Mwaka huu uwe mwaka wa mabadiliko ya kuona mambo ya maana kwa nchi yanafanyika

habi alex

Member
Dec 1, 2011
90
12
Naomba kutoa hoja kwamba mwaka huu uwe wa mabadiliko yatakayotokana na sisi wanyonge na silaha yetu kubwa ni kuwaumbua viongozi waongo, wababaishaji, wabadhirifu na wabinafsi. Tukiwafahamu kazi yetu iwe moja tu ni zomeazomea kila wapitapo na kuwaonyeshea mabango ya matendo yao. Hali hiyo itawafanya wabadilike na wajirudi wawe zaidi kwa maslahi ya wananchi.

Wewe, mimi, na wote tunaweza kuwa chachu na silaha muhimu ya mabadiliko ya tabia ya viongozi wetu wa umma.

Na tuanze sasa.
 
Back
Top Bottom