Mhache
JF-Expert Member
- Jun 20, 2008
- 345
- 24
Mvua iliyonyesha siku mbili tu katika jiji la Dar es Salaamu imeanza kuleta kero kwa watu. Mitaro imeanza kuziba, watu wa maeneo yasiyopimwa wameanza mtindo wa kuzibua vyoo vyao na marundo ya taka yamejaa katika maeneo mbalimbali ya barabara zetu. Barabara ya Morogoro maeneo ya Manzese Darajani kila kukicha kumejaa mizigo ya taka.
Kwa hali hiyo tutegemee magonjwa ya milipuko kama kipindupindu, kuhara na magonjwa ya tumbo, pia malaria kwani mvua inaandaa mazingira mazuri kwa mbu kuzaliana.
Je serikali inafanya nini kutatua kero hii? Na wananchi wana mchango gani katika kutatua tatizo la mitaro kuziba na taka kutapakaa kila kona ya jiji la Dar es Salaam?