Mwakyembe ageukwa

Huu ndio upuuzi unaoifanya nchi hii kubakia maskini. Rubani kazi yake ni kuendesha ndege, kuongoza shirika la ndege lazima uwe umebobea katika STRATEGIC Management na sio urubani. Paul Chizi alikuwa boss wa JETLINK, shirika la waKenya, kwa wakenya kumpa uboss mtanzania hawezi kamwe kuwa mbabaishaji, hata kidogo kwa vile kule kuna ushindani sana. Waziri Nundu alimuomba aache kazi kule aje kuokoa jahazi nchini kwake, nyie mnataka afanyiwe interview wakati credentials zake ziko clear!? Kwa muda mchache aliokaa amefanikiwa kuleta ndege ambayo ndo most competent kwenye soko la afrika masharika. Boeing 737-500 inabeba watu 108 na inatumia saa moja kamili DAR to Mwanza kwenye abiria wengi. Iko very efficient kwenye fuel. Precision wana boeing yao inabeba abiria 137 lakini mara nyingi haijai na inakula mafuta zaidi pia inatumia saa moja na dk 10 Dar to Mza. Fly 540 wanatumia Jet inabeba abiria 54 tu ingawa iko fuel efficient kama hii ya ATC lakini inatumia saa moja na dk 15 Dar to Mza. Kama umeenda kidogo shule calculate COMPETITIVE ADVANTAGE hapo then utaona kwa nini hata bei Bw Chizi aliweka chini kuliko bei za hao wengine. Jamaa wa mashirika binafsi huyu jamaa aliwanyima usingizi kabisa. Sisi tunaotumia huu usafiri mara nyingi tumehuzunishwa sana na kuondolewa kwa huyu jembe kwa alitupa bei ya ukombozi na ndege inakuwa full wiki nzima toka imefika. Labda kaondolewa kwa kuwa yuko KAMBI YA LOWASSA!!!!

Kwa nini amemwachisha kazi? Hilo ndilo muhimu. Any clue!?
 
nadhani itakuwa kweli,ukabila itakuwa ndio sababu.maabna hataki kusema sababu ya msingi,paul alikuwa anafanya vizuri.nyinyiemu hakuna aliyebaki wote ni vimeo hata huyo mwakyembe tupaa kule.huwezi tembea na mwizi wewe usiibe.

Tunatokwa jasho kubishia shirika lisilozalisha chochote - yaani walikua wanakula bure mishahara.

Mwache waziri mpya aje na mbinu zake kwa kutumia watu aliowaamini na kuwachagua kwa taratibu zilizopo, viwango vya elimu zao, utendaji na hata ukabila is ok ili mradi uzalishaji usipopanda naye ataondolewa. Akija waziri wa kabila lingine, ama hata wa kabila hilo hilo la M'kiembe bado naye itabidi irekebishe watu wake ili kuleta ufanisi.

Halafu vijikabila TZ vingiii na vina taboos nyingi tu, hata hujui uanzie wapi kuchagua anayefaa ili kuleta balance.
 
Chiza alikuwa ni kaimu, si lazima ukikaimu uwe full.
ni kweli haikuwa lazima,lakini sababu iliyotolewa haina maana hiyo unayoisema wewe.na mie ninavyoelewa watu walikuwa wakilipwa bila kufanya kazi kipindi cha yule fisadi aliyepelekwa mahakamani,toka paul aanze kukaimu,mambo yalibadilika, na mkuu alitetengua uteuzu hajasema kuwa paul alikuwa mfisadi,ila kasema taratibu na kanuni,hebu nyie ambao mnaona mwakyembe yupo right,tuambieni hizokanuni na taratibu zilizokiukwa.
 
Kumuita majina yaliyosababishwa na ugonjwa aliokuwa akiugua si sawa jamani. Jina lake linajulikana kwa nini hatumu'address' kwa jina lake?

Mlitaka asifanye mabadiliko huo uchunguzi ungefanyikaje wakati wanaochunguzwa bado wako vitini? Mbona Kigoda amefanya mabadiliko hamkuongea. Acheni afanye kazi jamani msiingilie kazi za watu. Chuki zisichanywe na kazi.
 
Kosa la Paul Chizi ni nini?

Kosa ni kulipwa mishahara wakati hawazalishi - na Chizi akiwa ndio bosi pale.
Tunajua wewe hulioni, lakini kushindwa kufanya juhudi mpaka shirika likasimama lenyewe hilo ni kosa kubwa kuliko yote uwezayo kuyafikiria.
 
On a serious note, Paul Chizi aliteuliwa na Mkuu wa Nchi kukaimu nafasi ya Ukurugenzi Mkuu wa ATCL.
Sasa Waziri huyu 'mpya' anakuja kutuambia uteuzi wake umetenguliwa mara moja kwa kusema kuwa vigezo vya uteuzi wake havikuzingatiwa.
1. Ina maana mkuu wa nchi alishauriwa tena vibaya na washauri wake?
2. Kwa hiyo kilichomwondoa kwenye ofisi ni kuwa vigezo havikufuatwa na si kwamba jamaa alikuwa non - performer?
3. Magazeti ya Tanzania sasa amepoteza mwelekeo maana vichwa vikuu vya habari vilikuwa na mwenendo wa kishabiki sana)(hakukuwa na objectivity).Maneno kama 'atimuliwa'; 'angolewa' , 'asimamishwa' ' aondolewa' ama 'afukuzwa' ndiyo yaliyotawala badala ya neno/msamiati mkuu wa KUTENGULIWA.
4.Namsifu sana Paul Chizi kwa kauli yake kwamba cheo ni dhamana, na hivyo yuko tayari kuwatumikia wengine watakaomhitaji
5.Je, vigezo sasa vimezingatiwa katika uteuzi wa Lusajo, kama kweli ameteuliwa?
6.Kwa nini visipitiwe vigezo upya ili Chizi ateuliwe upya na tuondoe dhana kuwa aliondolewa kwa Ukabila?
 
hata akimweka nani uzuri sifa anazo ndio muhimu hilo ukianza kuuliza mambo ya ukabila hatutafika
 
Kwa nini amemwachisha kazi? Hilo ndilo muhimu. Any clue!?

Kakurupuka tu baaada ya kuingizwa mkenge na wajanja wachache huko wizarani kwao kwa maslahi ya mashirika binafsi ya ndege. Kwa sasa ATC ndio inauza kuliko hayo mashirika ambayo yalikuwa yamekamata njia zote ambazo ATC ilitawala zamani. Mfano Dar to Nairobi Precision wanasafari zaidi ya tano kwenda na tano kurudi wakati ilikuwa zamani territory ya ATC. Dar to Mwanza Precision na Fly540 walikuwa na safaari tatu kwenda na tatu kurudi kila siku lakini kuna kila dalili kuwa watapunguza kubakia mbili baada ya TWIGA kukamata abiria wake wote. Ukali wote huu wa Twiga umeletwa na Bw Chizi kwa kuwa ametokea kwenye mashirika haya binafsi sasa njia pekee ni kumuondoa ili Twiga adhohofike kama zamani na mashirika yao yaendelee kutamba. Heri serikali ijiondoe katika biashara ya Ndege kuliko kufanya usanii wa mchana kama huu wa Mwakyembe
 
ni kweli haikuwa lazima,lakini sababu iliyotolewa haina maana hiyo unayoisema wewe.na mie ninavyoelewa watu walikuwa wakilipwa bila kufanya kazi kipindi cha yule fisadi aliyepelekwa mahakamani,toka paul aanze kukaimu,mambo yalibadilika, na mkuu alitetengua uteuzu hajasema kuwa paul alikuwa mfisadi,ila kasema taratibu na kanuni,hebu nyie ambao mnaona mwakyembe yupo right,tuambieni hizokanuni na taratibu zilizokiukwa.

Ukaimu? Ok ufanisi wake mbaya hivyo kuundiwa mzengwe ili aondolewe ni fair play.
 
Mi nasubri Mwakyembe mwenyewe aje aelee,Licha ya kudai Paul Chiz hakuteuliwa kwa mujibu wa taratibu sasa,ni kwa nini Mwakyembe asimhalalishe Paul Chizi kwa kumuidhinisha kwa utaratibu? Ni mapungufu gani aliyonayo Chiz ambayo Lusajo hana? Tuache unafiki,ATCL imeanza kuamka ikiwa mikononi mwa Chiz.Huyo jamaa alikomesha vitendo vya kwenda kutengeneza Ndege nje ili zitengenezwe bongo then gharama ipungue,Chini ya Chiz nauli ilipungua kwa upande wa ATCL kitu ambacho kilichochea ushindani wa kibiashara kiasi kwamba mashirika binafsi walimwonea gele.Tunahoji kwa manufaa ya taifa kwamba Urubani siyo tatizo but huyo Lusajo ana nini cha ziada? Suala siyo wivu wa kikabila ila uwazi na ukweli.Mimi ni kabila moja na Lusajo lakini sifahamu utendaji kazi wake ukiachana na hiyo sifa moja:RUBANI WA SIKU NYINGI
 
Basi wacha apange safu yake ili akipewa sumu asimsingizie mtu maana yake kwa unafiki huyu mzee anaweza akawa anaongoza.Alipokuwa India watanzania niombeeni nikurudi napasau jipu lote alipokuja kila mtu anajua alichokifanya.Bora angedanja tu kudadeki

Hivi unaweza kuwa na chuki na mtu kwa kiasi hiki kweli? Hope utaanza kudanja wewe kwanza.
Jadili hoja ya kufukuzwa Chizi na kuwekwa Lusajo katika nafasi ya kaimu mkurugenzi wa ATCL
 
Kosa ni kulipwa mishahara wakati hawazalishi - na Chizi akiwa ndio bosi pale.
Tunajua wewe hulioni, lakini kushindwa kufanya juhudi mpaka shirika likasimama lenyewe hilo ni kosa kubwa kuliko yote uwezayo kuyafikiria.
Haya unayoongelea wewe mshabiki yamekuwepo kabla ya Chizi, yeye kaingia zama za Omar Nundu zamani alikuwepo Mattaka(o) mwenye kesi mahakamani na alikuwa anatumiwa na makampuni binafsi kudhohofisha. Kuwapunguza wafanyakazi ATC inatakiwa serikali itoe hela za kuwalipa mafao kwa kuwa shirika halina. Sidhani kama Chizi angekurupuka, labda tumuulize Mwakyembe je AMETENGA fedha katika bajeti za kuwalipa mafao wafanyakazi wa ATC ili wapunguzwe? Kama hajatenga ina maana hata Lussajo hatakuwa na ujanja wa kuwapunguza hao wafanyakazi na tutabakia kwenye Vicious circle.
 
Ukaimu? Ok ufanisi wake mbaya hivyo kuundiwa mzengwe ili aondolewe ni fair play.
MR tom,taarifa kwa uma haikiwa sababu ya ufanisi,ila kanuni na taratibu.pia ujue yule alikuwa ni mkurugenzi kwenye shirika la wakenya na ni mara chache sana wakenya kumwamini mtz maana nadhani unajua.and ti tje eyes of the public yule jamaa amepiga mzigo tumeona mambo yake kalikuta shirika limekufa kajitahidi kufufua.sasa sababu ya kimsingi au hizo taratibu zilizokiukwa kwenye uteuzi ndio haswa,uma tunataka tuzijue la suvyo kweli imani kwa mkuu itapungua,asije akawa mzuri kukagua wenzake wakiwa jikoni,kumbe nayeye akikaa huko jikoni anaharibu,huo ndio wasiwasi wangu.
 
Umesema jambo la msingi sana. Let Mwakyembe tell Tanzanians Kama aliyetenguliwa uteuzi kuna justification in law and employment rules ya kufanya hivyo. Vinginevyo haitakubalika wa wasifu alio nao Mwakyembe. Ataeleweka vibaya sana tena sana na Bunge tutaliomba limwajibishe kama wenzake!!!

Tatizo lililopo hapa ni uandishi wa press release iliyomuondoa Chizi na wenzake kwani haikuwa wazi. La kujiuliza ni je mwandishi wa press release ile aliwachukulia wananchi ni "wadanganyika" kwa lengo la kutimiza ajenda yake? Au alificha taarifa nyingine kwa lengo la kutoa fursa za uchunguzi zaidi? La kuzingatia ni KWANINI AKINA CHIZI WALIONDOLEWA.
 
Hao wanaolalamika fukuza isije ikiwa kama jairo,safisa wapo watenda kazi kibao mtaani wanazagaa
 
Hayajui adha tunayopata tukiulizwa huku ughaibuni. Mfano, unaulizwa unatokea wapi? Najibu: Tanzania, swali lingine: Mna kampuni gani ya ndege? hapo ndiyo unaanza kuchukia uwepo wako pale, najibu: Aaahh eeeeeh mara ooooh, tunashirikiana na Kenya airways, mara Precision kumbe nako ni wizi mtupu hakafiki popote zaidi ya kuwapelekea abiria Kenyaairways. Ujanja ujanja mwingi kila kona nchi hii.

.......ha ha haaaaaa,mkuu,umenichekesha
 
Huu ndio upuuzi unaoifanya nchi hii kubakia maskini. Rubani kazi yake ni kuendesha ndege, kuongoza shirika la ndege lazima uwe umebobea katika STRATEGIC Management na sio urubani. Paul Chizi alikuwa boss wa JETLINK, shirika la waKenya, kwa wakenya kumpa uboss mtanzania hawezi kamwe kuwa mbabaishaji, hata kidogo kwa vile kule kuna ushindani sana. Waziri Nundu alimuomba aache kazi kule aje kuokoa jahazi nchini kwake, nyie mnataka afanyiwe interview wakati credentials zake ziko clear!? Kwa muda mchache aliokaa amefanikiwa kuleta ndege ambayo ndo most competent kwenye soko la afrika masharika. Boeing 737-500 inabeba watu 108 na inatumia saa moja kamili DAR to Mwanza kwenye abiria wengi. Iko very efficient kwenye fuel. Precision wana boeing yao inabeba abiria 137 lakini mara nyingi haijai na inakula mafuta zaidi pia inatumia saa moja na dk 10 Dar to Mza. Fly 540 wanatumia Jet inabeba abiria 54 tu ingawa iko fuel efficient kama hii ya ATC lakini inatumia saa moja na dk 15 Dar to Mza. Kama umeenda kidogo shule calculate COMPETITIVE ADVANTAGE hapo then utaona kwa nini hata bei Bw Chizi aliweka chini kuliko bei za hao wengine. Jamaa wa mashirika binafsi huyu jamaa aliwanyima usingizi kabisa. Sisi tunaotumia huu usafiri mara nyingi tumehuzunishwa sana na kuondolewa kwa huyu jembe kwa alitupa bei ya ukombozi na ndege inakuwa full wiki nzima toka imefika. Labda kaondolewa kwa kuwa yuko KAMBI YA LOWASSA!!!!

Mkuu mi si mtaalam wa hayo mambo lakini kama huu ndo ukweli Mwakyembe kakurupuka.Labda bado hajapona vizuri ndo maana anakurupuka.
 
WAZIRI MWEKYEMBE mtu mbaya hapo ni Katibu mkuu wa wizara hiyo nashangaa bado unamkumbatia hivi kweli na wewe hujui matatizo ya ATCL kuwa pamoja na mambo mengine kitu kinachoimaliza atcl 10%.Wizara hiyo ili ibadilike Hakuna budi kumpumzicha katibu mkuu.Hivi serikali haioni kuna nini pale bw Chiza sina uhakika ila alizibiti kwa kiasi pesa kutoka bila maelezo,sasa hilo nalo kwa katibu mkuu hakulipenda maana yeye ni mpenda pesa .haya ni mwaono wangu Kama kweli tunataka atcl isimame watendaji wakuu wizarani nao wabadilishwe kwani ni lazima wakae pale
 
Kweli tupu!

Back
Top Bottom