Mwakyembe akesha na abiria Tazara

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
[FONT=Georgia, Times New Roman, Times, serif][/FONT]WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe juzi usiku alikesha na abiria zaidi ya 1,000 waliokwama kwa saa 11 katika stesheni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) jijini Dar es Salaam kutokana treni kukosa mafuta. Kutokana na tatizo hilo, Dk Mwakyembe ambaye alifika katika stesheni hiyo mara baada ya kuwasili kutoka safarini India, aliahidi kuwashughulikia watendaji wa Tazara waliosababisha uzembe huo.

Dk Mwakyembe ambaye ametimiza siku 20 tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza Wizara ya Uchukuzi, alifika eneo hilo baada ya abiria wawili kumpigia simu na kuomba aingilie kati tatizo hilo. Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo.

Alipokutana na abiria baada ya Dk Mwakyembe kuwasili na kuingia katika ukumbi wa kupumuzika abiria wanaposubiri kuondoa, wasafiri walimshangilia kwa nguvu mara baada ya kujitambulisha kuwa ni Waziri wa Uchukuzi na amefika kutatua tatizo linalowakabili, ingawa ni usiku akiwa ametoka safarini India. Abiria hao waliokuwa na jazba walimwelezea waziri huyo kuwa kufika kwake eneo hilo ni uzalendo ambao hawakuutegemea na kutaka awapatie majibu ya chanzo cha tatizo na namna atakavyolitatua.

Awali, Kabla ya kuingia ndani ya ukumbi huo, uliibuka mvutano wa chini kwa chini baina yake na baadhi ya watendaji na wanausalama waliotaka asingie ukumbini kwa hofu ya kufanyiwa vurugu abiria hao waliokuwa na hasira. Lakini Dk Mwakyembe aliwataka watendaji wamfungulie mlango ili aingie ndani ya ukumbi kukutana na abiria hao. Alipofunguliwa mlango, Dk Mwakyemba akiwa ameongozana na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo waliokuwa zamu, aliingia ndani ya ukumbi na umati wa watu walimzunguka huku kila mmoja akitaka kuwakilisha kilio chake.

Mmoja wa abiria hao alipasa sauti na akisema; “Tunataka uje huku, mpaka muda huu hatujaondoka, hatuelewi chochote, hatujui kama treni itaondoka au hapana, na kama itaondoka itakuwa saa ngapi? Hawa Tazara wanadharau, wanatutesa! Tunaomba uje utusikilize na ueleze kama safari ipo au la”. Dk Mwakyembe aliwatuliza akisema; “Tulieni, tulieni! Nimekuja hapa kwa sababu baadhi yenu wamenipigia simu kunieleza kuwa mmekwama hapa kwa muda mrefu na mnahiji msaada ili muweze kuondoka.

“Mimi ndiye Waziri wa Uchukuzi, nimekuja kujionea mwenyewe na kuchukue hatua. Ninawaahidi hali hii katika kipindi hiki cha uongozi wangu haitajirudia. Nitahakikisha ndani ya muda mfupi kunakuwa na mabadiliko makubwa.” Baada ya maelezo hayo, abiria hao walianza kuzungumza kwa mpangilio na kumweleza waziri huyo kuwa kitendo cha treini ya abiria kuchelewa kuondoka bila taarifa yoyote kinawasababisha usumbufu mkubwa. Mmoja wa abiria hao, Paulo Michael alisema kama hali hiyo haitadhibitiwa inaweza kulipeleka taifa katika hali mbaya kwa kuwa wananchi wamechoka na kukataa tamaa.

“Mheshimiwa hivi sasa wananchi wamekata tamaa, kama watendaji wa mamlaka hii wataendelea kututesa namna hii …alilalamika Michael ambaye alionekana kukerwa na kitendo hicho. Alisema watu wakiwamo wanawake na watoto, wanateseka kutokana na uzembe wa watu wachache na kwamba, jambo hilo ni hatari kwa usalama wa nchi.

Akijibu hilo, Dk Mwakyembe alisema; “Kuhusu hili nawahakikishia kuwa halitatokea tena katika kipindi changu, natambua mmeumia, lakini nawaahidi kufanya mabadiliko, nipeni muda mfupi.” Abiria hao waliendelea kupaza sauti wakimtaka waziri huyo kutoondoka eneo hilo hadi watakapoondoka kwa kuwa watendaji hao wanaweza kuwadanganya. Hata hivyo, Waziri Mwakyembe kabla ya ombi hilo la abiria alikuwa ameahidi kuwa hataondoka eneo hilo hadi treni litakapoondoka.
 
hapa wa kulaumiwa ni sisi watanzania kwa uzembe makazini.. Na mfumo mbaya tulio nao
 
wapendwa,

hakukuwa na haja ya waziri kwenda kule, usiku na tena akijitangaza kuwa katokea india! kama ni uzembe wa tazara ana muda mzuri tu wa kushughulika nao na sio kwenda 'kufoka stesheni" uongozi wa mtindo wa maghufuli huu, haufai na hauleti tija yoyote zaidi ya cheap polarity.

any way, labda ndio karata zenyewe zinachangwa

mbarikiwe sana

Glory to God!
 
Huu mfumo ovyo wa kuteua hawa viongozi wabovu na wazembe kwenye makampuni yetu ndio unao tuharibia sisi vijana na kusababisa makampuni ya kigeni kuajiri maneja toka nje ya nchi.
 
wapendwa,

hakukuwa na haja ya waziri kwenda kule, usiku na tena akijitangaza kuwa katokea india! kama ni uzembe wa tazara ana muda mzuri tu wa kushughulika nao na sio kwenda 'kufoka stesheni" uongozi wa mtindo wa maghufuli huu, haufai na hauleti tija yoyote zaidi ya cheap polarity.

any way, labda ndio karata zenyewe zinachangwa

mbarikiwe sana

Glory to God!

Dk Mwakyembe ambaye ametimiza siku 20 tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza Wizara ya Uchukuzi, alifika eneo hilo baada ya abiria wawili kumpigia simu na kuomba aingilie kati tatizo hilo. Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo.

Dk Mwakyembe ambaye ametimiza siku 20 tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza Wizara ya Uchukuzi, alifika eneo hilo baada ya abiria wawili kumpigia simu na kuomba aingilie kati tatizo hilo. Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo.

...... sasa na mimi siku ATCL wakinichelewesha nikimpigia simu saa sita usiku atakuja "kushughulikia" pia?
 
wapendwa,

hakukuwa na haja ya waziri kwenda kule, usiku na tena akijitangaza kuwa katokea india! kama ni uzembe wa tazara ana muda mzuri tu wa kushughulika nao na sio kwenda 'kufoka stesheni" uongozi wa mtindo wa maghufuli huu, haufai na hauleti tija yoyote zaidi ya cheap polarity.

any way, labda ndio karata zenyewe zinachangwa

mbarikiwe sana

Glory to God!

Nachukia sana upumbavu huu!
wahusika wameuchapa usingizi, wewe waziri tena mgonjwa badala ya kwenda kupumzika unatafuta umaarufu usio na maana kabisa.
huo si uwajibikaji, unamnyima mkeo haki yake ya msingi.
kama waziri mzima unakesha station wakati wahusika wakuu wapo ambao ungeweza kuwaamuru muda wowote waje hapo kushughulikia hilo tatizo, akili yako haina akili! CHEAP POPULARITY itawamaliza nyie wakuu.
kuna sababu kweli ya kuwa na viongozi chini yako!?
Chickenshit!
sumu yataka upumzike ili ipotee ktk body yako. Have a plenty of time to relax and recline. Bado tunakuhitaji
 
Ukifanya makosa, usipofanya makosa.

Inanikumbusha nyimbo ya zamani: "tenda wema uende zako usingoje shukurani, binaadamu hawana wema".

"damned if you do, damned if you don't".
 
Ukifanya makosa, usipofanya makosa.

Inanikumbusha nyimbo ya zamani: "tenda wema uende zako usingoje shukurani, binaadamu hawana wema".

"damned if you do, damned if you don't".

Ndugu yangu Zomba, tatizo la watanzania ni kwamba hakuna wema unaoweza kuwafanyia wakaridhika nao. Vyote ni vibaya kwao mpaka wanaingia kaburini.

Ni mtindo wa ushabiki wa chekechekea. Tujipe moyo kwani tunasafari ndefu.
 
wapendwa,

hakukuwa na haja ya waziri kwenda kule, usiku na tena akijitangaza kuwa katokea india! kama ni uzembe wa tazara ana muda mzuri tu wa kushughulika nao na sio kwenda 'kufoka stesheni" uongozi wa mtindo wa maghufuli huu, haufai na hauleti tija yoyote zaidi ya cheap polarity.

any way, labda ndio karata zenyewe zinachangwa

mbarikiwe sana

Glory to God!

Dk Mwakyembe ambaye ametimiza siku 20 tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuongoza Wizara ya Uchukuzi, alifika eneo hilo baada ya abiria wawili kumpigia simu na kuomba aingilie kati tatizo hilo. Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo.

Kwenye Red: cheap polarity kivipi fafanua? sasa ulitaka akitoka India akalale Q Bar anywe bia weeeeeeeeeeeeeeeee ili iweje? Lipi bora kwenda kujionea matapishi ya Tazara au kutokwenda huku akisubiri taarifa za kupikwa kutoka kwa viongozi wa Tazara..
Uzembe mkubwa umefanyika yaani treni haina mafuta wewe una mbwela mbwela tu bila nguvu ya hoja. Ua tokin stupid.
 
Alifika stesheni katika hiyo saa 4:01 usiku na kukaa mpaka saa 6:30 usiku alipoondoka na hakukuwa na kiongozi yeyote wa ngazi za juu wa Tazara aliyefika kushughulikia tatizo hilo.
Hivi ni nini maana ya kukesha ?

Inabidi ifike wakati wa kuacha politizing issues na kuanza ku-walk the walk.., enough of talking the talk.., hii so called kukesha (ingawa sio kukesha) haitasaidia iwapo watu hawatawajibishwa au kitendo kama hiki kutokutokea tena. Abiria hawataki kukesha na kiongozi bali kusafiri na kwenda walipanga kwenda
 
..kwa kweli hawa CCM wanavyoongoza utadhani tumepata uhuru mwezi uliopita.

..they dont act and lead kama chama ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 30 sasa.
 
Abiria wamelipa nauli kwa nini mafuta yasinunuliwe?

Vile kwa Tanesco unakuta watumiaji wa LUKU ni wengi sana lakini etu shirika linakosa mafuta ya kuendeshea mitambo!!!
 
Back
Top Bottom