Muundo wa Muungano: Tanganyika tunataka 'Serikali moja, nchi moja, taifa moja'!

Jumaane,
Mimi naona kwa sasa hivi Zanzibar ndiyo inayo colonize Tanganyika kwa sababu yenyewe inajitawala na bado inashare kwenye Muungano. Unasema Tanganyika can't force Muungano wanaoutaka wao na Zanzibar, Je huoni kwa kusema hivyo unataka Zanzibar ndiyo i force Muungano wanaoutaka wao na Tanganyika? Marekani ni muunganiko wa nchi zaidi 40 ambazo zilikuwa na mchanganyiko wa nchi ndogo na kubwa. Maskini na Tajiri lakini wameunda serikali moja. Kwa nini Serikali moja iwe nongwa kwa Tanganyika na Zanzibar? Je nini mantiki ya Muungano kama bado kila muungana ana serikali yake?

Hoja ya Serikali tatu ni hoja ya wanasiasa kujitengenezea nafasi za ulaji.

Nakala: Mzee Mwanakijiji.

TUMBIRI (PhD, University of HULL, United Kingdom),
tumbiri@jamiiforums.com

Hizo nchi arubaini za USA uliwahi kuzisikia? na unaweza kutupa maraisi wao ? Watu wengine bana iko naburusa wengine.
 
Jumaane
Kinachoonekana hapa ni kwamba mwanakijiji anacampaign na kuadvocate for compete colonization of zanzibar by tanganyika

Sijakuelewa Mkuu, "Colonization" kivipi? Huo ndio muungano mzuri na wa haki. Two sovereign states zinakubaliana kuvunja sovereignity zao na kuunda nchi au sovereignty moja! Sasa nani anam'colonize' mwenzake? Mi nadhani hapo wenzetu Zanzibar itabidi watafute hoja nyingine hiyo ya colony haitakuwa na mashiko.
 
Watanganyika aliyewaroga ameshafariki jk nyerere huyu ndo alieridhia kupotea taifa la tanganyika (serikali) na kulibakisha taifa la zanzibar na mamlaka yake kamili ikiwa na rais wake na kila kitu chake kwa tamaa zake za kuimeza zanzibar. La kushangaza watanganyika wengi na Ujuaji wao wanshindwa kufahamu muungano huu ulikuwa ni baina ya nchi na nchi tena kwa mambo kumi na moja tu. Yaliobaki hayamo katika muungano hapa ndipo ukapita utapeli haya yasiokua ya muungano ukitowa kumi na moja kwa upande wa tanganyika tasimamiwa na nani katika huu muungano wakati tanganyika imepotea ? Watanganyika someni haya mambo kumi na moja ! Tukaburuzana na muungano feki mambo haya kumi na moja yakaongezwa kinyemela hadi leo yamefikia 40 lakini bado ndoto haijatimia.

Sasa ukweli usiopingika wazanzibar na umasikini wetu na udogo wetu bado hatupo tayari kuikosa nchi yetu pia hata huu muungano na tanganyika hatuutaki na tunasikia aibu kuambiwa sisi ni ndugu na watanganyika na hili mnalijua. Haya mambo ya zanzibar mzigo ni ngonjera zenu tu. Hakuna hata mtanganyika mmoja aneweza kuhoji kwa dhati muungano huu.hata kikwete akija kule zanzibar anakuja na heshima na adabu kama alomwagiwa maji. Watanganyika kwa kuongea hawana mpinzani sisi kama wazanzibar tushaonyesha kila kitu hatuutaki muungano huu.

Tuwachiwe tupumuwe kama ni muungano kaunganeni na burundi rwanda na uganda .
 
Endelea kuota mchana Mzee!km unataka hoja ya ipate nguvu ungemuomba Mzee wa Upako akamfufua Baba yako wa Taifa akusaidie kupigia debe serikali moja!
Hamna ujanja mtaimbo umeganda!

