Muungano kwanza katiba ifuatie ili kuepusha maafa!

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Serikali ya Jamhuri ya Muungano imekuwa ngumu sana kusoma alama za nyakati kuhusiana na maswala mengi sana muhimu na mwishowe kujikuta ikijadili namna gani itaokoa wahanga wa maafa ambayo tungeweza kuyaepuka awali kama tu tungesoma alama za nyakati na kushughulikia matatizo hayo kabla ya kutokea. Sitaki kwenda ndani sana kuhusiana na hilo kwa sasa kwa kuwa naamini wengi wanalijua hilo.
Ukifuatilia mijadala inayoendelea Zanzibar kuhusiana na Muungano na maoni juu ya marekebisho ya katiba utagundua nini kitatokea endapo serikali yetu SIKIVU itaendelea na mchakato wa kufanya marekebisho ya katiba bila kufuatilia kwa makini madai ya wazanzibari kuhusu Muungano.
Mengi sana yanasemwa kuhusiana na kasoro za Muungano na mabaya mengi yanaonekana yamesababishwa na Wanaoitwa Watanganyika (watu wa Tanzania Bara) kwa nia ya maksudi ya ama kuwapora au kuwadidimiza kiuchumi watu wa Visiwani. Iwe kweli ama si kweli, maneno mengi yanasemwa na karibu kila mtu (viongozi na waongozwa) kuonesha kwamba Tanganyika ni tatizo kwa Wazanzibar.
Sasa hivi ili uonekane Mzanzibari mzalendo na makini inabidi udai Muungano haufai na ubaya wa watanganyika kwa maendeleo ya Zanzibar. Uamsho wanaonekana kama wafanyafujo fulani lakini mawazo wanayoyawasilisha yanatoka kwa viongozi wa kisiasa tena baadhi yao ni wanaCCM.

MUHIMU:

Muungano wa Tanzania una kasoro kibao lakini tusidanganyane hata kidogo kwamba Watanganyika wanajua chochote kuhusiana na faida wanazopata katika Muungano tena eti kwa kuwafanyia hila wazanzibari kama ambavyo wengi wa wazalendo hao "makini" wa Zanzibar wanataka ionekane kwa wapiga kura wao.
Lakini pia tusiwe vipofu wa kushindwa kuona kwamba namna ambavyo serikali yetu imekuwa inafanya ili kuulinda Muungano huu si sahihi sana. Baadhi ya favours zimekuwa zinatolewa kwa watu wa Zanzibar ili kuulinda Muungano pasipo kuangalia hali halisi. Naamini mpaka leo Muungano kwa Tanganyika kwa mahesabu ni hasara zaidi kiuchumi kuliko faida (Cost>Benefit).Hapa mtanisamehe kwani nimeangalia haraka haraka mambo kama ajira katika vyombo vya Muungano, uhuru wa wazanzibari kunufaika na Tanganyika bila mipaka na uchangiaji wa gharama katika Muungano.
Ninachokiona sasa hivi baadhi ya Wazanzibar wapo tayari hata kusema uongo ili tu kuonesha jinsi gani Muungano ulivyo mbovu na hivyo kushangiliwa na wenye mtazamo huo.

USHAURI WANGU:
Kuna haja kubwa Muungano utazamwe upya, ujadiliwe na kupigiwa kura ya maoni kwanza ili kama utakuwapo, katiba ijadiliwe ikiwa na Muungano ndani yake. Kwa kuwa wazanzibar wanaonekana kupenda sana uzanzibari wao kwa nini watanganyika wasielimishwe juu ya faida wanazopata katika Muungano huo na gharama wanazolipia faida hizo?. I hate to say this but I believe Gharama wanazoingia watanganyika kwenye Muungano na wanachokipata kutoka huko vinapishana kwa kiwango cha kuwa hasara kwao kuliko faida. Ninachokiogopa leo ni hii dhambi ya ubaguzi tunayoanza kuifanya kwa kutuhumiana na kuzushiana ubaya bila sababu ili tu kushangiliwa na kupata tukitakacho.

Please! Please! Serikali ya Muungano ichukue hatua haraka kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa kukawa na vurugu nyingi tu kuhusiana na Muungano hata baada ya kujadili katiba kutokana na mbegu mbaya inayopandwa katika pilika pilika za hawa wanaodai nchi yao. Kama Mh. Rais Kikwete una nia ya dhati na Tanzania watazame hawa ndugu zetu na uwatimizie kiu yao ya ama kupiga kura ya maoni juu ya Muungano au kuwaacha wabaki na nchi yao kwa kuwa naamini baraza lao linaweza kusema hivyo endapo watapata nafasi.
Tafadhali Mkuu usisubiri jamaa waanze kuwaripua ndugu zao wa Bara kwa mabomu na silaha nyingine katika nia ya kupata matakwa yao ndiyo tuanze kutuma polisi na jeshi ili kuwazuia, kuzoa miili na hatimaye kujadili nini cha kufanya ili vurugu zisiendelee.
Kama faida wanayopata Watanganyika haizidi gharama za Muungano bora tuwaachie waende.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom