Muungano hauna mikataba wakuwa usivunjwe JK hii ni haki ya wananchi wa pande mpili moja ikiamua

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1]Kujadili Muungano sio haramu au zambi kama wenzetu wanavyo babaisha mambo kwa faida ya kutumeza .[/h]Written by amini // 22/11/2011 // Habari // No comments

Tanzania-map1-564x272.png
Jee sisi tulikuwa na sifa ya kijinchi chatu kungana au kuangamia?

VIONGOZI WETU WA SMZ WACHENI KUWEKA MBELE MASLAHI YA VYAMA NA KIPATO CHA MUDA HUKU ZANZIBAR INA YAYUKO.
Ndugu zangu wana wa Zanzibar fursa ya kuipapatua Zanzibar ktk kina kikubwa cha maji na tope tulichokwenda kuiweka Zanzibar yetu ni hii tulio nayo hivi sasa ambayo Wzanzibar tumeacha tafauti zetu za kisiasa za kulumbana ambako tukizidi kugawanyika na kuipoteza Zanzibar.
Ikiwa totakosa kuikinga Zanzibar hivi sasa ktk mwielekeo huu wa mchakato wa Katiba ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika ijitayo Tanzania, Basi tutegemee mafia mbeleni ya kumezwa ambayo dalili na ishaza zote ziko wazi kwa jambo hili.
Nilazima viongozi wetu wa Suk (Smz) mujifunge kibwewe ili kuinusuru Zanzibar kupotea na kuwa powerless, hakuna shaka kuwa Wananchi wa Zanzibar wamebanwa sana kusikika nguvu zao na kutowa dugudugu lao.
Na kinacho sikitisha sana nikuwa sio mbano huu na mbinyo huu tunafanyiwa na serekali ya Muungano tu, na hata Serekali yetu na vyombe vyetu vya Smz hushiriki kikamilifu kubinya mbinyo tena wakukamua kuwa sauti na joto la wananchi wa Zanzibar lisije juu.
Smz hutumia vizingiti vingi tu kukwamisha harakati za kuirudishia heshima yake Zanzibar kuwa ni nchi na sio miongoni mwa mikowa ya Tanganyiga ijitayo Tanzania hivi sasa.
Kama katiba itapita na swala sugu la Muungano litawachwa pempeni bila ya kukaa kitako nchi mbili zilizo unda huo Muungano wenyewe basi result ya Zanzibar nikumezwa katika mikowa mikubwa ya Tanganyika ijitayo Tanzania .
Mimi sikubaliana na Chadema badhi ya mambo lakini kuna mambo Fulani tunaweza kukubaliana nao vile vile? Na niyapi hayo niyale yenye faida na nchi yetu ya Zanzibar na Wananchi wake.
Chadema hawapingi ktk mfumo huu wa Katiba kuwepo na majadiliano ya watu wa pande mbili za Muungano na sio vyama ili kujadiliana maswala ya Muungano kama uwepo au laa, na kama utakuwepo wananchi watakubali basi uwe wa Serekali 3 yani Tanganyika, Zanzibar na ya Muungano kwa mambo yale ya Muungano tu.
Kwa hili mimi kama sikosei naona nikweli na nakubaliana nao Chadema hili, kwa sababu ikiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika ijitayo Tanzania kasema hazarani kuwa katika katiba hili swala la Muungano lisiguswe ispokuwa kuuimarisha na sio kuuvunja?.
Hili ni suala mimi binafsi linanitia wasi wasi mkubwa wakuona viongozi wetu wa Smz wanataka kupelekwa puto kuinakamiza ktk mikono yao, mana kila nikigawa isabu zangu naona sipoti jawabu nini wamekusudia viongozi wetu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar(Smz) ?.
Ikiwa katiba ina umuhimu sana hivi sasa kuliko kujuwa nafasi yetu Zanzibar iko wapi katika Muungano huu wa Zanzibar na Tanganyika ijitayo Tanzania, basi sihacha katiba hii hii ikaaja ikawawa nikitanzi kwa Zanzibar kukiepuka.
Na ikiwa kuna nafasi mzuri yakushikamana viongozi wa Smz na kutowa fursa na mwanya kwa wananchi wa Zanzibar basi muda ndio huu wakuweza kuutumia laa katiba ikipita na swala sugu la Muungano likaashwa kujadiliwa Mwanzo basi tusubiri maafa ya katiba na vipengele vyake kuizuru Zanzibar na kuizofisha.
Mimi nasema hakuna haja ya kutiwa kufuli na Jk kuhusu maswala ya Muungano kuvunjwa au kuto kuvunjwa hili ni swala ilikuwa washiwe wananchi wenyewe walijadili sio utachi wa chama au nguvu za Upande mmoja wa Muungano kuwa yeye ndio Baba kwa kuwa ana ardhi kubwa na watu wengi.
Kama upande moja utaona hauna haja ya kuwa na Muungano basi mawazo ya wengi na wananchi yanahitaji yaheshimiwe , na Muungano huu sio wa kulazimichana wala hakuna mikataba ilio tufunga .
Lakini inaonekana viongozi wetu wako wakimya kujadili Muungano kwanza kabla ya kujadili katiba, kwa sababu Muungano ndio uliokuja mwanzo halafu ukazaa katiba , kwa hio sio zambi wala uharamu wala ubaguzi kuvunja Muungano ikiwa upande moja wamehisi hawataki.
Kuna Wzanzibar wengi wameshindwa kujijuwa hivi sasa wapi tunaelekezwa , kutokana na mchakato huu wa katiba kukizi mahitajio ya Zanzibar ktk hatma ya nchi yetu kwenye Muungano.
Mimi nasema moja kubwa nililokuwa sikubaliani nao Chadema nikuirushia maboni sana Zanzibar badala ya kuwapika Wtanganyika kuanza mchakato wa kudai Tanganyika yao hazarani au kuvunja Muungano huu wenye utata mkubwa .
Nazani wangeanza harakati hizi Chadema basi hata Zanzibar wangepata support kuwango mkono na wangekuwa ni wazalendo zaidi kuliko uchama, lakini kusema leo kuwa Zanzibar na Raisi wa Zanzibar kapewa malako makubwa ktk mchakato wa katiba, hii nikutuonea Zanzibar.
Kumbuka Zanzibar nikiungo kilicho unga huo Muungano wenyewe wa Zanzibar na Tanganyika ijitayo Tanzania, bila ya Zanzibar kushirikiswa pakubwa ktk mambo ya Muungano basi Muungano hakuna wala hakuna hio katiba itwayo ya Muungano fake?.
Na ingekuwa Wabunge wate wa Muungano kutoka Zanzibar wametoka ktk Bunge la Muungano basi katiba isinge pitishwa wala kufanya kazi, hii ndio power tulionayo Zanzibar ktk maswala ya Muungano.
Na sizani kuwa ikiwa Zanzibar itashirikishwa ktk swala kubwa kama hili lenye hatma ya nchi mbili na watu wake kuwa Zanzibar ingie Bungeni kutokana na utachi wa vyama na uingi wa wabunge kuwa Muungano utakuwa salama ?.
Nazani Wabunge wetu Watamuriwa kurudi nyumbani Zanzibar haraka na kususia mambo yote yanayo husu Muungano e.g upigaji wa kura wa Raisi wa Muungano, kushiriki ktk vikao vya Bunge la Muungano na mambo yote yenye kuhusu Muungano.
Jee ikiwa hivyo huo Muungano utakuwa ktk hali gain? Kutakuwa tena na Muungano au ubabe wa uvamizi wa Tanganyika kuivamia Zanzibar bila ridha?.
Wzanzibar wanasema wacha Chadema kusema Zanzibar imepewa nguvu kubwa still Wzanzibar tunahisi hatuna nguvu na nguvu zote ziko Tanganyika zikisimamiwa na ilani na taratibu za chama cha ccm.
Kwanza lazima wafahamu Chadema kama kishingizio nikusema Zanzibar sio nchi kama vile Tanganyika sio nchi basi wanakosea pakubwa, Kwa sababu walio iua Tanganyika ni Watanganyika wenyewe kwa kuiticha Bunge la Tanganyika bila kuwachauri au kuwashirikicha Wzanzibar.
Na hii ilikuwa ni zamira mbaya ya Nyerere kutaka kuimeza Zanzibar kiujanja na kutoka hapo ndipo Zanzibar ikafa ki power ikawa powerless na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukawa hauna hadhi tena na chama cha ccm ndio kikawa ndio Muungano.
Sasa sio rahisi kwa Wzanzibar wenyewe kukubali kupoteza nchi yetu iliokuwa Dola kamili kuingizwa ktk mikowa ya Tanganyika kutokana tu eti Zanzibar ni ndogo ukilinganicha na mikowa mengine na population yake.
Sisi tunaona ufahari kujitenga ili kuondowa utata huu wa Muungano na Baadae mubakie Chadema na ndugu zake ccm kukamatana machati?. Na mujuwe kuwa Muungano utakufa Zanzibar pindipo ccm ikingoka Bara tatizo la Zanzibar kuzofika na kupoteza nguvu zake na utu wan chi yake ni viongozi tulionao ni wababaichaji kwa maslahi yao tu yakidunia siwo wazalendo wenye uchungu na nchi yao.
Kumbukeni Chadema kuwa hakuna mpumbavu yoyote au mjinga yoyote anae kubali Raisi wake ktk kungana awe memba baraza la Mawaziri au Waziri asio na wizara malumu , hata nyiyi Chadema sizani kama mungekubali upumbavu huu wanao tufanyia ndugu zenu.
Lakini hili lote ni unafiki wa ccm/Smz kujipakatisha na kuwa watifu wa maslahi yao binafsi kwa kikumbatia chama chenye wenyewe na lengo kuza utu wao na kuhisi kuwa Dodoma ndiko kwenye kutoka riski zao.
Tunawambia Chadema kuwa mamuzi ya viongozi wetu akiwemo Dr Shene sio mamuzi ya Wzanzibar, Wzanzibar hawana haja ya katiba wala Raisi wetu kupiga mogoti kwa Kikwete kuwa Waziri hii ni Shame& Sad kwetu wananchi wa Zanzibar ispokuwa tumewezwa na kutiwa ujamu kuvutwa.
Tungekuwa na viongozi Wzalendo basi tusingali fikiswa nchi yetu hapa ilipofika ninani alompa madaraka makubwa Kikwete kuwa yeye ndio yeye? Hili linatuma sana Wananchi wa Zanzibar kuwa hatuna viongozi wazalendo bali tuna wababaishaji tu kwa maslahi yao binafsi wakati ni hatari hata kwao mbeleni.
Kumbukeni viongozi wetu wa Smz kuwa kidogo mupewacho kuza nchi hasara yake nikubwa kwa jamii , hakuna nchi kubwa na ndogo ktk Muungano zote zinakuwa sawa vipi leo mambo yote muyavunganyie nyiyi , na sisi mutuhukumu kutokana na udogo wan chi yetu na watu wake?.
Muungu inusuru Zanzibar kutoka hapa ilipo egeshwa ktk kina kirefu cha maji na tope amini,
Muungu wanusuru viongozi wetu kuwabadilicha nyonyo ili watowe fursa kwa Wananchi wa Zanzibar wafanye kweli kama wao wameshindwa na kuwaonelea haya mabwana.
 
Back
Top Bottom