Mvua inayonyesha kanda ya kaskazini yaleta maafa Arusha!!

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,216
Mvua iliyonyesha jana hapa Jijini Arusha na hata pembezoni mwa mji imeleta maafa ya watoto watatu wa familia moja ya Mbayana Loshilaa anayeishi Wilaya Arumeru Mashariki Kata ya Mwandet karibu kbs na Shule ya Msingi Mwandeti kufariki.

Mvua ilianza majira ya saa kumi kasoro jana jioni na hao watoto walikuwa wanachunga na mara mafuriko yakaja na ndipo mmoja kt ya hao marehemu akataka kuvuka aende ng'ambo ya pili na hapo maji yalimpiga mweleka na hao wawili baada ya kumwona mwenzao hivyo wakaamua kutaka kumwokoa ndg yao na ndipo na wao wakawa njia moja na kati ya hao watoto wana umri wa miaka 12,14 na 15 na MUNGU awalaze mahala pema peponi watoto wasio na hatia.

Na wawili wamezikwa leo na mmoja atazikwa kesho!


Inasikitisha sana!
 
Maskini. . .
Mi sikujua ilikua kubwa kiasi hicho maana.kwetu imenyesha ya kawaida.

RIP. . .
Pole kwa familia!!
 
Ni pigo kubwa sana kwa familia, Mungu awape faraja wafiwa na alaze roho za marehemu pema peponi!
 
habari mbaya hii kamanda. Poleni.


Ni hbr mbaya sana na kwenye mazishi ya wale vijana wawili waliokwishazikwa jana nakwambia ni alhamanusura baba yao naye kujiua!

Hili ni pigo kubwa sana ktk jamii ya boma ile!
Ila hakika MUNGU atawapa rehema na moyo wa uvumilivu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom