Muumini yupo Twanga Pepeta siku hizi?

Kitty Galore

JF-Expert Member
May 24, 2011
345
100
Wadau nimemuona Muumin kwenye uzinduzi wa Twanga Pepeta uliofanyika pale Leaders, nae ni mmoja wa waimbaji wa Twanga, je huyu jamaa si alikuwa na bendi yake? nini kimempata na mbona anaonekana kachoka sana? na isitoshe alikuwa kimya kwa muda mrefu.
Hii imekaaje wadau.
 
siku nyingi saaaaana ndo aliyetunga wimbo wa penzi la shemeji ktk album mpya ya wanatwanga na kupepeta.
 
alichoka zaidi kipindi alipokuwa anahaha....Asha Baraka mlezi wa wana wanatukana weeee wanarudi palepale
 
kumbe alitokea pale pale, jamaa alikuwa hodari wa kuoa yule, enzi zake ilikuwa balaa sijui siku hizi
 
muumini ni mwanamuziki mzuri sana ila anaimba ssana mipasho. Pia hana ujanja wa kutunga nyimbo nzuri. Kadhalika anapenda kulalama sana kwenye nyimbo. Hajui kuvaa na wala hawezi kujiweka kwenye unadhifu. Hayo ni baadhi ya mapungufu yake
 
hahahahahahah hao wake zake sasa....wakwanza kikojozi akashindwa kuvumilia,wapili akawa anasaidiwa ile mbaya
 
naadhan ndo mwanamuziki anayyeongozaa kutangatanga katika bendi, hata hapo twanga haatomaliza miezi sitta utashangaa nayeye ameanzisha mapacha watano
 
mi naona wanamziki wetu wajifunze jambo. Siyo vizuri kuisema vibaya bendi uliotoka kwa kuwa hujui ya kesho endapo utarudi au lah.
 
muumini ni mwanamuziki mzuri sana ila anaimba ssana mipasho. Pia hana ujanja wa kutunga nyimbo nzuri. Kadhalika anapenda kulalama sana kwenye nyimbo. Hajui kuvaa na wala hawezi kujiweka kwenye unadhifu. Hayo ni baadhi ya mapungufu yake

Ninamshauri akaimbe taarabu, ndiyo sawa yake
 
muumini ni mwanamuziki mzuri sana ila anaimba ssana mipasho. Pia hana ujanja wa kutunga nyimbo nzuri. Kadhalika anapenda kulalama sana kwenye nyimbo. Hajui kuvaa na wala hawezi kujiweka kwenye unadhifu. Hayo ni baadhi ya mapungufu yake

Aisee...........

MU2.jpg

muumini.JPG
 
muumini ni mwanamuziki mzuri sana ila anaimba ssana mipasho. Pia hana ujanja wa kutunga nyimbo nzuri. Kadhalika anapenda kulalama sana kwenye nyimbo. Hajui kuvaa na wala hawezi kujiweka kwenye unadhifu. Hayo ni baadhi ya mapungufu yake

kuvaa hakuhitaji elimu ni damu ya nguo ukiwa nayo hata ukivaa nini unatokea!muumini hana damu ya nguo hata ukimpa container la pamba hamna itayompendeza!
 
Njaa si mchezo kaka jamaa alipokuwa na bendi alisema hataajiriwa tena kwenye bendi na hawezi kurudi kwenye bendi za Asha Baraka sasa kale mitapishi yake,tatizo la Muumini ni kujiona bila yeye hakuna kitu na yeye ndie kila kitu,wanamuziki mliowahi kupitia Twanga mtatangatanga weee huku na kule lakini likiwachwea mtarudi tena kulekule Twanga na mtaikuta vile vile
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom