Muuguzi adaiwa kumpiga mgonjwa wakati akimuhudumia jijini Mbeya

Pande zote mbili wasikilizwe kwa umakini sana,

Swala la kusukuma mtoto kabla ya muda muafaka linaweza kusababisha kifo cha mtoto,

Na swala la kulabua mjamzito kofi la uso nalo linaweza kumchanganya mjamzito network ikakata,

Hapa wasikilizwe wote kwa umakini mkubwa
Hapo mtoto akitoka na apgar score ndogo muuguzi anakuwa kwenye hot soup...ni bora amlaumu kwa kibao cha mapaja kuliko kumlaumu kwa mtoto mwenye utaahira wa akili
 
Katika hali ya kawaida huwezi kutupa kitu afu kikaangukia mita 1 mtoto akitoka baada ya kuzaliwa huwa yuko kama cm 50 kwenda kifuani . So kama mtoto hakuanguka basi aliwekwa kifuani na kwa utaalamu mtoto akizaliwa tu awekwe kifuani kwa mama ngozi kwa ngozi ili mtoto apate joto la mama
.vinginevyo mtoto atapata madhara ya baridi. Afu mtoto
 
Swala la kutosukuma baada ya mtoto kutoa kichwa hiyo ni mhimu sana kuruhusu mtoto kujigeuza bega la kushoto . Hali hii hutokea yenyewe na mama anatakiwa atii maelekezo ya muuguzi baada ya mtoto kujigeuza ndo mama anaweza kusukuma tena kwa ulaini zaidi. Mama akilazimisha madhara yake ni kuchanika uke na ujinga we kusukuma haraka mwisho wake ni RVF mpasuko wa msamba. Kina mama wa mbeya na mikelele yao misibani ndo walivyo huko labor. Mambo haya ni ya utaalamu wa kisasa. Period
 
Mama mmoja amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua katika hospitali ya Rufaa Meta ya jijini Mbeya na baada ya kujifungua muuguzi huyo akamchukua mwanae mchanga na kumtupia kifuani jambo ambalo amesema lilihatarisha uhai wa mwanae.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amefanya ziara ya kustukiza katika hospitali ya Rufaa ya wazazi Meta ya jijini Mbeya na kushuhudia msongamano mkubwa wa akina mama wajawazito hospitalini hapo, na alipofika katika chumba cha akina mama ambao wanasubiri watoto wao ambao wamewekwa katika chumba maalum cha joto, ndipo akakutanana na malalamiko ya mama Salome Waya ambaye amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua.

Kufuatia madai hayo, mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akalazimika kupitia nyaraka za mama huyo ili kumtambua muuguzi aliyemfanyia ukatili huo na akafanikiwa kumbaini kuwa anaitwa Beatrice Sanga ndipo akatoa agizo kwa mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini, Dk. Goodlove Mbwanji kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo ndani ya siku saba.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Goodlove Mbwaji amesema kuwa katika mazingira hayo hawezi kujitetea na badala yake atazingatia maelekezo ambayo amepewa na mkuu wa mkoa.
Hawa wakunga huwa wananyanyasa sana wanawake pale labour nadhan kwasababu wasjua pale unakuwa huna ujanja.mi Luna jiran yangu alijizalisha mwenyewe pale amana baada ya kumuita muuguzi bila mafanikio.na hii hupelekea wamana wengi na watoto kufariki
 
Huyo mama aliyepigwa ana shahidi ambaye ni mgonjwa? Je mama huyo kapewa PF 3 na kuonwa na daktari ambaye ni neutral? Kafungua RB namba ngapi? Partogram na APGAR Score zilikuwaje ilikujua progress ilikuwa rafiki au la? Je kuna njia nyingine ya kufanya rescustation zaidi ya kifuani? Na njia rahisi ya joto kwa mtoto ni kumweka wapi? Je Mzee Makalla ana ruhusa ya kuangalia file la mgonjwa?
 
Sio lazima upost, huna hoja ya maana kaa kimya, umeshawahi kuingia chumba cha kujifungulia? au unapost tu pumba zako? Vipi kama mzazi wako angepigwa na kutupiwa mtoto? Au mkeo, au dada yako? Tena mbele yako ukiwa unaona kwa macho yako mwenyewe!! Tutakaowabaini hatutawaonea huruma, kama kazi ngumu acha katafute iliyo rahisi sio kuchezea uhai wa watu, huyo mtoto alierushiwa mama mzazi fikiria kama angeanguka chini angepona? Tatizo kuvamia taaluma za watu, wito hakuna, uwezo wa kufikiri ni hafifu, tunakuja......tukikubaini ni sheria tu watachukuliwa
Povuuu mantiki hamna,stay you're.
 
Yawezekana alikuwa ana bana miguu kiasi kwamba angeweza kusababisha maafa kwa mtoto aliyezaliwa, na mara nyingi bila muuguzi kuwa mkali akimchekea mama anayezaa kwa woga anaweza kuua mtoto ndio maana wakati mwingine hata wanawafunga miguu kwenye kitanda ili asibane miguu. ila sasa ya kumtupia mtoto ndio sijaelewa, yawezekana alimpa mwanae kwa lugha ambayo haikuwa nzuri lakini kumtumpa na bado mtoto akawa hai hadi leo sijui!!!!!! hata hivyo na sie wagonjwa tumekuwa na ka kiburi Fulani siku hizi
 
Alichokifanya nesi ni sawa tu make mama yule angeua mtoto ni kesi ya nesi sema tu yule mama kaona ashitaki hata hivyo yule mama umri umeenda sana inawezekana alikuwa anazingua kweli. Lakini haina noma kwa vile kala vibao ila hajafa.
 
Mama mmoja amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua katika hospitali ya Rufaa Meta ya jijini Mbeya na baada ya kujifungua muuguzi huyo akamchukua mwanae mchanga na kumtupia kifuani jambo ambalo amesema lilihatarisha uhai wa mwanae.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amefanya ziara ya kustukiza katika hospitali ya Rufaa ya wazazi Meta ya jijini Mbeya na kushuhudia msongamano mkubwa wa akina mama wajawazito hospitalini hapo, na alipofika katika chumba cha akina mama ambao wanasubiri watoto wao ambao wamewekwa katika chumba maalum cha joto, ndipo akakutanana na malalamiko ya mama Salome Waya ambaye amedai kupigwa na muuguzi wakati akijifungua.

Kufuatia madai hayo, mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akalazimika kupitia nyaraka za mama huyo ili kumtambua muuguzi aliyemfanyia ukatili huo na akafanikiwa kumbaini kuwa anaitwa Beatrice Sanga ndipo akatoa agizo kwa mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini, Dk. Goodlove Mbwanji kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo ndani ya siku saba.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Goodlove Mbwaji amesema kuwa katika mazingira hayo hawezi kujitetea na badala yake atazingatia maelekezo ambayo amepewa na mkuu wa mkoa.
Serikali iwe makini na watu wake sasa, maana naona watu wameanza kudeka sasa. Yule mama tumemshuhudia akilalamika kupitia television, kwa alivyokuwa anaonekana kueleza inaelekea muuguzi aliamua kumpiga kofi ili asukume mtoto vinginevyo madhara yangetokea. kupigwa kibao kwa mama anayejifungua ni jambo la kawaida ili amalize kazi.yule mama anaonekana ni mvivu ikabidi muuguzi atumie maarifa ya ziada.
 
Nashauri taaluma ya uuguzi wafanyakazi waanze kuandaliwa mapema kiroho hii mambo ya kukimbilia afya ili kupata tu kazi haraka ni hatari mno kwa jamii
 
Tatzo la hii nchi kila MTU anajifanya anajua. Watu mnamuhukumu tu huyu nesi wkt inawezekana wakati wakujifungua mama anaambiwa sukuma atoe mtoto mama hasukumi. Sasa kupigwa Kofi iliatoe MTT au angeacha den MTT akafa kipi bora? Na mtt angekufa pia mngesema nesi kaua MTT

Mbona hii nchi kila kitu mnaingiza siasa?
 
Hili jambo kama hujawahi kushuhudia wakati mama anajifungua waweza kusema lolote unavyojisikia..ila tukae tukijua lile tendo ni la kufa na kupona.

Uzembe wowote wa aidha mama au nesi matokeo yake ni mabaya kuliko hicho kibao..hivi ni kwanini hatujiulizi sababu ya mtoto kupelekwa kwenye chumba cha joto? Kama kweli mama na nesi walitimiza wajibu wao sawasawa,kwa nini mtoto ametoka amechoka?
 
Watu wanapost tu akili yao inawazo watuma lkn uhalisi hawaujui. Huyo Mkuu wamkoa amethibitisha wamama wanao subiria kujifungua walikuwa n wengi hv anajua guides za WHO znataka mkunga audumie wamama wangapi kwa cku anapoingia kazn, je kulingana na mazingira yetu wafanyakaz wanatosha? Na hapo mtt akifa kwa uzembe Wa mama bado analaumiwa nesi

Wakat mwengine watu wanawaonea sana hawa manesi
 
Yawezekana haya mambo hutendwa na hawa ndugu watumishi kwa sababu moja au nyingine. Ambazo hata hivyo hazihalalishi kuumiza, kutesa au kudhalilisha iwe kimwili, kiakili au vyovyote. Na inasikitisha mno ingawa ukweli unabaki kwa anayetuhumu na mtuhumiwa.
 
Wewe!!! Tumezaa kwa kuelekezwa vizuri na sio mikofi na kutupiwa mtt. Manesi acheni tabia za kishetan..pam**aaaaff
Kwanza huyo mama walitakiwa kumshukuru kwanza huyo muuguzi kwa kumsaidia kujifungua ,nilishashuhudia labour Dada mmoja alipigwa vibao vya nguvu kwenye mapaja ,sababu alikuwa anabana miguu wakamwambia hasibane atanyonga mtoto hakusikia ikabidi atandikwe vibao akaachia,na mtoto akatoka salama.Mimi naona nesi alimpiga ili hasifanye uzembe,pale muuguzi hasipokuwa mkali wamama wananyonga watoto.
 
Wamelazmishwa??hujui ukunga na kz yyte ya yakitabibu ni wito na uwe na moyo wa huruma!!umpge anayejifungua???we utakuwa me ndo maana unaongea upupu!ukiona kz ngumu haikulipi unawaachia wnye wito na kz!km ni kwli adhabu ya kutosha inamuhusu mgumba hyo!!!!!
Tuwe tuna appreciate na kazi za wenzetu ingekuwa rahisi kama unavyofikiria si kila mtu angefanya,hakuna kazi ya wito ni ajira hiyo,fikiria ndio wewe tena mwanamke mazingira ya labour unayafahamu halafu unathubutu kusema hayo,hiyo kazi ni zaidi ya kujitolea,kuna muda wanahitaji kutumia ukali kuna wanawake wazembe na madeko ukiongezea walifanya uzembe si watoto wengi watakufa.
 
Yapo mazingira umkimchekea mjamzito tu basi tegemea kifo cha mama au mtoto,wakati mwingine wote huyo muuguzi kwa nini ampige yeye tu! Kati ya wote waliojifungua tafadhali umakini na ukomavu wa maamuzi unahitajika hawa wauguzi ni msaada mkubwa sana tuwahurumie sana.
Ni kweli kabisa husemavyo,vitanda vya wenzetu nchi zilizoendelea wanatumia vitanda vyenye chuma cha kuegemeshea mapaja kwa hiyo miguu inakuwa imening'inia lakini kwet hapa ni vitanda vya kawaida inamlazimu mama kupanua miguu mwenyewe na huwa inachoka vibaya ,sasa fikiria nesi naye alilemaa itakuwaje.
 
Back
Top Bottom