Mwaka mpya wa 2012: Tuimarishe ndoa zetu…

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Katika thread mbali mbali ambazo tumechambua mwaka huu wa 2011, binafsi nimefarijika na kufaidi michango ya wadau kuhusu taasis ya ndoa. Ndoa ni taasisi ni muhimu sana na kila mmoja wetu analo jukumu la kulinda ndoa yake na pia kutoa support kwa ndoa za marafiki zake. Ili ndoa idumu, kuna vitu ambavyo ni muhimu sana kuvipa kipaumbele. Hivi ni pamoja na,

1. Upendo….Ni muhimu kuonesha kwa maneno na vitendo kuwa unampenda mwenzio na kumthamini. In short, mke au mme anatakiwa awe nambari one siku zote…
…Kwenye hili suala huwa sitaki utani…my wife is always nambari one and I can give anything including my life to protect her!!

2. Heshima na uvumilivu…Bila kuyaonesha haya kwa vitendo lazima ndoa itayumba

3. Kujitoa (sacrifice)…Kama hauko tayari kujitoa kwa ajili ya mwenzi wako ni bora ubaki single au ukapursue line nyingine za maisha ikiwemo utowashi!!

4. Uaminifu….Hapa ni pagumu sana ila ni eneo nyeti…Ukishindwa basi tumia kanuni ambazo wadau walileta na kujadili hapa….Cheating should be avoided but doing it responsively ni sehemu ya uungwana kwenye ndoa

5. Consensus .. ni muhimu sana kukubaliana katika vitu vya msingi na kutekeleza hayo makubaliano kwa vitendo! Kuacha kila mtu afanye mambo yake kwenye ndoa ni sawa na kuwa na jeshi lisilo na kamanda…Lazima litasambaratika tu!

Yapo mambo mengine mengi na wadau wanaweza kuyaongeza. Hata hivyo kuna changamoto nyingi ambazo zimejitokeza hivi karibuni na wadau wanatakiwa kupambana nazo.

1. Uzoefu wa wanandoa unaotokana na kuwa na mahusiano ya ki-ngono kabla ya ndoa…
……Enzi zile watu walikuwa wanakutana wakiwa mabikra…hawakuwa na kitu chochote cha kufanyia reference. Je tunafanyaje kudeal na historia zetu za nyuma katika ndoa zetu ili zisituyumbishe?

2. Watoto waliopatikana kabla ya ndoa….Hili ni gumu sana especially kwa wanawake kuliko kwa wanume….Linachangiaje ku-destabilize ndoa??...Naomba michango ya wadau!!

3. Tofauti ya kipato…Hili ni janga jingine especially mwanamke anapokuwa na uwezo zaidi ya mwanamume. Hapa couples zinatakiwa kukubaliana jinsi ya kuhandle mambo ya pesa!

4. Infidenlity inayopata support ya technology mpya….Siku hizi ni rahisi sana kukutana na watu wapya na kuweka mambo sawa bila hata kutakiwa kusafiri…!! Wanandoa wanatakiwa kukwepa haya mambo ili kutowaumiza wenzi wao!

Naamini kuwa, tunatakiwa kuelewa kwamba kuna mabadiliko makubwa yaliyotokea hivi karibuni na hivyo tuchukue hatua mathubuti ili kuimarisha ndoa zetu,

Nawatakia heri ya mwaka mpya wa 2012!!

Babu DC (1947)
 
Cheat responsibly!!AAAMEN!!

Lizzy,

Tumejadili sana hili suala na watu wanakubaliana kuwa ni janga katika ndoa. Kuna watu hawawezi kuacha....

Hata wazee wetu walikuwa wanacheat sana ila walifanya hayo mambo kwa kwa heshima sana na ndiyo maana ndoa zao zilidumu sana.

Kwa hiyo, binafsi nitaendelea kuwa na imani na mke wangu na kumpenda sana, kama akiamua kucheat atahakikisha ananitunzia heshima yangu!!

Babu DC!!
 
Babu DC
asante kwa thread nzuri na pia kuombea mafanikio mema kwa walio kwenye ndoa
na wanaojianda kuingia kwenye ndoa kufwata mawaidha ya babu DC
Kuhusu swala la watto waliozaliwa kabla ya ndoa inaonekana kuwa kero kwa wanandoa
naona inatokana na mmojawapo kushindwa kukubali lililotokea
kuna jirani yangu kaka yake ameletewa mtoto aliyemzaa kabla ya ndoa kisa mkewe
amemkataa hataki kumwona kabisa amefanya kila vitimbi mpaka mtoto anatamani kijiua
lakini cha kushangaza huyo mama kabla ya kuolewa alikuwa na mtoto na huyo baba
alimpokea mtoto na kumlea kama wake kila alichohitaji alikipata sasa watu wanajiuliza
imekuwaje hataki mtoto aliyezaliwa na mumewe?! inasikitisha na ndoa ipo mashakana
maana kwa sasa huyo baba analewa sana hata hamu ya kurudi nyumbani kwa mkewe anaona taabu
anampiga simu kwa mdogo wake kila siku mtu mzima analia kwa kuona mwanae anateseka
ni wachache wanaokubali kulea mtoto aisiye wake
 
ila ume2sahau babu ss ambao bado 2po 2po, jaman nasi tuimarishe mahusiano ye2. 2zingatie ishu izo hapo juu.
 
ila ume2sahau babu ss ambao bado 2po 2po, jaman nasi tuimarishe mahusiano ye2. 2zingatie ishu izo hapo juu.

Pamoja na mengi ambayo yanawahusu pia, mnajiandaaje kuhandle hii kitu???

Uzoefu wa wanandoa unaotokana na kuwa na mahusiano ya ki-ngono kabla ya ndoa…
……Enzi zile watu walikuwa wanakutana wakiwa mabikra…hawakuwa na kitu chochote cha kufanyia reference. Je tunafanyaje kudeal na historia zetu za nyuma katika ndoa zetu ili zisituyumbishe?
 
Lizzy,

Tumejadili sana hili suala na watu wanakubaliana kuwa ni janga katika ndoa. Kuna watu hawawezi kuacha....

Hata wazee wetu walikuwa wanacheat sana ila walifanya hayo mambo kwa kwa heshima sana na ndiyo maana ndoa zao zilidumu sana.

Kwa hiyo, binafsi nitaendelea kuwa na imani na mke wangu na kumpenda sana, kama akiamua kucheat atahakikisha ananitunzia heshima yangu!!

Babu DC!!

Hivi babu heshima ni mkeo (simaanishi bibi) kucheat bila wewe kujua?Kitendo cha mwenzako kuingilia boma lako (hawezi kukuheshimu huyo) sini tayari mkeo hajakutunzia heshima yako? Au wanavyokaaga na kuanza kuelezana "ohh mune wangu zoba tu, hana lolote yule ndio maana nakuja kwako" "ohh mke wangu hana hadhi" ndio heshima inalindika?
Mpaka mtu akacheat hakuheshimu, huyo anaetembea nae hakuheshimu na kama kuna watu wengine wanaofahamu ukweli nao hawakuheshimu vile vile, hivyo sioni heshima inatunzwa vipi hapo.
 
mkuu hivi nyinyi kina Jacob Zuma mnaweza haya???????lol

Hahahahah,

Kaka mwaka huu tuko kikazi zaidi...Tunataka tuwakomboe hawa wajukuu,

Ile mipango yangu ya kuongeza mke wa 11 nimeifuta jana usiku baada ya kusoma ile thread nambari wani ya mwaka 2011 aliyoipeperusha Comrade Mbu!!

Naomba support yako katika haya mapinduzi!!
 
Lizzy na Babu DC wote mna maana moja

Tuimarishe ndoa ... cheat responsibly, love more, give more, achieve more, care more

Heppi Nyu Yia
 
Hivi babu heshima ni mkeo (simaanishi bibi) kucheat bila wewe kujua?Kitendo cha mwenzako kuingilia boma lako (hawezi kukuheshimu huyo) sini tayari mkeo hajakutunzia heshima yako? Au wanavyokaaga na kuanza kuelezana "ohh mune wangu zoba tu, hana lolote yule ndio maana nakuja kwako" "ohh mke wangu hana hadhi" ndio heshima inalindika?
Mpaka mtu akacheat hakuheshimu, huyo anaetembea nae hakuheshimu na kama kuna watu wengine wanaofahamu ukweli nao hawakuheshimu vile vile, hivyo sioni heshima inatunzwa vipi hapo.

Lizzy,

Katika maisha huwezi kukwepa point ambapo unatakiwa kuchague the best devil....Kwangu mimi that is the best...Kama ameamua kufanya ...basi nisijue....

That needs a big investment na naamini bado ananiheshimu...kwani si angeweza kuzungusha mzigo hata mbele yangu??
 
Lizzy na Babu DC wote mna maana moja

Tuimarishe ndoa ... cheat responsibly, love more, give more, achieve more, care more

Heppi Nyu Yia

Sina cha kuongeza au zawadi ya kukupa,

Happy New Year Bro!!
 
Hahahahah,

Kaka mwaka huu tuko kikazi zaidi...Tunataka tuwakomboe hawa wajukuu,

Ile mipango yangu ya kuongeza mke wa 11 nimeifuta jana usiku baada ya kusoma ile thread nambari wani ya mwaka 2011 aliyoipeperusha Comrade Mbu!!

Naomba support yako katika haya mapinduzi!!

sasa si itabidi uanze na talaka kwanza
mpaka abaki mmoja?au?????lol
 
Lizzy,

Katika maisha huwezi kukwepa point ambapo unatakiwa kuchague the best devil....Kwangu mimi that is the best...Kama ameamua kufanya ...basi nisijue....

That needs a big investment na naamini bado ananiheshimu...kwani si angeweza kuzungusha mzigo hata mbele yangu??
Haya bana. . . .ngoja nitulie mie.
 
Back
Top Bottom