Mwakalebela aigaragaza Takukuru mahakamani

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mwakalebela aigaragaza Takukuru mahakamani Send to a friend Friday, 25 February 2011 21:22

Tumaini Msowoya, Iringa
KESI ya pili ya kupokea rushwa kwenye mchakato wa kura ya maoni ndani ya CCM iliyokuwa ikimkabili Frederick Mwakalebela (41), imeondolewa mahakamani na mshtakiwa kuachiwa huru.

Kuondolewa kwa kesi hiyo kunafuatia pingamizi la awali lililowekwa na wakili wa Mwakalebela, Basil Mkwata.

Mwakalebela alikuwa mshindi wa kwanza kura za maoni za CCM nafasi ya ubunge wa Iringa Mjini mwaka jana, lakini jina lake liliondolewa na nafasi yake kupewa Monica Mbega, ambaye alishindwa na mpinzani wake, Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Mkwata, uliwasilisha pingimizi la awali la kisheria ukiomba kesi hiyo iondolewe mahakamani kutokana na upungufu wa kisheria uliofanywa na upande wa mashtaka, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (Takukuru).

Upungufu huo ni mtuhumiwa kushtakiwa kwa kutumia sheria mbili tofauti kwenye hati moja ya mashtaka, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Akiondoa shauri hilo mahakamani, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Festo Lwila, aliyekuwa anasikiliza shauri hilo alisema mahakama imeridhia pingamizi hilo.

Hakimu Lwila alisema mshtakiwa alishtakiwa kwa kutumia sheria mbili tofauti kwenye hati moja ya mashtaka, suala ambalo ni kinyume cha sheria na kinaweza kumsababisha ashindwe kuandaa utetezi wake ipasavyo.

Pia, Lwila alisema hapakuwa na sababu ya kuweka sheria mbili tofauti kwenye hati moja na kwamba, usahihi wa hati ya mashtaka unapaswa kuwa makini tangu awali inapoandaliwa, tofauti na hivyo ndio umemfanya Mwakalebela kuwa huru.

“Kutokana na sababu hii, mshtakiwa anakuwa huru na upande wa mashtaka mna hiari ya kuleta tena kesi hii ikiwa haina 'duplicate',” alisema.

Katika pingamizi hilo, Mkwata alisema tayari mshtakiwa ameshaadhibiwa baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kumwengua kwenye uchaguzi, hivyo kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani.

Awali, akisoma shtaka hilo Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Imani Mizizi, alidai kuwa Juni 20, mwaka jana, Mwakalebela alidaiwa kutoa hongo ya Sh100,000 kwa Hamis Luhanga ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkoga, ili awagawie wajumbe 30 wa CCM walioitwa kwenye kikao.

Mizizi alidai kuwa, Mwakalebela anadaiwa kutoa rushwa kinyume cha sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15(1)(b) kinachokwenda sambamba na sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010, kifungu cha 21 (1) (a) na kifungu cha 24(8).

Pia, Mahakama ya Mkoa wa Iringa Jumatatu ijayo inatarajia kutoa uamuzi iwapo kesi ya kwanza inayomkabili Mwakalebela (41) na mkewe Selina, iendelee kusikilizwa au iondolewe.

 
PHP:
Katika pingamizi hilo, Mkwata alisema tayari mshtakiwa ameshaadhibiwa baada ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kumwengua kwenye uchaguzi, hivyo kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani.
Hivi NEC ya CCM tangia lini kikawa chombo cha utoaji haki ambacho kinaweza maamuzi yake kuheshimiwa mahakamani?

Hoja ya huyu Mwanasheria wa Mwakalebela inamweka mteja wake pabaya.....................kwa sababu kinamna namna anakiri makosa pale anaposema tayari CCM ilikwisha kumwadhibu kwa makosa haya na hawezi kuadhibiwa mara mbili..................................huwezi kumwadhibu mtu asiye na kosa na hapo mahakamani yalikuwa ni makosa ya kijinai ambayo CCM haina uwezo nayo.............na sababu za CCM kuliondoa jina laki siyo kwa sababu ilimtia hatiani kwa makosa ya jinai ila kwa sababu alikuwa ana kesi Mahakamani..........................

Some lawyers leaves a lot to be desired...........................................
 
Huyo mwanasheria wa mwakalebela kweli ametoa a very weak argument! eti mwakalebela alishaadhibiwa na chama chake! Kwa hiyo mahakama na chama do work in parallel? Shame
 
TAKUKURU yamng'ang'ania Mwakalebela


na Francis Godwin, Iringa


amka2.gif
SIKU moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, katika shitaka lake la rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Iringa Mjini, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa imekusudia kuendelea na kesi hiyo.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mwanasheria wa TAKUKURU mkoani hapa, Ntimu Mizizi, alisema maamuzi ya mahakama hiyo chini ya Hakimu Festo Lwila ameyakubali na kuwa mapungufu yaliyokuwemo awali katika kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2010, taasisi hiyo inayafanyia kazi na kufungua kesi yenye maelekezo ya mahakama.
Alisema maamuzi ya mahakama katika kesi hiyo yameonekana ni mazuri na yenye maelekezo ya kina zaidi kuliko ilivyokuwa kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Joseph Mungai, ambapo mahakama haikuingia kiundani zaidi kama ilivyo katika maamuzi madogo ya kesi ya Mwakalebela.
Alisema kesho kutakuwa na majibu sahihi dhidi ya uamuzi wa TAKUKURU kuendelea na kesi hiyo ama la.
Mahakama hiyo chini ya Hakimu Lwila ambaye alikuwa anasikiliza shauri hilo, aliiondoa kesi hiyo na kumwachia huru mtuhumiwa huyo baada ya kuridhika na hoja moja ya upande wa utetezi kwamba kulikuwa na mapungufu ya kisheria kwenye hati ya mashitaka.
Mapungufu hayo ni mtuhumiwa kushitakiwa kwa makosa mawili kwenye hati moja ya mashitaka, hivyo kumfanya mtuhumiwa ashindwe kuelewa kwa usahihi kosa linalomkabili, kitu ambacho kinaweza kumfanya ashindwe kuandaa utetezi wake.
Aidha, Mwakalebela kesho ataendelea na kesi nyingine namba 8 ya mwaka 2010 ambayo inamkabili yeye pamoja na mkewe, Selina, ambayo ipo hatua ya kutolea hukumu pingamizi la kisheria iwapo iondolewe mahakamani au la.
 
Toka mwanzo wenye macho tulijua kuwa ile ni janja ya JK kuwadhibiti watu waliokuwa tishio kwake!
 
Back
Top Bottom