Mtumwitu,
Ingawa suala la elimu ya juu ni la mwungano zingatia kwamba Tanzania bara ina idadi kubwa zaidi ya raia kulinganisha na Zanzibar. Hapa hatuwezi kuwa sawa kwa sawa. Bara tuna watu millioni 34 na uchwea wakati Zanzibar millioni mbili hawafiki. Na katika suala la uongozi hatuwezi kuwa nusu kwa nusu kwa mantiki hiyo ya upande mmoja kuwa na idadi kubwa zaidi. Lakini Mwalimu alijitahidi. Hata Mwinyi aliletwa bara na Mwalimu kwa ushauri wa Marehemu Babu. Kuhusu nafasi za juu Zanzibar, kama mwungano umewabana basi hiyo si haki. Mkilalamikia hilo nitakuwa upande wenu.
 
Jasusi
Sasa Unaona Ni Fair Pale Wizarani, Tokea Waziri Hadi Maofisa Wote Kuwa Ni Upande Mmoja?

Kodi Ya Mikopo Wapo Wazanzibar Pale Au Kwa Kuwa Ni Kidogo?

Halafu Hebu Nielemishe Standard Hii Pia Ndio Inavyofanyiwa Rwanda Na Burundi Kwenye Eac? Nnakusudia Mabo Ya Muungano Nchi Kwa Nchi Inaenda Na Idadi Ya Watu? Au Hapa Tu Tanzania
?????////
 
Mtumwitu,
Sijasema ni fair. Kuna wakati waziri mdogo wa elimu alikuwa Mzanzibari. Haya ni mambo tunayoweza kuyazungumzia katika ufuatiliaji wa kero za mwungano wetu. Kuhusu Rwanda na Burundi mimi nadhani wanachotaka zaidi katika mwungano ni kulinda maslahi yao--unajua hawa ni landlocked. Wanategemea Tanzania na Kenya kwa bidhaa zinazoingia kutoka nje. Wao sidhani watajali sana mambo ya uwiano wa madaraka etc. At least ndiyo impression ninayopata kutoka kwa Wanyarwanda na Warundi niliozungumza nao.
 
wakuu wa vikosi vyote vya ulinzi toka tuanzishe muungano kumekamatwa na tanganyika.

wakuu wajeshi polisi na kwengineko au ndio yale yasemwayo tumemuondoa mkoloni mweupe na kumpelekea nchi mkoloni mweusi?

jee unajua kuwa wazanzibari kwa kuona tunaonewa humuita muasisi wa mapinduzi ni dalali?
 
Mtumwitu:Sasa Unaona Ni Fair Pale Wizarani, Tokea Waziri Hadi Maofisa Wote Kuwa Ni Upande Mmoja?

Kodi Ya Mikopo Wapo Wazanzibar Pale Au Kwa Kuwa Ni Kidogo?

Halafu Hebu Nielemishe Standard Hii Pia Ndio Inavyofanyiwa Rwanda Na Burundi Kwenye Eac? Nnakusudia Mabo Ya Muungano Nchi Kwa Nchi Inaenda Na Idadi Ya Watu? Au Hapa Tu Tanzania

Muungano wa Tanzania ni mgumu sana kwa sababu Tanzania bara haina serikali kama ilivyo Zanzibar na sababu moja kubwa ambayo Mwalimu (RIP) aliieleza ni gharama kubwa kwa nchi kama yetu kuwa na serikali tatu. Kuwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali ya Mapinduzi Zanzibar na serikali ya Tanzania bara. Kwa hiyo ilikubaliwa kwamba Serikali ya Muungano ndio itakuwa inafanya kazi kwa Tanzania bara vile vile khe... khe kheeheeeeeee............pana kazi hapo.

Sasa kutokana na hayo makubaliano sio rahisi kuona vyeo vingi vinakwenda kwa Zanzibarians kwenye serikali ya muungano kwa sababu hawa wanakuwa vilevile wafanyaji kazi wa serikali ambayo haipo (in theory) ya Tanzania Bara, zanzibar wana serikali ya mapinduzi kwa hiyo unapoandika malalamishi au manung'uniko ni lazima ulielewe hilo kwanza pili rais wa Zanzibar ametambuliwa kwenye katiba kutokana na upande gani rais atatoka - rejea wakati Mzee ruhksa alipokuwa rais.
 
mtumwitu......

kazi kweli kweli ktk masuala ya MUUNGANO,lkn mie JK anaweza kulirekebisha hili suala na kupatikana MUAFAKA.


Dua.....

unajua ndugu tatizo kila mtu anaona anaonewa,wabara wanaona wao wanaonewa kwani wanaona wanaibeba znz,wa-znz na wao wanasema kama tunakuoneeni tuwaacheni kila mtu na lake.
lkn mie binafsi nimekuwa nikijiuliza kwa nn mfano EAC mpaka leo imekuwa ngumu kuundwa?inaonekana kila mmoja mjanja kuliko mwenzake,kila kitu inatyaka kiwekwe hadharani ndio mambo yaendelee sio yale mambo ya kuvutana.
 
Nduguzangu Rejeeni Hesabu ya Mwalimu (RIP) kwamba 1+1=2 na sio 3 kama Alhaj Abood Jumbe alivyokuwa anadai.Mwalimu alivurugana sana na Sheikh Jumbe kuhusu suala zima la Muungano.Mzee Jumbe yupo Bara (Mjimwema) ni mzungumzaji mzuri,atawadokeza nini kilitokea mpaka akaambiwa anachafua hali ya hewa!.Mtumwitu au Dua muoneni Mzee Jumbe mpate Hekima yake kuhusu Muungano.
 
Ahsante Ila Nnasikia Mzee Jumbe Yu Hoi, Sasa Tutaweza Kuzungumza Nae?

Nakumbuka Rais Mstaafu Wa Zanzibar Alhajji Salmin Amour Alisisitiza Sana Kuwa Muungano Uzungumzwe Kabla Ya Wazee Waliounganisha Kumalizika Wote, Maana Kitakuja Kizazi Mbele Hakitoelewa Kitu Ikiwa Mambo Hayajawekwa Wazi. Sasa Sijui Waliyazingatia? Au Ndo Walimuona Koma Ndooo.
Ila Suala Hili Likiachiwa Litaligharimu Gharama Nzito Huko Mbele.
 
Jamani hivi kweli wazanzibar mnaweza kumuomba Jumbe azungumzie muungano? Hapo itakuwa ni kufirisika kwa kimawazo ni Jumbe ambaye alikuwa hautaki muungano ameondolewa na huyo huyo kakimbia kuishi Zanzibar. Tatizo la muungano ni wazanzibar bado wana fikira za miaka 90 iliyopita kuwa zanzibar ilikuwa dola inafahamika, sasa leo hii wanasahau tyuko karne nyingine kabisa. Na kibaya zaidi hakuna mzanzibar aliye mkweli kuhusu muungano, hata hawa akina Shein, leo hii wanyime madaraka basi utasikia wanavyousema muungano kwa ubaya wake , wengi wa viongozi wa Zanzibar kwao muungano ni wa maana ili waendelee kuwakandamiza wenzao visiwani.
 
hapo yomba yomba nnakupa five kuwa viongozi wa zanzibar wengi wao wanajali maslahi yao.

lakini ukweli wazanzibari walio wengi huu muungano hawaufagilii, sasa hawa wanapokuwa na madaraka hujifanya waumini wa muungano kwa kulinda maslahi ya muungano, ila wakiwa nje hurudi kuupaka muungano ili waonekane kwenye jamii ya zanzibar kuwa hawajawasaliti, walijitahidi kudai maslahi.

ama kuhusu zanzibar kuwa dola lenye nguvu na maarufu miaka 90 iliopita hii nnawapa hi waliojitahidi kulitetea na kulitumikia dola letu kufikia hapo, nilitegemea tusirudi nyuma tusonge mbele muungano nilitaraji kuinyanyua zaidi kuliko walipotuacha wakoloni, lakini wao ndio wametukandamiza na tumekuwa duni duni kabisa.

hujiuliza tuliuungana ili tuwe duni?
 
ama kuhusu zanzibar kuwa dola lenye nguvu na maarufu miaka 90 iliopita hii nnawapa hi waliojitahidi kulitetea na kulitumikia dola letu kufikia hapo, nilitegemea tusirudi nyuma tusonge mbele muungano nilitaraji kuinyanyua zaidi kuliko walipotuacha wakoloni, lakini wao ndio wametukandamiza na tumekuwa duni duni kabisa.

hujiuliza tuliuungana ili tuwe duni?

Mtumwitu,

Hii ndio Zanzibar ilivyokuwa miaka 90 iliyopita yaani kabla ya Muungano
Imagine the effect electricity had on Zanzibar when it was first introduced.

"Darkest Africa" had always stood near to old Zanzibar, and dark it was. Beyond the coast were the dense tropical forests; with mists and rains and sheer vegetative mass that could blot out light even at mid-day. At night, past the firelight, an impenetrable darkness stretched as far as the eye couldn’t see. Even from a high place the stars were much more noticeable than the weak lights of the scatted settlements.

Weak as they were however, contrasted with the harsh darkness of the bush, those lights advertised humanity and civilization like no other marker. That lesson was well learned by the people of Zanzibar. In early Africa light meant civilization. Lighting therefore became important to the people of the islands, and lights were used symbolically, as markers of their own civilization.

Oil lamps were widely used in houses and in most public buildings in old Zanzibar. By 1870 Oil Street lights had been installed along the major streets in Stone Town. These street lights ran out of town, past the harbor, south towards Mbweni.

Ten years later imported electric lights became available in Zanzibar, they were immediately embraced by the elite as the perfect symbol of modernity, wealth and sophistication. The Sultan arranged for the first electrical power station to be built near the harbor Palace complex. The station generated only a few hundred kilowatts of power but the Sultan quickly put to them use illuminating as many royal buildings as possible. The Lighthouse which stood in front of his palace was soon festooned with so many decorative colored bulbs that sailors from the west began referring to it as "the Sultans Christmas tree."

After the war of 1896 the pace of electrification increased. The palace was restored and dozens of new lights were added to the exterior. The old Light house had been destroyed in the war but a new "electric tower" soon took it's place.

In 1904 the Zanzibar Government signed a contract with the American firm, Arnold Cheney and Co. to build the famous Bububu Railway. Less well know is the fact that the Americans also undertook the task of installing electrical power lines along the track right of way. This was the beginning of the general electrification of the islands.

Wherever the rails went metal poles were installed and power lines strung overhead. By 1906, long before even London obtained them, Stone Town had electric street lights. Electric lights were then added to the entrances of many buildings. These early exterior lights featured large bulbs and huge glass domes; some still survive today.

Some we can only recall only thru pictures.

As the new century progressed more electrical capacity was added and Stone Town truly became a city of lights.

Today if one looks closely you can still find evidence of this early lighting exuberance scattered about the city.
 
Bora Tuendee Kufikilia UZURI wa Serikali moja!!!..
Serikali moja, Mabunge mawili!! -Kama ilivyo UK!!-vitu kama vile House Of lords/ House of Commons!! House Of Loard Kule Zanzibar!!
commons kule Dodoma (hapa)!!-Ni aibu Kuuvunja Muungano!! Kwanza -Tunajirudisha nyuma sisi wenyewe.....................

Tatizo na mafanikiao ya Muungano...Yana tokana na wazo la mwanzo
Lilikua ni nini///!!lili beba nini???.....Tusiogope Kufikiria...
 
Hati ya Muungano ilivyokuwa inavurugwa tangu 1964

Na Nizar K Visram

Wakati Tanganyika ilipopata Uhuru mwaka 1961 uwezo wa kutawala uligawanywa baina ya Gavana Jenerali na Waziri Mkuu. Hiyo ndiyo katiba ya Uhuru tuliorithi kutoka kwa wakoloni. Mfumo huo uligeuka na kuwa Jamhuru mnamo 1962. Tukapitisha katiba mpya ambayo ilimpa Rais uwezo wote aliokuwa nayo Gavana na Waziri Mkuu.

Chini ya katiba hiyo Rais akawa mkuu wa nchi, mkuu wa serikali, jamadari mkuu wa majeshi na akawa na uwezo wa kuzuia sheria yoyote inayopitishwa na bunge kwa kukataa kuisaini. Rais akapewa uwezo wa kuteua makamo wake na mawazi. Akapewa uwezo wa kuongoza baraza la mawaziri ambao waliwajibika kwake.

Katika katiba ya Uhuru mawaziri walikuwa wanawajibika kwa bunge. Katiba ya Jamhuri ukaondoa uwezo huo wa Bunge na mawaziri wakawa wanawajibika kwa Rais. Bunge likapokonywa meno na likawa kibogoyo, kwa vile likawa halina uwezo wa kusimamia serikali. Kwa kweli Rais akawa na uwezo hata wa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya.

Tanganyika ilirithi Bunge lenye wajumbe 71 waliochaguliwa, wote kutoka chama cha TANU, na kumi walioteuliwa. Katika kutunga katiba ya jamhuri, kilichofanyika ni kuwa bunge likajipa uwezo wa kujibadili na kuwa baraza la kutunga katiba (constituent assembly). Ni baraza hili ndilo lililopitisha katiba ya jamhuri

Ni katika mazingira haya ndipo Hati ya Muungano (Articles of Union) ikasainiwa baina ya Jamhuri ya Wananchi wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. Hati hiyo ilisainiwa na Rais Mwalimu Nyerere kwa niaba ya Tanganyika na Rais Sheikh Karume kwa niaba ya Zanzibar. Na ndipo ikazaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuliambiwa kuwa kuundwa kwa muungano huo ni matokeo ya karne nyingi ya mahusiano ya kihistoria baina ya wananchi wa bara na visiwani.

Pamoja na hayo ukweli ni kuwa Hati ilisainiwa bila ya mjadala miongoni mwa wananchi na hata miongoni mwa wanachama wa chama tawala. Ni matokeo ya maamuzi ya viongozi yaliyowashitukiza wananchi. Hata chama cha Umma Party kilichoshirikiana na chama cha Afro-Shirazi katika kuleta Mapinduzi na kuendesha serikali, hakikushauriwa kabla ya kusainiwa Hati.

Labda ni kutokana na hulka ya muungno wenyewe. Licha ya hiyo sababu ya mahusiano ya kihistoria, kuna sababu zingine ambazo zimekuwa zikijitokeza hivi karibuni. Haya yameanza kueleweka zaidi baada ya tafiti kufanyika na baada ya kufichuliwa kwa nyaraka za siri za watawala wa Marekani. Nyaraka hizi zinazungumzia kuundwa kwa Muungano kutokana na vita baridi baina ya Marekani na kambi ya Kisoshalisti iliyoongozwa na Muungano wa Kisovieti (USSR)

Kenya, Uganda na Tanganyika zilipata uhuru wake wa kisiasa kwa kupitia mazungumzo na wakoloni. Hakujakuwa na mapigano au vurugu, kinyume cha Zanzibar ambako mapinduzi yaliashiria kushika hatamu kwa viongozi wa mrengo wa kushoto kama akina Abdulrahman Babu wa Umma Party na wenzake wa Afro-Shirazi Party.

Marekani na Uingereza zilipata mshituko mkubwa kuhusu mapinduzi haya ya kimaendeleo. Mara moja ujumbe ulitumwa kutoa kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani mjini Washinton, Dean Rusk, kwenda kwa mabalozi wake mjini Nairobi, Kampala na Dar es Salaam. Mabalozi hao waliagizwa wazungumze na Marais Kenyatta, Obote na Nyerere ili wamuelimishe Sheikh Karume kuhusu “hatari” anayokabiliwa katika ushirikiano wake na Umma Party

Haya yanathibitishwa na Amrit Wilson ambaye ni mwandishi wa kitabu cha “US Foreign Policy: The Creation of Tanzania” (sera ya mambo ya nje ya Marekani na kuundwa kwa Muungano wa Tanzania). Yeye alimhoji aliyekuwa balozi mdogo wa Marekani huko Zanzibar wakati wa mapinduzi, Bw Franc Carlucci ambaye alikubali kuwa serikali yake ilimshawishi Mwalimu Nyerere kuhusu kuundwa kwa Muungano. Carlucci baadaye akaja kuwa mkuu wa shirika la kijasusi la CIA.

Naye mwandishi Susan Crouch, katika kitabu chake kiitwacho “Western Response to Tanzanian Socialism 1967-1983” (nchi za magharibi zilivyopambana na Ujamaa wa Tanzania) anaeleza jinsi CIA ilivyofanya juu chini ili kuunda mazingira ya Muungano kwa kuchochea wasiwasi miongoni mwa viongozi wa Afrika Mashariki kuwa Zanzibar ilikuwa inamezwa na ukomunisti.

Ni wasiwasi huu ndio uliowaingia viongozi wa Tanzania wakati ule, wasiwasi dhidi ya Umma Party. Lakini pia Karume alikuwa na tatizo ndani ya ASP yenywe. Baada ya kushindwa kwa mara nyingine kuunda serikali kufuatia uchaguzi mwengine wa Julai 1963, viongozi wenzake walianza kumkosoa na kukosa imani naye.

Hawa ni akina Othman Shariff waliotaka kuchukua nafasi yake. Pia kulikuweko na akina Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Ali Twala na Hassan Nassor Moyo ambao walielekea kushirikiana na Umma Party ikiongozwa na akina Babu, Ali Sultan, Ali Mahfoudh, Salim Rashid na Badawi Qullatein. Karume kwa hiyo alipokabiliwa na ushauri wa kuunda Muungano alikubali mara moja. Hamu yake iliongezeka hasa baada ya “motisha” alizopewa na CIA kama ilivyoelezwa katika nyaraka zake.

Ndipo Hati ya Muungano ilipotiwa saini na marais Nyerere na Karume. Hati hiyo ikaorodhesha mambo kumi na moja ambayo ni ya muungano. Muundo wa serikali ukawa na makamo wa rais wawili, mmoja kutoka bara na mwingine kutoka Zanzibar ambaye ndiye Rais wa Zanzibar.

Baada ya kutiwa saini Hati hiyo ilitakiwa iridhiwe na bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.Inasemekana huko Zanzibar jambo hili halikufanyika. Hii inathibitishwa na watu kadha waliokuwa na madaraka wakati ule. Wa kwanza ni Bw Salim Said Rashid aliyekuwa katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.

Pia Mwanasheria Mkuu wa mwanzo baada ya Mapinduzi, Bw Wolfgng Dourado, naye anathibitisha kuwa Hati haikuridhiwa na Baraza. Mwengine ni Abubakar Khamis Bakary aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu na waziri wa sheria na katiba. Yeye alipitia vitabu vyote vya sheria na kumbukumbu kuanzia 1964 na hakuona popote Hati hiyo kuridhiwa na Baraza la Mapinduzi.

Kwa hiyo baada ya Hati kusainiwa na marais wawili ikaridhiwa na bunge la Tanganyika lenye wabunge kutoka TANU. Kisha katiba ya Tanganyika ikarekebishwa na ikawa katiba ya muda ya Muungano iliyopitishwa na bunge la TANU. Katiba mpya ikapitishwa kama vile ni katiba ya zamani inarekebishwa tu.

Katiba ya kudumu ilitakiwa ipitishwe baada ya kuundwa kwa baraza la katiba (constituent assembly). Ilitakiwa ipitishwe katika muda wa mwaka mmoja lakini ilichukua hadi 1977. Na hilo baraza la katiba ambalo kwa kawaida huwa linashirikisha jamii nzima halikuundwa.

Tunachosema hapa ni kuwa hakukuwa na mjadala wa kitaifa wakati wa kutia saini Hati ya Muungano, wakati wa kupitisha Katiba ya Muungano ya mpito na hata pale Katiba ya kudumu ilipopitiswa. Hakukuwa na mijadala ya kitaifa na kakukuwa na baraza la katiba.

Katiba ya muda nayo ilifanyiwa marekebisho kadha.Moja ni kuhusu kuongezwa kwa mambo ya muungano, yaani kupunguza mamlaka ya serikali ya Zanzibar. Hii ni kinyume cha Hati ya Muungano. Rekebisho lingine la 1975 ni kupunguza mamlaka ya Bunge na kuongezea mamlaka Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya TANU.

Matokeo yake ni kuwa chama (NEC) ndicho chenye mamlaka kamili katika mambo yote ya kisiasa na kitaifa. Kilichokuwa kikifanyika kabla sasa kikapewa nguvu ya kikatiba, kwani kabla ya hapo chama tayari kilikuwa kinatawala katiba. Kwa mfano Azimio la Arusha utekelezaji wake ulipitishwa na NEC na kuridhiwa na bunge. Kwa hiyo chama kikawa na uwezo wa kutawala dola moja kwa moja bila kupitia bunge.

Chama kikazidi kupata nguvu baada ya kifo cha Rais wa Zanzibar, Mzee Karume na nafasi yake iliposhikwa na Aboud Jumbe. Yeye huyu alirahisisha njia ya kuunganisha vyama vya TANU na ASP na kuundwa kwa CCM mnamo 1977. Kamati ya kuunda katiba mpya ya chama ni hiyo hiyo iliyopewa kazi ya kupendekeza katiba ya Muungano.

Ikawasilisha muswada wa katiba ya Muungano kwa NEC ambayo ilikaa katika kikao cha siri cha siku moja. Baada ya hapo mswada huo ukapelekwa katika Bunge likikaa kama Baraza la Katiba. Bunge lilipitisha katiba baada ya kukaa kwa muda wa saa tatu na wabunge saba kuchangia. Kabla ya hapo Waziri Mkuu aliwakumbusha wabunge kuwa uwezo wao ni mdogo kwa vile mswada huo ulipitishwa na chama ambacho ndicho kinachoshika hatamu.

Hivi ndivyo ilivyopitishwa katiba ya kudumu ya 1977, bila ya mjadala au mashauriano ya kitaifa kama ilivyotakiwa na Hati ya Muungano. Kwa mujibu wa Hati hiyo NEC haikuwa na mamlaka ya kupitisha katiba.

Mnamo January 1982 NEC ilipendekeza mabadiliko ya katiba ambayo kwa mara ya kwanza yaliwasilishwa kwa wananchi wayajadili kwa muda wa mwaka mmoja. Wananchi walitekeleza wajibu na haki yao hiyo kwa bidii zote. Mapendekezo ya wengi yalikuwa ni kupunguzwa kwa mamlaka ya Rais na kuongezwa kwa mamlaka ya Bunge. Ikapendekezwa kuwa katiba iwe na kifungu cha haki za kimsingi (bill of rights).

Huko Zanzibar watu wakadai uhuru zaidi katika kujiamulia mambo yao pamoja na kupitia upya Hati ya Muungano. Mjadala ukapamba moto. Baada ya miezi minane mjadala ukafungwa ghafla na NEC ikatangaza kuwa “hali ya hewa ya kisiasa imechafuka” Ilisemekana Rais Jumbe alitiwa hanjam mpaka akalazimishwa kujiuzulu. Yeye na Waziri Kiongozi wake walishutumiwa kuwa ndio ‘waliochafua’ hali hiyo huko visiwani

Kilichofanyika ni kuwa Jumbe alitayarisha waraka aliokusudia kuuwasilisha kwa Rais Nyerere akiomba kuitishwa kwa mahakama maalum ya katiba ili kungalia iwapo katiba iliyopo ilikiuka Hati ya Muungano. Kabla ya waraka huo kuwasilishwa ‘ulipotea’ na ukaibuka kwenye meza ya Mwalimu ambaye aliifikisha katika kikao cha NEC ili ijadiliwe.

Inasemekana katika mdalala mkali uliofuata, mmoja kati ya wapinzani wakali wa Rais Jumbe alikuwa Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na washiriki wenzake. Jumbe akajiuzulu na Ali Hassan Mwinyi akateuliwa na NEC kugombea urais wa Zanzibar. Maalim Seif akateuliwa kuwa Waziri Kiongozi

Nini hasa kilichochafua hali ya hewa? Katiba ilitakiwa iongoze mgao wa madaraka baina ya serikali ya Zanzibar na ya Muungano. Katiba hiyo nayo ilitakiwa iwe inaongozwa na Hati. Hii haikufanyika hasa pale mambo ya ndani ya Zanzibar yalipopunguzwa na mambo ya Muungano yalipoongezwa. Ndani ya Zanzibar jambo hili lilipingwa hata miongoni mwa viongozi. Kupitishwa kwa katiba ya Muungano ya 1977 na kuvunjwa kwa ASP na nafasi yake kuchukuliwa na CCM huko visiwani, kulisaidia katika kufunika upinzani huu mpaka pale mjadala ulipofunguliwa na NEC. Chini ya Sheikh Karume kuvunjwa kwa ASP ilibaki kuwa ndoto ya wale waliotaka kuimarisha Muungano.

Jumbe alisaidia kuvunjwa kwa ASP na kuundwa kwa CCM, chama ambacho mwishowe kilimvua madaraka. Haya yasingetokea kama kila upande ungelikuwa na chama chake kama ilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo uongozi mpya wa Zanzibar haukudiriki tena kuzungumzia masuala haya. Kilichobaki sasa ni kuzungumzia ‘kero’ tu baina ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi.

Mwaka 1992 katiba ikabadilishwa tena ili kuanzisha mfumo wa vyama vingi. Wakati huo huo kulifanyika mabadiliko ya kimsingi, kinyume cha Hati ya Muungano. Hati ilisema kuwa iwapo rais anatoka bara basi Rais wa Zanzibar atakuwa makamo wake. Badala yake makamo wa rais sasa akawa ni mgombea mwenza.

Suala likaibuka kuhusu wadhifa na nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Muungano. Kilichofanyika ni kumfanya Rais huyo awe sehemu ya baraza la mawaziri la Muungano. Rais wa Zanzibar anatokana na katiba ya Zanzibar na siyo ya Muungano. Kwa hivyo kwa yeye kukaa katika kebineti ya Muungano ni kitu kisichoeleweka.

Matatizo ya katiba ya Muungano yamejitokeza katika sura kadha. Kwa mfano pale Zanzibar ilipojiunga na jumuiya kimataifa ya kiislamu (OIC) kulizuka mtafaruki mkubwa baina ya uongozi wa bara na Zanzibar.

Halafu tena mnamo 1993 kikaja kikundi cha wabunge wa CCM waliojiita G55 ambao walidai mfumo wa serikali tatu. Mwalimu aliingilia kati na kuwakemea G55 akiwaambia hawangeweza kutetea sera hiyo wakati wakiwa ndani ya CCM. Kutetea serikali tatu ni kwenda kinyume cha Hati ya Muungano na kwa hiyo ni kosa la usaliti. Hakuna aliyeuliza mbona Hati yenyewe imekuwa ikichezewa na watawala tangu 1964? Kwa mara nyingine suala la serikali ya Tanganyika likazimwa na halikusikika tena mpaka hivi karibuni.

Baada ya kufariki kwa Mwalimu suala hilo likajitokeza kwa nguvu zaidi. Mfano mmoja ni ile kesi iliyofunguliwa mnamo 2003 na Wazanzibari kumi wakidai kuwa Muungano ulikuwa batili. Wamtaka Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar awasilishe Hati ya Muungano. Aliiambia mahakama kuwa hajawahi kuiona! Ikasemekana kuwa haipo.

Kesi hiyo imefifia lakini suala la Hati ya Muungano litaibuka tena. Kule Uingereza wamekuwa na Muungano kwa karne kadha lakini mahakama ya huko mnamo 1953 ilitoa amri kuwa bunge la Uingereza halikuwa na uwezo wa kuvuruga hati ya muungano (Act of Union) baina ya England na Scotland kwa vile hati hiyo iko juu (supreme) ya vyombo vyote vya utawala.

Nasi tunahitaji mahakama inayothubutu kusema hivyo kuhusu Hati yetu ya Muungano wa Tanzania.nizarvisram@ctvsatcom.ne. Kwa makala zaidi na picha, tembelea; http://mjengwa.blogspot.com
 
Bora Tuendee Kufikilia UZURI wa Serikali moja!!!..
Serikali moja, Mabunge mawili!! -Kama ilivyo UK!!-vitu kama vile House Of lords/ House of Commons!! House Of Loard Kule Zanzibar!!
commons kule Dodoma (hapa)!!-Ni aibu Kuuvunja Muungano!! Kwanza -Tunajirudisha nyuma sisi wenyewe.....................

Tatizo na mafanikiao ya Muungano...Yana tokana na wazo la mwanzo
Lilikua ni nini///!!lili beba nini???.....Tusiogope Kufikiria...



Endelea kufikiria...wakati tuna jiuliza uliza..kuhusu east Afrika....
Basi tutumie muda huo!! Kujenga Serikali Moja....

sasa Sirikali ianze Kutafuta siri mpya....

hofu Yangu Ni Globle worming Sijui Hicho ni Kiingereza sahihi....
si unajua Visiwa Vina kabiliwa na Ongezeko la Maji Baharini?
 
1.hivi hii dola ambayo wazanzibari wanatukumbusha kwamba ilikuwa na nguvu na heshima kubwa haikujengwa kutokana na biashara ya UTUMWA?

2.kama dola hiyo ilijengwa kutokana na biashara ya UTUMWA, je watumwa hao hawakuwa wakitokea maeneo ya TANZANIA BARA?

3.Hatuwezi kugawana nusu kwa nusu ktk Muungano huu. Zanzibar ni nchi ndogo sana, kieneo, idadi ya watu, na kwa wakati huu kiuchumi.

4.Ni vigumu kwa wapemba kwenda ku-invest kwao. wata-invest nini? hakuna soko Pemba kutokana na idadi ndogo, na purchasing power ndogo ya watu wake.

5.Pemba hakuna miundo mbinu kwa hiyo si rahisi kufanya shughuli za uzalishaji mali huko, halafu uje kushindana ktk soko la Tanzania Bara na wazalishaji walioko huku.

6.Nadhani WAPEMBA katika ujumla wao ni moja kati ya jamii za Tanzania zenye uwezo mkubwa kifedha. Ninachoshauri wawekeze ktk elimu, na miradi ya huduma za jamii, na wakati huohuo waishinikize serikali kuboresha miundombinu kisiwani humo.
 
Kati ya waandishi ambao wamenifunza kwa kiasi kikubwa kuandika ni bwana Visram... Nimekuwa nikimsoma tangu akiandikia magazeti ya serikali. Makala yake hii imejenga hoja kubwa zaidi ya haja ya kujua hiyo Hati ya Muungano inasema nini... kuna mtu anayaweza kuiweka hadharani?
 
Mtumwitu,

Hii ndio Zanzibar ilivyokuwa miaka 90 iliyopita yaani kabla ya Muungano
Imagine the effect electricity had on Zanzibar when it was first introduced.

"Darkest Africa" had always stood near to old Zanzibar, and dark it was. Beyond the coast were the dense tropical forests; with mists and rains and sheer vegetative mass that could blot out light even at mid-day. At night, past the firelight, an impenetrable darkness stretched as far as the eye couldn't see. Even from a high place the stars were much more noticeable than the weak lights of the scatted settlements.

Weak as they were however, contrasted with the harsh darkness of the bush, those lights advertised humanity and civilization like no other marker. That lesson was well learned by the people of Zanzibar. In early Africa light meant civilization.

Lighting therefore became important to the people of the islands, and lights were used symbolically, as markers of their own civilization. Oil lamps were widely used in houses and in most public buildings in old Zanzibar. By 1870 Oil Street lights had been installed along the major streets in Stone Town. These street lights ran out of town, past the harbor, south towards Mbweni.

Ten years later imported electric lights became available in Zanzibar, they were immediately embraced by the elite as the perfect symbol of modernity, wealth and sophistication. The Sultan arranged for the first electrical power station to be built near the harbor Palace complex. The station generated only a few hundred kilowatts of power but the Sultan quickly put to them use illuminating as many royal buildings as possible. The Lighthouse which stood in front of his palace was soon festooned with so many decorative colored bulbs that sailors from the west began referring to it as "the Sultans Christmas tree."

After the war of 1896 the pace of electrification increased. The palace was restored and dozens of new lights were added to the exterior. The old Light house had been destroyed in the war but a new "electric tower" soon took it's place. In 1904 the Zanzibar Government signed a contract with the American firm, Arnold Cheney and Co. to build the famous Bububu Railway. Less well know is the fact that the Americans also undertook the task of installing electrical power lines along the track right of way. This was the beginning of the general electrification of the islands.

Wherever the rails went metal poles were installed and power lines strung overhead. By 1906, long before even London obtained them, Stone Town had electric street lights. Electric lights were then added to the entrances of many buildings. These early exterior lights featured large bulbs and huge glass domes; some still survive today.

Some we can only recall only thru pictures.

As the new century progressed more electrical capacity was added and Stone Town truly became a city of lights.
Today if one looks closely you can still find evidence of this early lighting exuberance scattered about the city.

JEMBA NIMEFURAHISHWA SANA NA MAENDELEO YALIYOFANYIKA..LAKINI UNAJUA PESA ZA KULETA HAYO MAENDELEO ZILITOKA KWENYE UTUMWA ,MASHAMBA YA WAARABU YA KARAFUU YALIYOLIMWA NA WATWANA WEUSI,KODI YA MELI/VYOMBO VILIVYOPITA UNGUJA,na pia tukumbuke himaya ya zanzibar ilikuwa pamoja na OMAN,kwa hiyo bila shaka pesa nyingi pia ilitoka oman.
lakini unapojivunia umeme na majumba ya sultan ukumbuke kando tu maeneo ya michenzani kwenda mbele miaka hiyo zilisheheni MBAVU ZA MBWA za kina KABWELA!
LAKINI napata wazo...kuna watu wanafikiri pamoja na dhuluma zote zile ,bora SULTANI,sasa hiyo ina maana serikali ya mapinduzi zanzibar haijafikia matarajio ya wengi?
 
Back
Top Bottom