sumu inamaanisha either ni serikali au maana yake imeshindwa kujua mpiga sumu hivyo hiyo ni kashfa in simple ni kwamba hastahili kuwa waziri. jamaa uwaziri anautaka, fasta katangaza amepona na anaanza kuvua kofia ili aonewe huruma. pole yako, wenzako uliowakuta wameshasema wanaachana siasa uchwara.
 
Hana lolote huyo kimbora mwacheni afe tu??

Halafu mim nashindwa mwelewa kabisa wapiga kura wake wanataka kujua yaliyo msibu yeye anajifanya anaficha.

Hapo hapo anawakana kwa kudai hajalishwa sumu na mambo ya afya yake ni ishu private mara anawavulia kofia raia anamaanisha nin huyu??

Kweli kafirisika ki fikra na elimu yote aliyonayo?? Huo ndio mwishowe wa kufikiria sijui??
 
Hili sizani kama ni suala la kumlaumu mh. Mwakyembe, bali ni kumuombea kwa sababu kilichotokea na kinachoendelea kutokea kwa mh. Mwakyembe ni moja ya madhara mengi ambayo tunayaishi ikiwa ni matokeo mabaya kabisa yanayosababishwa na MAFISADI pamoja na UFISADI wenyewe. Angalia chenji ya rada hakuna mtanzania aliyehusika(rejea taarifa ya habari ya ITV 30/03/2012 usiku) kupanda holela kwa gharama za umeme, na umeme wenyewe sio wa uhakika. Vifo vya watu vinavyotokana na kutumia maji yenye sumu katika migodi mkoani Mara na migomo ya madaktari kwa kutaja machache. Kinachotakiwa kila mpenda nchi kwa nafasi yoyote aliyonayo mahali popote ahakikishe anakuwa kamanda wa kupambana na UFISADI kwa maana halisi na sio kwa kutajwa na vyombo vya habari, vinginevyo kuna siku tutajikuta tunakuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.
 
sasa kwa hali yake ilivo anaweza tena kuendelea vizuri na kazi za uwaziri?? kwa nini asiwe mzalendo akaachia hiyo nafasi ili apate muda waa kupumzika na kucheki zaidi afya yake!!yaani wapiga kura wake wanamwona huruma na kutaka kujua kilichompata mbunge wao yeye anasema waache majungu??acha afe na kamba shingoni!!

umesema vema mkuu, kumuonea huruma mwakyembe ni kujikondesha, shikeni majembe mkalime, akifa nendeni mkamzike kimya kimya full stop, kwani chochote mtakachoongea amewaambia hayo ni majungu, mumkome!!!!!!
 
Hili sizani kama ni suala la kumlaumu mh. Mwakyembe, bali ni kumuombea kwa sababu kilichotokea na kinachoendelea kutokea kwa mh. Mwakyembe ni moja ya madhara mengi ambayo tunayaishi ikiwa ni matokeo mabaya kabisa yanayosababishwa na MAFISADI pamoja na UFISADI wenyewe. Angalia chenji ya rada hakuna mtanzania aliyehusika(rejea taarifa ya habari ya ITV 30/03/2012 usiku) kupanda holela kwa gharama za umeme, na umeme wenyewe sio wa uhakika. Vifo vya watu vinavyotokana na kutumia maji yenye sumu katika migodi mkoani Mara na migomo ya madaktari kwa kutaja machache. Kinachotakiwa kila mpenda nchi kwa nafasi yoyote aliyonayo mahali popote ahakikishe anakuwa kamanda wa kupambana na UFISADI kwa maana halisi na sio kwa kutajwa na vyombo vya habari, vinginevyo kuna siku tutajikuta tunakuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

sumu umeitaka mwenyewe sa kwaninini unataka uombewe. Tuache wanakyela tupalilie mipunga yetu, sias zako hazieleweki
 
Kwanza mjadala wa ugonjwa wake alishaufunga yeye mwenyewe, pili Mwakyembe hajalishwa Sumu maana alishasema mpaka jina la ugonjwa wake unaitwaje. Tuache porojo na ujinga wa Mwakyembe.
 
Nchi yetu inaelekea kubaya! yaani waziri ni mgojwa lakini haondolewi ilihali hawezi na hataweza kufanya kazi ipasavyo kwa sababu tu kuogopana na kulindana huku nchi ikiwa taabani. kweli tutafika? wamaziri mwaka sasa hawapo ofisini wanaumwa kweli hakuna mtz wakuziba nafasi?
 
Mwakyembe aliamini vita ya ufisadi inepaisha na hivyo akajifanya maarufu kuliko hata jimbo la kyela.sasa anasema akiona upepo si mzuri hatagombea.Dhambi ya unafki itamfune mwakyembe..kauli yake aliyosema kwamba "wangeyasema yote basi serikali yote ingeanguka" itamtafuna kwelikweli na mimi nasema bora imtafune kwelikweli.Mwakyembe lazima atuambie watanzania yale aliyoyaacha katika ripoti yake ya richmond ili tuwajue wachawi wote wanaofanya nchi ikae gizani mpaka leo.katika biblia tunasoma habari za Annania aliyeficha sehemu ya mali yake kwa Mungu madhara yake akafa hapohapo.Mwakyembe atoe maelezo kwa nini Mungu asimwadhibu kwa kuficha mambo kama Annania.
 
Mwakyembe aliamini vita ya ufisadi ingempaisha na hivyo akajifanya maarufu kuliko hata jimbo la kyela.sasa anasema akiona upepo si mzuri hatagombea.Dhambi ya unafki itamfune mwakyembe..kauli yake aliyosema kwamba "wangeyasema yote basi serikali yote ingeanguka" itamtafuna kwelikweli na mimi nasema bora imtafune kwelikweli.Mwakyembe lazima atuambie watanzania yale aliyoyaacha katika ripoti yake ya richmond ili tuwajue wachawi wote wanaofanya nchi ikae gizani mpaka leo.katika biblia tunasoma habari za Annania aliyeficha sehemu ya mali yake kwa Mungu madhara yake akafa hapohapo.Mwakyembe atoe maelezo kwa nini Mungu asimwadhibu kwa kuficha mambo kama Annania.
 
maoni mazuri kabisa....new Tanzania is on the way!

lets speak facts as they are! mwakyembe hajawasaidia watanzania kwa lolote lile, I remember tuzo ya 94b ambayo yeye na sita ni chief architect
 
Sio vizuri, hayo ndio majungu ambayo amesema watu waache, chukulia kama ungekuwa unaumwa wewe kisa umewekewa sumu.
 
Nilikuwa namkubali sana Mwakyembe,kwa hili nadhani kapigwa bit na ma jasusi wa CCM kwamba akiendelea kuchonga ngenga wanamtoa uhai rasmi,kaogopa ndo maana alipo kuwa Dar akasema mjadala kuhusu afya yangu ufungwe na sikunyweshwa sumu.Alipo kuwa India alisema amewekewa sumu,sasa kaenda kyela anavua kofia na gloves,Huyu jamaa kama anataka apone,aseme ukweli na kama mbwai na iwe mbwai tu.Hakuzaliwa na uwaziri,ona walivyo mchakaza bado anatetea CCM tu...
 
Mwakyembe bana, sasa amevua miwani kofia na gloves ili watu wajadili kitu gani?Si alisema asijadiliwe kuhusu afya yake?

Unafiki una costs zake na hilo bado halioni, ama kweli no wonder the say "you cant teach an old dog a new trick"

Kurudi kwake ofisini ni dalili kwamba adui yake yuko nje ya serikali anayoifanyia kazi?
 
Sio vizuri, hayo ndio majungu ambayo amesema watu waache, chukulia kama ungekuwa unaumwa wewe kisa umewekewa sumu.

Praff ngoja nikusaidie

1. huyu bana alijipambanua kuwa yeye ni mpinga ufisadi...lakini in the same government ya kifisadi akapewa uwaziri na akakubali

2. huyu bana hakumuhoji Lowassa kuhusu richmond na akamhukumu kwa ushahidi wa vi-note na mazingira

3. akasema waziwazi kuwa hakusema yote kuhusu richmond ila kuna mengine aliyabakiza ambayo yangemshtua kila mtu!!

4. waligombania eneo moja na rostam aziz kwa ajili ya kufulia umeme, na by this time kila mtu akajua kumbe naye ni mjasiriamali aliyeko serikalini na ana mradi wa kufua umeme wa upepo, hili halikujulikana kabla ya tume ile ya bunge

5. kabla ya hapo kumbuka aliongoza mapambano ya kuvunja mkataba ambaoleo hii tunadaiw bilion 94!!!

6. akasema ataeleza kila kitu kuhusu wabaya wake waliompa sumu

7. amerudi anasema tusimjadili juu ya afya yake, yet anawafunulia watu upara wake

swali ni nani anayetaka kumuua

1. Kikwete ambaye hakutajwa kwenye richmond scandal na yeye ndiye chief architect wa richmond

2. au EL analipiza kisasi

3. au mtu yeyote yule anayetumia mwanya huu kumdhuru , walikuwa na uadui wa siku nyingi

?????????????????
 
Back
Top Bottom