Mwafrika wa kike kumuunga Mkono Mheshimiwa Kikwete

Hoyaaaaa....

Ilianza May 7th,

May 14th - Checked
May 21st - Checked
May 28th - Checked
June 04th - Checked

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Kikwete amepata breathng room ya mwezi mzima lakini ameshindwa kufanya chochote kuhusu EPA, Richmond na Buzwagi na mengineyo mengi?!

Kazi inaanza sasa rasmi!

I am sorry JK, this is too much to handle!
 
Hoyaaaaa....

Ilianza May 7th,

May 14th - Checked
May 21st - Checked
May 28th - Checked
June 04th - Checked

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Kikwete amepata breating room ya mwezi mzima lakini ameshindwa kufanya chochote kuhusu EPA, Richmond na Buzwagi?!

Kazi inaanza sasa rasmi!

I am sorry JK, this is too much to handle!

Bado anavuta kasi mpya,nguvu mpya na hali mpya zitakapo anza twaweza kuona makeke yake lakini bado sasa hajapata ile kasi ya kuanza anadai bado hajapata uzoeefu
 
Okay!

Habari kwamba kuna watu wanatoa vitisho huko serikalini kuwa watabomoa serikali ya Kikwete kama akiwashughulikia kwa makosa yao ya ufisadi zimefikia kipimo cha juu kabisa cha uvumilivu. Sina sababu ya kuanzisha mjadala wa kujua kama ni kweli au ni propaganda ingawa mpiganaji mwenzangu Kubenea amehakikisha kuwa hii habari ina ukweli ndani yake.

Ninakumbuka vizuri juhudi za mzee wa kasungura na ndege iliyoishiwa mafuta AKA morani AKA mzee wa tripi AKA zungu la Richmonduli AKA Lowasa alivyojaribu kujisafisha kwa kuwatumia kina Balile na wenzake lakini in the process kulipa kisasi kwa kina Mwakyembe na wenzake (JK?) waliomshushua bungeni.

Nimevisikia kwa makini vitisho vya mzee wa vijisenti na kunywa sumu AKA mzee mpenda mbichi (wanafunzi wa shule) AKA mzee wa kashfa kibao kabisa za wizi na ufisadi Tanzania AKA Chenge na lawyer wake kuwa "watalipiza kisasi" na kuwaumbua wote wale wanaowafuatilia kwenye kesi ya wizi.

Nimevisikia pia vitisho vya Patel, Manji, Rostam, Kagoda, Mramba na wezi wenzao kibao kuwa watahakikisha utawala wa nchi na sheria unakuwa mgumu kwa vile watu wanafuatilia ulaji wao. Kwa yote haya, hili la kumtisha hadi Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali yake limefikia kipimo cha juu. Haijalishi kama Mkapa anahusika au ni Apson na wanausalama wenzake. Katika hili hakuna cha mswalie yeyote.

Nimeamua kumpa Kikwete nafasi ili afanye kweli katika hili. Najua kuwa alinidisapointi Butiama lakini kwa sasa nampa tena nafasi nyingine ya kufanya kweli na kuwa supporter wake kila mara anapowachukulia hatua mafisadi. Nitaacha kumpondea Kikwete kwa mwezi mzima (Kikwete-Bashing-Free posts for a month). Niko nawe mheshimiwa sana raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Ingawa najua bado hujafanya chochote kwenye wito wangu wa kupunguza bei ya nishati Tanzania lakini sasa nakupa nafasi tena ya kutokomeza ufisadi na mafisadi toka kwenye serikali yako. Kwa hili utapata free ride toka kwangu na free media attacks kwa wale maadui zako wote watakaojaribu kuleta propaganda zao hapa JF na kwingine kote ambako kazi zangu zinafika.

kwa mwezi mzima, mwafrika wa kike anamuunga mkono Kikwete katika juhudi zake za kutokomeza ufisadi Tanzania.

Asante.

Are you talking of the same president who previosuly said we have no problems with the money lost in our reserves? The president who have left the culprits walking freely in the Dar Es Salaam streets? the president who is afraid to act? Unless you are a hypocrite, you cannot defend this president, he is a culprit number ONE!
 
Hoyaaaaa....



Kazi inaanza sasa rasmi!


Kazi inaanzia wapi mama?
1) Shule zinafungwa hazina chakula
2) Mfumko wa bei wa bidhaa uko juu
3) Mpaka sasa hakuna kitegauchumi chochote cha kuingizia serikali pato bado ni zile zile za fisadi mkapa
4) Hospitali hazina madawa
5) Njaa ndiyo hiyooo imeinyemelea nchi (Mungu atusaidie)
6) Migomo mashuleni na vyuoni kuongezeka (migomo karibu 10 ktk nusu mwaka huu)
7) Maliasili (gold, diamond, silver, misitu, wanyama etc) bado inasombwa
8) Ajira bado hakuna vijiwe vinazidi kuongezeka (zamani kahawa ilikuwa ya wazee tu lakini siku hizi vijana wamejaa )
9) Barabara hazijengwi (manyoni-tabora-kigoma, iringa-dodoma-arusha)
10) kilimo ndo kabisa
11) Mafisadi bato wanakata mitaa

kwa hiyo timu ya mpira wa miguu kazi inaanzia wapi?
 
Kazi inaanzia wapi mama?
1) Shule zinafungwa hazina chakula
2) Mfumko wa bei wa bidhaa uko juu
3) Mpaka sasa hakuna kitegauchumi chochote cha kuingizia serikali pato bado ni zile zile za fisadi mkapa
4) Hospitali hazina madawa
5) Njaa ndiyo hiyooo imeinyemelea nchi (Mungu atusaidie)
6) Migomo mashuleni na vyuoni kuongezeka (migomo karibu 10 ktk nusu mwaka huu)
7) Maliasili (gold, diamond, silver, misitu, wanyama etc) bado inasombwa
8) Ajira bado hakuna vijiwe vinazidi kuongezeka (zamani kahawa ilikuwa ya wazee tu lakini siku hizi vijana wamejaa )
9) Barabara hazijengwi (manyoni-tabora-kigoma, iringa-dodoma-arusha)
10) kilimo ndo kabisa
11) Mafisadi bato wanakata mitaa

kwa hiyo timu ya mpira wa miguu kazi inaanzia wapi?

kazi imeanza sasa ya kumwekea presha Kikwete na serikali yake hadi kieleweke. Hata akipewa muda naona hafanyi chochote kile anachoahidi kufanya kila mara.
 
Back
Top Bottom