Mwakyembe augua ghafla Bungeni

Mwakyembe, .

Mbona ghafla unakuja na maajabu? Kuna ushahidi gani kuwa wao ni wahusika? watu kuugua ni nature usitafute sababu zisizo msingi....kama jazba na mafisadi wote tunalo lakini hii extremism ya kiarabu waachie hawo waarabu.
 
Last edited by a moderator:
Mwakyembe, akifa tu hawa inabidi ....

Kokolo hiyo mipango yako ya kuzimu uifanye wewe mwenyewe na hao "wenzako" JF haiwezi kutumika kama sehemu ya kupanda, kulea, au kuchochea matumizi ya nguvu kwa ajili ya malengo ya kisiasa.

Napinga mawazo yako, napinga mipango yako kwa kauli kali kabisa inayowezekana, na ninaomba ufute maneno yako na kuyatenganisha na JF. Kama una mipango yoyote ya kihalifu (kama ulivyodokezea) iwe mawazoni au standby mipango hiyo usiihusishe na JF kwa namna yoyote ile.
 
Last edited by a moderator:
Mwakyembe, akifa tu hawa inabidi .....

Loose cannons kama hawa tusiwasahau rekodi zao jamani.

Katika ulimwengu huu wa mapinduzi ya habari na utandawazi, labda ni vigumu sana kuzuia mawazo kama haya kusikika. Haiwezekani kufuatilia na kufungia kila hoja-kioja inayoandikwa mtandaoni. Tena, inawezekana ni bora kujua kwamba, ok, kumbe kuna watu wenye mawazo ya aina fulani katika jamii au jamvi fulani.

Lakini nadhani mtu akishasema vitu kama hivyo hapo, pamoja na wale wenye tabia ya ku rant matusi na kejeli, inabidi tuweke rekodi vichwani na hata kesho na kesho kutwa wakija kama wastaraabu tuwe makini kujingiza kwenye mjadala wowote nao. Watu kama hawa wanaitwa "loose cannon," ama mzinga uliolegea. Kwamba hata kama akitulia kwa muda, kuna siku atabwatuka kitu cha kukuacha na bumbuazi kama mzinga ambao una nati zilizolegea ulivyo hatari ya kuachia mabomu bila kutegemewa na askari wa kikosi cha mizinga.

Senti mbili zangu hapa ni kwamba aina ya utu wa mtu ikishajulikana, isiwe inasahaulika, na rekodi na sifa mbaya zimfuate mtu mpaka akiri kakosea, kama ambavyo wote tunakosea. Tatizo, nadhani, watu wana recover credibilty haraka mno hapa!
 
Last edited by a moderator:
Kuhani.. mitandao inaweza kutumika kurecruit, kupanga, na kutekeleza vitendo vya kihalifu. Katika uhuru wa maoni na mawazo ni vizuri kujua mawazo mabaya nayo yapa, lakini ni jambo jingine kuyakubali, kuyahifadhi na kuyavumilia. Na ni hatari zaidi kutoa nafasi kwa watu kusambaza mawazo ya kihalifu kwa kisingizio cha uhuru wa maoni. Kwenye ukumbi uliojaa watu kama ukumbi wa sinema mtu akipiga kelele "moto, moto" kiutani akidai ni uhuru wa maoni mtu huyo atashitakiwa kiuhalifu kama kutatokea madhara kwa watu kwa sababu ya kukimbia kuokoa maisha yao.

Mawazo ya kokolo ni zaidi ya uhuru wa maoni, ni mawazo yenye kupakana na kupanga uhalifu. Hivi kweli Mwakyembe akifa (mungu aepushie mbali) halafu mmoja wa aliowataja hapo tukasikia ameraruriwa na risasi, JF tutaweza kusimama na kusema hatukuonywa? No sir, mawazo ya namna hiyo hayana nafasi hapa.
 
Mwnjkk,

Wala simaanishi jamaa apeteshwe na uhuru wa mawazo. Tena mimi condemnation yangu nadhani inaenda mbali zaidi.

Nasema, mawazo yake hayo siyo ya kuyakemea tu mara moja na kuyasahau. Kwamba, hicho kirekodi chake kichafu kimfuate siku zote. Kesho na kesho kutwa akitulia, akajikausha kana kwamba hakuharibu, basi tuwe makini kujumuika nae kwenye mijadala mwingine kana kwamba ni mzima huyu. Ki ujumla nadhani tupo wote.
 
Mwakyembe, akifa tu hawa inabidi ....

WARNING!!!
Kokoko mchango wako ni wa kichochezi sidhani kama ndiyo lengo la hapa JF. Tunalaani mbinu zako na tutamuomba rasmi MOD aifute thread yako. Sipendi hata kuota mawazo yako.
 
Last edited by a moderator:
Ama kweli wewe ni KOKOLO, mwingine ni picha tu. Siamini kama JF nayo ni kokolo. Hiyo lugha Mkuu uliyotumia siamini kama inakubalika katika jamii yetu. Ingawa tuna demokrasia lakini sidhani kama hiyo lugha ina nafasi katika jamii yetu na vilevile kwenye Mtandao wetu huu JF. Sidhani kama utapungukiwa kitu kama ukiamua ku-apologize.
 
wandugu lazima muelewe ukitaka kumuua mbwa, mpeni jina baya... Kwa wale wanaokumbuka yaliyotokea mwezi Februari wanajua ni jinsi gani kina Mwema walijaribu kutuhusisha na mambo ya kighaidi.. now it seems somebody want to give them a reason to point at..
 
wandugu lazima muelewe ukitaka kumuua mbwa, mpeni jina baya... Kwa wale wanaokumbuka yaliyotokea mwezi Februari wanajua ni jinsi gani kina Mwema walijaribu kutuhusisha na mambo ya kighaidi.. now it seems somebody want to give them a reason to point at..

Kumbe unapinga kwa kuwaogopa wakina mwema? Mimi nilidhani ni itikadi
 
yeah.. ndio maana nimeshangaa mtu anayetaka sifa baada ya kufa... yeye atazipataje.. ndio maana madikteta wote hupenda sifa zao hapa hapa..
 
Mwakyembe, akifa tu hawa inabidi ....


Huyu naye ni wa wapi?mbona anakuja na strategies chafu ambazo zinakemewa hapa JF kwa nguvu zote.Hii tunaikemea kwa nguvu sana
 
Last edited by a moderator:
Mungu kupe nguvu Dr. Mwakyembe upone haraka na akuzidishie ujasiri. Naamini ni ugonjwa wake ni jambo la kawaida na sipendi kulishusisha na kazi zake za kibunge mana njia ya mwongo ni fupi tu na mfa maji atapatapa ila atayanywa tu.

aluta continua mapambano yanaendelea, hata shetani ni mzuri kwao
 
WARNING!!!
Kokoko mchango wako ni wa kichochezi sidhani kama ndiyo lengo la hapa JF. Tunalaani mbinu zako na tutamuomba rasmi MOD aifute thread yako. Sipendi hata kuota mawazo yako.
Bubu Msemaovyo,

Ahsante kwa ukemeaji wa namna hii pamoja na amanigk + Mzee Mwanakijiji... Ningefuta mchango wake lakini ni bora ubakie hapa ili wengine watambue wazi kuwa si dhamira ya JF kuwa sehemu ya kuchochea vurugu.

Aidha, ni njia pekee ya kuwafahamisha wengine wenye nia hizi kutozileta hapa kwani tutalazimika kuwafungia kwa mawazo machafu kiwango hiki.

Njia mbadala haziwi hivi, tunazo njia za busara kufanya tunayotaka kuyafanya na si kwa mapendekezo ya KOKOLO.

Ahsanteni kwa wote mnaoyaponda mawazo ya kichochezi ya namna hii.

KOKOLO, you're not banned as this' your 1st warning and NEVER come out with such ideas at JF.

Invisible
 
Last edited by a moderator:
Umewatosa unafikiri utaachwa. Hata Sumbawanga tutakwenda. aaahaaaaa!! Weweeeeeeeeee!!! Sio mimi nisemayo hayo ni wale mafisadi uliwauumbua mzee. Nenda kamuone babu akukazie kinga shauri yako.
 
yakae kwa muda tu mzee halafu yaondolowe.. tusitukuze hayo, tutaendelea kuyapinga moja baada ya jingine....
 
yakae kwa muda tu mzee halafu yaondolowe.. tusitukuze hayo, tutaendelea kuyapinga moja baada ya jingine....

Sioni kama yamepingwa ila ameambiwa si vizuri kuweka mipango hiyo kwenye public ,pengine ni kinga za mafisadi ndio ziliomfanya ayaanike mambo hazarani , pengine kuna ka ukweli fulani huwezi kujua ,pengine wamepanga iwe siri ila huyu kaona akimbile JF na kuleta ujumbe ambao utakuwa umeshafika.
Ila kitu kimoja ambacho ningependa muelewe ,haya malezo ya jamaa yanaonyesha muelekeo wa wapi nchi inaaza kuelekea ,aidha hayo nayaweka katika kundi letu la la kiCCM kwa ule msemo wake ni mawazo yake binafsi lakini on future view ni kikomo ambacho binadamu anakuwa hana njia nyingine ya kujikwamua kutoka kwa utawala mmbovu,ingawa hapo kuna mtu alisema kuwa ziko njia nyingi za busara ,mmfahamu tu mnaweza kutumia njia hizo zote na zikashindwa na kugonga ukuta mfano ni Zimbabwe ,sehemu nyengine ni Kenya pia kule kwa KukuwaZabanga ,weka mbali Somalia ,as nilivyowahi kusema kuwa nyoka hatari alikwisha tambaa sehemu nyingi hapa Afrika na amepiga hodi katika mipaka yetu ila sasa anapanga njia ni namna gani ataingia Tanzania.
 
Kuugua kwa Dr. Mwakyembe kutupe fundisho au kutukumbushe zaidi ya tunavyotaka kufikiri.

1. Kuugua si ajabu, ikiwa ni pamoja na kufa. Kwani iko siku sote tutakufa iwe kwa kuugua au tu siku imefika.

2. Nadhani itakuwa si vibaya tukichukua hili kama kumbusho kuangalia afya zetu mara kwa mara, si lazima kwenda India au kwingineko.

3. Kuna umuhimu wa kubadili muundo wa maisha yetu, eneo ambalo huenda viongozi wengi wa Tanzania hawalizingatii yaani "Maisha Bora" ambayo yanachanganya mazoezi,lishe bora na nafasi ya kupumzika japo kwa kiasi. Sisemi Dr. Mwakyembe hakuwa anafanya hayo ila tu kwa kumbukumbu zangu kumekuwa na hali hizi karibu kwenye kila kikao cha bunge.

4. Ugonjwa ni ugonjwa hata kama ni "miwaya" kama baadhi walivyotaka kuelekeza hapa, bado mtu anastahili huruma fulani. Jifikirie ungekuwa wewe usingependa watu wa kuhurumie? Sidhani Dr. Mwakyembe alihitaji stunt ya namna hii kama exit policy yake, bali ni maradhi tu yametokea.

5. Kwa vile JF ni forum ambayo inasomwa na kuheshimika na wengi nadhani kuna umuhimu wa watu kufikiria mara mbili kabla hawajasema wanachotaka kusema, pamoja na uhuru walio nao. Uhuru bila kipimo ni utumwa.
 
Back
Top Bottom