Alhabaad amka,
Watanganyika tumeshaangalia mbali, madai ya serikali moja tunajua fika zanzibar haitaridhia, hivyo muungano utavunjika ndicho tunachotaka. Sisi hatudai kuvunja muungano kwa jazba bali tunatumia akili. Sasa serikali moja ikikataliwa, Tanganyika itazuka na zanzibar kama ilivyo kwa sasa itaendelea. Kwa upande wa tanganyika kitakachofuata, tuta-tight sheria za makazi (ondoa wapemba na waunguja), kodi kwa bidhaa za zanzibar, umeme cut-off, gharama za kupeleka wagonjwa wa moyo india kutoka zanzibar kwishiney. Na zanzibar kwa upande wake ifukuze watanganyika wanaokaa zanzibar sijui mtawapata wapi hahahahhaaaaaaa. Tunataka tutue zigo la misumari (zanzibar) tulilotwishwa miaka nendarudi
 
Hapo upo upande wangu kabisa mkuu, pamoja sana! Yaani akina zito na CDM kwa ujumla wananiudhi sana make wameshupalia serikali tatu wakati ni hoja isiyo na mashiko kwa wananchi bali kwa wao wenyewe wanasiasa

Basi jamani kumbukeni kutoa maoni yenu kwenye tume ya kurekebisha maoni (kwa e-mail au online kama huna nafasi ya kwenda mkutanoni). tusiishie kukutoa maoni yetu hapa tu na kulalamika kwani haisaidiii.
 
Kuna mambo ambayo baada ya kusherekea kile kilichoitwa miaka hamisini ya uhuru wa Tanzania Bara, hatutakiwi kukizungumzia nacho ni muungano wenye serikali mbili ndani yake. Kama yalikuwa majaribio nafikiri miaka hamsini inatosha kabisa kujuana vizuri, hivyo basi tunaweza kuchagua aidha kuungana na kuwa nchi moja au kutengana kabisa ili kila mtu ajitegemee. Ushauri wangu ni kwamba tukatae serikali mbili na kuunga mkono serikali moja.
 
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!

Unakusudia serikali ya Tanganyika pekee? Sasa hapo sijui siku zote umekuwa ukizunguka nini. Hii ina maana ni kuvunja Muungano au sivyo? Kwani unaposema muombe serikali moja na wengine hawataki nini maana yake ?
Serikali mbili zilikuwa zikiwanufaisha nyinyi kwa kila hali kwani mkibeba haki za Zanzibar kwa maendeleo yenu na kuwaachia wazanzibari wakijuhudumia kwa shida baada ya kuwanyanganya nyenzo za maendeleo.
Hili la gharama Mwanakijiji ni kuwa Zanzibar ndio iliyokuwa ikigharimika. Ilikuwa ikihudumia Serikali na huduma zote za wazanzibari kwa gharama zao na kwa kutambuwa hili ndio maana hamtaki serikali tatu kwani mtakuwa kama walivyo Zanzibar sasa hivi, yaani kuhudumia serikali yenu ya Tanganyika na baadae mtowe mchango kuihudumikia Serikali ya Muungano. Ujanja huo wazanzibari wanaouelewa na lilibaki ni nyie kutowa uamuzi wa kuvunja Muungano.
 
Tusikubali kwenda serikali tatu. Kwa vile tumekatazwa kutaka kuvunja Muungano - japo waliotukataza hawana uwezo huo - na kwamba tunaweza kujadili "muundo" bora wa Muungano. Ninawasihi watu wa bara kudai "Serikali moja, taifa moja, na nchi moja". Haya mambo ya serikali mbili nchi mbili au serikali tatu nchi mbili hayaingii kichwani na ni jitihada za kujaribu kuibeba Zanzibar. Wakati umefika tudai uwepo wa serikali moja tu ya kitafa kwenye nchi moja.

Ninafahamu kabisa matokeo ya watu wa bara kutaka hili. Jambo pekee ambalo tusikubali kuuziwa (CCM na upiinzani wanataka hili) ni serikali tatu. Serikali tatu ni mzigo ambao hatuwezi kuubeba na wala hatupaswi kuubeba. Nawasihi wenzangu tukate kuongezewa mizigo. Tuwe na serikali moja, taifa moja na nchi moja. Sasa kama hili lina maana Zanzibar iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" na bara iwe "serikali moja, taifa moja na nchi moja" basi na iwe.

Tuwasaidie Zanzibar watoke kwenye Muungano kama hawataki serikali moja kwani mbili hawataki na tatu tutajipa mzigo zaidi!

SAY NO TO SERIKALI TATU!!

Iambie tume ya Warioba - hatutaki serikali tatu!!
Ni wazo zuri Mwanakijiji. Lakini mie naungana nawe kuwa wazanzibar hawawezi kukubali serikali moja kwahiyo ni wazi kuwa muungano utavunjika. sasa tujiulize kuwa baada ya muungano kuvunjika nini kitafuata: Mie nadhani kuwa baada ya muungano watanganyika na wazanzibar kwa muda fulani wote tutakuwa na furaha sana ila baada ya muda hali itabadilika. Kwa upande wa zanzibar hawataweza kusimama kama taifa kwa miaka zaidi ya ishirini: sababu zipo nyingi moja ni kuwa zanzibar haijawahi kuwa moja, wapemba na waunguja ni mahasimu wasioweza kwa namna yoyote ile kuishi pamoja kwa amani, pili mzigo utaongezeka sana kwa zanzibar maana uwekezaji katika polisi, usalama na jeshi utakuwa mkubwa sana hasa kwa kuwa zanzibar itajikuta ni nchi yenye uchumi mdogo sana ktk ukanda unaowekeza sana ktk nguvu za kijeshi wa Afrika mashariki.
Tatu gharama za maisha zitapanda sana kwa kuwa sasa huduma za umeme na nishati zingine zitagharamiwa na mzanzibar kwa asilimia mia.
Nne kutakuwa na matatizo makubwa ya ardhi na mahitaji makubwa ya chakula kwa sababu wazanzibar wengi waliotapakaa kila mahali Tanganyika wakimiliki mashamba makubwa, biashara na wengine wakifanya kazi watalazimishwa kurudi zanzibar kwa haraka tena huenda bila kubeba chochote.
Mwisho wakati zanzibar ikitegemea utalii na karafuu, utalii utaathirika sana kwa sababu wengi wa watalii wanapenda sasa kwenda zanzibar wakijua wataunganisha pia bara kutembelea vivutio mbalimbali vilivyoko bara, baada ya muungano kuvunjika watatakiwa kuchagua kati ya kwenda zanzibar lakini wakose kilimanjaro, serengeti, ngorongoro, mikumi na sehemu zingine au waende moja kwa moja Tanganyika.
Haya na mengine mengi yatasabisha kuibuka kwa enzi mpya ya zanzibar ambayo hakuna mzanzibar ataisahau.

Kwa upande wa Tanganyika hakutakuwa na tofauti kubwa sana, ila changamoto kubwa itatokana na kufeli kwa zanzibar. Zanzibar ikifeli kwa juu juu itakuwa kama vile waarabu wataanza tena kuiendesha zanzibar lakini ukweli ni kuwa haitakuwa hivyo maana hata bila kupatikana kwa mafuta, kitendo cha gesi nyingi kupatikana ktk pwani ya bara na uranium nyingi ndani ya bara itafanya mataifa makubwa yaanze kuiyumbisha zanzibar ili yapate nafasi ya kudhibiti biashara ya nishati. Bila shaka hawatakuja moja kwa moja bali pataanza kutokea uasi mwingi ktk zanzibar lengo ni kuwa kila taifa litataka kuweka serikali kibaraka, kwa kuzingatia hali iliyokuwepo kabla ya muungano siondoi uwezekano wa Tanganyika kuwa moja ya mataifa yatakayokuwa yakijaribu kuweka serikali vibaraka ktk zanzibar ili kujihakikishia usalama. Hali ikiendelea kuwa mbaya basi Tanganyika inaweza hata kuingia vitani dhidi ya tawala za zanzibar zitakazokuwa zikitumiwa na watu wa mbali dhidi ya Tanganyika. Hali hii itasababisha pesa nyingi sana za watanganyika zitumike kuliimarisha jeshi kuanzia angani, majini na nchi kavu na hivyo kudunisha huduma za kijamii.

MAONI YANGU

Watanganyika tukubali serikali tatu ikiwa tu itaonesha kuwa gharama za uendeshaji wa serikali ya muungano zitakuwa nusu kwa nusu bila kujali idadi ya watu ktk Tanganyika na zanzibar. kama hilo haliwezekani basi tupinge serikali tatu kwa gharama yoyote ile.

Kama wazo la kubeba gharama nusu kwa nusu limeshindikana basi ndio tuwe tayari sasa kuipigania serikali moja hata kama itamaanisha kuuvunja muungano.

Kama muungano utavunjika basi tujiandae pia kujenga uwezo wa kukabiliana na maadui wakubwa zaidi ya wanaotuzunguka kwa sababu lazima wataikalia zanzibar kwa maslahi ya kibiashara. Hapa mfano ni comoro, ambapo Tanzania imekuwa mara kadhaa ikipeleka vikosi kuzima chokochoko za vibaraka wa wafaransa.
 
Watu >43millions wanazidiwa ujanja na watu <1million. Wazenji wana proportion kubwa ya watetezi na mabunge 2 yanayowatetea wao tu wanaoishi ndani eneo la km za mrada 3000 tuu eneo ambalo ni dogo kuliko wilaya nyingi huko bara. Inashangaza hayo maeneo yanayoitwa mikoa ni sawa na eneo la kijiji au kata bara. Tuache ujinga wafurushwe au wakubali tuwe na serkali1 na kuondoa baraza la mapinduzi na la wawakilishi. Huu ni uchuro utakaoigharimu historia ya nchi hii .
 
Watanganyika aliyewaroga ameshafariki jk nyerere huyu ndo alieridhia kupotea taifa la tanganyika (serikali) na kulibakisha taifa la zanzibar na mamlaka yake kamili ikiwa na rais wake na kila kitu chake kwa tamaa zake za kuimeza zanzibar. La kushangaza watanganyika wengi na Ujuaji wao wanshindwa kufahamu muungano huu ulikuwa ni baina ya nchi na nchi tena kwa mambo kumi na moja tu. Yaliobaki hayamo katika muungano hapa ndipo ukapita utapeli haya yasiokua ya muungano ukitowa kumi na moja kwa upande wa tanganyika tasimamiwa na nani katika huu muungano wakati tanganyika imepotea ? Watanganyika someni haya mambo kumi na moja ! Tukaburuzana na muungano feki mambo haya kumi na moja yakaongezwa kinyemela hadi leo yamefikia 40 lakini bado ndoto haijatimia.

Sasa ukweli usiopingika wazanzibar na umasikini wetu na udogo wetu bado hatupo tayari kuikosa nchi yetu pia hata huu muungano na tanganyika hatuutaki na tunasikia aibu kuambiwa sisi ni ndugu na watanganyika na hili mnalijua. Haya mambo ya zanzibar mzigo ni ngonjera zenu tu. Hakuna hata mtanganyika mmoja aneweza kuhoji kwa dhati muungano huu.hata kikwete akija kule zanzibar anakuja na heshima na adabu kama alomwagiwa maji. Watanganyika kwa kuongea hawana mpinzani sisi kama wazanzibar tushaonyesha kila kitu hatuutaki muungano huu.
Tuwachiwe tupumuwe kama ni muungano kaunganeni na burundi rwanda na uganda .
Nina uhakika hufuatiliii mijadala na kama unafutailia basi huelewi kinachoongelewa.

Nimewahi kumuuliza ndugu yangu Baru baru swali lifuatalo:
Katika mambo 11 ni yapi Tanganyika inafaidika nayo kwa kuinyonya ZNZ
2. Kwa vile mambo 11 yaliyoongezwa nje ya 11 ya yaliosainiwa moja ni elimu ya juu! Sasa hebu tufahamishe Elimu ya juu iliyoongezwa ni kwa vipi linawaumiza WZN

Ukijibu hayo mawili basi tutaendelea na mnakasha. Kama huna jibu peleka mzalendo.net wakusaidie na kama hawana basi njia nyepesi ni kuzima computer yako au kama utaiwasha basi usome wenzako wanasema nini.

Hili la Kikwete kuja ZNZ kwa heshima linanitatiza maana Rais wa ZNZ anachaguliwa Dodoma! na pia Rais wa ZNZ ni mjumbe wa baraza la mawaziri ambalo JK ndiye mwenyekiti. Unaona jinsi unavyoshindwa kuangalia mambo ee!
Anyway, jibu maswali hayo ili tuendelee achana na porojo zingine.
 
Serikali moja ndo jibu. Unguja kiwe kitongoji (Shehia) cha mkoa wa dar, na pemba kiwe kitongoji cha Tanga, kama hawataki, tuwakalie kimabavu.
 
Naunga mkono hoja 100% Tanganyika sio koti limetiwa sasa litupwe jalalani? Shibe ya mafisadi wanataka kugawa nchi yetu kwa kivimbiwa! Tanzania nchi 1 serikali 1
 
Mwanakjiji naunga mkono hoja ya serikali moja,taifa moja,watu wammoja. Hili linawezekana kwa wote wenye nia maana hata Chama cha TANU na ASP waliungana na kuunda CCM. Sasa kama jeshi la wananchi na polisi ni moja, vyama vya kisiasa ni moja, bunge ni moja. Sasa kwanini tushindwe kuwa na serikali moja?

Mbadala ni muungano uvunjike kila upande urudie hali yake kabla ya mwaka 1964.

Pia siye Watanganyika "hauogopi maumivu tunakabili tu maumivu"
 
Last edited by a moderator:
Nina uhakika hufuatiliii mijadala na kama unafutailia basi huelewi kinachoongelewa.

Nimewahi kumuuliza ndugu yangu baru baru swali lifuatalo:
Katika mabo 11 ni yapi Tanganyika inafaidika nayo kwa kuinyonya ZNZ
2. Kwa vile mambo 11 yaliyoongezwa nje ya 11 ya yaliosainiwa moja ni elimu ya juu! Sasa hebu tufahamishe Elimu ya juu iliyoongezwa ni kwa vipi linawaumiza WZN

Ukijibu hayo mawili basi tutaendelea na mnakasha. Kama huna jibu peleka mzalendo.net wakusaidie na kama hawana basi njia nyepesi ni kuzima computer yako au kama utaiwasha basi usome wenzako wanasema nini.

Hili la Kikwete kuja ZNZ kwa heshima linanitatiza maana Rais wa ZNZ anachaguliwa Dodoma! na pia Rais wa ZNZ ni mjumbe wa baraza la mawaziri ambalo JK ndiye mwenyekiti. Unaona jinsi unavyoshindwa kuangalia mambo ee!
Anyway, jibu maswali hayo ili tuendelee achana na porojo zingine.
Mkuu wangu hawa watu wanadanganywa sana na wanasiasa wao. Kila jambo liloongezwa ktk mktaba wetu wa muungano ni kwa matakwa ya serikali ya Mapinduzi kwa ajili yao na kwa nafasi ya Zanzibar ktk muungano huu lakini bado wanahitaji, wanahitaji hawachoki kutaka kilichobakia ni moja tujitenga nao. Hilo koti wanalosema linawatia joto mbona ndilo wanalitumia kila wanapoenda kuomba kazi wasivae misuri na kanzu?.

Hiyo serikali moja mnayoitaka, ndio itakuwa kutumia nguvu sasa, maana sii kitu wanachokiombea kabisa isipokuwa wale waliokuwa ktk jumuiya ya Pan African ambao kwa Zanzibar ya leo hawapo na kama wapo wameisha poteza tumaini. Hivyo serikali moja italeta mgogoro kubwa kuliko huu na mwisho wake tutauvunja Muungano, hivyo kwa nini kazi yote hii wakati tunaelewa mwisho wake? Hivi tunatafuta serikali zipi zinafaaa sii kutokana na malalamiko ya Wazanzibar?

LET ZNZ Goo ndio suluhisho tena nadhani tuwalazimishe wafanye referendum japokuwa utawasikia wakiitaka serikali ya muungano ndio igharamie. Tunajua fika waloingia ndoa hii hawataki talaka isipokuwa watoto wao na kwa kadhi haendi mtoto kuomba talaka bali mzazi.
 
Ha ha ha ha! ''Kadhi kaingia mjini watu hawataki kuomba talaka''
Mkuu Mkandara, miaka michache iliyopita waliamua kuwa na ZMA(Zanzibar maritime Agency) kwasababu SUMATRA inawabana wasifanye biashara. Imekuja julikana kuwa kumbe ZMA hailipi ada kule Internationa Maritime Organization.
ZMA ni chaka la viongozi kusajili meli kwa bendera za 'koti' na kulipiwa ada na fedha za 'koti' ili wafanye biashara na Iran

Mkuu,wabia wa ZMZ mmoja ni yule yule anayehubiri kuvunjika kwa muungano kwa njia ya uani. Sasa hivi hasemi kwasababu amesogezwa karibu na sania la ubwaba na kupewa wadhifa wa pili wa kugawa nyama.
Hawa mayahe wenzangu wanashabikia tu hawajui adha itakayowakuta, hawajiulizi kwanini kila kiongozi wa ZNZ ana makazi Tanganyika na anaishi Tanganyika

Tena tukiwauliza katika mambo 11 wanayodai Tanganyika inafaidika na nini hawana jibu.
Kimya chetu kiliwafanya waone kuwa wana hoja za maana sana. Siku hizi kimya, hoja zao zimevunjwa vunjwa na MZNZ mwenye akili na ufahamu amekaa kimya, lakini akina Yakhe wamebaki kudanganya kule mzalendo.

Mkuu Kibona, zaidi ya uliyosema Tanganyika ni soko kubwa sana la Zanzibar. Hilo halina ubishi hata wao wanajua.
Kuvunjika kwa muungano tena katika hali ya chuki walioijenga kutawaumiza sana.

Angalia mahusiano yetu na Zambia, Kongo, Burundi, Msumbiji, hakika huwezi kuona kama kuna tofauti ya nchi hizo. Wazambia wapo tu wengi Tanganyika kama walivyo Watanganyika Lusaka. Kwa vile tupo katika misingi ya kuheshimiana na kuthaminiana huwezi sikia kelele dhidi yao.

Kwa Zbar siku muungano ukivunja sijui nini kitatokea maana Watanganyika wana hasira sana si kwasababu wanawachukia WZNZ bali wamechukizwa na WZNZ.
Nafahamu ugumu utakaowasibu katika biashara na ajira, elimu na afya na hiyo itakuja kwasababu tu si huyu ni MZNZ! anayejiona bora sana sasa ni wakati wa kumtenda. It is coming just a matter of time. Huko maofisini siku hizi wanaonja joto ya jiwe, wanapewa 'live' ondoka rudi kwenye nchi ya neema yenye mito na maziwa ya asali

Hizo gharama za ulinzi ulizosema hazitaongezeka kwasababu hata sasa hivi gharama za jeshi ni za Mtanganyika asilimia 100. Kitakachotokea ni kuzihamishia gharama hizo zibaki Tanganyika kama ilivyo.
Lakini pia lazima tuelewe kuwa kuna mabilioni yanakwenda ZNZ bila hesabu. Juzi ofisi ya makamu wa Rais imepewa bilioni 32 kwa ajili ya ZNZ, yaani makamu akitaka kunywa chai na UAMSHO ofisini hizo ndizo gharama za usafiri nk.

Sasa hivi wapo kimya! tunasema hamkani si shwari LET ZNZ GO!
Sisi Tanganyika tuna uzoefu wa kusimama wenyewe.
Kenya walipotupiga bao mwaka 1977 tulisamama kidete na bado tunasonga mbele.

Hakuna serikali 3, mahusiano au mkataba
Ima serikali 1 ambayo hamtakubali na hapo tunasema LET ZANZIBAR GO! Nothing to lose!
 
nina uhakika hufuatiliii mijadala na kama unafutailia basi huelewi kinachoongelewa.

Nimewahi kumuuliza ndugu yangu baru baru swali lifuatalo:
Katika mambo 11 ni yapi tanganyika inafaidika nayo kwa kuinyonya znz
2. Kwa vile mambo 11 yaliyoongezwa nje ya 11 ya yaliosainiwa moja ni elimu ya juu! Sasa hebu tufahamishe elimu ya juu iliyoongezwa ni kwa vipi linawaumiza wzn

ukijibu hayo mawili basi tutaendelea na mnakasha. Kama huna jibu peleka mzalendo.net wakusaidie na kama hawana basi njia nyepesi ni kuzima computer yako au kama utaiwasha basi usome wenzako wanasema nini.

Hili la kikwete kuja znz kwa heshima linanitatiza maana rais wa znz anachaguliwa dodoma! Na pia rais wa znz ni mjumbe wa baraza la mawaziri ambalo jk ndiye mwenyekiti. Unaona jinsi unavyoshindwa kuangalia mambo ee!
Anyway, jibu maswali hayo ili tuendelee achana na porojo zingine.

wewe ni mmoja wa wale wanaofumbia mambo ya msingi katika muungano huu feki kila kitu kipo wazi. 1 tupia sector ya muungano katika mambo ya uhusiano wa kimataifa (foreign affair ) jinsi mnavyoinyonya znz propotions kwa mabalozi. 2 ulinzi na usalama nafasi zote juu imechukua tanganyika zanzibar kumejaa majeshi wasio na faida pale znz. Na mambo mengi tu naamini unayafahamu.

