Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Tangu mfumo wa vyama vingi uanze miaka 20 iliyopita, siku zote CCM imekuwa ikiuchukulia Muungano kama mtaji wao wa kisiasa (political capital) dhidi ya vyama vya upinzani.
Walileweshwa na imani hiyo, wakajisahau kabisa kama vile wamekuwa wamejisahau katika mambo mengi tu kwa kuyachukulia for granted.
Hata hili la kuandika Katiba mpya CCM imekuwa inaona kwamba Muungano utawapa nyenzo fulani dhidi ya wapinzani katika azma yao ya kuweka Katiba wanayoitaka na walianza kwa kusema Muungano usiguswe, na hapo hapo kuwapa Wazenji sauti kubwa katika Tume ya Katiba.
Eneo la watu 1.5m wamepewa ujumbe katika Tume hiyo sawasawa na eneo la watu zaidi ya milioni 40. Ni tofauti kabisa na uwakilishi wao katika Bunge la Muungano, ule wa kuchaguliwa viti 50 kwa zaidi ya viti 200 kwa upande wa Bara.
Sasa mambo yanabadilika, na Muungano unaanza kuwa ni mzigo kwa CCM yaani liability na unaweza kabisa kuiangusha. Yanayotokea Zenji sasa hivi ni ishara ya hilo ninalolisema. CCM wanaanza kuuona Muungano kama shubiri kwake.
Naleta mada hii kwa ajili ya kujadiliwa.