nakubaliana na mawazo ya Phillemon Mikael. Mfumo wa utawala ZNZ-- serikali,baraza la wawakilishi,bunge, na vyombo vya dola, ni MZIGO mkubwa kwa UCHUMI wa Zanzibar.
 
Salaam wana JF...!!
Kuna mada zimenivutia kwa kiwango fulani, kiasi ya kwamba imeniwiya kuianzishia thread yake maalum...
Najuwa kuna mada inaendelea kuhusiana na upigaji wa kura kuhusiana na kuendelea kwa muungano au kutoendelea (TUVUNJE MUUNGANO?). Naomba nieleze kidogo ninacho kifahamu kuhusiana na historia ya nchi izi mbili, yaani Tanganyika na Zanzibar, na pale nitapokwenda kombo basi naomba msisite kunishika mkono na kunielekeza kule ninapotakiwa kwenda insha'Allah...!!
 
Tanganyika Na Zanzibar Kabla Ya Muungano

TANGANYIKA:

Tanganyika ilikuwa imeendelea tangia karne ya 7 kwa maana ya tangia mwaka 800BK. Japokuwa Historia inaonyesha wafanyabiashara wa kutoka Iran na Middle East waliingia East Afrika kwenye karne ya kwanza 1BK Lakini hawakuishi Zanzibar. Eneo hilo warumi na wagiriki walikuwa wanaliita Azania. Kufikia karne ya 9BK eneo la Kilwa liliuzwa na kununuliwa na Mfanyabiashara Ali bin Al-Hasan, kipindi ambacho biashara na nchi za jirani kama Zimbabwe na Somaria (Mogadishu) kwa kuuza dhahabu chuma na pembe za ndovu pamoja na bidhaa za nguo na viungo kutoka Asia zilikuwa zimeshamiri. Baadae mji wa kilwa (Quiloa) kufikia mwaka 1100 mpaka mwaka 1500 mji wa kilwa ilukuwa maarufu sana kwa bishara mpaka wakaweza kuwa na fedha yao binafsi. Kipindi hicho bwana Ali bin al-Hasan alijenga msikiti mkubwa sana baada ya kuja mfanyabiashara kutoka Morocco Ibni Batuta. Biashara ilipanuka mpaka pwani ya Afrika kusini kwa Mwana Mtapa(sijui kama unamfahamu) (Kilwa hipo Km 300 kusini mwa Dar es salaam). Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu. Kipindi hicho kiswahili kilikuwa kinatumika pwani. Na neno kiswahili linatokana na neno la kiarabu Sohar kwa maana ya pwani. Waarabu (kutoka Oman) walikuja na kustawi hapo zanzibar baada ya kuwaondoa wareno kwenye karne ya 17 BC yaani mwaka 1652. Japokuwa walikuwepo lakini walikuwa wachache sana. Wareno biashara yao kubwa ilikuwa pamoja na kukamata watumwa kwenda kuwauza nchi za mbali. Kwa hali hii hata wale ndugu zangu watumbatu na wahadimu hawakusalimika. Imam Sultan bin Seif kabla ya kurudi zake Omani aliiteuwa familia ya El-Harthy kuitawala zanzibar. Je unafahamu hilo? Leo hii Kilwa Kisiwani ni kati ya Hifadhi ua Kiutamaduni muhimu sana za Tanzania. Kilwa Kisiwani imeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage). Kuja kwa Wareno katika Karne ya 17 ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne za 18 na 19. Biashara ya utumwa ilikuja kushamiri sana baadae na kuingia mpaka bara unyamwezini baada ya Sultan Seyyid Said, kutaka watumwa zaidi kwa ajili ya mashamba ya karafuu kule Zanzibar na Pemba. Na wafanya biashara wa kibrazil walipoona kuwa bishara yao.

ya kukamata watumwa haiwaendei vizuri kule Afrka Magharibi wakaamishia kukamata watumwa Afrika Mashariki. Na ndipo hapo Mfanya biashara Hamed bin Mohammed (Tippu Tip) alipokuja kupata umaarufu Bwana huyu alikuwa nusu mwarabu na mwafika aliye zaliwa hapo Zanzibar. Upande mmoja wa wazazi wake
walikuwa watumwa. Japokuwa Arabian geographer Yakut aliingiza kwenye ramani Kisiwa cha unguja kwa kukiita LENGUJA. Na si UNGUJA kwenye karne ya 11 NA 12 . Na wakazi wa huko walikuwa Watumbatu na wahadimu. Neno Zanzibar linatoka na neno la kiiran Bazrangibar, likiwa na maana ya "Bazrangi coast" Baadae mji
ukaitwa Zangibar. Hili neno baadae shortened to Zangibar and was slightly altered etymologically to produce the word "Zanzibar". Watumwa wa kiafrika ambao walikuwa wakitokea Bazrangibar (Zanzibar) walijulikana kama zangi or zingi, ikiwa na maana ya "a native from Zangibar".

ZANZIBAR:
Mji wa Zanzibar ulikuwa miongoni mwa miji maarufu ya kibiashara miongoni mwa miji ya kale miji muhimu ya Kiislamu ya wakati huo, kama vile Iraq na Misri. Mafanikio haya yote yalikuja kipindi ambacho biashara ya watumwa wakati wa kutawala Sultan Sayyid, yeye alikuwa na mashamba mengi ya mikarafuu, mashamba haya yalileta pesa nyingi Visiwani. Karafuu ilikuwa zao muhimu sana kwa Uchumi Zanzibar. Kama sehemu nyingi ya Afrika Ukulima ulikuwa ni sehemu kubwa ya uchumi wa Zanzibar. Mazao kama mbata, mwani, pilipili hoho, na baadhi ya viungo vya kwenye vyakula vilipandwa na kuuzwa nchi mbali. Watu wakilima mazao ya chakula kama mahindi, viazi vitamu, ndizi, muhogo, mtama, mchele, na kunde. Uvuvi ulikuwa umeshamili sana visiwani. Kwa kipindi kile cha nehema kilitetereka kwa sababu ya uvamizi wa wareno. Wareno waliofika wakati huo waliwanyang’anya Waislamu mali zao na kudai mali nyingi kama kodi, waliopinga miji yao iliangamizwa. Wareno sio tu walitaka utajiri, walinuia kuupiga vita Uislamu pia. Hayo ni pamoja na kujaribu kuwashawishi watawala wa kienyeji kubadili dini na kufuata imani ya Kikristo. Ingawa Wareno hawakufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwatoa wenyeji katika imani ya Kiislamu, misafara ya kibiashara ilizuilika, kwa hali hiyo, hali ya maisha ya Waislamu zikateremka. Misikiti haikuendelea tena kujengwa katika kipindi hicho, baadhi ya viunga vya miji vilihamwa na Misikiti ikawa magofu na kuporomoka kabisa. Hatimaye Wareno walipigwa vita na kuondoshwa kwa msaada wa kijeshi kutoka ufalme wa Oman. Katika karne ya 18 AD hali ilirejea kuwa ya kawaida, ujenzi mpya ukaanza pamoja na jitihada za kutafuta na kuendeleza elimu ya dini. Walimu wa dini walikuja kutoka nchi za Kiarabu, hasa Masheikh wa Kisunni kutoka nchi za kusini ya Bara Arabu, baadhi yao wakiwa ni wafanyabiashara. Maarufu katika hao ni Sheikh Muhammad Abdulwahab (1703 – 1792 AD). Kadhalika huu ulikuwa wakati wa kuanza kwa biashara na nchi za Ulaya ambayo baadaye mfalme Said bin Sultan aliiendeleza. Karne ya 19 AD elimu za maarifa ya Uislamu.

ziliendelea. Watawala wa kifalme kutoka Oman ambao walikuwa wa madhehebu ya Ibadhi walishughulikia dola na biashara hawakuingilia itikadi za Kisunni na Masunni hawakuingilia watu walioitakidi Ushia. Zanzibar ilikuwa sana kiuchumi na kisiasa ilidhibiti karibu mwambao wote na kufanywa kituo kikuu cha biashara yote ya nje hasa mali kutoka bara. Wanazuoni wa miji ya Mwambao walitembeleana kubadilishana elimu na kufanya biashara, walitunga vitabu na kufungua madrasa kubwa kubwa za kufundisha elimu ya dini, wengine walikwenda nje kusomesha kama vile Uganda na kwingineko.Kwa hiyo, Zanzibar ikawa pia ni chemchem ya dini. Kama ilivyokuwa miji iliyokuwa na Waislamu wengi na dini kuwa na nguvu zaidi, kama Zanzibar, Waislamu wakafikia hatua ya kufuata sharia chache katika Uislamu, zinazohusu ndoa na mirathi na watawala wakiwateua makadhi kushughulikia hayo. Unguja Makadhi wa Kisunni ndio waliokuwa wengi na Pemba Makadhi wa Kiibadhi ndio waliokuwa wengi. Hali ya Zanzibar kibiashara na kiutamaduni iliwavutia sana.

Wazungu na walikaribishwa na mfalme wa Kioman. Na wao kama kawaida yao hawakuja peke yao Walifuatana na Misheni zao za Kikristo. Hali ya Zanzibar ikazilea Misheni hizo kwa hali ya Mabara ilivyokuwa, haikuwa rahisi Misheni kuanzia huko. Kwa vile Uislamu ushamiri sana Zanzibar, Wamisheni pia walifurahia fursa ya kuanza harakati zao Zanzibar kuendeza Ukristo, kwa matumaini kuwa wakifanikiwa kubadilisha imani ya Kiislamu Zanzibar itakuwa ni rahisi kuifanya jamii nzima ya Mwambao kuwa ya Wakristo. La muhimu ni kuwa Wazungu hatimaye walichukua hatamu za dola (ukoloni ukaanza) wakashika kisu mpini, ikawa Waislamu wameshika kwenye makali. Khatima ya jamii ya Waislamu Zanzibar ikawa katika mikono ya Waingereza. Hali nzima ikabadilika. Hadi kufikia karne ya 20 elimu ikafifia pamoja na utamaduni wa Kiislamu, Waislamu wakadharauliwa pamoja na dini yao.

MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR:
Mwaka 1961 wananchi wa Tangayika walipata uhuru wao. Chama kikubwa cha wakati huu kilikuwa chama cha TANU na kiongozi wa chama alikuwa Julius Nyerere. Na ndie aliyekuwa rais wa kwanza wa nchi. Mwaka 1963 mwezi wa desemba tarehe 9 wananchi wa Unguja walipata uhuru kutoka kwa Waingereza. Kabla ya mapinduzi kulikuwa na vyama vya Afro-Shirazi Party (ASP) na Zanzibar Nationalist Party (ZNP). Washirazi na Waafrika wengi walikuwa wana-ASP. Waarabu wengi walikuwa wana-ZNP. Pia, chama cha ASP kilikuwa chama cha watu wa Ng'ambo na wale walioishi mashambani na chama cha ZNP kilikuwa chama cha watu walioishi mjini. Vyama viwili hivi vilipigania uhuru na walishinda.

Waingereza waliondoka na wananchi walipiga kura. ASP, chama cha watu wengi, kilipata viti vichache ingawa ZNP, chama cha watu wachache, kilipata viti vingi. Baadaye, Washirazi wengi waliondoka ASP na waliunda chama cha ZPPP na waliunguana na ZNP kwa kufanya serikali. Mwezi wa Januari mwaka 1964 kulikuwa na mapinduzi. Nyerere na watu wa TANU waliwasaidia ASP ambayo ilikuwa ikiongozwa na Karume. Walifanya mapinduzi yaliyopelekea kumwagika kwa damu nyingi zisizo na hatia damu za waislam. Sultani alifukuzwa na kukimbilia Uingereza. Watu wengi wenye asili wa Oman walirudi kwao Oman.

BAADA YA MUUNGANO:
Mwezi wa Aprili mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana nakuzaliwa nchi mpya ya Tanzania. Baada ya muunguano, Mwalimu Nyerere alitaka serikali moja tu ya muungano walakini wananchi walitaka serikali nyingi. Mwishowe, waliamua kwamba iliwabidi wafanye serikali mbili: moja ya muungano na moja ya Zanzibar. Nyerere alieleza uamuzi huu ulikuwa bora kwa sababu Wazanzibari wangehamaki kama wasinge pata serikali yao. Na kama wakifanya serikali tatu (ya Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano) umoja wa nchi ungeharibika kabisa. Kila sehemu ya nchi ingekuwa na serikali na kusingekuwa na masikilizano yoyote yale. Kwa hivyo, waliamua kufanya serikali mbili badala ya moja au tatu. Nyerere alifanya mabadiliko makubwa ya kisiasa lakini ya kisiri siri, haswa Bara. Waislam wengi waliondolewa madarakani na kupewa wasomi wa kikristo. Wasomi hawa wa kikristo ndio hao walikuja kuiangamiza nchi na kufilisi. Mali za mashirika ya umma na viwanda viliendeshwa kama vyao, alikuwa mtu akiharibu hapa anapelekwa pale. Hali hii ambayo ilitokea Bara iliharibu pia uchumi mdogo ulokuwepo pale Zanzibar. Hali ilikuwa mbaya zaidi sana pale walipoamua kutaifisha mali za watu na viwanda vya wazungu matokeo yake mkonge pamba, karafuu kukosa soko duniani, Viwanda vingi vikawa magofu, tukapelekwa vitani bila kupenda baada ya vita tukaambiwa tufunge mikanda miezi 18 ikawa miaka zaidi ya 18 balaa juu ya balaa. Na watoto baada ya kuwapeleka shule wakaishia kuwa chipukizi... sijiu walikuwa wanachipukia kuelekea wapii yaani balaaa tupu, ndo mana kizazi cha sasa hakina busara zaidi ya matusi tu...(Mnisamee). Hivi sasa kwa hakika uchumi wa Zanzibar na hata wa Tanganyika, una hali mbaya sana licha ya kauli za kupotosha zinazotolewa na viongozi wa Tanzania na SMZ kwamba uchumi umekua. Labda umekuwa matumboni mwao. Na hili halina shaka kwani linaonekana wazi. Wao wakiumwa tu wanapanda ndege haoo ulaya kutibiwa walala hoi wenzangu na mie wanaishia mnazi mmoja au pale Muhimbili (kama si kwa Kairuki kama unao mshiko), na hapo ukifika huduma za matibabu zinahuzunisha, tunashuhudia watanyika na Wazanzibari walio masikini wanavyo hangaika sana kutafuta huduma hizo, kwa vile hawana uwezo wa kugharimia matibabu yao ikiwemo kujinunulia dawa wanazo andikiwa na madaktari. Waliolazwa nao usiku ukifika kazi kusikiliza vilio vya mapaka tu nyau nyau baaasiii...

Zanzibar na hata huku Tanganyika, kumekuwepo na ucheleweshwaji mkubwa wa mishahara ya wafanyakazi ambayo tangu hapo ni midogo mno na haitoshelezi mahitaji ya lazima ya wafanyakazi hao. Huduma za maji na umeme zimekuwa mbaya mno. Hali ya skuli zinahuzunisha kwa walimu kukosa hamu ya kufanyakazi kwani walimu hawana vitendea kazi hata vya kuazima. Kwa kweli viongozi wa Tanganyika na SMZ inabidi wabadirike sasa wasisubiri mpaka wabadilishwe na wananchi kwani itapofikia wananchi kusema HAPANA wajue kiama chao kiatanzia hapa hapa duniani, Ahera zitaenda hesabu tu...

UBAGUZI:
Kuhusu ubaguzi ulikuwepo tangia hapo mwanzo kabla ya muungano. Sina maana kuwa nautetea muungano la hasha lakini palipo na kweli tutaweka kweli. Ubaguzi ulilwetwa na ukoloni wa kiingereza, kwani ni kawaida ya wakoloni popote ulimwenguni wanapotawala, lazima watumie mbinu za kuwagawa wananchi (ili waendeleze utawala wao) Ikiwa kwa njia za kidini, ukabila, rangi, utajiri, uwezo wa kimaisha na hata kimadhehebu. Katika Zanzibar Muingereza alitumia njia za kuwagawa wananchi kwa kutumia asili za makabila yao. Aliwafanya wenye asili za Kiarabu wajione kuwa wao tu ndio wenye haki za utawala kwa sababu Mfalme wa nchi anatokana na asili yao. Aliwafanya Washirazi yaani, Wahadimu, Watumbatu na Wapemba wajione kuwa wao tu ndio wenye kila haki za nchi kwa sababu wao ndio waliowaita Waarabu kutoka kwao Oman kuja kuwasaidia kumuondoa Mreno. Aliwafanya Waafrika (weusi) wajione kuwa wao tu ndio wenye kustahiki utawala wa Zanzibar kwa vile Zanzibar imo katika Bara la Afrika. Na uchumi wa nchi akawapa wenye asili za Kihindi, wananchi walianza kujigawa mafungu mafungu na walianza kufungua Jumuiya zao za Kikabila. Waarabu walifungua yao, Washirazi walifungua yao, Waafrika walifungua yao na Wahindi walifungua yao na Wangazija wakafungua yao. Na ndani ya hizo hizo, zilijitokeza zengine na kila moja ilikuwa ikijitapa kwa upande wake. (Zambi hii ya ubaguzi ndo inawala mpaka leo wazanzibar…!! Na kuiondoa itakuwa kazi kubwa kuliko wanavyo fikiria). Japokuwa baadae jumuiya ya kiarabu ilipeleka pendekezo amabalo lilikataliwa na muingereza la kutaka kila mtu awe na haki sawa ya kupiga kura na waache kuwachagulia wajumbe wa kwenye Baraza la Kutunga Sheria. Lakini haya yote yeshapita, kinachotakiwa wazanzibar waondoe kwanza tofauti zao wenyewe. Mimi siamini kuwa wanaoipenda CCM wote ni kutoka Unguja tu, hata wapemba wamo, na hata hiyo CUF hata waunguja pia wamo. Lakini kutoka na wenyewe kuacha Uislam wao na kukumbatia siasa za chuki na jazba leo hii hakuna masikilizano. Kila kukicha Watanganyika.... Watanganyika... Watanganyika...!!! Ndugu zanguni Imani bila matendo itakufalia kitu gani? Dunia ya sasa inataka matendo na si maneno matupo....


Mada hizi nilikwisha ziandika kule zanzibarwebsite... ila hapa nimezifanyia mabadiriko kidogo ili ziendane na mustakabari tunaotaka kuuzungumzia. Nahisi tutakuwa tumepata mwanga kwa kiwango fulani...!!​
 
Unasubiri Nini Besty!!!!? aaaaaaaah!...
Maliza kazi...ni mawazo tu.....alie sahihi tumfuate.....

Uongo hauna nafasi tena!!
 
Tuaminiane...na anae aminiwa abebe dhamana ...kweli!!! kwa moyo wake WOTE!!!!...uongo Hauna nafasi!!
 
Ni kweli!!!....sio tu kwenye muungano wetu hata katika mambo mengi hapa Duniani.....
 
haya mambo yanaitaji busara zaidi kuyajadili... ila nvyojua mijazba itakuwa mingi tu humu...!! tusubiri tuone...
 
Mimi nina jambo moja linanisumbua sana kila ninaposoma mada zinazo husu muungano haswa kule zanzibarwebsite. Wazanzibar wengi wanatuhumu kuwa muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar unawaletea dhiki ya hali ya juu sana, kiuchumi na kiutamaduni. lakini mie nashindwa kuelewa hivi kweli Tanganyika inafaidika na nini katika muungano huu?

Hali ya uchumi Zanzibar inajulikana kuwa hakuna rasilimali za kutosha kuendeleza nchi. Zamani kulikuwa na karafuu. Tena karafuu ya znz ilikuwa ni ya kiwango bora kabisa. Leo hii karafuu ya znz haina thamani kama ile iliokuwa nao, isitoshe bado viongozi wa znz wanajirimbikizia kununua wao karafuu yote ya znz kwa pesa kidogo sana kiasi hata mkulima hafaidiki na jasho lake, na bado waznz wanalahumu muungano. Hebu tupeni sababu yakinifu ni vipi Muungano umedumaza maendeleo ya znz. Leo hii waznz wengi wamejazana Tanganyika, wamefungua maduka na ni wafanya biashara wazuri tu, na hii ni kwa sababu Population ya Watanganyika ni kubwa na soko la bidhaa ni la kutosha [(http://www.tanzania.go.tz/censusdb/index.html). Watanganyika wapo 33, 461, 849, ukilinganisha na Waznz 981, 754. Waznz wanafanya 29.32% ya Watanzania wote, walioko TZ].

Sasa ni kwa nini Biashara hizo zisifunguliwe Pemba na Unguja? Au kwa sababu waznz wengi wapo nje ya bara la Afrika (UK, Canada na USA?), Je ni wangapi leo hii wameendeleza kwao? Mimi nadhani tatizo lipo kwa viongozi na wananchi wenyewe wa znz. Kwani hata maadili ya Uislam hakuna siku hizi na hii hipo chini ya waznz wenyewe wala si swala la muungano. Kuna haja ya waznz kubadilika sasa, waondoe chuki zao kwanza za upemba na uzanzibar. Waachane na haya mambo ya CUF na CCM, na nguvu zao waelekeze kwenye Undugu wao, ndio utawakomboa. Siasa za kiafrika bado sana haziwezi kuwaletea ukombozi hata kidogo.

Watanganyika na wazanzibar wana mahusiano ya muda mrefu sana, kuna Watanganyika ambao wameo Zanzibar au kuolewa na pia kuna Wazanzibar ambao wameoa au kuolewa Tanganyika. Kwa asili duniani kote hakuna mwenye asili ya visiwani, wakazi wa visiwani wote ni waamiaji kutoka bara pamoja na sehemu zingine za mwambao wa pwani. Haya majina ya Zanzibar, Pemba, na Unguja unajuwa asili yake? Je unajuwa wakazi wa mwazoni wa visiwa vya pemba? Neno Pemba lina asili ya Msumbiji. Au neno Mkanjuni linatokana na neno la kimakonde lenye maana ya mkorosho.

Je uoni kuwa inawezekana kuwa wakazi wa pemba wana asili ya bara?

Wazanzibar wengi wanajinasibisha na Uarabu zaidi kuliko uafrika wao, je nikisema kuwa haya ni mawazo ya kitumwa nitakosea? Mnapowatukana watu kutoka bara mnajitukana wenyewe...., Wengi wao huwakumbatia waarabu, washirazi na baadhi ya wahindi kuwa asili yao Zanzibar na kuwabagua wanaotoka Tanganyika. Hawa waarabu, washirazi na wahindi na watanganyika ambao leo hii ni raia wa zanzibar ni nani yupo karibu zaidi na zanzibar. Possibility ya uhamiaji ya mtu toka Tanganyika na anayetoka Asia ni nani mgeni? Fikra za ubaguzi, ubwana na utwana ndizo zinawala mpaka leo wazanzibar kuiondoa itakuwa kazi kubwa kuliko wanavyo fikiria.

Mnisamehe... Ni mawazo tu...
 
JJ.....muungwana alivyoingia madarakani alikiri kuwa muungano una matatizo na amelifanyia kazi hilo suala ndio maana amemteua EL na bwana nahondha kukaa pamoja kuongelea hili suala,kuwa na subra ndugu yangu huenda muafaka ukapatikana.
 
Kuna kitu ambacho mimi huwa kinanitatiza,hivi makubaliano yote yaliyopitishwa na waasisi wa muungano yaliwekwa wazi ama ni siri kwa raia wengine? maana tusije kuwa tunabishana wakati jamaa walikubaliana zaidi ya tunayoyaona hadharani.

Kitu kingine ni contribution ya nchi zote mbili kwenye muungano maana from my understanding I believe SMZ wanapata ruzuku kutoka bara9I could be wrong on this)
 
Muhandisi,

kweli unaamini kuwa EL na Nahodha wanaweza wakaleta suluhisho... ok let wait and see
 
Admin!
Kuna mada mbili za muungano hapa ,Tafadhali zifanyie maarifa ili tuchangie kwa mtiririko mzuri bila ya kuitawanya michango huku na huku na kupoteza muelekeo.
 
Tatueni kero za Muungano kabla ya Shirikisho`

2007-03-17 09:26:00
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar


Rais wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar, Bw. Abdalla Abbas, amesema Tanzania haipaswi kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki kabla ya kutatuliwa kero za Muungano.

Aliyasema hayo jana katika semina ya uhamasishaji wananchi kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel, Zanzibar.

Semina hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha.

Alisema kero za Muungano zimekuwa za muda mrefu, hivyo kuingia katika mfumo wa Shirikisho wa nchi wanachama wa Jumuiya kabla ya kutatua kero hizo kunaweza kuleta msuguano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

``Kuna haja ya misuguano iliyopo katika Muungano iondolewe kabla ya Tanzania kuamua kujiunga katika Shirikisho la Afrika Mashariki,`` alisema Rais huyo.

Alisema Zanzibar imekuwa ikisahaulika katika mipango ya miradi ya maendeleo inayoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mfano wa mradi wa maendeleo ya ukanda wa Ziwa Victoria.

Alisema iwapo Zanzibar ingehusishwa katika mradi huo, ingeweza kunufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na mazingira yake, hasa katika kupata mbinu bora za matumizi ya bahari na uzalishaji katika sekta hiyo.

Akichangia katika semina hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshugulikia Fedha na Uchumi, Zanzibar Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema wafanyabiashara wa Zanzibar wamekuwa wakipata vikwazo wanapopeleka mizigo yao katika soko la Tanzania Bara.

Alisema kuna haja ya vikwazo hivyo kuondolewa ili pande zote ziweze kunufaika na sekta ya biashara.

Alieleza kuwa suala la ushuru katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki linahitaji kuangaliwa kwa umakini mkubwa kwakuwa Zanzibar haitanufaika na sheria ya kulinda biashara inayozalishwa ndani kama ilivyopitisha katika Jumuiya hiyo.

Waziri Makame alisema Zanzibar inategemea bidhaa za unga, mchele na sukari kutoka nje ya nchi na kama itatumia bidhaa hizo kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo wananchi wataumia kwa vile zinauzwa kwa bei kubwa ikilinganishwa na zile zinazotoka nje ya nchi.

``Kuwalazimisha wananchi wa Zanzibar kununua bidhaa kutoka ndani ya nchi wanachama ni kuwazidishia mzigo,`` alisema Waziri Mwinyihaji.

Alisema jambo la msingi ni kuinua uwezo wa wazalishaji wa ndani, hasa katika sekta ya kilimo ili bidhaa wanazozalisha ziweze kupatikana kwa gharama nafuu.

Hata hivyo, viongozi wa kisiasa katika semina hiyo walisema bado kuna haja ya Zanzibar kuwa mwanachama katika Jumuiya hiyo kwa kujitegemea badala ya kuingia kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano.

Mwakilishi wa jimbo la Matemwe (CCM), Ame Mati Wadi, alisema haoni sababu kwa Zanzibar kutopewa fursa ya kujiunga na Jumuiya hiyo kama mwanachama anayejitegemea.

Alisema inashangaza kuona nchi za Rwanda na Burundi zimepewa nafasi ya uanachama katika Jumuiya hiyo, lakini Zanzibar haipewi.

SOURCE: Nipashe
 
JK gave many political statements lakini he cannot act at all . Aliyasema haya na anayajua kwamba yako lakini alijikanyaga pale kweney semina elekezi kwamba hapakuwa na mpasuko . Sasa swala hili ni zito mno ndani ya CCM hawawezi kuchukua maamuzi ya manufaa kwa Taifa na ukweli ni kwamba if possible tuachane na Zanzibar wawe na Nchi yao na sisi tubakie Tanganyika badala ya makelele yasiyo kuwa na maana kila mara .
 
Honourable Omar Sheha, Mussa [ CCM ]
Chumbuni Constituency

Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi hii ya kuchangia kwa maandishi chini ya Kanuni ya 49(7) na kwamba nakupongeza wewe kwa kuteuliwa kwako kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mwaka 2005 hadi 2010.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru wananchi wa Jimbo langu la Chumbuni kwa kunichagua kuwa Mbunge wao kwa kipindi hiki cha 2005 hadi 2010; na kwa jumla nawashukuru vile vile kukipa ushindi Chama cha Mapinduzi kule Jimboni kwangu Chumbuni kwa nafasi ya Rais na ya Mbunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 uliofanyika tarehe 12 Desemba, 2005.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasa naomba kuchangia hotuba ya Rais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ukurasa wa 16 hadi 17 juu azma yake ya kuimarisha Muungano wetu pamoja na kuondoa kero za Muungano zilizobakia na kuiwezesha Zanzibar kupata maendeleo zaidi ya kiuchumi katika kipindi chake cha Awamu ya Nne ya Serikali ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, katika kuteleleza azma hiyo ya kuondoa kero za Muungano na kuisadia Zanzibar ipasavyo, basi mambo yafuatayo yazingatiwe:_

(a) Uhusiano wa kifedha uliokuwepo baina ya iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kabla ya Muungano wa mwaka 1964 na baada ya Muungano wetu Aprili, 1964.

(b) Utaratibu wa sasa ulioleta kero, hasa kwenye eneo la kodi za Muungano (Fiscal Policy) ambapo nahisi ndio kero kubwa baina ya pande mbili.

(c) Kutekeleza na kufanya jitihada za kuondoa mambo ambayo ni vikwazo vya Muungano wetu kama ilivyokwishaamuliwa kwenye taarifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, taarifa ya Kamati ya Shellukindo ya tarehe 27 Septemba, 1994, ambayo ni taarifa ya Serikali ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikifuatilia nini kilitokea baada ya Muungano wetu wa hiari, hasa mahusiano ya kifedha yalivyokuwa baina ya pande zetu mbili baada ya Muungano wa Aprili, 1964. Serikali zote mbili, ile ya Mapinduzi Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano, walikuwa ni Wanachama wa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (East African Currency Board).

Mheshimiwa Spika, baada ya Uingereza (waliokuwa watawala wa eneo la Afrika Mashariki) kuzipa uhuru nchi zote nne za Afrika Mashariki - Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar mnamo kipindi cha miaka 1961 hadi 1963, nchi zetu mbili (ambapo sasa ni moja inayoitwa Tanzania), zilimiliki mtaji kwenye Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki, ambao ulirejeshwa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, mnamo mwaka 1992 hadi 1994 pande mbili za Muungano zilikubaliana kuwa IMF, Shirika la Fedha la Dunia, wapewe kazi ya kuchunguza uhusiano huo wa kifedha na katika ripoti yao ya Machi 1994, ilishauriwa kuwa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 1965 ibadilishwe ili Zanzibar nayo kupewa haki ya hisa zake kwa mujibu wa mtaji wake uliorejeshwa Tanzania kutoka Bodi hiyo ya Sarafu ya Afrika Mashariki mwaka 1966 hadi 1972.

Mheshimiwa Spika, baada ya kazi hiyo na Ushauri wa IMF ilikubaliwa na pande zetu mbili kuwa tusitazame nyuma kwa kuepuka kugombana, bali tupige mstari na kukubaliana yafuatayo kuanzia mwaka 1994 (Miaka 30 baada ya Muungano wetu):-

(a) Tuwe na Benki Kuu moja, Sarafu moja;

(b) Tuwe na Mamlaka Moja ya Fedha, Sera moja ya fedha; na

(c) Tuwe na usimamizi mmoja wa Mabenki na vyombo au Taasisi za Fedha.

Mheshimiwa Spika, hayo yalitekelezwa na pande zote mbili na kuanzia Julai, 1995 sheria mpya ya BOT ilianza kutumika pande zote mbili za Tanzania na kuiwezesha Zanzibar kupata gawio la 4.4% pamoja na kufungua na kuweka hesabu zake ndani ya Benki hiyo hadi sasa.

Mheshimiwa Spika, mgao huo wa faida ya BOT kwa Zanzibar, mwaka 1995 ulifanywa kwa formula ya muda tu na ripoti yenyewe ya IMF ya Machi/Aprili 1994 ilieleza hayo. Sasa ni miaka kumi na nne imepita bado gawio la Zanzibar limebaki pale pale. Hili ni kero kubwa la Muungano.

Mheshimiwa Spika, ili kuondoa kero hiyo kubwa kuliko zote, Tume ya Pamoja ya Fedha (Joint Finance Commission) iliyokwishaundwa chini ya kifungu cha 134 cha Katiba ya Tanzania, sasa imalize kazi yake ya kupendekeza kwa Serikali zote mbili, ili kuona mgao wa hisa wa Zanzibar unaboreshwa na kufikia angalau ya 11% au zaidi, kama mtaji wa Zanzibar ulivyokuwa ndani ya Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki, ambao umetajwa kwenye Ripoti ya IMF (Appendix II) ukurasa wa 16.

Mheshimiwa Spika, yakifanyika hayo kwenye eneo la uhusiano wa kifedha, basi Tanzania itakuwa imeondoa kabisa kero hiyo kubwa ya Muungano.

Mheshimiwa Spika, kwenye eneo la Kodi za Muungano (Fiscal Sector) kero kubwa ni utaratibu wa sasa ambao uliwekwa tokea mwaka 1977. Utaratibu wa sasa ambao unatekelezwa na SMT na ambao unaumiza upande mmoja na utaratibu huo ni wa kubakisha kodi za bidhaa zinazozalishwa Tanzania Bara na ambazo hutumika kwa wananchi wa Zanzibar (Consuming Area) kodi hizo kubakia Bara. Bidhaa kama Sigara, Bia, Saruji, Soda na kadhalika, kodi za Viwandani VAT na Excise Duty ambazo ni kodi za forodha, ni vyema sheria zote husika zibadilishwe katika Awamu hii ya Nne, ili kero hii iondoke, kwani Zanzibar hainufaiki pamoja na kodi ya mapato (PAYE).

Mheshimiwa Spika, endapo Serikali ya Muungano itafanya mabadiliko hayo kwenye sekta ya fedha (Monetary) na sekta ya Kodi (Fiscal) basi Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne pamoja na Bunge lake hili, itawezesha Zanzibar kufaidika milele na kudumisha Muungano wetu kwa kuondoa kero hizi. Zanzibar nayo, itaweza kulipa mchango wake wa Muungano kutokana na Mapato yatokanayo na Monetary/Fiscal Sector.

Mheshimiwa Spika, yote hayo ili yatendeke, Tume ya Fedha ya Pamoja, ambayo sasa imeanza kazi zake, iharakishe hayo na Wizara za Fedha na Muungano zishirikiane kusimamia hayo na mapendekezo ya awali yaanze kutekelezwa angalau kuanzia Julai, 2006

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo, naunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa tarehe 30 Desemba, 2005.
 
Honourable Salim Hemed, Khamis [ CUF ]
Chambani Constituency

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madini ni Wizara muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi wa kisasa, uchumi endelevu. Hakuna mwekezaji yeyote awe wa ndani au wa nje atakayekuja kuwekeza ikiwa upatikanaji wa umeme sio wa uhakika. Kwa hiyo, Wizara kutokana na matatizo yaliyoikumba nchi yetu mwaka 2006 na mwaka 2005, athari zake kiuchumi zimeonekana wazi, hivyo Wizara haina budi ikajiandaa kikamilifu kwa Bajeti hii ili mapungufu hayo yasijitokeze tena.

Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huu sasa nianze kuchungia.

Kuhusu Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC). Hili ni Shirika muhimu sana Tanzania kama vile NDC kwa sababu ndiyo chombo pekee hapa nchini chenye mamlaka ya kufanya utafiti wa mafuta ya gesi. Naipongeza Serikali kwa kutatua tatizo kubwa la Ofisi pale TPDC baada ya malumbano marefu kupatiwa sehemu ya jengo la Mafuta House kwa ajili ya kutunza nyaraka muhimu za Kampuni za Miamba (Siemic Data).

Mheshimiwa Spika, pamekuwa na malalamiko mengi sana kuhusiana na suala la mafuta na gesi hasa upande wa Zanzibar. Hii inatokana na mambo mengi, lakini kwa upande wa Kambi ya Upinzani kuhusiana na suala hili, sisi tunajiuliza suala moja tu ambalo naamini Mheshimiwa Mbunge wa Chama Tawala nao wanajiuliza au wanapaswa kujiuliza pia kwamba TPDC ilianzishwa kwa Government Notice No. 140 ya tarehe 30 Mei, 1969 Act No. 17 ya mwaka 1969 ya Mashirika ya Umma. Maana yake ni kwamba TPDC ni Shirika la umma na sio Shirika la Muungano. Lakini pia TPDC linafanya kazi chini ya Wizara ya Nishati na Madini ambayo nayo sio ya Muungano. Lakini katika ibara ya 4(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyongeza ya kwanza mafuta na gesi vimetajwa kuwa ni vya Muungano.

Mheshimiwa Spika, sasa itakuaje vitu vya Muungano vishughulikiwe na Shirika na Wizara zisizokuwa za Muungano? Sio ukiukwaji mkubwa na wa makusudi wa Muungano kwa vyombo ambavyo sio vya Muungano. Hili ni moja kati ya kero za Muungano na vyombo husika, lazima kutatua kero hii.

Mheshimiwa Spika, sheria ya uchimbaji wa mafuta, The petroleum exploration and production Act, inatamka kwamba itafanya kazi Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Lakini kuna tetesi kuwa iliridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano, lakini haikuridhiwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kama hili ni kweli, hali hii itakuaje?

Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika Zanzibar Laws Decree 1951, pamoja na regulation ya mwaka 1952 kuhusu mining (mineral) ambayo ndiyo iliyotumika tarehe 16 Desemba, 1953, British Resident for Zanzibar kwa wakati ule Visiwa vya Unguja na Pemba, Decree hiyo hadi hii leo haijafutwa na pia imetamka waziwazi kwamba mafuta yakipatikana ni mali ya Zanzibar. Je, huu sio mgongano mwingine mkubwa wa kikatiba?

Mheshimiwa Spika, swali la uwakilishwaji wa Zanzibar, hivi sasa Serikali ya Zanzibar ina uwakilishi dhaifu katika Serikali ya Muungano. Huwezi kusema kuna u-member wa Bodi wanaowakilisha maslahi ya Zanzibar. Mjumbe wa Bodi anaweza akawa ni mtu yeyote. Je, katika TPDC na katika Wizara ya Nishati na Madini vyombo vyenye mamlaka ya mafuta na gesi vinawawakilishi gani kutoka Zanzibar, ambao unaweza kukubali kama mdau au kukataa kwa maslahi ya Zanzibar na kwa mujibu wa sheria ya nchi. Zanzibar inafaidika vipi? Huwezi kusema kuwa Zanzibar inafaidika na umeme wa gesi kutoka Ubungo, ambao huingizwa katika grid ya Taifa na baadaye kupelekwa Zanzibar.

Kwa taarifa, Zanzibar inanunua umeme huo kama ambavyo Mombasa itaweza kununua au Mji mwingine wowote wa nchi ya jirani. Faida halisi ya gesi itapatikana ikiwa zitajengwa pipelines hadi unguja na Pemba ambako vitajengwa vinu vinavyoweza kutumia gesi kule tena, kwa gharama za Mfuko huo huo wa gesi. Hii itahakikisha upatikanaji endelevu wa umeme Visiwani na kuacha kuitegemea submarine cable iliyopo sasa ambayo tayari imezeeka. Nashukuru sana.
 
tatizo si kuachana wakati tushazaa, ni kurekebisha hizi kasoro na kukiandaaa kizazi chetu katika mustaqabali mwema.
 
Back
Top Bottom