Mwakilishi wa CCM azomewa kwenye kongamano

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2] Mwakilishi wa CCM azomewa kwenye kongamano [/h] Jumatatu, Septemba 03, 2012 05:27 Na Arodia Peter

MWAKILISHI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Godwin Kunambi, juzi alipata wakati mgumu wakati alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu msimamo wa chama chake kuhusu Katiba mpya.

Tukio hilo lilitokea jijini Dar es Salaam wakati wa mjadala wa Katiba mpya ulioandaliwa na Jukwaa la Katiba.

Kabla Kunambi hajazomewa, alianza kwa kueleza msimamo wa chama chake na kusema ni mambo gani yanayotakiwa kuendelea kuwamo katika Katiba mpya inayoandaliwa.

“Sisi kama chama, tunaona tuendelee kuheshimu misingi ya kikatiba kwa maana ya mihimili mitatu ya dola, umuhimu wa kuendelea kuwa na muungano wa Serikali mbili na zaidi misingi mikuu kama vile ardhi kuendelea kuwa mikononi mwa miliki ya Serikali,”alisema Kunambi.

Wakati akiendelea kusema hayo na mengine, ukumbi mzima ulilipuka na kukatiza hotuba yake huku baadhi ya washiriki wakimzomea na kumtaka akae chini.

Wakati wa tukio hilo, Kibamba alipata wakati mgumu kuwatuliza, lakini waliendelea kupiga makofi mfululizo na kufanya yale aliyokuwa akiyazungumza yasisikike kabisa.

Awali, Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar, Profesa Abdul Sharif, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, matatizo yake hayatokani na wananchi wa pande mbili, isipokuwa ni mfumo ulioasisi muungano huo.

Alisema kwamba, muungano uliopo, uliharibiwa tangu mwanzo na waasisi wa wake kwa kuwa hakuna chombo chochote cha kisheria visiwani humo kilichoridhia muungano huo.

“Katika hili Zanzibar ilipunjwa zaidi kwa sababu hakuna chombo chochote cha kisheria kilichoridhia uhalali wa muungano huo, hakuna tangazo lolote lililotolewa katika Gazeti la Serikali kuarifu umma kuhusu maridhiano ya Muungano huo, mambo yote yalikwenda kienyeji na hii ndiyo sababu nchi zingine kama Zambia ambazo awali zilitaka kuungana nasi zilisita kufanya hivyo,”alisema Profesa Sharrif.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, alisema wataendelea kuongoza Watanzania kufuatilia hatua kwa hatua kwa umakini mkubwa ili ipatikane Katiba nzuri zaidi katika historia ya Tanzania.

Hamida Issa kutoka Biharamulo, Kagera alisema, Katiba mpya ijayo inatakiwa kutamka wabunge wa Viti Maalum wanapaswa kuwajibika kwa wanawake wote na si vyama vyao kama ilivyo sasa.

Naye Adam ole Mwarabu, ambaye amejitambulisha kuwa mwakilishi wa jamii ya wafugaji, alisema Katiba ijayo inapaswa kutambua sehemu ya mila, desturi, tamaduni na ujuzi wa asili ili uhifadhiwe na kutambuliwa na katiba hiyo.

Mshiriki mwingine, Martina Kabisama, kutoka Taasisi ya Masuala ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika (SAHRINGON), alisema Tume Huru ya Uchaguzi lazima itamkwe kwenye Katiba.

“Tusipokuwa na Tume huru ya Uchaguzi, haki ya raia inakuwa imeminywa,” alisema.


[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
tatizo la hao wanaopelekwa huko huwa wanajali sana ugali wanyumbani bila ya kujali maslahi ya wabongo.. ndio wa hivyohivyo hao kwa suala la kuzomewa wameshazoea..
 
Alijitambulisha kuwa ni mwanasheria wa CCM,hivi kweli yule ni mwanasheria?mbona anaonyesha ana upeo mdogo sana,mwenye CV yake aidondoshe tuione
 
Ni kazi kweli kuitetea ssm kwa sasa especialy kwenye maeneo yenye watu waelewa, nawaonea huruma sana vijana wenzangu ambao wapo ssm, hawaeleweki hata kama ni wazuri kiasi gani. Kusema kweli ssm inachukiwa sana sehemu kubwa ya nchi hii.
 
Ni kazi kweli kuitetea ssm kwa sasa especialy kwenye maeneo yenye watu waelewa, nawaonea huruma sana vijana wenzangu ambao wapo ssm, hawaeleweki hata kama ni wazuri kiasi gani. Kusema kweli ssm inachukiwa sana sehemu kubwa ya nchi hii.

Kumbe issue ni kuchukiwa na siyo hoja za msingi? teh teh teh, kwa jinsi hii hatufiki.
 
Alijitambulisha kuwa ni mwanasheria wa CCM,hivi kweli yule ni mwanasheria?mbona anaonyesha ana upeo mdogo sana,mwenye CV yake aidondoshe tuione

unashangaa yule kuwa mwanasheria mkuu! je wale waliteuliwa kwenye mahama na sehemu zingine wakati elimu mbovu, ndo washindwe kuwaeka hawa kwenye vyama vyao mkuu, hahaha
 
Ni ujinga kuzomea badala ya kusikiliza hoja na kupinga kwa hoja.

mazuzu ndio huwa yanazomea
 
Alijitambulisha kuwa ni mwanasheria wa CCM,hivi kweli yule ni mwanasheria?mbona anaonyesha ana upeo mdogo sana,mwenye CV yake aidondoshe tuione

LLB alone doesn't make a lawyer, likewise, CPA or ACCA, etc, don't on themselves make an Accountant. One needs more than a mere certificate to shoulder a professional title.
 
mtu mzima umepiga suti yako kali ukamuaga mke wako halafu unaenda kuzomea watu wanaotoa maoni yao,ni ulimbukeni uliopituka mipaka
 
LLB alone doesn't make a lawyer, likewise, CPA or ACCA, etc, don't on themselves make an Accountant. One needs more than a mere certificate to shoulder a professional title.

empty minded like you always argue non sense
 
Ni ujinga kuzomea badala ya kusikiliza hoja na kupinga kwa hoja. mazuzu ndio huwa yanazomea
Wee nawe upo katika dunia gani, hivi kuna mtu yeyote wa CCM anayeweza kujenga hoja ya maana? Ikiwa huyo raisi wenu hajui nini sababu ya umaskini wa nchi na wananchi wake, nani mwingine anayeweza kuongea kitu cha maana?. Kwa ujumla ndani ya CCM hakuna jambo la maana la kuwaambia wenye akili timamu wakakuelewa.
 
Ni ujinga kuzomea badala ya kusikiliza hoja na kupinga kwa hoja.

mazuzu ndio huwa yanazomea
ukiona hivyo hakuwa na hoja kwa nini wengine wasikilizwe yeye azomewe,kinyume chake yeye ndo alikuwa zuzu,anazomewa halafu anaendelea kuongea we unaona akili ya kawaida hiyo?
 
Ni ujinga kuzomea badala ya kusikiliza hoja na kupinga kwa hoja.

mazuzu ndio huwa yanazomea


Inauma eeh?
Kama sio wewe uliyezomewa basi aliyezomewa ni nduguyo.......liwalo na liwe tutawazomea mpaka mkome!
 
Kumbe issue ni kuchukiwa na siyo hoja za msingi? teh teh teh, kwa jinsi hii hatufiki.
Miaka 50 ya Uhuru hatujafika popote pamoja na rasilamli tele tulizonazo, fedha yetu inaengelea kushuka thamani, wazungu wanakuja kuchimba madini yetu halafu wanatuachia mrahaba asilima 3! Waarabu wanakuja kutorosha twiga wetu wazimawazima !
Watu wanakwapua fedha BOT wanakiri kosa Mwenyekiti wa ssm anawasamehe na kuwaambia warudishe fedha walizokwiba! tutafika kweli?
Ndio maana ssm haipendwi hata wakija na hoja gani watazomewa tuu,
Na haya mauaji yanayofanyika sasa, ssm itaendelea kuchukiwa sana.
nawashangaa na kuwaonea huruma vijana wote wanaoshabikia ssm,
jana nilikuwa natoka church kimara kulikuwa na kikao cha uvccm pale kimara mwisho kuna kijana akawa amepiga shati lake la kijani akapita sokoni wachuuzi wakaanza kumzomea kijana wa watu kisa kapiga nguo za ssm.
Ni ukweli uliodhahiri watu wengi hawaipendi ssm ukiwauliza kwa nini wengine hawana majibu ya ndani sanasana watakuambia ssm ni mafisadi .
 
Kumbe issue ni kuchukiwa na siyo hoja za msingi? teh teh teh, kwa jinsi hii hatufiki.

Hici ccm inaweza kweli kuwa na hoja za msingi? Hoja zipi hizo zinazoweza kuifikisha nchi hapa ilipo? hata maoni aliyoyatoa ni matope matupu. Muungano wa serikali mbili ni muungano wa aina gani? Muungano wa kweli ni Muungano wa serikali moja ama serikali tatu tu. Wanajiumauma tu hawana jipya mafisadi wakubwa.
 
Back
Top Bottom