Muziki TZ II: Sikinde Vs Msondo Nani Zaidi?

Apr 27, 2006
26,588
10,374
- Wakuu nawakilisha tena samahani sana, je vipi kuhusu hizi bendi mbili zenye ushindaniwa siku nyingi sana je nani anamzidi mwingine? Maana wote vigongo vyao vinafahamika sana na sisi wapenzi wa muziki bongo, lakini kati yao kuna mmoja ndiye kinara kuliko mwenziwe, eti anaweza kwua nani?

- Nawasilisha mada.

FMES!
 
Hapo mzee wa sauti ya umeme ni pagumu ila kwa upande wangu naona sikinde na sababu hasa ni Bitchuka. Enzi zile safu ya mashambulizi sikinde ilikuwa kali Bitchuka, chidumule na kina king Enoch, komputa Mwanyiro, Mulenga hilo balaa.

Yaani kila siku za wikiendi ni siku za furaa vijana....
 
- Mkuu heshima mbele sana, una maana hawa chini au?



* Cosmas Thobias Chidumule
* Vocals, Musician

* Habibu Abbas
* Drums, Musician

* Abel Balthazar
* Guitar, Musician, Soloist

* Hassani Bitchuka
* Vocals, Musician

* Joseph Bernard
* Saxophone, Musician

* Michael Bilali
* Guitar, Soloist, Musician

* Max Bushoke
* Vocals, Musician

* Michael Enoch
* Saxophone, Musician, Bandleader

* Abdallah Gama
* Guitar, Guitar (Rhythm), Musician, Soloist

* Muhiddin Maalim Gurumo
* Vocals, Musician

* Juma Hassan
* Saxophone, Musician

* Mohamed Iddi
* Guitar, Guitar (Rhythm), Musician, Soloist

* Hamisi Juma
* Vocals, Musician

* Boniface Kachale
* Trumpet, Musician

* Shaban Lendi
* Saxophone, Musician

* Francis Lubua
* Vocals, Musician

* James Mhilu
* Engineer

* Hamisi Mirambo
* Trumpet, Musician

* Henry Mkanyia
* Guitar, Soloist, Musician

* Joseph Mulenga
* Guitar, Musician, Soloist

* Suleiman Mwanyiro
* Guitar (Bass), Musician

* Ibrahim Mwinchande
* Trumpet, Musician

* Julius Mzeru
* Guitar (Bass), Musician

* Ally Omari
* Tumba, Musician

* Kessy Omojo
* Organ, Musician

* Chipembere Saidi
* Drums, Musician

* Muharami Saidi
* Guitar, Soloist, Musician, Guitar (Rhythm)

* Machaku Salum
* Trumpet, Musician

* Mashaka Shaban
* Tumba, Musician

* Huruka Uvuruge
* Guitar, Soloist, Musician, Guitar (Rhythm)

* Benno Villa
* Vocals, Musician

* Ally Yahya
* Trumpet, Musician

* Mlimani Park Orchestra
* Main Performer
 
Hapa mambo yote yalikuwa kwenye "Sikinde Ngoma ya ukae" Nakumbuka baada ya mihangaiko ya weekend Mjini lazima jioni mtu uhudhurie DDC Magomeni Kondoa kwenye Nginde....Wakati huo wakitamba na nyimbo zao Iba,Taxi driver,Hapendeki n.k nakumbuka kuna jamaa alikuwa anakaa Mwembechai kutokana na upenzi wake wa Sikinde aliitwa Juma Sikinde...
 
mimi naona mnashindwa kuelewa, huyu jamaa haulizii kwa wakati uliopita kama nimempata vizuri, yeye anataka kujua msondo na sikinde nani mkali, jibu lake ni rahisi kwa maoni yangu msondo ni kiboko.
 
Wadau, nakubaliana na YE kuwa katika list ya FMES kuwa miongoni mwao kuna wengi wametangulia mbele ya haki,Bendi zote zipo chali kwa sasa japo TBL imeanzisha Promo ya kunywa SAFARI Lager changia Msondo na DDC wamewapatia vyombo Sikinde,japo kuna kipindi hasa miaka ya 80 na 90 mwanzoni Sikinde chini ya Tino Masinge RIP,Benno Villa Anthony,Hassan Rehan Bitchuka,Abel Baltazar RIP,Shabaan Dede,Machaku Salum RIP,Cosmas Thobias Chidumule,Machael Enock KING ENOCK RIP nk...walikuwa juu sana kisha kikaja kipindi cha Msondo wakati huo kulisheheni kina TX Moshi William RIP,Suleiman Mwanyiro RIP,Suleiman Mbwembwe RIP,Athuman Momba RIP,Joseph Maina RIP,Muhidin Maalim Gurumo,Saidi Mabera nk... ila kwa kujumisha yote MSONDO MUSIC BAND IPO JUU!!!
 
Wakuu, hapo pagumu lakini mwisho wa siku MSONDO ni NGOMA KUBWAAAAAAAAA...... anytime mwanangu ni MSONDO tuuuuuuuu, BABA LA MUZIKI
 
- Wakuu tupo wote hapa, kwa maoni yangu sasa hivi Msondo Ngoma ya Wa-Tanzania, iko juu sana tena sana kuwalinganisha na Sikinde ambao wako chaliii.

- Safari ya bendi hizi mbili inatokea mbali sana, originally Msondo walikuwepo hata kabla Sikinde hawajaibuka,enzi hizo za 80s, bendi kali zilikuwa ni pamoja na Afro 70, Urafiki Jazz wana Chua Ngoma, Dar International ya Baltazari yaani Super Bomboka, Moro Jazz na Super Volcano za Mbaraka, TK Lumpopo ya Kilaza, Western Jazz Saboso, Jamhuri Jazz wanyama wabaya, Vijana Jazz, kama, Bima Lee ya Roy, na Msondo Ngoma Afya.

- Baadhi ya wapigaji wa Msondo kama Gurumo, walitoka na kuungana na wengine kutoka Dar International kama Gama, Mulenga, Baltazari, Chidumule, na Hamisi kutoka Biashara Jazz, waliungana na kuunda Mlimani Park yaani Sikinde. Wakaanza na style mpya kabisa kimuziki bongo na kuweza kuwa juu sana kuliko bendi zote, isipokuwa Marquis tu.

- Lakini baada ya muda kukawa na tabia ya wananmuziki wa Msondo na sikinde kuhama na kurudi, sasa ikwa Bitchuka ndiye kingmaker anapokwenda ndiko kunakokuwa bomba, halafu siku moja ghafla Bitchuka, na Gurumo wakamua kwenda Ndekule, Mlimani na Msondo kidogo zife kabisaa, ingawa Dede alijitahidi sana kule Mlimani, lakini haikuchukua muda kule Ndekule, wakaanza tena kuhama hama in the process wakaiua kabisaa Ndekule, sasa ligi ikarudi tena kati ya Msondo na Sikinde.

- Msondo wakamchukua TX Moshi (Hamis Kishiwa) kutoka Polisi Jazz, katika kujaribu kuziba tatizo la Bitchuka, haikusaidia hapa Mlimani yaani Sikinde wakawa juu sana in the 90s, infact wakawa hawana mpinzani kabisaa kwa bongo. Lakini investment ya Msondo kwa TX-Moshi, ikaanza pole pole ku-pick up na hatimaye Gurumo akarudi tena Msondo na kutulia kabisaa, halafu Msondo wakamuongezea Mkulu Fresh Jumbe, ndipo walipopata jibu la kuwakalia juu Sikinde maana sasa Bitchuka kule Sikinde akaanza kua ni mwimbaji wa kawaida, huku Moshi, Jumbe, na Boma Lee wakiipandisha Msondo chati ya juu na vibao kama Binti Maringo, hii ilikuwa ni mwanzoni mwa mwaka 2000, since then mpaka TX-Moshi alipofariki, Msondo walikuwa juu sana tena bila mpinzani.

- Kwa maoni yangu nikwamba sasa hivi bendi zote mbili zipo juu ya mawe, mpaka watakapoanza tena, maana wote hawajatoa album mpya hivi karibuni sasa tunawasubiri tuone itakuwaje, lakini ninaamini kwamba Bitchuka in the absence of Moshi na Fresh Jumbe kule Msondo, Sikinde wataibuka kidedea.

Respect.

FMES!
 
Wadau,Muimbaji wa BIMA LEE aliyeimba wimbo wa Asia mwanakwetu anaitwa nani?? Nakumbuka niliuona mwaka 1987 katika maadhimisho ya mbio za mwenge kwenye sinema ambayo ilikuwa inatuburudisha kipindi hicho... Naomba sana sana... ilinisisimua sana...
 
Mie ni mpensi wa nginde pia wa msondo ngoma, hivyo kwangu mimi wote ni wakali maana kuna nyimbo zao nyingi nikisizikia redioni kama nilikuwa natoka basi hurudi na kusikiliza mpaka ziishe maana zilikuwa zinanigusa sana kwa maneno yake ya busara, jinsi zilivyoimbwa na muziki uliopangwa ukapangika. Nilikuwa morogoro miaka hiyo kikazi basi nginde wakashuka mjini wakati ule ile MV mapenzi ilikuwa ni moto wa kuotea mbali basi wamasai kibao halafu wao cheza yao kama ngoma zao za kimasai wanaruka juu tu basi mimi nilikuwa sina mbavu basi subordinate wangu mmoja inaelekea muziki ulikuwa umempitia kushoto akatoa bomu, "Duh! Hii bendi inabidi ihamie Dar maana muziki wao ni mzuri sana" ;) Njemba nyingine haimkummezea ikampa pale pale hii bendi inatoka Dar :)
 
Wadau,Muimbaji wa BIMA LEE aliyeimba wimbo wa Asia mwanakwetu anaitwa nani?? Nakumbuka niliuona mwaka 1987 katika maadhimisho ya mbio za mwenge kwenye sinema ambayo ilikuwa inatuburudisha kipindi hicho... Naomba sana sana... ilinisisimua sana...

Kama sikosei huyo alikuwa ni KAKERE sifahamu kama yupo hai huyu mtu pia walikuwapo akina Mobali Jumbe KABLA HAJA GERY NASHEN DUDUMIZI NA NYIMBO ZAKE ZA MAKULATA, PESA ZANISUMBUA, NK
 
Kama sikosei huyo alikuwa ni KAKERE sifahamu kama yupo hai huyu mtu pia walikuwapo akina Mobali Jumbe KABLA HAJA GERY NASHEN DUDUMIZI NA NYIMBO ZAKE ZA MAKULATA, PESA ZANISUMBUA, NK

Nashukuru Kakere unayemzungumzia kama ni Juma Kakere basi yu hai...:) Nashukuru anyways... acha tu hii ardhi imemeza vipaji vingi sana Jerry Nashon RIP alikuwa ananikuna sana enzi hizo...:(
 
- Mkuu heshima mbele sana, una maana hawa chini au?



* Cosmas Thobias Chidumule
* Vocals, Musician

* Habibu Abbas
* Drums, Musician

* Abel Balthazar
* Guitar, Musician, Soloist

* Hassani Bitchuka
* Vocals, Musician

* Joseph Bernard
* Saxophone, Musician

* Michael Bilali
* Guitar, Soloist, Musician

* Max Bushoke
* Vocals, Musician

* Michael Enoch
* Saxophone, Musician, Bandleader

* Abdallah Gama
* Guitar, Guitar (Rhythm), Musician, Soloist

* Muhiddin Maalim Gurumo
* Vocals, Musician

* Juma Hassan
* Saxophone, Musician

* Mohamed Iddi
* Guitar, Guitar (Rhythm), Musician, Soloist

* Hamisi Juma
* Vocals, Musician

* Boniface Kachale
* Trumpet, Musician

* Shaban Lendi
* Saxophone, Musician

* Francis Lubua
* Vocals, Musician

* James Mhilu
* Engineer

* Hamisi Mirambo
* Trumpet, Musician

* Henry Mkanyia
* Guitar, Soloist, Musician

* Joseph Mulenga
* Guitar, Musician, Soloist

* Suleiman Mwanyiro
* Guitar (Bass), Musician

* Ibrahim Mwinchande
* Trumpet, Musician

* Julius Mzeru
* Guitar (Bass), Musician

* Ally Omari
* Tumba, Musician

* Kessy Omojo
* Organ, Musician

* Chipembere Saidi
* Drums, Musician

* Muharami Saidi
* Guitar, Soloist, Musician, Guitar (Rhythm)

* Machaku Salum
* Trumpet, Musician

* Mashaka Shaban
* Tumba, Musician

* Huruka Uvuruge
* Guitar, Soloist, Musician, Guitar (Rhythm)

* Benno Villa
* Vocals, Musician

* Ally Yahya
* Trumpet, Musician

* Mlimani Park Orchestra
* Main Performer
FM ES NA Wapenzi wengine wa muziki wa Tz,
Asanteni kwa kuenzi muziki wa nyumbani hasa ule wa bendi.Hizi bendi mbili pamoja na kutokuweza kusema nani zaidi , kwa mawazo yangu naona zina mfanano sana kwa sababu wanamuziki wake huwa wanahama toka bendi moja na kwenda nyingine na in the process wanasababisha muziki ufanane sana.Kuna kipindi ilikuwa vigumu kutofautisha Msondo, Sikinde, Bima Lee etc! Ikaja kipindi wanamuziki wengi wakahama kutoka Msondo au sijui Mlimani na kwenda OSS - Enzi za Chatu Mkali na MV mapenzi.Huko nako wakapeleka sauti za akina Gurumo na Bushoke hadi kufanya OSS iwe kama Mlimani au Msondo japo kwa kufanya hivyo pia waliboresha muziki wa OSS.
Lakini hasa kilichonishtua siyo huu mpambano bali naangalia economics za hizi bendi.Listi uliyoitoa hapo Juu FM ES inaonyesha jumla ya wanamUziki zaidi ya 30. HiI IDADI NI KUBWA MNO NI KUGAWANA UMASKINI TU! Najua kuna kipindi Sikinde na nadhani hata Msondo walikuwa wanalipwa mshahara kama waajiriwa na si kutegemea labda gate collection.Pamoja na hayo wanamziki wetu inabidi kuangalia tena upya na kujipanga ili kuweza kuwa na ufanisi zaidi -huwezi kuwa na bendi kubwa hivyo halafu ukategemea wanamuziki wafaidike vya kutosha.
 
Mkuu unatakiwa ukumbnuke kuwa muziki sasa hivi hapa Tanzania ni kama umekufa. Sehemu nyingi ya nyimbo tunazosikia leo redioni unaweza kucheka. Sasa hivi nyimbo zilizop-popular ni zile ambazo ni copy. Kuna zinazoitwa bongo flavor ambazo ni copy ya American music na nyingine ambazo ni copy ya Afrika Kusini.
Kuja kwenye swali lako, kama sikosei unazungumzia Msondo na Sikinde, hasa before 1985 hao jamaa wataendelea kuwa the best, na itaendelea kuwa vigumu sana kujudge nani ni zaidi kati ya wawili. Ukisikiliza nyimbo zao leo na ukasikiliza mpya utaoa by far bado wao ni best. Toka composition, compilation, kupanga betu lugha etc etc. ni vigumu sana kusema nani zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom