Mwakilishi SSRA apewa vidonge ndani Geita Goldmine Ltd

Nilimsikia akihojiwa sijui ndo mkurugenzi wa SSRA anaitwa Irene ... alikuwa jana clouds... kwa kweli nilichefuka sana... wanaonekana wamepewa jukumu la kuhakikisha huu uchafu unafanikiwa!!! Eti anasema kama asilimia 90 ya mshahara umeshindwa kuifanyia maendeleo hiyo 10 pia hutaweza kuifanyia chochote. Kwa kweli nilitamani nitoboe radio nikamkwide!!! kwanza sio 90% maana hapo kuna payee... mshahara unapokea kila mwezi na sio makusanyo kama ilivyo kwa hizo akiba zetu wanazotaka kutuibia...!!

Hili li Irine Isaka halina akili hata punje. Alihenya kuisomea hiyo PhD kwa kupigwa miti mingi na sijui kama aliimaliza au vipi? Kichwani kweupe, taasisi ile kubwa inamshinda. Imagine anafanya consultation kwa vitu ambavyo yeye kama kiongozi wa mamlaka zote za Social security angewapa mwanga. She can not think beyond horizon. Matokeo yake anadharauliwa sana na some senior leaders wa pension funds. Hana lolote ni kimeo tu.
 
Anawadanganya nini hapo? Mbona hakuja kuchukua maoni kabla hiyo sheria haijatungwa? Nionavyo mimi wabunge wetu too selfish, wanapitishaje sheria gandamizi kama hii halafu wanakuja na propaganda zao maisha bora kwa kila mtz? Are they serious? Mungu nisaidie niondoke nchi hii bora nikawe mkimbizi rwanda
 
Nipo hapa ukumbi wa mgodi wa GGM yupo mwakilishi toka SSRA anayejulikana kwa jina Ngowi anajribu kutoa ufafanuzi wa sheria kandamizi ya SSRA lakini watu hawamwelewi hali ni tete wafanyakazi wanadai hawakushirikishwa uzalishaji umesimama ...nitwapa updates

Sheria ni nzuri ila sema walitakiwa kuwaelimisha wafanyakazi. Mimi binafsi naipenda
 
mjumbe auwawi. tusimamishe kazi zote tulilekebishe hili kwanza. Duu inauma sana hasa kwa sisi vijana. HAIWEZEKANI LIWALO NA LIWE.
 
inauma sna,ila wakulaumiwa ni wabunge waliotnga&kuptisha sheria,kwni wao hawaguswi kbsa,coz aftr 5yr wanapewa mafao yao
 
Jamani inabidi wafanykazi wote tuandamane kuelekea ofisi za SSRA wakatuambie huu utumbo wameupta wapi?
 
Mwalimu Nyerere alipata kusema hivi "mtu mwenye akili, akikuambia jambo la kipumbavu, nawe ukatoka hapo ukimuamini na kuchekelea kama zuzu, basi ujue atakudharau"

Tukiendelea kucheka cheka na upuuzi huu, basi tumekwisha... Solidarity forever now than ever!!
 
Wabunge wametuangusha expecialy wa ccm.Rais nae kapigilia msumali wa moto kwa kusaini sheria mbovu kama hii.haka kasheria ni kandamizi sana.hv walio pitisha sheria kama hii waliangalia upande wa pili wa sh kweli??khaaa
 
Wewe kama ni gamba shauri zako tutakupasha na wewe huko huko, unatetea chama cha mabwepande ili iweje. Walioahidi maisha bora kwa kila mtanzania ni akina nani tena eti kwa kasi zaidi, Hari zaidi na nguvu zaidi. Hii ndo kasi yenyewe, hata uitete vipi CCM imo ndani kwa 100% na hili haliiiachi ng'o hata kwa dawa. Wao kazi ni kugonga meza tu.....!!

acha mawazo mgando jaribu kuruhusu ubongo wako japo ufikiri kidogo siyo kila jambo magamba kwani wote waliopo PPF, NSSF nk ni magamba? chamsingi wafanyakazi wote kuungana ili kutetea maslahi yetu
 
jamani kila kitu si kusingizia ccm cha msingi wafanyakazi wote tuunganishe nguvu bila kujali itikadi za vyama, maslahi yetu hayategemei itikadi bali umoja wetu

Sawa mkuu/ Umoja huo utaupataje kama ccm tayari wamewagawa watu katika mafungu ya "wenzetu" na "wapinzani"? Huoni kinachoendelea bungeni kwa mfano?
 
acha mawazo mgando jaribu kuruhusu ubongo wako japo ufikiri kidogo siyo kila jambo magamba kwani wote waliopo PPF, NSSF nk ni magamba? chamsingi wafanyakazi wote kuungana ili kutetea maslahi yetu

Nafikiri bongo lako lina matatizo ya kuelewa, bila shaka limekandamizwa na gamba zito kiasi kikubwa...........

Have ever thought beyond your thoughts?
 
VERY STUPID DECISION!
Nalipa PAYE almost 40% ya mshahara wangu, uliobaki nalipia kodi tena kwa kila ninachonunua 18%! Nakatwa NSSF 10%, mwajiri wangu ananibana kunipa mshahara mkubwa akidai anatoa 10% kunilipia NSSF. ina maana zaidi ya nusu ya kipato changu kinarudi serikalini kwa ajili ya kodi na PAYE..... wadau mnalijua hilo?

maskini huyu mie nimefanya kazi karibu 14 years, na mchango wangu sasa ni zaidi ya 70M! hata utaratibu wa sasa hususani NSSF kwamba ukifika 15 years ya kazi, unakuwa pensinabo! hata ukiacha kazi na umefikisha miaka hiyo 55, unalipwa robo, ingine unaanza kulipwa kidogo kidogo kwa mwezi sooo kigodo huku wakiombea ufe! then that is the end!
life span ni ndogo so mabilion ya pesa yamekuwa yakiachwa hata kwa utaratibu uliopo juzi! sasa wakaona hizo zinazobaki hazitoshi badala yake wanataka watu wafe wengi na zibaki zaidi... ndio lengo la SSRA na serikali yake ambayo niliitiii hadi juzi nilipochoma kadi ya CCM! kwa mara ya kwanza nimewaelewa wa Tunisia/Libya/Egypty.

Mama huyu wa SSRA anatuambia eri unakatwa 10% tu na kama maendeleoa ungefanya na hio 90% (kasema Jahazi) eti hio 10% itakusaidia nini! what the hell is this?

nilitaka niache sawa kazi za mwajiri wangu ili nichukue mtaji nijianzishie ujasiliamali na niajiri wa Tz wenzangu wapo mtaani, sasa wanakuja na uchawi huu.

siamnini kama wabunge walijadili, watu kwa sasa tunafuatilia sana n bunge, iweje hii ipite hivi hivi? ona maoni ya watu hapo juu, nenda jamii forum.. ina maana hatukuona haya yote, walichojadili ni kinachofanana tu wala sio direct la kusitisha mchango wa kujitoa. au vile wabunge mafao yao hupokea baada ya miaka 5 hawayaoni haya?

If wabunge wetu walijadili na kulielewa hili, basi wanastahili tuanze kwa kuwapiga mawe! ndio
tumechoka na vitu kama hivi ambavyo vinahitaji kufikia kwa kichwa chepesi.

nina hasira sana

mdau
Nokoyani
 
1. Wabunge wote ni wasaliti kwenye hili. Iweje wao sheria isiwahusu, hiyo ni rushwa ya kupitisha sheria.
2. Wafanyakazi wote lazima tuungane kwenye hili, kama mgaya anaogopa mabwepande sisi tuko tayari kwenda huko. Hapa hakuna siasa, hapa kuna uhai.

Kabisa SSRA wamewapa wabunge rushwa hiyo ili wapitishe hyo sheria jambazi,kwani ingekuwa na wabunge mafao yao wanayazuia wasingeipitisha kamwe!
 
Back
Top Bottom