Muundo wa jiji la dar es salaam

Mwamanda

Senior Member
Feb 24, 2009
150
48
Salam aleko

Suala la muundo wa jiji la DSM nimeona ni vizuri nililete hapa jamvini ili lifahamike na kwani nahisi ni chanzo cha jiji kudorora katika kutoa huduma kwa wananchi.
Awali jiji la Dsm lilikuwa ni Tume ya Jiji ambayo ilikuwa chini ya bwana Keenja.Ufanisi wake ulikuwa mzuri.Lakini baadaye serikali iliunda manispaa tatu ya Temeke,Kinondoni na Ilala na halmashauri ya Jiji la Dsm kila manispaa ikiwa na mamlaka kamili.Na jiji kubaki na stendi ya mabasi ubungo na Dampo kuu la Pugu ,awali lilipendekezwa liratibu manispaa zote tatu za jiji lakini serikali hakuandaa utaratibu muafaka.
Matokeo ya muundo huu mpya yanajionyesha hali ya miundo mbinu hususani mifereji na pia uchafu sio nzuri.Mji unakua kiholela .Pengine ni wakati muufaka kufikiria muundo(mfumo) bora utaokuwa na ufanisi mkubwa maendeleo ya DSM .
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom