Mwaka wa kwanza,Kituko cha kwanza...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ni kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo. Naingia kukata tiketi ya Arusha. Nimeshaipata. Sasa wakati natoka nje,nawakuta madereva wa taksi na bajaji wanawazonga vijana wawili:mmoja msichana,mmoja mvulana. Nikasogea kuona na kusikia. Walikuwa wanazongwa ili wapande kwenye ima bajaji au taksi ili wapelekwe UDSM kwakuwa ndio wamefika kama wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Kwa uzalendo wangu kama mwana-UD wa zamani nikaingilia kati na kuinunua kesi. Nikawasogeza pembeni wanafunzi wale. Wakaniarifu mengi. Kubwa ni kwamba wanataka kufika UDSM. Wamebeba unga,mchele,maharage,mafuta ya kupikia na mafuta ya taa. Wa kike amebeba na sufuria na baadhi ya vyombo vya chakula. Si mchezo!

Sasa kituko: wakaniarifu kuwa wao ni ndugu wanaotokea Bukoba. Wakasema kuwa wameambiwa nyumbani kuwa wakae chumba kimoja ili kupunguza gharama. Wahakikishe inakuwa hivyo. Ni lazima. Itawezekanaje ikiwa UDSM kuna hosteli za kike na za kiume? Mwisho mwishoni,nikawachukua garini mwangu hadi UDSM. Nimewashusha stendi ya Utawala.Nikawauliza:mnahitaji msaada wowote mwingine? Wakajibu:'hapana kaka.Hapa tumeshafika.Asante sana'. Kazi ipo...
 
Naona umekutana na kina nshomile! Haya bwana. Ukimtafuta baada ya wiki tatu atakukana kabisa kwamba hajawahi kutana nawe.
 
Mi nilifikiri haya mambo kwa miaka hii yameisha, kumbe bado yapo!, kuna haja ya wageni wa maeneo mbali mbali nchini kupata taharifa ya mahala uendapo mapema, vinginevyo utaingia kwenye mitego ya matapeli.
 
dah isee......

Nimependa kuona kuna watu wachache wenye moyo kama wako, maana miaka hii mambo yalivyoharibika watu wanaogopa kusaidia mtu wasomjua
 
Duuuuuh! Hiyo kweli vuta nikuvute........ Wameambiwa wakae chumba kimoja....... Akili za mbayu wayu changanya na zako.... Otherwise, labda huko walikotoka walikua wanaishi chumba kimoja pia! Watakua wanamaanisha wanachotaka fanya..... Ila kwa mm waishi chumba kimoja hata km hostels wangewaruhusu haiwezi ingia akilini..... Yaani wao hawataki kbs kupigwa EXILE kbs?
 
aisee hawakua na nsenene kweli.ungewapiga picha kabisa then unaomba contacts zao baada ya mwezi unawatafuta
 
Back
Top Bottom