Muziki wa taarabu wa zamani Vs taarabu ya sasa.....!!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,047
21,519
Salaam,
Zamani sana nilikua mpenzi wa nyimbo za mwambao wa pwani (taarab) na kikubwa nilivutika na tungo za wasanii mahiri wa mziki huo zamani kama kina marehemu mzee Issa matona, Siti bint Saad, marehemu bi Kidude, wakina Shakira, marehemu Nasma Khamis Kidogo na wengine niliosahau,
Taarabu ya zamani mtu ulikua unapata ladha halisi ya mwambao kutokana na ala za muziki walizokua wanazitumia na pia nyingine zilikua zinatoa mafunzo.
Ila mziki huu kwa sasa si mziki tena, ni majanga. Tangu walivyo introduce viduku kwenye taarabu, na mipasho kuongezeka basi ile ladha halisi ya zamani ni aghalabu kuipata. Pia mziki huu umekua ndio kipenzi cha wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga) mpaka imekua kero maana kwa sasa hata mtu huwezi kutoka na mke wako kwenda kwenye show ya taarab maana ni laana tu huko, hakufai kabisa!
Wengine wanaweza kusema mbona taarabu ya sasa ni nzuri tu kwa mifano ya wasanii wachache kama kina Mzee Yusuph, Isha na wengineo lakini hii haibadilishi factor kwamba muziki wa taraabu umebadilika sana.

I miss them days....!!!!
 
Umeonae hii ndio tarab ele engine ni rusha kooo na inafundisha sana kupasuana mikuu_du ninashukia sana tarabu ya akina omar kopa
 
Sauti inaumiza mpaka kwenye hii sauti ni ya kununua kwa gharama yoyote
 
Taarab ni zamani siku hizi taarab inapotea taratibu na kuna rusha roho sijui na upuuzi gani mwengine.
Ssalaam 3aleykum W W,,, YaaBinti Nass ? Kefik... WahaShtuniii..? Nakutakia kulo kheyr daima. Mwenyeezi Mungu akulinde na kukuNusuru kwakila baya na acho ya Mahasidi.AMIN Dua'a zako usitusahau.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom