Mwakyembe anasikitisha! Walaaniwe wanaohusika!

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Nimetokwa machozi nilipoona picha ya Mh Mwakyembe gazeti la mwananchi ya leo akizungumza na Sitta akiwa bado hosipitalini. Mwli wake umekuwa kama nyoka. Kama ni watu walimpa sumu ili watu wapate madaraka walaaniwe

Picha kubwa: https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=41762&d=1321869350

UPDATE:

Jan 03, 2012


Maskini Dk. Mwakyembe!

• ANYONYOKA NYWELE, KOPE, NDEVU, VINYWELEO VYOTE

Na Mwandishi wetu

HALI ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, inasikitisha kwani licha ya kupata matibabu nchini India na kuendelea na tiba hiyo hapa nchini, hali yake siyo ya kuridhisha.

Watu wa karibu na Dk. Mwakyembe waliopata fursa ya kumwona, waliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa afya ya waziri huyo maarufu nchini bado siyo ya kuridhisha kwani amenyonyoka nywele, kope, nyuzi na hata vinyweleo vyote mwilini.

Mbali ya hali hiyo, Dk. Mwakyembe hulazimika kuvaa gloves mikononi na miguuni, fuluna au mashati marefu pamoja na traksuti au suruali ili kufunika mikono na miguu yake ambayo licha ya tiba anayoendelea kuipata, ngozi yake ina hali mbaya kutokana na kuathirika na ugonjwa wa ajabu uliompata.

Kwa mujibu wa habari hizo, kucha za vidoleni na miguuni zimeoza na zina rangi nyeusi, miguu na mikono yake imepasuka mithili ya mtu mwenye magaga ambayo wakati mwingine hutoa damu na kumsababishia maumivu makali.

"Kwa jinsi alivyo, Dk. Mwakyembe hawezi kwenda ofisini leo au kesho. Siha yake ukimwangalia ni nzuri na anaongea kwa sauti kama kawaida, lakini ngozi yake iko vibaya, kichwani hana nywele wala kope, nyusi…

"Anahitaji muda zaidi wa kupumzika na kuendelea na matibabu," alisema mmoja wa watu waliofanya ziara ya kwenda kumwona nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watu wa karibu na waziri huyo walioshuhudia mkanda wa matibabu yake akiwa India, waliliambia gazeti hili kuwa ukiuangalia, utatoa machozi kwani picha zake zinatisha.

Mkanda huo ambao Dk. Mwakyembe hupenda kuwaonyesha watu wanaofika nyumbani kwake Kunduchi Mtongani kumjulia hali, unamwonyesha katika sura na muonekano tofauti kabisa na jinsi alivyo na kama unauangalia leo bila kuambiwa, huwezi kubaini kama ni Waziri Mwakyembe.

"Ukiuangalia mkanda wa matibabu yake, unaweza kutoa machozi, unasikitisha sana. Kwa kifupi Dk. Mwakyembe amepata mateso makubwa yaliyotokana na ugonjwa ambao hadi sasa haujulikani," alisema mtoa habari wetu.

Hata hivyo ingawa taarifa rasmi ya serikali haijatolewa, ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo nchini India ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri, inadaiwa kueleza chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kuwa umetokana na sumu kali aliyowekewa hapa nchini.

Taarifa za Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu, mara ya kwanza ziliibuliwa rasmi nchini na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi chake cha dakika 45 kilichorushwa hivi karibuni, alisema wasiwasi huo unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele aliyoondoka nayo nchini kwenda India.

Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema alipokwenda kumwona Dk. Mwakyembe nyumbani kwake, alipata mshtuko mkubwa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza katika umri alionao kushuhudia ngozi ya mtu ikitoa unga.

Sitta alikaririwa akisema, "Kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya Dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha."

Hata hivyo, Sitta alihojiwa na polisi kuhusiana na taarifa hiyo kwa madai kuwa ingeweza kuhatarisha amani, lakini alipotakiwa kutoa ushahidi anadaiwa kutoa ushahidi wa habari za kwenye mitandao ya kijamii.

Kabla ya Dk. Mwakyembe kwenda India kutibiwa, kulikuwa na uvumi kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi huyo kulishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha wala kuthibitisha habari hizo.

Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliporejea nchini, Dk. Mwakyembe alisema ripoti ya ugonjwa wake iko serikalini.

Hata hivyo, serikali hadi sasa imekataa kuitoa hadharani ripoti hiyo ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Apollo, India, waliomtibu Dk. Mwakyembe.

Habari zaidi zinasema kuwa mwanasiasa huyo amepania kuianika ripoti hiyo hadharani kama serikali itaendelea kuifanya kuwa siri.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, alipoulizwa kuhusiana na ripoti hiyo, alisema kuwa suala hilo haliwahusu na kama wameipokea hawezi kuzungumzia.

Alisema Dk. Mwakyembe ndiye anaweza kuzungumzia na hajui kama imepokelewa au la.

"Hata kama tumeipokea, sina ruhusu ya kuzungumza, mfuate mwenyewe Dk. Mwakyembe akueleze kwani sisi hatuwezi kutaja ugonjwa uliokuwa unamkabili," alisema Nyoni.

Mwakyembe alipelekwa India Oktoba 9 mwaka jana na kurejea nchini Desemba 11 mwaka jana.

Taarifa za awali, zilisema Dk. Mwakyembe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Lakini, taarifa hizo za ugonjwa wa kisukari zilipingwa na baadhi ya washirika wake wa karibu kisiasa ambao waliamini naibu waziri huyo alilishwa sumu.


CHANZO: Tanzania Daima
 
Hata Mimi pia machozi yananitoka jee niamini hadithi ya Jason Bourne kweli watu wanakuwa na roho mbaya kiasi hiki kutesa kiumbe kingine kwa ajili ya mambo ya dunia mmh kweli binadamu anaweza kuwa mnyama ,yule aliyesema jana hakuna matumaini yakupona namwona alisema kweli tumuombe mungu atende miujiza
 
Watu wa CCM ni wauaji kabisa na sisi huku Mbeya hatuwataki kabisa.

Kama mutaweza wakataeni kabisa wanawachukulia watu wenu hivi Mwandosya ,Mwakyembe sijui kwa nini alikubali uwaziri na kusaliti nafsi yake angebaki na misimamo yake ile ijulikane moja naona wanaMbeya toeni somo kwa CCM waauaji wakubwa
 
iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nalia mimi,huyo ndio basi tena,swala la kupona halipo hapo Madaraka jamani matamu,ila watu hawamwogopi mungu bana
 
iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii nalia mimi,huyo ndio basi tena,swala la kupona halipo hapo Madaraka jamani matamu,ila watu hawamwogopi mungu bana

Sasa Magamba Wanataka Kuuwa WATU Woote wenye akili na uelewa!! Wanataka Nani aongoze Hii Nchi? Wanataka watu Design ya Lusinde? Duh Huruma hadi Aibu Kwa Taifa!!
 
Dalili zote alizonazo Dr. Mwakyembe zinaonyesha aliwekewa sumu ya mionzi ijulikanayo kama THALIUM-201. Vilevile yawezekana akawa alichanganyiwa na kiasi kidogo sana cha POLONIUM-210. Mojawapo ya dalili hizo ni mwili kuota magamba na ukurutu na kunyonyoka kwa nywele ambazo zote Mwakyembe zimejionyesha. Dalili zimegawanyika katika makundi mawili kama zilipo hapa chini.

Neurology

  • Signs take 2 to 4 days to develop with the severity dependent upon the level of poisoning.
  • There is peripheral neuropathy with marked leg and foot tenderness and paraesthesia. Weakness may be difficult to elicit because of pain and it tends to be mild.
  • With severe neurological involvement, respiratory paralysis can be fatal at the end of a week.
  • Examination of the eyes and face may show loss of the lateral half of the eyebrows, drooping eyelids, facial nerve palsy, ophthalmoplegia.
  • Specialist examination is required with slit lamp assessment and documentation of colour vision.
  • Keratitis and corneal opacities occasionally occur.
Dermatology
  • Hair loss, rashes and palmar erythema take 2 to 4 weeks to appear.
  • There is atrophy of the hair follicles. Alopecia is so characteristic that it should prompt suspicion. The hair loss primarily affects the scalp, temporal parts of the eyebrows, the eyelashes, and the limbs. Less often, the axillary regions are affected.
  • Early signs are not specific and include scaling of the palms and soles and acneform lesions of the face.
  • One month after the poisoning, Mees' lines (transverse white lines on the nails) appear in the nail plate. They also occur in arsenic poisoning and renal failure.
  • Other findings may include crusted eczematous lesions, hypohidrosis, anhidrosis, palmar erythema, painful glossitis with redness of the tip of the tongue, stomatitis and hair discoloration.
  • There is a characteristic band-like dark pigmentation of the scalp that develops within 4 days.

MATIBABU

Mtu akilishwa kiasi kikubwa cha Thaliium-201 anaweza kutibiwa kwa kupewa PRUSSIAN BLUE ambayo kwa kitaalamu inapunguza "half life" ya hiyo mionzi kwa 50%.

TATIZO LINAKUJA PALE AMBAPO MTU AMEPEWA POLONIUM-210 KWA KWELI HAINA TIBA. VILEVILE INATEGEMEANA NA KIASI AMBACHO MTU AMEPEWA KWANI TATIZO KUBWA NI KUWA POLIUNM-210 HUENDA KUJIBANZA KATIKA SIFONGO ZA MIFUPA (BONE MARROW) NA KUZIHARIBU KABISA HIVYO MTU KUPOTEZA UWEZO WA KUZALISHA CHEMBECHEMBE HAI NYEKUNDU (RED BLOOD CELLS).

"Alpha particles emitted from polonium-210 can disrupt cell structures, fragment nuclei, damage DNA, and cause cell death".



Takwimu zinaonyesha kuwa Russia ndiyo nchi inayozalisha kwa wingi Polonium-210 kiasi kipatacho gramu 100 kwa mwaka kwa matumizi ya kuzalishia Umeme.

Polonium-210 ndiyo iliyotumika kumuua jasusi wa kirusi Alexander Litvinenko aliyekuwa anaishi Uingereza baada ya kupata hifadhi ya kisiasa. "German investigators say the radioactive polonium-210 used to kill a former Russian spy in London would have costed $25 million on the black market."


images
images
images


Picha kabla na baada ya kuugua (juu Alexander Litvinenko na chini Dr. Mwakyembe)

attachment.php
images
images




WARNING!

Huu ni ushauri unaweza kuufuata au ukaacha. Usivute sigara maana moshi wake una mvuke wa POLONIUM-210 ambao ndiyo chanzo cha kansa ya maini na mapafu kwa wavuta sigara. Hii ndiyo sababu sigara zinapigwa vita ila serikali kamwe haiwezi kuwaambia tatizo lake kubwa ni nini.

"A study published in the American Journal of Public Health (2008) suggests that tobacco companies have known about the danger of polonium in cigarette smoke for over 40 years. Monique Muggli, who led the review, examined over 1,500 internal documents from tobacco companies. Most of these have never been published and were made available through legal action. Muggli wrote, "Internal tobacco industry documents reveal that the companies suppressed publication of their own internal research to avoid heightening the public's awareness of radioactivity in cigarettes".

Download the findings at
http://ajph.aphapublications.org/cgi/reprint/AJPH.2007.130963v1
 
Kama mutaweza wakataeni kabisa wanawachukulia watu wenu hivi Mwandosya ,Mwakyembe sijui kwa nini alikubali uwaziri na kusaliti nafsi yake angebaki na misimamo yake ile ijulikane moja naona wanaMbeya toeni somo kwa CCM waauaji wakubwa

Namuombea apone,arudi nyumbani tukalijenge Taifa. Lakini siku zote afahamu angejiondoa CCM kipindi kile historia ingemtendea haki kama mmoja wa wana wa nchi hii ambao walisimama kidete kulinda mali na pesa za Watanzania.
 
Palalisote inaonyesha uko kwenye eneo lako la kjidai ISIPOKUWA tatizo kama hilo dawa yake ni nini? Hakika Siku za mwisho zaja na hao wanaothubutu kufanya unyama huo watakiona. Mungu epushia mbali yasiendelee haya madudu.
 
watu wanagonga glasi kwa hali ya mwakyembe..na sasa wameamua kupita na kusafisha majina yao kupitia nyumba za ibada........
 
Dalili zote alizonazo Mwakyembe zinaonyesha aliwekewa sumu ya mionzi ijulikanayo kama THALIUM-201. Vilevile yawezekana akawa alichanganyiwa kwa kiasi kidogo sana na POLONIUM-201. Mojawapo ya dalili hizo ni mwili kuota magamba na ukurutu na kunyonyoka kwa nyele ambazo zote Mwakyembe zimejionyesha. Dalili zimegawanyika katika makundi mawili kama zilipo hapa chini.

Neurology

  • Signs take 2 to 4 days to develop with the severity dependent upon the level of poisoning.
  • There is peripheral neuropathy with marked leg and foot tenderness and paraesthesia. Weakness may be difficult to elicit because of pain and it tends to be mild.
  • With severe neurological involvement, respiratory paralysis can be fatal at the end of a week.
  • Examination of the eyes and face may show loss of the lateral half of the eyebrows, drooping eyelids, facial nerve palsy, ophthalmoplegia.
  • Specialist examination is required with slit lamp assessment and documentation of colour vision.
  • Keratitis and corneal opacities occasionally occur.
Dermatology
  • Hair loss, rashes and palmar erythema take 2 to 4 weeks to appear.
  • There is atrophy of the hair follicles. Alopecia is so characteristic that it should prompt suspicion. The hair loss primarily affects the scalp, temporal parts of the eyebrows, the eyelashes, and the limbs. Less often, the axillary regions are affected.
  • Early signs are not specific and include scaling of the palms and soles and acneform lesions of the face.
  • One month after the poisoning, Mees' lines (transverse white lines on the nails) appear in the nail plate. They also occur in arsenic poisoning and renal failure.
  • Other findings may include crusted eczematous lesions, hypohidrosis, anhidrosis, palmar erythema, painful glossitis with redness of the tip of the tongue, stomatitis and hair discoloration.
  • There is a characteristic band-like dark pigmentation of the scalp that develops within 4 days.
Nalink hii na ile thread ya jason bourne then naamini kweli duniani kuna watu wana roho kama ya paka,ngumu na isiyo na huruma....
 
Mmmh inauma sana tulimtegemea sana ktk mapambano sasa tunasubiri miujiza ya mwenyezi Mungu tu, Namwomba sana Mungu ili huyu mtz mwezetu arudi hai ili atueleze ukweli wa richmond, ukweli waliouficha ili kumwokoa jk.
 
Palalisote inaonyesha uko kwenye eneo lako la kjidai ISIPOKUWA tatizo kama hilo dawa yake ni nini? Hakika Siku za mwisho zaja na hao wanaothubutu kufanya unyama huo watakiona. Mungu epushia mbali yasiendelee haya madudu.

asante kaka kwa ufupi ikiwa mtu amepata kiasi kikubwa cha Thaliium-201 anaweza kutibiwa kwa kupewa PRUSSIAN BLUE ambayo kwa kitaalamu inapunguza "half life" ya hiyo mionzi kwa 50%.

TATIZO LINAKUJA PALE AMBAPO MTU AMEPEWA POLONIUM-210 KWA KWELI HAINA TIBA. VILEVILE INATEGEMEANA NA KIASI AMBACHO MTU AMEPEWA KWANI TATIZO KUBWA NI KUWA POLIUNM-2010 HUENDA KUKAA KATIKA SIFONGO ZA MIFUPA (BONE MARROW) NA KUZIHARIBU KABISA HIVYO MTU KUPOTEZA UWEZO WA KUZALISHA CHEMBECHEMBE HAI NYEKUNDU (RED BLOOD CELLS).

Alpha particles emitted from polonium-210 can disrupt cell structures, fragment nuclei, damage [FONT=Palatino Linotype,Palatino][FONT=Palatino Linotype,Palatino]DNA[/FONT][/FONT], and cause cell death.
 
Back
Top Bottom