MWAKYEMBE AMPONZA SITTA - Ahojiwa Polisi kuhusu tuhuma za sumu

polisi wanachokiongea hawakielewi sawasawa. mtandao siku hivi unahabari nyingi za kuaaminika. mbona magazeti wanayaamini kwani wanakaa wangapi kuandika habari moja.
........wanaelewa, tena vizuri sana, pointi hapa ni kwamba wanajifanya hawaelewi; swali, wanajifanya hawaelewi kwa manufaa ya nani?
 
..kama Dr.Mwakyembe amelishwa sumu madaktari wake huko India wanapaswa kuhoji suala hilo na kuomba uchunguzi wa jinai kufanyika.

..madaktari hao wanapaswa kuripoti kwa polisi wa India, baada ya hapo suala hilo linapaswa kuwasilishwa kwa polisi wa Tanzania ambapo mgonjwa[Dr.Mwakyembe] ametokea.
 
.
.kama dr.mwakyembe amelishwa sumu madaktari wake huko india wanapaswa kuhoji suala hilo na kuomba uchunguzi wa jinai kufanyika.

..madaktari hao wanapaswa kuripoti kwa polisi wa india, baada ya hapo suala hilo linapaswa kuwasilishwa kwa polisi wa tanzania ambapo mgonjwa[dr.mwakyembe] ametokea.
  • hao.... Polisi wa tanzania ndio hao wanaruka kimanga
 
Mtu Chake,

..nadhani hakuna waandishi wa habari nchi hii.

..kwenye nchi za wenzetu waandishi wa habari wangeanzia kuihoji hospitali aliyolazwa Dr.Mwakyembe?

..ni makosa kwa hospitali kutibu mgonjwa aliyelishwa sumu bila kutoa taarifa zake kwa Polisi.

..hospitali kama Apollo hawawezi kukubali jina na heshima yao ichafuliwe kwa madai kwamba hawajatoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu mgonjwa wao aliyelishwa sumu.

..kama Apollo wametoa taarifa polisi basi waandishi wanapaswa kuuliza ni nini kinaendelea ktk kutafuta ukweli kuhusu jinai hiyo.

..baada ya hapo sasa ndipo waandishi wanaweza kurudi Tanzania na kuanza kuwahoji wakina Manumba na Saidi Mwema.
 
Siyo mara zote kuhojiwa kunatoa ripoti ya ukweli.
Yawezekana amehojiwa ili kutengeneza ripoti ya kusafisha wahusika.
Kumbukeni ya Jairo, Luhanjo na CAG! pia PCCB na Richmond.
 
Sijui kuna nini hapa au ndio kazi yule mchawi ambaye Dr Mwakyembe alimuongelea awali?
 
Ingekuwa kweli Sitta akiwa rafiki mkubwa wa mwakyembe angeenda na ushahidi wa daktari, acheni kununuliwa kwa propaganda za kijinga, akili za Cameroon na Masaburi changanyeni na zenu
 
mmiliki wa gazeti mwenyewe ni wale wale.
sitta naye mnafiki.
mwakyembe get well soon.
ila polisi wa tanzania wana maajabu ,badaala ya wao kuchunguza na kutafuta ushahidi wao wanamwambia sitta ndo awaletee ushahidi....shame on them.
 
Kwa wakuu,ndio kusema kwamba, Dr wetu Mwakyembe atakufa tu,kutokana na hali aliyonayo sasa? Wataalamu jamani tuambieni
 
Yaliomo yamo,mbona wao wamekataza maandamano kwa hofu ya alshabab siku hiyohiyo wanahimiza watu wajae uwanja wa taifa kuangalia staz na Chad
 
Habari kuu, Mtanzania

*Ahojiwa Polisi kuhusu tuhuma za sumu

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi nchini limemhoji Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kuhusiana na tuhuma alizotoa akidai mafisadi wamempa sumu Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye yupo nchini India kwa matibabu.

Chanzo cha habari cha kuaminika ndani ya jeshi hilo kimesema, baada ya Sitta kuhojiwa na kutakiwa kuwasilisha ushahidi wa tuhumu alizotoa, alipeleka ushahidi ambao uliwashangaza wengi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

“Mzee baada ya kutoa zile tuhuma, tuliona si jambo dogo, linaweza hata kuhatarisha amani ya nchi hivyo tukaona ni busara tumhoji, atupatie ushahidi wake, ili sisi kama wanausalama tuufanyie kazi.
“Lakini kilichotuchekesha na kutushangaza, akatuletea ushahidi kutoka kwenye mitandao ya jamii, akijua kabisa ule si ushahidi mbele sheria pamoja na kuwa yeye ni mwanasheria.“Katika mambo yanayoandikwa kwenye mitandao ya jamii, kuna mengi ya kweli na uongo, ndio sababu hata wachangiaji wengi hawaweki majina wala anwani zao hali, sasa ni vipi mtu anazungumza mambo mazito kwa ushahidi wa aina hiyo?” kilihoji chanzo chetu.Katika ushahidi huo wa Sitta (nakala tunayo) pia yeye binafsi anatajwa kuwa mmoja wa walengwa katika mkakati wa kuua watu kadhaa.

Wengine waliotajwa ni Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi, Saed Kubenea.
Sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini, alisema wasiwasi huo unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele aliyoondoka nayo nchini kwenda India, ambayo ni mara ya kwanza kuishuhudia katika kipindi chote cha maisha yake.Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha ITV katika kipindi chake cha Dakika 45, kilichorushwa hivi karibuni.“Ijumaa iliyopita nilikwenda kumuona nyumbani kwake, Kunduchi Mtongani.

Nilishtuka sana. Kwa sababu umri wangu sasa wa zaidi ya miaka 65, sijaona mtu anajishika halafu inatoka vumbi, inadondoka chini kutoka kwenye ngozi,” alisema Sitta.
Aliongeza: “Kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya Dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha.”Alisema inatisha zaidi hasa baada ya madaktari bingwa nchini kushindwa kugundua kitu kilichomsababishia Dk. Mwakyembe kupatwa na hali hiyo, hadi anaondoka kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.

Hata hivyo, alisema anamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuamua Dk. Mwakyembe apelekwe India kwa madaktari bingwa, ambako itajulikana nini kilichomsababishia hali hiyo.
“Lakini kilichokuwa kinaonekana dhahiri pale ni uwezekano wa kitu cha hovyo kuwa kimefanywa cha aina labda ya sumu,” alisema Sitta.Hata hivyo, alisema anamuachia Mungu kwani kila mtu ana siku yake ya kuondoka duniani.

Akijibu swali namna anavyoliona suala la kuugua huko kwa Dk. Mwakyembe, Waziri Sitta alisema ni kama limechukua sura ya kuwekeana sumu na vitisho.

Hata hivyo, alisema suala hilo linabaki kuwa ni sehemu ya mapambano na kukumbusha kila mwanadamu amezaliwa siku moja, hivyo kufa ni lazima.
“Kwa hiyo, sijui mambo haya yamefanywaje. Mimi napata vitisho kwenye simu. Utaona namba zangu za simu nabadili mara kwa mara kwa sababu natishiwa sana.

Na vita bayana ipo kwenye magazeti yao,” alisema Waziri Sitta.
Kabla ya Dk. Mwakyembe kwenda India kutibiwa, kulikuwa na habari kwenye magazeti kuwa alikuwa amelishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha waka kuthibitisha habari hizo.
Wadau hii sasa inatisha sijui tufanye je, Mhs Mwakyembe anasikitisha kwa hali yenyewe ni hivyo!!!!!!!!!! Lakini kuna siku Mungu atalipa ovu kwa ovu, yote hii ni RICHMOND, DOWANS, na SYIMBION POWER NINI???????Maana Mwakyembe ni shahidi muhimu, kama Balali alifichwa unategemea nini, Mungu Baba okoa taifa la Tanzania toka mikononi mwa mafisdi na wauaji!!!!!!!!!!

 
..kama Dr.Mwakyembe amelishwa sumu madaktari wake huko India wanapaswa kuhoji suala hilo na kuomba uchunguzi wa jinai kufanyika.

..madaktari hao wanapaswa kuripoti kwa polisi wa India, baada ya hapo suala hilo linapaswa kuwasilishwa kwa polisi wa Tanzania ambapo mgonjwa[Dr.Mwakyembe] ametokea.

ugonjwa wa mwakyembe hauwezi kuchunguzwa na polisi uwezzo huwana. lazima watafute wataalamu toka nje.
 
Mtu Chake,

..nadhani hakuna waandishi wa habari nchi hii.

..kwenye nchi za wenzetu waandishi wa habari wangeanzia kuihoji hospitali aliyolazwa Dr.Mwakyembe?

..ni makosa kwa hospitali kutibu mgonjwa aliyelishwa sumu bila kutoa taarifa zake kwa Polisi.

..hospitali kama Apollo hawawezi kukubali jina na heshima yao ichafuliwe kwa madai kwamba hawajatoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu mgonjwa wao aliyelishwa sumu.

..kama Apollo wametoa taarifa polisi basi waandishi wanapaswa kuuliza ni nini kinaendelea ktk kutafuta ukweli kuhusu jinai hiyo.

..baada ya hapo sasa ndipo waandishi wanaweza kurudi Tanzania na kuanza kuwahoji wakina Manumba na Saidi Mwema.

Nakubaliana na wewe mkuu hii nchi waandishi wengi wa habari ni njaa tupu ni watu wa kitu kidogo

Nadhani tuwaombe wale jamaa(waandishi) wa KTN wafanye uchunguzi wale ni kiboko hawaogopi kitu,tukiwapa kazi wale jamaa ni wiki tu mambo yote hadharani,sio hawa wa kwetu wameweka ushabiki wa vyama mbele
 
Hivi kwanini Sita aitwe? Kwanini serikali isiseme Mwakyembe anaumwa nini? Sita anasema kweli, hali halisi ya Mwakyembe, sasa wanamhoji badala wangetuambia Mwakyembe anaumwa nini, full comedy with human life, which is not replaceble....
 
tangu nimezaliwa sijawahi kuona kama kumuua mtu ni solution.afterall kila mtu lazima afe one day so is better to find another alternative to fight agaiinst your enemy and let him last to see the results
 
Hivi kwanini Sita aitwe? Kwanini serikali isiseme Mwakyembe anaumwa nini? Sita anasema kweli, hali halisi ya Mwakyembe, sasa wanamhoji badala wangetuambia Mwakyembe anaumwa nini, full comedy with human life, which is not replaceble....
NA NI KWANINI UMEPITA MUDA MREFU SANA KUMUHOJI TOKA SAMWEL SITTA ATOE KAULI HY?? Kwanini hawakumkamata sitta siku ileile au kesho yake akathibitishe tuhuma hizo nzito za mauaji??NASHAWISHIKA KUAMINI KUWA NI KWELI.
 
polisi hao hao ndo wanahangaika kutafuta waliondika waraka wa 2858.kama habari za mitandaoni si za kweli kwa nini moja waitilie mkazo na nyingine iwe mshangao? kwa kauli hiyo basi hata mtu akitishiwa kwa maneno ama hata sms waignore
ushahidi upi walioutaka..?bado tupo mbali sana.kurukia maneno.basi waidefine role ya jeshi liwe na kazi ya kunyamazisha watu na kuzima maandamano
 
Back
Top Bottom