Mwafrika wa kike kumuunga Mkono Mheshimiwa Kikwete

Okay!

Habari kwamba kuna watu wanatoa vitisho huko serikalini kuwa watabomoa serikali ya Kikwete kama akiwashughulikia kwa makosa yao ya ufisadi zimefikia kipimo cha juu kabisa cha uvumilivu. Sina sababu ya kuanzisha mjadala wa kujua kama ni kweli au ni propaganda ingawa mpiganaji mwenzangu Kubenea amehakikisha kuwa hii habari ina ukweli ndani yake.

Ninakumbuka vizuri juhudi za mzee wa kasungura na ndege iliyoishiwa mafuta AKA morani AKA mzee wa tripi AKA zungu la Richmonduli AKA Lowasa alivyojaribu kujisafisha kwa kuwatumia kina Balile na wenzake lakini in the process kulipa kisasi kwa kina Mwakyembe na wenzake (JK?) waliomshushua bungeni.

Nimevisikia kwa makini vitisho vya mzee wa vijisenti na kunywa sumu AKA mzee mpenda mbichi (wanafunzi wa shule) AKA mzee wa kashfa kibao kabisa za wizi na ufisadi Tanzania AKA Chenge na lawyer wake kuwa "watalipiza kisasi" na kuwaumbua wote wale wanaowafuatilia kwenye kesi ya wizi.

Nimevisikia pia vitisho vya Patel, Manji, Rostam, Kagoda, Mramba na wezi wenzao kibao kuwa watahakikisha utawala wa nchi na sheria unakuwa mgumu kwa vile watu wanafuatilia ulaji wao. Kwa yote haya, hili la kumtisha hadi Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali yake limefikia kipimo cha juu. Haijalishi kama Mkapa anahusika au ni Apson na wanausalama wenzake. Katika hili hakuna cha mswalie yeyote.

Nimeamua kumpa Kikwete nafasi ili afanye kweli katika hili. Najua kuwa alinidisapointi Butiama lakini kwa sasa nampa tena nafasi nyingine ya kufanya kweli na kuwa supporter wake kila mara anapowachukulia hatua mafisadi. Nitaacha kumpondea Kikwete kwa mwezi mzima (Kikwete-Bashing-Free posts for a month). Niko nawe mheshimiwa sana raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Ingawa najua bado hujafanya chochote kwenye wito wangu wa kupunguza bei ya nishati Tanzania lakini sasa nakupa nafasi tena ya kutokomeza ufisadi na mafisadi toka kwenye serikali yako. Kwa hili utapata free ride toka kwangu na free media attacks kwa wale maadui zako wote watakaojaribu kuleta propaganda zao hapa JF na kwingine kote ambako kazi zangu zinafika.

kwa mwezi mzima, mwafrika wa kike anamuunga mkono Kikwete katika juhudi zake za kutokomeza ufisadi Tanzania.

Asante.

Mwafrika wa Kike...Ushahidi tafadhali!
 
Mwafrika wa Kike...Ushahidi tafadhali!

Ushahidi wa nini mkuu kati ya haya?

1. Lowasa ameahidi kujisafisha na kulipiza kisasi?
2. Chenge na Lawyer wake wametishia kumwaga mboga?
3. Mafisadi wengine wanatishia wanaowafuatilia?
4. Kwamba sitam-bashi Kikwete for a month?
5. Kwamba Kikwete anapanga kuunda baraza jipya?
 
One must have an incredibly inflated ego to speak of oneself in public in the third person. What's even more confounding is placing one's "name" right next to the leader of a country of 34 million plus people in a most nonchalant manner as if you both shared the same VIP status?! What a disgrace!
Kweli sasa wewe ni Myama Hatari!
Anyways M. wa Kike na yeye pia si ana haki?
Kwani hata yeye hawezi kugombea uraisi akitaka!
Tafadhali elewa kuwa hata kama kuna wakati tunatofautiana kimawazo haina maana kuwa tuna shushana na kudharauliana!
Na ndio maana hata viongozi wetu wanatudharau!
 
jmushi,

Huyu nyama hatari anatafuta sababu nyingine ya kufungiwa kama vile ambavyo amekuwa anakuja na majina kibao hapa na kutukana watu na kutoa matusi kibao.

Ngoja aendelee kuropoka for now!
 
Ushahidi wa nini mkuu kati ya haya?

1. Lowasa ameahidi kujisafisha na kulipiza kisasi?
2. Chenge na Lawyer wake wametishia kumwaga mboga?
3. Mafisadi wengine wanatishia wanaowafuatilia?
4. Kwamba sitambashi Kikwete for a month?
5. Kwamba Kikwete anapanga kuunda baraza jipya?

1)Lowassa alijiuzulu na Rais alikiri kusikitishwa!
2)Chenge alirudishwa madarakani na asingekuwa amejiuzulu kama sio kashfa ya Vijisenti ambayo Rais mwenyewe hakuijali na keshasema wasijali kuitwa mafisadi!
3)Yeye kama Amiri jeshi mkuu ana mamlaka makubwa ya kupindukia kuweza kuwashughulikia mafisadi wote wanaohatarisha usalama wa whistle blowers pamoja na wananchi wanaokerwa na ufisadi! Yeye bado kufanya hivyo!
Kina Kubenea waliposhambuliwa..Alienda pale Hospital na kuwaambia kuwa wawe makini na wanachokisema!
Was he on their side?
Aliwapa ulinzi ama aliwaambia wawe makini and they are on their own?
4)La kupanga baraza jipya ndio hizo siri nazosema zimwagwe!
NB:
1)Wapi Balali?
2)Wapi ripoti ya kamati ya madini!?
Are we still counting down?
 
Haya yote ni kweli mkuu na we are still counting down!?

Nilichotoa hapa ni offer ya Kikwete-Bashing-Free month! ila pia nina hakika kuwa yote matano niliyohi-lite hapo juu ni kweli kuhusu Kikwete kwa sasa hivi.

Kumbuka kuwa sitoi sifa kwa Kikwete bali ninazuia madongo kwa muda wa mwezi mmoja ili kumpa breathing room afanye something. Ninaweza kuwa wrong katika hili na kama muda huu ukipita na yeye asifanye chochote (kama ilivyotokea miaka yote hii), basi tegemea a very loaded Kikwete bashing hapa JF na kwingineko.
 
Honestly there is part of me wants to trust the president like before BUT he hasn't won me back yet!
Hatutaki aturidhishe wote...IS EITHER YUKO NA MAFISADI AMA YUKO NA WANANCHI!
There's no neutrality!
NB:Kuhusu hili la madini..Mh Zitto ameomba uvumilivu hadi hapo watakapo ikabidhi report!?
Again like i said..Ana mamlaka makubwa mno ya kuweza kuumaliza ufisadi bila hata ya kusua sua!
 
Huku Wengi Wameridhika Baba Zao Wameshachota Wako Wamepumzika Wanatucheka Sisi Tunavyowajadili Na Kutudhihaki

Kweli Nyani Ni Nyani Tu , Atakurushia Jiwe Tu Angalau Mara Moja Katika Maisha Yake Ili Unyani Wake Uendelee Kuwa Vile Vile
 
WHAT

?
 
....then you must be dumbest for taking your time, reading and contributing in this thread!!
.....lets play oddball, uuuunh.......

Haiwezi hardball huyo.... ukimbana kidogo tu anakimbilia matusi kibao. Wakati kina Mike na Max wameshikwa na polisi na kupelekea JF kupotea hewani, alikuwa akiingia kwenye blogs zingine na kushangilia yaliyotokea huku akitoa matusi kibao tu!

Yuko flawed na haiwezi hii game!
 
Hivi huyu Max ni Maximillan Msuya?
If thats him then i know the dude!
 
Ushahidi wa nini mkuu kati ya haya?

1. Lowasa ameahidi kujisafisha na kulipiza kisasi?
2. Chenge na Lawyer wake wametishia kumwaga mboga?
3. Mafisadi wengine wanatishia wanaowafuatilia?
4. Kwamba sitam-bashi Kikwete for a month?
5. Kwamba Kikwete anapanga kuunda baraza jipya?

Aunt:

Hivi tunakwenda wapi? Kamuzu Banda pamoja na udikteta wake na mabaya aliyowafanyia watu wa nchi zake, kwenye uchaguzi uliomtoa madarakani aliweza kupata kura nyingi kutoka kwa watu wa kabila lake.

Lowassa kamchemsha bado watu wa kwao wanasema wanaonewa na waliandaa maandamano makubwa ya kumpokea.

Chenge na naona katikisa kwao kwa mapokezi ya nguvu.
 
Ndugu yangu, si unajua hata Mugabe kuna watu wanamuunga Mkono. Hii inatisha ila kuna dalili nzuri huko mbele ya safari.
 
Mwafrika wa Kike,

JK kakuahidi nini? Maana siku hizi inabidi tuwe tunauliza kwasababu mafisadi
wamepata nguvu na wananunua watu hata JF kwi kwi kwi!!!

Nina uhakika utakuwa dissapointed muda sio mrefu, JK habebeki siku hizi. Naona hata akina Kawawa wataanza kumkimbia.
 
Mtanzania,

Nadhani utashangaa kusikia kuwa wakati nikijiandaa kuanzisha hii thread ili kumpa JK nafasi kwa mwezi mmoja, nilikuwa nimejiandaa kwa siku tatu kuandika thread ya kumpondea JK kwa kiwango ambacho hakijaonekana hapa JF hasa baada ya aliyosema Singida kuhusu mafisadi.

Nilibadilisha mawazo muda mfupi tu baada ya kusikia maneno ya kutia kichefuchefu ya Chenge na Rostam Azizi. Nimeahidi kumpa JK a free ride for a month. Sio kwamba nitaanza kumsifia hapa JF, ila tu sitampondea kwa nguvu kwa mwezi mmoja kama ilivyo kawaida yangu ya kuita makosa yake kwa majina bila kupamba.

Sidhani kama JK anapesa za kutosha kulipa watu kama mimi maana atafilisi serikali kujaribu ku-match malipo ninayolipwa na mzee wa Kiraracha AKA mkombozi wa wanawake AKA kiongozi wa chama cha wafanyakazi Tanzania AKA kiongozi wa upinzani aliyepigwa mabomu na FFU kuliko mwingine yoyote yule AKA mzee wa pilau - Augustine Lyatonga Mrema ........ lol
 
Naona spinmasters wa Kikwete washaweza ku-convince.

Kinachotokea hapa ni "confuse and delude"

Kikwete and his spinners are blowing things and distorting facts to their political advantage.In some instances, they do not even need to do that, the unhealthy respect for authority ensures that newspaper editors will speculate in favor of the big man.Some innocent bystanders mistake the staged shrapnel and ensuing hullaballoo for signs of effort and real war.Others laugh away the charade. sighting track record.

Politics hasn't changed since Sun-Tzu. Makaveli and Juvenal.

Nothing but "bread and circuses"

Wait a minute, we don't even have the bread to claim that, just circuses!
 
Aunt:

Hivi tunakwenda wapi? Kamuzu Banda pamoja na udikteta wake na mabaya aliyowafanyia watu wa nchi zake, kwenye uchaguzi uliomtoa madarakani aliweza kupata kura nyingi kutoka kwa watu wa kabila lake.

Lowassa kamchemsha bado watu wa kwao wanasema wanaonewa na waliandaa maandamano makubwa ya kumpokea.

Chenge na naona katikisa kwao kwa mapokezi ya nguvu.
Kikwete anajua everything bana!
Trust me njia anayoichukua ni smart lakini with plenty of unavoidable consequences!

Noma ni kuwa anataka awaridhishe wote!
Mafisadi wamem konvince kuwa demokrasia pia itumike ili na wao waende wakawagawanye wananchi!
Hawakutakiwa kupewa nafsi hiyo!
 
Mwafrika wa kike,

naomba baada ya siku 30 niwe "reminder", maana nahisi unaweza terminate kabla ya muda!!! kwi kwi kwi

Pia tunaomba baada ya siku 30 utupatie feedback ya JK na mapambano dhidi ya MAFISADI. Na uzuri ndani ya siku hizi 30, tutapatiwa ripoti ile ya MADINI! So itakuwa mapambano juu ya mpambano!! Maana hapa itamgusa hadi yule rafiki yake wa kwa Bw. "kichaka"!!
 
Back
Top Bottom