Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?

suala hili huamsha hamasa na jazba katika kila forum linapojadiliwa. nadhani tatizo ni kila upande kujaribu kuvutia kwake, na kuunyooshea upande mwingine kidole.

kwa maoni yangu Muungano unawagusa zaidi wananchi wa ZNZ kuliko wale wa Bara. Naweza ku-speculate kwamba kila Mzanzibari ana jamaa yake aliyeko Bara, lakini si kila Mbara mwenye jamaa yake ZNZ.

Mara nyingi Watanganyika wanagutuka kwamba wako ktk Muungano baada ya kusikia manunguniko au mtafaruku kutokea ZNZ. Tanganyika ni kubwa mno, na Watanganyika wengi kama nilivyoeleza hawana habari au hawaathiriki na Muungano kwa namna ile unavyowaathiri Wazanzibari.

Muungano huu una matatizo, hata Raisi wetu amekiri kuwepo kwa matatizo, bila ya kuyabainisha. Ni vigumu kufahamu viongozi wanashughulikia tatizo lipi ktk Muungano, na hatua gani wamefikia ktk kulitatua. It will take time.

Wakati tunawasubiri taarifa ya viongozi kuhusu kutatuliwa kwa matatizo ya Muungano, mimi nawaomba wazanzibari wajadili ni jinsi gani wanaweza kuutumia muungano kufaidika mmoja-mmoja, na taifa la ZNZ kwa ujumla wake.

Badala ya kunyoosheana vidole, na kuzungumzia MATATIZO, wananchi tujadili jinsi ya kutumia OPPORTUNITIES zilizopo sasa hivi. Unajua wakenya wanatulilia tuungane nao. Now, what are the KENYANS seeing in TANGANYIKA, that ZANZIBARIS are missing?
 
Nadhani ulikuwa na maana ya 2.9% au sio?
Umechambua vizuri mada, lakini nadhani ushawishi wa kutaka muungano uvunjwe huenda unatokea nje kwa sababu ya historia ya visiwani. Kuna baadhi ya watu wanaodhania kuwa faida zaidi itapatikana pakiwepo na ushirikiano wa karibu zaidi na Oman kuliko na Tanganyika!

Lakini........ enzi hizi ni za uwazi na za uhaki wa kibinadamu popote duniani (isipokuwa labda Iraq na Darfur). Watu wapewe uhuru wa kuamua wakipendacho wenyewe. Latvia walikuwa kwenye himaya ya kisoviet bila matakwa yao. Leo hii himaya hiyo haipo tena. Hakuna kitu cha kuogopa pande zote mbili za muungano. Wape watu waamue wenyewe wanalolitaka.
 
Ila kadri siku zinavyokwenda muungano unazidi kubomoka, issue ya wimbo wa taifa/bendera nasikia kuna kamepni ya zanzibar kutaka sarafu yake yenyewe.
Hivi Zanzibar inachangia chochote kwenye Serikali ya Muungano(Monetary) ama mapato yake ni ya kuendesha serikali yake yenyewe?
 
sasa sheria ya mwaka 1952/53 si ilikwua ni miaka kumi kabla ya muungano, inamaa bado haijabadilishwa tuu?
 
Tatizo ni mfumo wa muungano wenyewe. Viongozi wetu wote waliopo madarakani na waliopita wanajua mfumo wa muungano tulio nao umepitwa na wakati. Suluhisho ni kuwa na ama serikali moja tu ya muungano au kuwa na serikali tatu ya Zanzibar, ya Tanganyika na ya Muungano na kupata ridhaa ya wananchi walio wengi wa nchi hizi mbili.
 
Kuwa na serikali tatu itakuwa ni gharama kubwa za kujitakia nadhani serikali moja inatosha ila the tricky part inakuja Zanzibar itakubali?
 
Hili la serikali moja naona liko wazi Zanzibar haiwezi kukubalia kwa sababu nahisi ikiwa kwa serikali mbili wanaona hawatendewi haki je kwa serikali moja itakuwaje?
 
tattizo kuwa haki haitendeki, na huu muudo sio, nnaamini kuwa hatuna budi kuukubali ukweli tuwe na serikali tatu ambalo ndio wazo la wengi japo baadae wataalamu waliona running cost ya serikali tatu ni kubwa.

na second alternative serikali moja, hii ikifanywa kwa uadilifu nnahakika ndio best kwani itapunguza hizo running cost kwa pande zote.

ila inapaswa kufanywa kwa uangalifu sana, moja hili suala la kusema hatuangalii upande tunaangalia uwezo sisi wazanzibari hatulitaki hata kulisikia.

maana kwa misingi hiyop mtakuja kusema mpaka waziri kiongozi wetu hafai maana mnao wengi wenye sifa kuliko yeye(jokes).
 
ha ha Mtumwitu, I'm not trying to instigate ila issue ya serikali moja nayo ina vikwazo vingi kimoja wapo ni within Zanzibar kwenye (Pemba na Unguja) sasa kama upande mmoja unaona unaonewa si ni blaa kubwa hapo. this is off the track ila nimegundua kuwa ITV ilikuwa haifiki Pemba sasa kwa mwendo huo ndugu zangu wa Pemba si wanaona wanaonewa kutoka serikali zote mbili
 
Wapemba wanawekeza DSM na UK!Sio ChakeChake. Pengine wanafikiria ChanguChangu ama ChakoChangu.Wooh
 
--------------------------------------------------------------------------------

Wapemba wanawekeza DSM na UK!Sio ChakeChake. Pengine wanafikiria ChanguChangu ama ChakoChangu.Wooh
Asha Abdala,

hebu tuwekee wazi hapo una maana gani??
 
jasusi.....

itawezekanaje kuwekeza pemba ilhali hakuna maji,umeme,barabara etc?hiyo ni ngumu ndugu yangu,maendeleo yanakuja haraka kutokana na kupatikana na huduma muhimu kama hizo.

JJ.......

leo nimepata nafasi ya kujibu baadhi ya hoja,majukumu ndugu yangu ya masomo yananifanya nishindwe kuingia JF kila wakati,naomba nikuulize...

NN MSIMAMO WA CUF KTK MUUNGANO MARA TU WAKISHIKA MADARAKAN......?au sisi MnaOTUITA MACHOGO(wa-wazanziBARA)mtaturejesha kwetu tanga?


hebu tueleze inasemakana SSH katibu mkuu wa cuf alipokuwa w/kiongozi alikuwa anawasaidia sana wa-pemba in terms of skolaships etc,jee unaweza kututhibitishia hilo.
 
Babu yangu!! 73..ame sema Kuvunja muungano Ni AIBU!!

Turekebishe Tu..pale Tuanpo ona haifai..
Lakini Kuuvunja- Ni Kushindwa Kujitawala....
Nafikiri kila Kitu kikiwa nisirikali...Basi hatuta fika...
Kuna kitu ambacho watu wanapenda kukifahamu...

sort of Questions Of trust!!

Ukweli ndio utakao amua kwa sababu uongo ndio unao taka kuuvunja muungano...
 
Gigo
Jee Kuna Utayari Wa Kutosha Kuliweka Suala Hili Wazi Lijadiliwe, Just Kuna Ushkaji Tu.

Mficha Maradhi Mauti Yatamuumbua
 
Mtumwitu,
Toa hoja tuizungumzie. Bwana Engineer, kupeleka umeme Pemba ndio uwekezaji ninaouzungumzia. Tupeleke umeme, tujenge barabara na miundombinu mingineneyo pamoja na kurahisisha usafiri, malalamiko ya Wapemba yatapungua.
 
Malalamiko Tuliyaoredheshan I Mengi
Mfano Kwa Nini Elimu Ya Juu Ni Ya Muungano Lkn Toka Tupate Uhuru Imeshikiliwa Na Upande Mmoja Tu?
Viongozi Wote Upande Mmoja Kiasi Ambacho Huoni Sura Ya Kimuungano
Hata Nafasi Za Juu Zanzibar Tunabaniwa
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom