Mwakilishi jimbo la Bububu afariki dunia

Wanabodi.
Muwakilishi wa Jimbo la Bugubu, Salumu Mtondoo, amefariki dunia leo mjini Zanzibar.

SOURCE; TBC HABARI.
 
mzee soma thread zilizopita kabla ya kuleta *****. Uzi huu umekuja asubuhi na umejadiliwa kama kurasa zaidi ya nne
 
Mwakilishi Zanzibar afariki


na Mauwa Mohammed, Zanzibar

MWAKILISHI wa jimbo la Bububu kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Salum Amour Mtondoo, amefariki katika hospitali ya Rufaa Mnazimoja, mjini Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, ilisema marehemu amefariki majira ya saa 4.30 asubuhi ya jana katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

Kificho alisema marehemu mtondoo amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi ambapo alilazwa katika Hospitali ya Mnazimmoja tangu Jumatatu baada ya kuugua ugonjwa wa kisukari.

Kificho alisema baada ya marehemu kupelekwa hospitali aligundulika kuwa kiwango cha sukari kilifikia 180 na presha ilikuwa imepanda sana, ambapo awali aliwekwa katika wodi ya Mapinduzi Mpya kabla ya kuhamishwa katika wodi ya Mapinduzi Kongwe hadi juzi alipozidiwa na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hadi kifo chake.

Mara baada ya kufariki mwili wa marehemu Mtondoo ulipelekwa katika jengo la Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya heshima ya mwisho mbele ya wajumbe wa baraza hilo.

Marehemu ambaye ameacha wake watatu na watoto 12 atazikwa leo nyumbani kwake Bububu.
 
kwa taarifa ya tbc mchana huu ni kwamba tayari mazishi yamefanyika na wameonyesha watu wakiwa makaburini kumsitiri ndugu yetu huyo.mungu aiweke pema roho yake.ameen
 
Mbona wewe umeandika na haikufutwa?Tuhuma zingine ni ishara ya kutojiamini
 
[h=3]Mazishi Ya Mwakilishi Jimbo La Bububu Zanzibar Yafanyika[/h]



Zanzibar Na Marzuk Khamis Maelezo Zanzibar Mamia ya Wananchi wa Zanzibar wanatarajiwa kushiriki katika mazishi ya aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la BUBUBU Marehemu Salum Amour Mtondoo aliefariki Dunia katika Hospitali mkuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kichwa. Kwa mujibu ya ratiba ya shughuli za Mazishi iliotolewa na Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar imeeleza kuwa mnamo sasa tatu za asubuhi maiti ya Marehemu itaondoka Mijini kuelekea Bumbwini Kijijuini kwao kwa kusaliwa na baadae kuzikwa. Katika Mazishi hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud atasoma risala na baadae Baraza la Wawakilishi Zanzibar itatoa risala yake itakayosomwa na Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho na baadae Familia ya Marehemu Salum Amour Mtondoo itatowa tamko la shukrani. Tangu Uchaguzi Mkuu Kumalizika wa Mwaka 2010 huyu atakuwa Mwakilisdhi wa pili kufariki Dunia ambapo Mwakilishi wa kwanza kufariki ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini ambae pia alikuwa Mbunge aliechaguliwa na Baraza la Wawakilishi Marehemu Mussa Khamis Silima wote hao wawaili ni kutoka chama cha Mapinduzi.
 
Huyo alikuwa anawakilisha znz pekee nadhani.
Hata hivyo wawakilishi wanawakilisha eneo linalolingana na kata tu huku petu.
Namtakia kila la heri katika safari yake mpya aliyoianza.
 
Back
Top Bottom