Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Haya ni mawazo yangu binafsi na hayawakilishi mawazo ya chama changu wala mtu mwingine yeyote.
Suala la CHADEMA, CUF, NCCR, TLP NA UDP kurushiana shutuma mbalimbali limekuwa jambo la kawaida. Kwa wengine ni jambo linalotia hofu. Hofu kubwa ni kwamba itakuwa vigumu kuishinda CCM.
Lakini wenye hofu hiyo hawaoni hofu kwamba muungano au ushirikiano huo pia unaweza kuwa mwisho wa upinzani hapa kwetu.
Hii hofu nyingine ina matokeo yale yale, ugumu wa kuishinda CCM.
Kwa hali ya siasa ya nchi kwetu kwa sasa, CCM itashindwa na chama kimoja chenye nguvu na sio muungano wa vyama vingi visivyo na nguvu badala yake vina wanasiasa (sio viongozi) wanaotafuta ulaji na kuganga njaa kwa kisingizio cha upinzani. Vyama hivyo pia vina wanasiasa ambao uelewa wao ni mdogo au umefunikwa na maslahi zaidi.
Hakuna haja wala sababu ya vyama vilivyo upinzani kuungana au kushirikiana katika hali ya sasa hivi. Huo utakuwa muungano au ushirikiano wa kinafiki sana. Upinzani utakuwa umepata pigo hilo likitokea.
Wote tumeshuhudia kwa muda mrefu mawazo na maono ya wanasiasa walioko upinzani. Kila mmoja anajifikiria yeye, halafu chama chake (ambacho ni yeye pia), halafu wanaomzunguka (ambao ni yeye pia) na mwisho watanzania ambao ni wafuasi wake (sio wananchi).
Sasa wanasiasa hawa wakiungana au kushirikiana nini kitatokea? Kenya vyama vya upinzani viliungana. Wakashinda uraisi. Baada ya hapo? Mpaka sasa hivi wanachojisifia ni Katiba mpya. Katiba ambayo kabla hawajashinda waliahidi itapatikana mapema mno. Watu walikufa na maelfu kukimbia makazi muungano wa upinzani ulipochukua. Kisa? Raila na Kibaki........wanasiasa wa upinzani zamani!
Kama ambavyo tunaona muungano wa Zanzibar na Tanganyika una matatizo yake, basi ni hivyo hivyo muungano au ushirikiano wa vyama vya siasa hapa kwetu. Wanasiasa wetu wana matatizo makubwa. Angalia wanayoyasema, wanavyoyasema na wanaowasemea.
Natoa mifano.
Toka tar. 31/10/10 hawa waliotajwa hapa chini wamesema nini hadharani kuhusu hali ya uchumi ya nchi na dunia, mipango ya ajira, mabadiliko ya hali ya hewa, uhusiano wa kimataifa, mfumo wa elimu nk. Hapa sizungumzii matamko yao kwamba hali ni mbaya au kupinga kwao ufisadi. Hilo wote tunajua na tunaona.
Wamezungumza nini kuhusu kubadilisha hali hiyo mbaya zaidi ya kuongea kwa ujumla? Nani anajua mawazo yao binafsi na uwezo wao kuhusu hayo? Tusirudishane kwenye ilani za vyama.
Augustine Lyatonga.....amesema nini?
John Cheyo..........amesema nini?
James Mbatia........amesema nini?
Ibrahim Lipumba.............amesema nini?
Freeman Mbowe...........amesema nini?
Tumekuwa na wanasiasa mabingwa wa kukosoa bila kutoa suluhisho. Wao kazi yao ni kuhudhuria misiba, sherehe za kitaifa, makongamano, kutoa pole wakati wa majanga, kutembelea watoto yatima na kutoa misaada ya baiskeli. Halafu anajiita kiongozi! Mpinzani!
Nchi inateketea, badala ya kusaidia isiishe yeye anasubiri acha iishe ili nije kuongoza mimi 2015. Nikisema cha kufanya sitaweza kuing'oa CCM. Haya ni makosa makubwa.
CUF wabaki kama CUF na CHADEMA wabaki kama CHADEMA. Kila kimoja kifanye kazi yake ya siasa. Ukweli wa nani bora utajulikana tu.
Mungu aepushe mbali mawazo ya Lipumba, Mbatia, Mrema, Cheyo na Mbowe kuungana au kushirikiana. Hata kwa kusoma hayo majina kwa pamoja utaona mwili unavyosisimka. Mungu atuepushe.
CCM itaondoka madarakani, na hii itakuwa mapema mno. Itatokea haraka na kwa ufanisi mkubwa. Hakuna jinsi wataondoka tu.
La msingi ni nani atachukua nafasi yao baada ya wao kuanguka? Sikubali hao wote kwa pamoja wachukue hiyo nafasi. CHADEMA watachukua. Kama chama na si kama umoja wa vyama.
Naamini.