Kwa ufupi na urefu muungano hatuutaki tuwachiwe tupumuwe kwani lazima mbona mmekuwa ving'ang'anizi ? Na haya mambo ya kuamuliwa mambo yetu dodoma ndo hatuyapendi haswa . Tupeni urais wa muungano basi 2015 mpate adabu yenu !tutawafanya kuliko alivyowafanya kikwete !
 
Wewe unaangalia idadi ya mabalozi, sijui balozi akiwa MZNZ ndiyo inakuwaje! Lakini pia jiulize unapotaka mabalozi wawe wengi kwanini ukiambiwa deni la taifa unakimbia? Deni la taifa ni mzigo wa Tanganyika. Hebu fikiria kidogo, kuna WZNZ wangapi wana nafasi kubwa sana huku bara, halafu fikiria tena, wale wabunge 50 pale Dodoma nani analipa gharama zao! Angalia katika picha pana kuliko unayoiona sasa.

Sijui kama unajua kuwa BLW akiwemo Spika wanalipwa mishahara kutoka hazina Dar es Salaam! unajua hilo kweli!

Ulinzi na usalama nafasi zote zimechukuliwa na Watanganyika ni halali kabisa.
ZNZ haina bajeti ya ulinzi kwanini huulizi hilo.
Huwezi kupewa nafasi kama una mchango sifuri. Wewe unafikiria vyeo hufikirii inachangia nini.
Narudia ZNZ haina bajeti ya jeshi wala Polisi, inachangia sifuri katika gharama za ulinzi wa taifa! period.

Hakuna Mtanganyika anayeng'ang'ania, BLW lipo, Baraza la mapinduzi lipo, wimbo wa taifa wa ZNZ upo, Bendera nzuri ipo, katiba ipo, Rais na makamu wawili wapo, sasa mnashindwa nini kuondoka? Mbona mumeunda baraza la mitihani, mumebadili katiba, mumeunda ZMA kwa ushirika na Iran n.k. Hakuna anayewauliza. Muungano mnashindwa nini.

Kwakweli maoni yako ni too low lakini yanawakilisha sehemu kubwa sana ya WZN kama asilimia 90.
Wao wanataka wapewe hata wasichostahili, ukiwauliza wanachangia nini hawasemi, lakini jibu ni kuwa katika muungano Zanzibar inachangia sifuri I mean Zero inachukua 7% pamoja na kukataa kulipa bili za umeme, SUMATRA, ulinzi na Usalama, Elimu ya juu, gharama za kuwatunza akina Mama Karume, Mwinyi, Salimin, Jumbe nk.

Tatizo la WZNZ wanauangalia muungano kwa vitu vya hovyo sana na si kwa maana ya muungano na faida au hasara .
Sikiliza mtu anayesema hakuna IGP Mzanzibar tangu uhuru, sasa Mwinyi alikuwa Rais wa JMT amebadilisha vipi maisha yako! uwepo wa IGP au Waziri mzanzibar unakusaidiaje wewe unayejisaidia baharini! haya ndiyo maswali mnapaswa kujiuliza.
Halfu ujiulize fursa mnayopata ndani ya muungano vs IGP mzanzibar kipi bora.
Fikirieni kidogo haihitaji certifcate bali busara tu.

As long as mnataka vya bure,we will attach strings!

LET ZNZ GO!
 
Hatutaki serikali Tanganyika ni mzigo kwa Tanganyika.

Kweli kabisa hatutaki serikali ya Tanganyika.....Tunataka nchi ya tanganyika.......
sikudhani mzee wewe unakosa busara kutambua hili
Zanzibar (nchi9 ipo, Tnganyika iko wapi?
unaropoka leo ati Tanganyika ni mzigo, si wataubeba watanganyikia wenyewe? au umesahau msemo "mzigo mzito mtwishe mnyamwezi..................!"
 
Viongozi wa juu wanashirikiana na wageni toka znz kuifilisi tanganyika. Muungano gan wakuwafanya wenyeviti wa vijiji (wanaochaguliwa na watu 100-2000)kuwa wabunge sawa na wabunge (wanaochaguliwa na watu 20-500,000) hii siyo sawa and this arrangement is the most stupidy ever in the world. Who is fooling who?!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Na hii Tanganyika nayo ni kubwa sana ,hakuna serikali ambayo itaweza kutenda haki kwa Mikoa yote ,ili kupunguza mzigo kwa serikali ni bora ikagawanywa mapande manne.

Majimbo eeh; l support that, linchi ni kubwa mno kulitawala kicentral.
 
Back
Top Bottom