Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?

MKJJ

Tunaomba utuwekee ya draft Umoja wa kuunganisha EAC ambayo inajadiliwa sasa.
 
Wabunge waibana Serikali kuifanya Z’bar nchi ya kigeni

HabariLeo;
February 01, 2007


KERO za muungano zinazidi kubainishwa na kuwakera wabunge na sasa wamehoji taratibu za Mamlaka ya Mapato (TRA) kuifanya Zanzibar kama nchi ya kigeni.

Mbunge wa kwanza kukerwa na hali hiyo ni Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) ambaye alihoji utaratibu wa TRA wa kutoza ada ya dola za Marekani 2,500 kwa watu wanaotumia gari zenye namba za Zanzibar zinapotumia barabara ya Tanzania Bara na kuwahesabu kama raia wa kigeni.

Dk. Mwakyembe ambaye alidai kuwa na fomu za TRA mkononi wakati anatoa hoja yake alisema fomu hizo zinaonyesha upungufu huo ambao aliita ni dosari katika Muungano. Alisema Muungano wa kweli unaonyeshwa katika bishara ya ndani pamoja na matumizi ya sarafu moja.

Mbunge huyo alisema miaka 42 ya Muungano, bado dosari hiyo ipo na akahoji Serikali imekuwa inafanya mipango gani kuondoa dosari hizo ambazo alisema zinachochea hisia ya migongano badala ya maelewano.

Katika eneo lingine ambalo Dk. Mwakyembe alilizungumzia ni uamuzi unaofanywa na Naibu Kamishna wa TRA aliyepo Zanzibar kutokuwa na uzito kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia Zanzibar ambapo ushuru wa bidhaa hizo hukadiriwa upya mara zinapoteremshwa Tanzania Bara.

Alisisitiza kuwa kiutendaji TRA inaichukulia Zanzibar kama nchi ya kigeni na akahoji utaratibu huo wa kuichukulia Zanzibar kama nchi ya kigeni kuwa unakiuka Katiba ya nchi na hati ya muungano. Mbunge mwingine ambaye alizungumzia eneo hilo ni Mbunge wa Kwamtipura, Zuberi Ali Maulid (CCM) ambaye naye aliitaka Serikali kutoa tamko kuhusiana na kasoro hizo.

Alisema yeye ni mwathirika mmojawapo katika siku za hivi karibuni baada ya kutozwa ada hiyo ya dola za Marekani 25,000. Hoja za wabunge hao zilionekana kumwingia Waziri Mkuu Edward Lowassa, ambaye alilazimika kusimama baada ya majibu ya Naibu Waziri wa Fedha, Abdisalaam Khatib na kueleza kuwa kero hiyo ambayo imeelezwa kwa upana na wabunge itazungumzwa kwenye Kamati ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi.

“Hoja ya Mwakyembe na Maulid nazichukua na nawahakikishia jambo hili tunalishughulikia katika mazungumzo yetu yanayoendelea kati yangu na Waziri Kiongozi,” alisema Lowassa ambaye alionekana kama kutuliza jazba za wabunge ambao wakati fulani waliguna wakati Khatib anatoa majibu ya nyongeza.

Kitendo cha wabunge kuguna wakati Naibu Waziri huyo anatoa majibu ya nyongeza hakikumfurahisha Spika na kuingilia kati: “Waheshimiwa wabunge Oda tafadhali naomba usikivu wenu.” Awali akijibu hoja za wabunge hao, Khatib alisema tofauti hizo zilikuwepo kutokana na Zanzibar hapo awali kutotumia mfumo wa Asycuda II+ wakati Bara wanatumia mfumo huo.

Alijitetea kuwa kwa sasa mfumo huo tayari umewekwa Zanzibar na tatizo hilo limemalizika.

“Ambaye ana tatizo baada ya mfumo huu kuanza ajeanieleze,” Alisema na kusababisha wabunge kuguna. Pia alifafanuakuwa ukaguzi wa bidhaa kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam unalenga katika kuhakikisha kuwa bidhaa zote zinazoingizwa Tanzania Bara zinafuata utaratibu ulio sawa kwa ajili ya kuleta ushindani wa soko ulio huru na wa haki kwa bidhaa kutoka pande zote mbili
 
BILA KUANGALIA HISTORIA YA ZANZIBAR, MUUNGANO NI NDOTO

Na, Antar Sangali,Bagamoyo

Zanzibari yaani Unguja na Pemba ni Taifa dogo lenye historia pana kuliko nchi nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Na bila kuangalia Historia ya Zanzibar kiundani ni vigumu sana kukiunganisha kisiwa hicho kisiasa na kudumusha Muungano wa Tanzania uliodumu kwa miaka thelathini na mbili (32).

