Muuzaji si anajulikana………………....!

Yale mama wakati huyo mitaa hiyo yalikuwa ni akina Mama Koku..Ulikuwa ujawa checkbob nini?Pole ulikuwa bado unavaa chacha zako za plasti nini?Wakati huo lazima uwe namokasini mguuni na sunglass ndo usinigepigwa..
 
Nompongeza kaka yako kwa maamuzi MAGUMU aliyofanya kukurudisha kijijini,inaonyesha ulikuwa mhuni kweli kareti za kichina?,kulia kama paka?,kuvamia kina dada? LO! baba Ngina!!!
 
Story yake inajitegemea, tena hiyo ni Nouma, lakini nataka nibadili ID Maana hawa wanangu wakuda wakijua watamweleza
Nitaiweka hapa wiki ijayo kwa ID hii..........................Naona Cantalisia katoa macho, wala sitaitaja hapa. Nitaku-PM kapipi wangu.........LOL


hahahaaaa haina haja ya kubadili ID.......We unajulikana tu kwa mwandiko wako!!!
Hata hivyo poa tu we niPM mi nitaihifadhi, ninatamani kweli kujua the way ulivokuwa unarusha mistari kwa mama ngina!!
 
Leo naharibu,
Unajua huwa ana stail yake tukishafika hm huwa anajidai ananipenda oohhh,mwisho wa mwezi nitakupa ile hela ya simu,akiona nimekaa na mama ananirushia jero kwenye simu yangu,
Asa leo bila msimbazi naharibu hata akinipunguzia buku!!


Leo mpaka kieleweke aisee!!!!
halafu dada zako mbona siwaoni leo.......au kesha wahonga???
 
Naomba kujua mdogo wangu Cantalisia, Wifi yangu King' na Niece wangu Husny ni wepi katika hilo kundi... Wale watatu wenye mabaunsa AMA wale washobokaji wa kiingilish cha Bush? lol

Nimeipenda hii Mtambuzi.


On a serious note; Uvaaji wa sasa mijini ukiwa jogoo wa shamba waweza fikiri kweli yupo sokoni....:eyebrows:

Kwasababu imekuwa ngumu sana kutoutisha mimi nawashauli walaji siyo mbaya wakijaribisha maana anaweza mtu akawa yupo sokoni alafu ukadhania ni uvaaji wasasa hivyo kupunguza Turnover
 
huuu....!!!haaaaa....!! mastaaaaa....!!!mtambuzi raiti hiya. yu noo miii...???. mara chalii. hahahhaaaaa...!!
 
Leo mpaka kieleweke aisee!!!!
halafu dada zako mbona siwaoni leo.......au kesha wahonga???

Washakula Chapaa, unacheza na wekundu wa msimbazi.................Ni huyu Canta tu ndiye anayenipandisha presha na mikwala yae ili apate nyingi kuwazidi wenzie.................Huyu mtoto huyuuu......... Muone vile....................LOL
 
Ilikuwa ni mwaka 1988 nikiwa nimekuja Dar kwa kaka yangu baada ya kumaliza kidato cha nne na kufeli vibaya huko kijijini. Tulikuwa tukiishi kariakoo mtaa wa Sukuma. Kaka yangu alikuwa amepanga chumba kimoja na alikuwa ni muajiriwa serikalini katika ule mpango wa Direct employment baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka mmoja uliopita. Nilikuja ili kaka yangu anisaidie kupata kibarua huku mjini.

Alikuwa bado hajaoa, ingawa alikuwa na rafiki yake wa kike. Kuna wakati huyu rafiki yake alikuwa anakuja kisha wanananiliu, halafu anaondoka. Mara nyingi ilikua ni usiku ambapo ilikuwa ikimlazimu kaka kunipa hela ili niende sinema za usiku pale Odeon au Avalon. Hizi sinema za usiku zilikuwa zikianza saa sita usiku na kuisha asubuhi. Siku moja kama ilivyokuwa kawaida ya kaka, alikuja huyo mpenzi wake, akanipa hela ili niende hizo sinema za usiku ili wapate muda wa kujivinjari kama ilivyo kawaida yao. Alikuwa anajua kuwa mimi ni mpenzi wa sinema kwa kuwa huko kijijini kulikuwa hakuna hayo mambo ya sinema.

Nilipofika pale Odion nikawakuta wasichana fulani na kwa jinsi walivyokuwa wamevaa nikajua ni wale wasichana wanaojiuza usiku maeneo ya Magoti. Nikiwa bado nina tongotongo za ushamba wa kijijini nikajitutumua na kumfuata mmoja na kumuomba niwe naye kwa usiku ule.‘Kwa nini unanitongoza kama vile nimekuwa Malaya?' Aliniuliza baada nya kumwambia shida yangu. Kwa akili yangu ya kijijini nilijua ni Malaya anayejiuza lakini anajifaragua tu. 'Kwani muuzaji si anajulikana tu. Wewe sema dau lako twende tukamalizane.' Nilisema kwa kujiamini. Yule msichana alikasirika na kuanza kunishushia matusi. Wale wenzake watatu nao wakaingilia. Halafu ghafla ikatokea mijamaa miwili iliyoshiba hasa. Wale wasichana bila kuulizwa wakawa wanashitaki kwa ile mijamaa. Bila hata kuuliza ile mijamaa ikanivaa kutaka kunipiga, nikajifanya nawatishia kuruka sarakasi za Kichina kama Bruce Lee huku nikitoa mlio kama wa Paka.

Weweee…………., ile mijamaa ilivaa na kunitandika kisawasawa, waliokuja kuniokoa ni walinzi wa pale kwenye sinema, lakini nilikuwa nikitoa damu mdomoni na uso ulikuwa umevimba kama kiboko. Wale walinzi waliniuliza ninapoishi nikaawambia, ikabidi wawaombe vijana fulani waliokuwa wanaishi maeneo hayo ya Kariakoo wanisindikize nyumbani, kwani nilikuwa hoi hata kutembea nilikuwa nachechemea.
Wakati huo ilikuwa ni usiku wa manane. Tulipofika nyumbani wale jamaa waligonga mlango kwa fujo hadi wapangaji wote katika nyumba ile wakaamka.

Miongoni kwa majirani walioamka kulikuwa na mabinti fulani nilikuwa nikiwaringia kwa kiingereza changu cha bush kuwakoga kuwa ni msomi, na walikuwa wananichukia kweli kutokana na tabia yangu hiyo ya kujifanya mjuaji. Nilipowaona wale mabinti niliishiwa na nguvu kwani nilijua kila kitu kitakuwa peupe. Kaka aliponiona katika hali ile alishtuka sana na kuwauliza wale jamaa walionisindikiza, ni kitu gani kimenipata.
Wale jamaa walikuwa kama waandishi wa habari, kwani hawakumung'unya maneno, walisimulia kila kitu bila kuficha. Niliwaona wale mabinti wakikonyezana kisha wakacheka kicheko cha umbeya na kusema, ‘leo msomi kakutana na wasomi wenzie.' Sikujibu kitu nilibaki kuwangalia huku nikiwa nimetahayari.

Kaka alikasirika sana na alinichukua na kunipeleka hospitali kwa matibabu, lakini aliniahidi kwamba nikipona lazima anirudishe kijijini kwani hayuko tayari kuishi na muhuni. Ni kweli kaka alikuwa amedhamiria, kwani baada ya siku tatu nilipata nafuu na alinipeleka stendi pale Kisutu na kunipakia kwenye basi kunirudisha kijijini. Nilirudi jijini Dar mwaka mmoja baadae nikiwa nimepambazukiwa.

Asante kwa kunisaidia kucheka sana leo .
Enzi hizo nilikua natambaa nadhani.
 
Back
Top Bottom