Historia ya Zanzibar kabla na baada ya kupita Mapinduzi ya mwaka 1964 unaweza kuita ni historia inayowahusisha majini na wanadamu katika jumla ya maisha na ustawi wa maendelo [yao] iwe kisiasa , kijamii na kidemokrasia. Na ikiwa unaweza kuanza katika kubaini kiini cha historia ya kweli bila shaka unaweza kuijua na kuitambua vema Zanzibari yaani Unguja na Pemba, watu wake, akhlaq zake , silka na viongozi wake waliopita, waliopo, na wanaopigania kushika utawala. Kiufupi, Zanzibar ilikuwa na makundi ya kijamii, kikabila, na kirangi tokea zama na zama kulingana na maisha ya watu wake na maendeleo yao siku baada ya siku.

Zanzibari [Unguja na Pemba] ni visiwa vilivyobeba hazina kubwa ya historia yenye mchanganyiko mkubwa wa damu katika vizazi vya jamii yao, na hilo si jambo linaloweza kubezwa na kupuuzwa unapojaribu kuzungumzia hali ya Muungano. Zanzibar hailingani japo thuluthi kihistoria na Tanganyika nchi ambayo imeungana na Zanzibar na kupatikana kwa Taifa la Tanzania April 26, 1964.

Mfumo wa vyama vingi vya siasa ulipoanzishwa chini ya Sultan ukisimaiiwa na katiba ya Kiingereza, vyama vya siasa vilivyoanzishwa vilikuwa na sura ile ile ya makundi na hata kupelekea majina ya vyama hivyo kuwa na majina ya kikabila mathalan African Association (AA) na Afro Shiraz party (ASP). Joto la kisiasa lilipelekea kuanzishwa kwa vyama vingine baadaye vya Zanzibar National Pary (ZNP) Chama cha Kikomonisti cha Zanzibar, Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP) na UMMA.

Mfano, Chama cha ASP kilichoanzishwa mwaka 1957, ZNP 1955, ZPPP 1959 na UMMA 1963 wagombea wake walitokana na vyama vyao au Jumuiya za kidini na kikabila. Sher M. Chowdhiry alisimama kwa Muslim Association, Ibun Saleh alisimamishwa na Comoria Association na baadhi ya wagombea wengine walisimama kama wagombea binafsi mathalan Anverali Mukri, Abdullah Busaidy, Abdul Mukri na Haji Juma.

Katika uchaguzi Mkuu mwaka 1957 ASP kilichoongozwa na Abeid Aman Karume kilipata jumla ya kura 45,172 sawa na asilimia 50.6 , na ZNP cha Ali Mokhsin Al-Barwan kikapata 31,681 sawa na asilimia 35.5. Lakini katika mwaka 1961 ASP ilipata jumla ya kura 53,232, ZNP 26,572,na ZPPP cha Mohamed Shamte aliyejiengua toka ASP kilipata 4,57 .

Swali kubwa la msingi la kujiuliza ni kwaniniMapinduzi mwaka 1964 yalitokea licha ya ushindi waliopata ZPPP baada ya kuunganisha viti vyao na ZNP na kuunda serikali ili kupewa uhuru toka katika koloni la Kiingereza lililokuwa likilinda maslahi ya utawala wa Kisultan tokea mwaka 1890?

Kundi la wananchi waliokuwa weusi waliunganishwa pamoja na ASP katika kuhakikisha wanapata haki za kujitawala na ustawi wa kumiliki uchumi na njia kuu za uzalishaji mali na vitega uchumi ili kuondokana na Umwinyi na Ubwenyenye uliokuwa ukihodhiwa na kundi la waarabu na machotara.

Waafrika weusi hawakuhisi abadan kama walikuwa na haki katika visiwa hivyo na hivyo kuweka mkazo zaidi wa kuweza kupata madaraka ya utawala na hasa ukichukulia wakati huo vuguvugu la mabadiliko ya ukombozi duniani na hususan Barani Afrika kuanza mara bada ya kumalizika vita ya pili ya dunia.

ASP iliona madaraka ya utawala chini ya ZNP na ZPPP ni sawa na kubaki hisia zile zile za utawala wa Kiingereza na Kisultan katika Zanzibar na hivyo kulazimika kuandaa Mapinduzi yaliyomwaga damu za watu na hatimaye kupata nafasi ya kushika utawala uliowaunganisha wazanzibar wote katika umoja na maelewano mapya visiwani humo.

Mapinduzi ya ASP yalitimia kwa mchango mkubwa wa kundi la vijana wasomi na wanasiasa wa siasa za Lenin na Karl Max waliojiengua toka Umma Party wakiongozwa na Mjamaa Abdulrahman Babu hadi kufanikiwa kwa Mapinduzi hayo 1964.

Hasama, chokochoko na chimbachimba za kisiasa huku Wazanzibar wakizidi kuhitalafiana ilizidi kuchukua sura mbaya zaidi zikianzia ndani ya ASP yenyewe, wakaanza kunyoosheana vidole vya kutaka kupinduana na wengine kukamatwa na kufungwa magerezani katika mahakama za ‘kimapinduzi” ambazo hazikuwa na mifumo ya sheria ili kupima haki na wajibu kwa wafungwa.

Viongozi kadhaa waliokuwemo katika serikali ya kwanza ya Abeid Aman Karume walianza kuhitalafiana wakiwemo aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais Kassim Abdula Hanga, na wengine akina Othman Shariff, Saleh Saadalah, Mdungi Ussi, Jaha Ubwa, Idrisa Majura na wengine kadhaa wakasehelea magerezani ambapo hakukuwa na mifumo ya sheria ili kupima haki na wajibu.

Mwaka 1964 yakapita mapendekezo ya kisisaa katika kujenga Muungano wa Taanzania na Zanzibari, Mwalimu Nyerere na Mzee Karume walikubalina katika mambo kumi na moja [eleven articles of Union] na masuala hayo yapitiwe na kutazamwa upya na pande zote mbili iwapo yanakidhi haja ifikapo mwaka 1974.

April 7, 1972 Rais wa kwanza wa Visiwa hivyo Karume alipigwa risasi na Luten Homoud Mohamed na kumpotezea maisha yake. Kundi kubwa la viongozi waliohusishwa na tuhuma walikamatwa ma wengine kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Sheikh Aboud Jumbe akashika madaraka kurithi kiti cha Karume na ulipofika mwaka 1977 Jumbe alikubali rai ya Julius Nyerere ya kuunganisha vyama vyao vya ASP na TANU kwa maslahi ya mataifa yao na kujenga umoja zaidi wa kitaifa, CCM ikazaliwa. Lakini hili linatajwa na wasasisa wajuzi kama ulikuwa ni mpango wa kuikinga serikali ya Mapinduzi isipinduliwe tena na kundi lililopinduliwa mwaka 1963.

Jumbe na Nyerere walihitalafiana katika dhana nzima ya muundo wa Muungano. Ni wazi kwamba Jumbe hakuafiki utekelezaji wa makubaliano 11 ya Muungano uliosainiwa na Karume na Nyerere mwaka 1964 na kuamsha hoja ya kuwepo kwa serikali tatu. Mwalimu Nyerere msimamo wake ulikuwa ni serikali mbili kuelekea moja huku Jumbe na Waziri wake Kiongozi Ramadhan Haji Faki wakisisitiza 1+1=3 Nyerere akisema 1+1 siku zote ni = na 2.

Lakini Jumbe na Faki wakati wakiingia katika kikao cha Kamti Kuu ya CCM Taifa tayari nyaraka za hoja ya Jumbe zilikuwa mikononi mwa Nyerere alizopelekewa na Seif Shariff Hamad akimtuhumu Jumbe kuandaa kuvunja Muungano. Mtafaruku mkubwa ulizuka, mchafuko na hali mbaya ya hewa ya kisiasa ikatangazwa kuikumba Zanzibar na hatimaye Jumbe akalazimishwa kujiuzulu Dodoma bila ya ridhaa ya ASP ili kulinda maslahi ya umoja wa kitaifa na Muunagno wa Tanzania. Macho ya seif na kundi lake lililojiita Progressive la akina Shaaban Mloo, Ali Haji Pandu, Khatib Hassan likamezea mate na kuona huo ni wakati wao muafaka wa kukalia kiti cha utawala wa Zanzibar. Kinyume na matarajio yao kundi la Liberators la akina Abdalla Natepe, Nassor Moyo, Said Bavuai, Ahmed Ameir, Khamis Daruwesh na wengine wakaibaini dhamira hiyo ya vijana kukataa mgombea asitoke katika kundi hilo.

Kimsingi matumaini ya Seif Sharif Hamad baada ya kutupwa na Idris Abdul Wakili yalianza kuamsha upya mjadala ma mabishano makali ya kisiasa na ndipo kundi toka Pemba lilipoamka na kudai wapemba wanatengwa katika medani za Urais wa Visiwa hivyo. Kampeni za urais wa Wakili zilikumbwa na uzito na mzigo wote wa lawama akatupiwa Seif kwa kudhoofisha kampeni dhidi ya ushindi wa Wakili Pemba.

Hata hivyo kimsingi ipo semi iliyomea Visiwani humo kwamba wapemba hawatofaa kushika madaraka ya uatwala katika seriakali ya Mapinduzi Zanzibar, kwasababu hawakushiriki katika harakati za Mapinduzi na ZPPP ya Shamte ilikataa kuunganisha viti vyake na ASP ili kupata uhuru mwaka 1963.

Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM haikuridhishwa na hoja za akina Seif na kundi lake hasa za kuhoji masuala ya Muungano na hivyo maamuzi ya CCM yakawa ni heri wapinzani wao wakawa nje ya chama chao kuliko kubaki ndani ya chama hicho na kuendele kupingana kinyume na sera na msimamo wa CCM.

CCM iliwafukuza Seif na wenzake na hatimaye ikapelekea Waziri Kiongozi huyo wa zamani kuishia gerezani kwa kile kilichodaiwa baadaye kwamba alikutwa na nyaraka za siri za serikali na hivyo akabaki kizuizini kwa miaka mitatu hadi shauri lake lilipotupwa na mahakama ya rufaa Tanzania mwaka 1992.

Kufukuzwa kwa Seif na wenzake Dk Salmin Amour na Dk Salim Ahmed Salim waliona tayari mwanya kuirithi nafasi ya Wakili endapo muda wake wa kujiuzulu ukifikia jambo linalodaiwa yale mawazo ya ki-Progressive ya akina Salmin, Adam Mwakanjuki, Issack Sepetu na Salim na wengine yakafifia ghafla na kubadilisha mwelekeo.

Harakati za kudai mageuzi ya kisiasa zikaanza visiwani Zanzibar, Shaaban Mloo, Ali Haji Pandu, Maulid Makame, Soud Yusuf Mgeni wakaunda Kamati Huru ya mageuzi ya kisiasa (KAMAHURU) kwa lengo la kuishinikiza SMZ ikubali mabadiliko ya kisiasa na kufuta mfumo wa chama kushika hatamu.

Kundi hili ni kundi lililotoka katika mikono ya CCM, baadhi yao ndiyo waliyomsaliti Jumbe katika kumuona ana lengo la kuvunja Muungano, ndilo kundi lililompiga vita Wakil asiwe Rais na kudai kuna ghiliba ya kura ndani ya CCM mpaka akawa Rais wa awamu ya nne Zanzibar.

Wazanzibar wanajiuliza iwapo matlaba na matarajio yao yangeweza kutimia ndani ya CCM kundi hili lingeweza kuthubutu kutoka CCM na kuanzisha mageuzi ya demokrasia?, Au ni baada ya kufukuzwa na kushindwa kuyafikia malengo walioyakusudia ya kushika madaraka ya utawala?

Moja kati ya madai ya CUF ambako kuna kundi kubwa la waliofukuzwa toka CCM ni kwamba CCM imevuruga matakwa ya Muungano toka masuala 11 hadi kufikia zaidi ya 24 kinyume na makubaliano, dai jingine mfumo unaofa sasa ni wa serikali tatu badala ya mbili ili kuipa nafasi pana Zanzibar kujiamulia mambo yake yenyewe.

Kila mzanzibar na Mtanganyika anafungua masiko na kujiuliza: je, hivi zile hoja za Jumbe za kutaka serikali tatu sasa zimetekwa nyara na CUF? Hivi Jumbe alitoswa kiroho mbaya tu ili asiwe kikwazo cha watu kufikia matlaba na dhamira zao? Hivi ni kweli kwamba hili kundi [CUF] linalilia maslahi na kuwaunganisha wazanzibar au ni kundi linalopigania kupata madaraka baada ya kushindwa kuyapata wakiwa ndani ya CCM?

CCM inashikilia kutaka kudumisha Mapinduzi daima ya kihistoria,huku CUF inapigania na kuhakikisha uhuru uliopatikana 1963 chini ya uchaguzi uliokuwa huru na haki unaheshimiwa na kusema Mapinduzi yabaki kuwa ni historia huku wakituhumu chini ya kauli mbiu ya Mapinduzi Daima hayapatikani mazingira ya demokrasia hususan ya uchaguzi huru na haki.

CCM chini ya SMZ na SMT wanahimiza kuwa asiyethamini Mapinduzi ni msaliti na hafai japo kupewa madaraka ya Mtaa huko Zanzibar kwasababu Mapinduzi hayo ndiyo yaliyoondoa ubwama na utwana, kujenga ustawi sawia, na pia kuleta heshima kwa wazalendo wa nchi hiyo. Hayo tumeyasikia sana kila tunapokuwa tunakaribia kuelekea kwenye uchaguzi mkuu huko Visiwani. CCM inadai hadharani kuwa wapinzani hawa wa leo [Visiwani] ni wale wale waliopokonywa madaraka na ASP mwaka 1964. lakini CUF inasema haina minasaba na vyama vyote vya kizamani yaani ASP, ZNP, UMMA wala ZPPP. Je? Makundi haya mawili ni makundi yanayotazama maslahi ya nchi au yanagombania madaraka ya utawala kwa manufaa yao binafsi? Je, maneno ya Mwalimu ya kuunda seriakali ya umoja wa kitaifa huko visiwani yana nafasi kweli leo hii!?

Ni jambo la busara kutazama historia ya kisiasa huko Visiwani tukianzia enzi za ukoloni hadi leo na kisha kulinganisha na matokeo ya chaguzi zote zilizowahi kufanyaika huko ili kujua ni kwanini chaguzi hizo zimeamuriwa kwa idadi ndogo tu ya kura.

Na ingawa CCM nayo haiko radhi kuona inapoteza historia yake azizi ya kupigania Mapinduzi ya 1964, Zanzibari inahitaji viongozi na watu wake kuvumiliana, kustahamiliana, kushirikiana na ikiwezekana kuunda serikali ya pamoja kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010. Hili ni muhimu kwasababu CUF ikishindwa uchaguzi ujao itadai imeibiwa kura. Imedai hayo mwaka 1995, 2000 na 2005. Zanzibar inahitaji kutazamwa kwa macho ya huruma maana kuvurugika kwa amani visiwani humo ni mzigo mkubwa kwa upande wa Bara. Vilevile, wananchi wa Visiwani wasisahu kuwa bila ya kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano, amani na utulivu Visiwani humo ni ndoto. Maelewano ya Mpemba na Muunguja yaliyopo hivi sasa yatatokomea kama moshi ikiwa Muungano utakufa leo hii.

Mungu ibariki Tanzania!
 
Maneno,
mwambie huyo Antar Sangali kuwa historia ya Zanzibar inaaza kwetu baada ya mapinduzi...nyuma ya hapo ni historia ambayo inatakiwa tuiepuke kabisa na tuwe makini tukorudi huko!

Kabla ya Mapinduzi, Zanzibar ilikuwa haina tofauti na South Afrika chini ya makaburu ama Zimbabwe na uhuru waliopata hauna tofauti na nchi hizo chini ya Botha na Ian Smith!...
Uhuru ambao sisi Watanzania waafrika hatuutambui!
Kuijenga Zanzibar mpya ni kutazama uhusiano wa nchi hizi na kuondoa kabisa fikra za kitumwa hasa zinazoenezwa na watumwa wa mkoloni.
 
Jee tufanyeje ili kupunguza au kumaliza kabisa kero za muungano wetu

Rais wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar, Bw. Abdalla Abbas, amesema Tanzania haipaswi kuingia katika Shirikisho la Afrika Mashariki kabla ya kutatuliwa kero za Muungano.

Aliyasema hayo jana katika semina ya uhamasishaji wananchi kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyofanyika katika ukumbi wa Salama, Bwawani Hotel, Zanzibar.

Semina hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha.

Alisema kero za Muungano zimekuwa za muda mrefu, hivyo kuingia katika mfumo wa Shirikisho wa nchi wanachama wa Jumuiya kabla ya kutatua kero hizo kunaweza kuleta msuguano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

``Kuna haja ya misuguano iliyopo katika Muungano iondolewe kabla ya Tanzania kuamua kujiunga katika Shirikisho la Afrika Mashariki,`` alisema Rais huyo.

Alisema Zanzibar imekuwa ikisahaulika katika mipango ya miradi ya maendeleo inayoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mfano wa mradi wa maendeleo ya ukanda wa Ziwa Victoria.

Alisema iwapo Zanzibar ingehusishwa katika mradi huo, ingeweza kunufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na mazingira yake, hasa katika kupata mbinu bora za matumizi ya bahari na uzalishaji katika sekta hiyo.

Akichangia katika semina hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshugulikia Fedha na Uchumi, Zanzibar Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema wafanyabiashara wa Zanzibar wamekuwa wakipata vikwazo wanapopeleka mizigo yao katika soko la Tanzania Bara.

Alisema kuna haja ya vikwazo hivyo kuondolewa ili pande zote ziweze kunufaika na sekta ya biashara.

Alieleza kuwa suala la ushuru katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki linahitaji kuangaliwa kwa umakini mkubwa kwakuwa Zanzibar haitanufaika na sheria ya kulinda biashara inayozalishwa ndani kama ilivyopitisha katika Jumuiya hiyo.

Waziri Makame alisema Zanzibar inategemea bidhaa za unga, mchele na sukari kutoka nje ya nchi na kama itatumia bidhaa hizo kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo wananchi wataumia kwa vile zinauzwa kwa bei kubwa ikilinganishwa na zile zinazotoka nje ya nchi.

``Kuwalazimisha wananchi wa Zanzibar kununua bidhaa kutoka ndani ya nchi wanachama ni kuwazidishia mzigo,`` alisema Waziri Mwinyihaji.

Alisema jambo la msingi ni kuinua uwezo wa wazalishaji wa ndani, hasa katika sekta ya kilimo ili bidhaa wanazozalisha ziweze kupatikana kwa gharama nafuu.

Hata hivyo, viongozi wa kisiasa katika semina hiyo walisema bado kuna haja ya Zanzibar kuwa mwanachama katika Jumuiya hiyo kwa kujitegemea badala ya kuingia kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano.

Mwakilishi wa jimbo la Matemwe (CCM), Ame Mati Wadi, alisema haoni sababu kwa Zanzibar kutopewa fursa ya kujiunga na Jumuiya hiyo kama mwanachama anayejitegemea.

Alisema inashangaza kuona nchi za Rwanda na Burundi zimepewa nafasi ya uanachama katika Jumuiya hiyo, lakini Zanzibar haipewi.

SOURCE: Nipashe

April 26 tunasheherekea miaka 43 tangu kuungana baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Kuna matatizo mengi yamejitokeza tokea muungano huu kuasisiwa wazanzibari kwa upande wao wanahisi kuwa muungano unawanyanyasa na kuwabigija kimaendeleo na kiuchumi na na mengi tu na kwa upande wa pili wa shilingi kuna wenye hisia kuwa wazanzibari wanapendelewa sana na Tanganyika imeumizwa sana kuingia kwenye muungano huu.

Hivi sasa tukikarabia miaka 43 ya muungano wetu tumo tukijiandaa kuingia kwenye shirikisho la Afrika Mashariki.

Jee ni vipi tutaweza kupunguza kero zilizopo na kuhakikisha kila upande wa jamhuri yetu hauhisi kuwa unaburuzwa au kunyanyaswa.
 
Nionavyo mimi huu Muungano haujakuwa wazi, kuna mamabo mengi yamefichwa na kuna usiri mkubwa na wala sijui kwa nini viongizi wetu hawajauweka wazi huu Muungano kuna kitu gani hapa???

Nadhani umefika wakati kuweka kila kitu wazi wakati wa kufichana umekwisha, kama kweli tunataka kutatua hili tatizo, baada ya kila upande kulalamika unanyanyaswa au unakandamizwa.

Tuwe wakweli katika hili suala, nafikiri kungeliundwa tume ya kuchukua maoni kwa pande zote mbili za Muungano kama inavyofanywa sasa hivi katika Shirikisho la Afrika Mashariki, then waulizwe wananchi ni Muungano gani wanaoutaka, sio kuforce mambo.

Vile vile jambo jengine viongozi wangelikaa pamoja na kuyapitia tena makubaliano ya Muungano na kuona lipi linafaa kuwepo katika Muungano na lipi litolewe katika Muungano ili kutatua hili tatizo
 
Tatizo la Muungano wa Tanzania linaburuzwa kwa muungano mwingine wa EA ili watu waendelee kujificha kufanya ufisadi wao. Kama tumeshindwa kutatua matatizo yaliyopo sasa tutaweza ya nchi tano?
 
Mimi nadhani hatujawa wawazi katika Muungano wetu, kwa mfano kuna vipengele vingi tu vimeingizwa kinyemela katika Muungano bila ya kupata ridhaa za pande zote mbili.

Huu Muungano unajadiliwa chinichini tu mimi sielewi kwa nini, au kuna maslahi ya watu hapaaaa????
 
kuna hii wizara ya kushughulikia kero za muungano ambayo inaongozwa na Mh Hussein Mwinyi, pia na ile kamati ya waziri kiongozi na waziri mkuu EL hebu jamani mwenye data atupatie ni kweli zimeweza kuyazungumza hasa matatizo ya muungano na kuyapatia suluhisho hizi kero za muungano?

halafu huyu makamo wa rais kazi zake ni zipi katika muungano? maana nnaona kazi zake nyingi zimekuwa upande mmoja tu wa muungano na wakati yeye anatoka upande ambao hauwakilishi jee hili vipi?
 
Sincerely, mimi naamini muungano hauna "kero" kama CCM na wengine wanavyosema. Tatizo la muungano ni "muundo". Huwezi kuwa na muungano wa nchi 2 halafu ukabaki na nchi huru, ukaziita zimeungana. I think our style of union is unique.

Tatizo hakuna anayekubali kuwa muundo ni tatizo. Sasa hivi ukishughulikia kwa pupa gogo hili la "muungano" linaweza likavunjikia mikononi mwako. Hilo ndio weeeeeeeengi wanaogopa.

Federation Gvt would solve 95% of the so "kero" za muungano.
 
Muungano ni siasa Zanzibar ni Tanzanian hakuna nchi mbili hapo, labda 1960's. Lakini Zanzibar inabidi wachangamke na waanze kusoma na kufanya kazi kama Watanzania wengine. Mambo ya passport yameisha, mihula ya kupokezana uraisi imeisha, Rais anachaguliwa Dodoma, hakuna jeshi ukiangalia vizuri Zanzibar itanufaika zaidi kama itakuwa mikoa badaya ya nchi feki. Zanzibari haiwezi kujitenga kwani inategemea sana bara kwa kila kitu umeme, elimu, pesa, ulinzi. Vilevile hauwezi kutenganisha ndugu kwenye nchi mbili Zanzibar na Tanganyika ni ndugu na Wanzanzibari wengi wana ndugu bara hivyo haita make sense kuwatenganisha. Kama hutaki kukaa Tanzania ondoka nenda nje lakini Zanzibari ni Tanzania na haitabadilika.
 
Ndugu zanguni nadhani hili tatizo au haya manunguniko ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatatuandama mpaka makaburini mwetu.Yaelekea manunguniko mengi kuhusu muungano huu wetu yanatokea huko Zanzibar na Pemba.

Jambo la busara sasa ni kumwambia rais JK na pia rais Karume kuwa wakati wa kura za 2010 watu wa Zanzibar na Pemba wapige kura moja zaidi.Kura hii ihusu muungano "YES" or "NO". Matokeo ya hii kura maalum ikiwa 50% YES na 50% "NO" itabidi kura hii urudiwe tena.Kama matokeo ya pili ni 51% "NO" na 49 % "YES" basi hakuna budi ya kuendelea na muungano wetu, tutauvunja.

Tukisha uvunja muungano basi Tanganyika na Zanzibar zitakuwa nchi mbili tafauti kama zamani. Tutawauzia umeme kama kawaida kwa vile hii ni biashara na tutafanya mikataba ya kibiashara nao kama hivi sasa tunavyofanya mikataba na nchi nyingine.

Hii bughudha ya muungano itatuondokea kama tutafanya hivi.Wazanzibari watajiamulia wenyewe wanavyotaka kufanya.
 
utakapovunjika tu....wazanzibari watatengana...sie wapemba,nyie waunguja!.

halafu haitatosha...wanajiona wao waunguja zaidi watawafuata wakina mazrui bububu na wapemba wengine kwantipura,malindi na kwingineko na kuwaaambia waende kwao pemba[mazrui kwao si pemba hata hivyo,labda oman na hapohapo bububu]

hii itapelekea civil war huko zenj bar[na kama tanganyika ikiingilia,zanzibar itakuwa koloni au mkoa au kibaraka]

sidhani[kwa hali ya kisiasa ilivyo hivi sasa]itakuwa ni kwa best interest ya zanzibar[si wazanzibari]kuondoka muunganoni. hakutakalika!
 
hapa ndipo watanganyika wanapotufanya sie wapumbavu yaani sie wazanzibari tutashindwa kuishi huu si ukweli hata chembe.

wazanzibar tokea asili wanaishi kwa umoja mbali ya kuwa kuna tofauti ndogo ndogo ambazo nchi zote hazikosi, humu tulizungumza matatizo ya wachagga TRA ukweli ubaguzi upo na ukabila bara upo tena sana mbona hampigani, Zanzibar nnaamini tunaweza kujitawala na tukaishi vizuri tu.

mungu atuepushe na civil war leo na kesho. sisi tunaweza kujitawala na tulijitawala wenyewe kabla ya muungano nani alikuja kusuluhisha vita na wapi walikimbilia wakimbizi wa unguja na wapemba kabla ya muungano? nijibiwe masuala haya.

sisi tunataka fairness na si chengine sie tunaamini umoja ni nguvu na hata juzi kama ulifatilia kuhusu suala la Afrika mashariki nini walisema wazanzibari?

wanasema wao wanapenda umoja lakini iweje zanzibar isiwemo hali na wao ni nchi? pili ushiriki wetu kama taifa utakuwaje? wazanzibari daima hutaka fairness na si upendeleo.
au tuseme tuje bara kuomba uhuru tena baada ya kujikomboa 64.

kuna bwana mmoja alikuwa mkuu katika chama tawala alisema huyu hatumtaki kwa sababu baba yake alikuwa dalali wa zanzibar, si kwa maana anamchukua mwanzilishi wa taifa letu la hii hali tunayoenda nayo ni sawa kama ameiuza zanzibar.

na kama hujui historiya ya zanzibar tokea asili wazanzibari ni watu wa matani na maskhara
wapemba huitwa wapemba watu wabara walikuwa wakiitwa wa mrima wanyamwezi na mengi lakini hakupigwa mtu wala kuuliwa mtu waulize wazee wako.

na hii ndio maana hata sisi wazaramu kule zanzibar tulifka na sasa ni wazanzibari.
dhambi kuamini kuwa zanzibar ni waarabu au wapemba tu, tuko wengi wahindi, wamanyema, waburundi, wamalawi,wakenya, waganda na kocho kocho ya anuwai ya watu.
tumeishi na kuchanganyika kwa raha buheri.

ukweli udogo wa nchi yetu isiwe sababu ya kutubana na kutufirigisa
 
hapa ndipo watanganyika wanapotufanya sie wapumbavu yaani sie wazanzibari tutashindwa kuishi huu si ukweli hata chembe.

wazanzibar tokea asili wanaishi kwa umoja mbali ya kuwa kuna tofauti ndogo ndogo ambazo nchi zote hazikosi, humu tulizungumza matatizo ya wachagga TRA ukweli ubaguzi upo na ukabila bara upo tena sana mbona hampigani, Zanzibar nnaamini tunaweza kujitawala na tukaishi vizuri tu.

mungu atuepushe na civil war leo na kesho. sisi tunaweza kujitawala na tulijitawala wenyewe kabla ya muungano nani alikuja kusuluhisha vita na wapi walikimbilia wakimbizi wa unguja na wapemba kabla ya muungano? nijibiwe masuala haya.

sisi tunataka fairness na si chengine sie tunaamini umoja ni nguvu na hata juzi kama ulifatilia kuhusu suala la Afrika mashariki nini walisema wazanzibari?

wanasema wao wanapenda umoja lakini iweje zanzibar isiwemo hali na wao ni nchi? pili ushiriki wetu kama taifa utakuwaje? wazanzibari daima hutaka fairness na si upendeleo.
au tuseme tuje bara kuomba uhuru tena baada ya kujikomboa 64.

kuna bwana mmoja alikuwa mkuu katika chama tawala alisema huyu hatumtaki kwa sababu baba yake alikuwa dalali wa zanzibar, si kwa maana anamchukua mwanzilishi wa taifa letu la hii hali tunayoenda nayo ni sawa kama ameiuza zanzibar.

na kama hujui historiya ya zanzibar tokea asili wazanzibari ni watu wa matani na maskhara
wapemba huitwa wapemba watu wabara walikuwa wakiitwa wa mrima wanyamwezi na mengi lakini hakupigwa mtu wala kuuliwa mtu waulize wazee wako.

na hii ndio maana hata sisi wazaramu kule zanzibar tulifka na sasa ni wazanzibari.
dhambi kuamini kuwa zanzibar ni waarabu au wapemba tu, tuko wengi wahindi, wamanyema, waburundi, wamalawi,wakenya, waganda na kocho kocho ya anuwai ya watu.
tumeishi na kuchanganyika kwa raha buheri.

ukweli udogo wa nchi yetu isiwe sababu ya kutubana na kutufirigisa


we kalaga bao tu!

niliyoyasema nimeyaona na hiyo ndio tathimini yangu.sasa,nawe una uhuru wa maoni! lakini tusifiche ukweli!huko hakutakalika!
 
we kalaga bao tu!

niliyoyasema nimeyaona na hiyo ndio tathimini yangu.sasa,nawe una uhuru wa maoni! lakini tusifiche ukweli!huko hakutakalika!

Ni mawazo Tu!!....Ni Mitizamo tu!! ..Dunia Nzima watu wanaishi pamoja!! sasa sisi-Tunacho taka kukivunja Ni Nini?...

Mawazo Kwamba tumeungana!!?

vyo Vyo-te vile itakavyokua maana Itabaki palepale!!
 
Ni mawazo Tu!!....Ni Mitizamo tu!! ..Dunia Nzima watu wanaishi pamoja!! sasa sisi-Tunacho taka kukivunja Ni Nini?...

Mawazo Kwamba tumeungana!!?

vyo Vyo-te vile itakavyokua maana Itabaki palepale!!

tunaongelea endapo muungano utavunjika....umeni-quote ila sijakuelewa...au haya ndio mawazo yako tu?mtizamo wako tu?na ndio mchango wako tu!
 
Neno Muungano.... Lina weza- lika- kawa lina wavuruga mawazo yenu.... Lakini naana yake..
Itabaki Vile vile....
....

Kupinga Mawazo Ya Nyerere...Ni wasa na Kupingana Na Mzazi wako.....sasa huu Ndio Utamaduni wetu?
sasa Tuna weza Tuka rekebisha Kero tu..ili Kupata maana halisi!!
Hii ni kazi ya wanao taka Muunago Uendelee..

Kwa wa sio taka..Basi wajue kwamba Hivi sasa inawezekana kabisa Ku fikiria na kujua Itakuaje!!
 
Kuna malalamiko mingi kutoka upande mmoja wa Muungano (Zanzibar) kuwa unaonewa na kuuliwa uchumi wake na upande wa pili wa Muungano (Tangayika) na vile vile kutokupewa nafasi ya kuongoza ofisi nyeti za Muungano kama za Ulinze, Elimu, Mambo ya nje n.k. Na upande mwengine wa Muungano (Tanganyika) nao pia unasema unaonewa. Je ukweli ni upi?

Je malalamiko haya yameletwa na mfumo wa Muungano au ni Wanzanzibari tu wenyewe hawakujipanga uzuri??

Kuengezeka kwa mambo yaliyokubalika katika Muungano wakati unaanzishwa (yaani mambo kumi na moja)je Zanzibar na Tanganyika zilishauriwa ? au ni utaratibu gani ulitumika kuyaongeza hayo mambo kumi?

Je tufanye nini ili kuuboresha Muungano wetu?

naomba kutoa hoja.
 
Mmm..!! mkono wataka kula lakini mwili na akili vyafanya woga...!! sijui nichangieee... maana haya mambo mazito... unajuwa kuwa chakula cha serikali ni mwnanchi... na chakula cha mwananchi ni kura yake...
na chakula cha mwandishi ni kalamu yake... Nami nishaanza kuhisi njaa... njaa...
Naomba kutoa hoja....!!
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom