Mutungirehi: mwanasiasa mahiri kazimikia wapi?

Mechard Rwizile.
Mwongozo wako ni mzuri sana. Tuombe kama wabunge vijana makamanda kama watayasoma haya na kuyafanyia kazi.
 
Mkuu Feedback, aliyekuwa anavalia suruali tumboni aliitwa Ladislaus Malima, walipoingia utawala na kuchimbwa mkwala na Afisa utawala, wakati ule Prof. Masenge, yeye alipotoka aliwaambia watu kuwa 'mimi simo anayeendelea na mgomo shauri yake!', akatokomea mtaani ingawa walipofukuzwa viongozi wa kunji naye alikuwemo.

Maswi alikuwa Vice President wa Mutungirehi, wakati ule tulimwita Chacha Maswi, baada ya Mutungirehi kushushwa hightable pale Nkurumah na kuishia dispensary, Chacha alikaa mezani akatangaza 'DEMOKRASIA IMECHUKUA MKONDO WAKE, na tukaendelea na mkutano kila mtu akidahania yangeishia hapo.

Malima classmate wangu pale FOE. nakumbuka baada ya kubonyea kwa mkwara wa prof Masenge , FOE walikuwa hawampend kabisa, akigombea uongozi wowote hapewi. Baadayelijiunga na NCCR mageuzi akapiga siasa...juzi juzi alikuwa mkurugenzi wa RITA, japo naambiwa nako wamemtimua.

Maswi alitembelea kazini wangu juzi nikampa tour na maelezo ya tunachofanya...lakini nilikuwa naiuliza huyu mbona yuko familiar hivi! Kumbe mzee wa kunji! JF ni kiboko hata kuliko google.
 
Ana unafki gani? Yaonekana unamjua vizuri had huko kwao ruhita. In actual fact jamaa ni mzuri kujieleza isipokuwa watu wa kyerwa mlitaka awe anawanunulia pombe na kuwaonga pesa. Mazingira enzi zake kuhusu upinzani zilikuwa mbaya sana.upinzan ulikuwa uhasama/chuki na ata kupeana sumu. Watu wa kambi ya ccm waliumia kushndwa na mtu ambaye hakuwa na pesa isipokuwa mdomo na elimu, wakti yule wa ccm alikuwa milionea,anawanzesha pombe,gari mnapanda bure huku akidhibiti waganda wasinunue kahawa anunue yeye kwa bei anayotaka.kumbuka mwaka 2005 ndiye mbunge alikuwa kachangia sana bungeni. Bunge lilipokuwa linaisha wanasema aliishi kijijini kitwe na gari yake ilikuwa ambulance jimbon kwerwa.nimempgia rafiki yake ambaye yuko kaisho na walisoma wote

Nadhani kama unamjua vizuri kuanzia chuo kikuu, alafu kdcu mpaka ubunge wake utanielewa . Ni kweli wapo waliotaka pombe lakini wapo waliokuwa wanataka maendeleo . Wanaotaka pombe siku zote hawapigi kura
 
Ni heri mganda/chequevera mtendea mema kwa watanzania kuliko mtanzania fisadi, tunamwomba azihuishe upya ndani ya CDM. Tunajua safari ya Ukombozi ni ngumu sana, lazima baadhi yetu wachoke kabla ya kurudi na nguvu mpya.
 
JF bwana ni CHIBOKO kuliko hata google kwa kuoekua mambo.
 
Nadhani kama unamjua vizuri kuanzia chuo kikuu, alafu kdcu mpaka ubunge wake utanielewa . Ni kweli wapo waliotaka pombe lakini wapo waliokuwa wanataka maendeleo . Wanaotaka pombe siku zote hawapigi kura
nakuakikishia kwa 100%, karagwe anayepewa pombe ndiye mpiga kura. Mbunge aliyepo ameleta maendeleo gani tofauti na kununua kahawa kwa bei ndogo?umeingiza ubaguzi wa kabila/koo. Ni muono mbaya kusema sio m-tz ni muhima.wewe karagwe unatoka sehemu hipi.ukiitaja tu basi nitakwambia wewe ni mtz uliyetoka wap.je maendleo unayozungumza yanaletwa na m-tz wa aina hipi?ubaguzi wako ni mbaya kwa karne hii.nafikiri jf ingekuwa ya kwako basi,ungetaka wanachama wawe unaowapenda,wapost unachokitaka,wahima wa ruhita wasingepata nafasi ya kuchangia nk. Umoja wetu unaanza kuaribiwa na mawazo ya hovyo kama ya kwako. Je karagwe nayo ina ukabila na ukanda?
 
Kuzungumzia ukabila na udini kwenye siasa ni ujinga wa kuitikia kila jambo bila kujaribu kulipima kwa akili yako. Hoja hapa ni wapi aliko mwanasiasa mahiri bwana Benedicto Mutungirehi ma kwamba tunamtafuta ili kumtaka arudi kwenye uwanja wa siasa tena. Habari ya kabila lake nani kakuulizeni? Idara ya Uhamiaji si ipo? Kama siyo M tz nani amekuulizeni? Mijitu mingine hovyo kanisa. Hupotosha kila jambo. Kwani hata wewe ni mtz? Babu yako angekuwepo ungemuuliza asili yenu, ungejishangaa.
 
nakuakikishia kwa 100%, karagwe anayepewa pombe ndiye mpiga kura. Mbunge aliyepo ameleta maendeleo gani tofauti na kununua kahawa kwa bei ndogo?umeingiza ubaguzi wa kabila/koo. Ni muono mbaya kusema sio m-tz ni muhima.wewe karagwe unatoka sehemu hipi.ukiitaja tu basi nitakwambia wewe ni mtz uliyetoka wap.je maendleo unayozungumza yanaletwa na m-tz wa aina hipi?ubaguzi wako ni mbaya kwa karne hii.nafikiri jf ingekuwa ya kwako basi,ungetaka wanachama wawe unaowapenda,wapost unachokitaka,wahima wa ruhita wasingepata nafasi ya kuchangia nk. Umoja wetu unaanza kuaribiwa na mawazo ya hovyo kama ya kwako. Je karagwe nayo ina ukabila na ukanda?

nadhani umenielewa vibaya sana na siwezi kubadili mapenzi yako kwa Mtungilehi, katika makala mbalimbali ya karugendo ameonesha kuwa huyu mtu ni mhima , na wahima wanakaa tz,ug, rdc,rw n.k. Mbunge wa sasa Mr.Katagira ni hovyo zaidi na mtungirehi ni zaidi ya huyu mtu lakini si bora kiasi cha kuwa mbunge wa Kyerwa kulingana na historia ya alikopita. Binafsi natoka Isingiro na naweza kukukaribisha kuja tukaongea zaidi
 
Kajunju
Wewe unastahili kufanya kazi na CIA. Ni kamanda mzuri kwa upekuzi.
Jitahidi hadi aache maandiko yake hapa kupitia kwenye akaunti yako yako ya JF.
Kwa namna ya siasa ilivo sasa yeye ni mtu muhimu sana. Mwanaume hafi huku anajiona.

Mkuu Royals, nimefuatilia post zako kwenye hii thread kwa muda mrefu sana, uko very inspirational, hakika unaweza kumfufua mfu wewe, nakuomba uende pale magogoni ukamtie moyo Rais wetu sababu simuelewi elewi, naona kakata tamaa kabisa.
 
nakuakikishia kwa 100%, karagwe anayepewa pombe ndiye mpiga kura. Mbunge aliyepo ameleta maendeleo gani tofauti na kununua kahawa kwa bei ndogo?umeingiza ubaguzi wa kabila/koo. Ni muono mbaya kusema sio m-tz ni muhima.wewe karagwe unatoka sehemu hipi.ukiitaja tu basi nitakwambia wewe ni mtz uliyetoka wap.je maendleo unayozungumza yanaletwa na m-tz wa aina hipi?ubaguzi wako ni mbaya kwa karne hii.nafikiri jf ingekuwa ya kwako basi,ungetaka wanachama wawe unaowapenda,wapost unachokitaka,wahima wa ruhita wasingepata nafasi ya kuchangia nk. Umoja wetu unaanza kuaribiwa na mawazo ya hovyo kama ya kwako. Je karagwe nayo ina ukabila na ukanda?

Inamaana hata kutaja kabila la mtu ni kosa sasa??
 
nadhani umenielewa vibaya sana na siwezi kubadili mapenzi yako kwa Mtungilehi, katika makala mbalimbali ya karugendo ameonesha kuwa huyu mtu ni mhima , na wahima wanakaa tz,ug, rdc,rw n.k. Mbunge wa sasa Mr.Katagira ni hovyo zaidi na mtungirehi ni zaidi ya huyu mtu lakini si bora kiasi cha kuwa mbunge wa Kyerwa kulingana na historia ya alikopita. Binafsi natoka Isingiro na naweza kukukaribisha kuja tukaongea zaidi

nashukuru kuwa haukuwa na nia mbaya kumtaja mtungireh kuwa ni muhima.kumbuka ata awe fr karugendo akiandika kitu basi kimepita au kinakubalika.watu wa karagwe wanajulikana kama wanyambo,wa-tz. Haya mambo ya koo mara ulitoka wapi ni uchuro.jinsi ulivyotumia neno muhima na hovyo hukuwa na nia nzuri. Nilitegemea mwanzo uandike kuwa licha ya mtungireh kuwa hovyo...huyu tuliyenae ni hovyo zaidi. kumbuka watu wa kaisho walio wengi mlimpiga vita mtungireh. Mimi sio mnyambo ila nimefanyia kazi huko 15 yrs. Mtu huyu alipendwa kwa hoja isipokuwa wakti hule watu walikuwa mbumbumbu sana.hakuna sim,tv na radio ilikuwa tbc tu.ata isingiro mlikuwa hamfuatilii mbunge kafanya nini kwan nyie ni mashabik wa radio za uganda<kigezi,capital fm,radio great africa etc>.no zake nilipewa na jamaa yuko hapo isingiro.
 
Bwana kajunju nashukuru kwa kufatilia habari za kyerwa kwa karibu , ninachotofautiana na wewe ni kuwa Mtungirehi kapita pengi siyo ubunge wa kyerwa tu . Huko madudu yake huyaongelei. Ni si sahihi kuwa watu wa kyerwa kuwa wanapenda pombe ndo wampigie kura mtu maana mara ya kwanza kashinda ubunge akiwa masikini zaidi kuliko alipogombea 2005 kama ingekuwa pombe asingepata hata hizo kura za kumpa ushindi maana uwezo huo hakuwa nao. kwenye Lugha hasa kinyambo ,kingereza na kifaransa anaweza sana na mie ningempigia kura kama uchaguzi ungenikuta katika eneo lolote kama tu anagombea na katagira
 
Bandugu,
Lengo la huu ni kumyafuta Mutungurehi huko aliko na kwamba jinsi alivokuwa mjenga hoja mzuri bungeni wakati ule, kama angekuwa amekutana na hili vuguvugu la sasa lingemfaa zaidi kwa kuwa bunge sasa linaogopeka kwa kuwa lina vichwa vingi vikali kama yeye.
Hoja ya kuwa kabila gani, kafanya nini bungeni kwake na yoote yaliyo nje ya topic nani kayauliza?
Alama za nyakati zinaonesha kuwa wakati ule aliwahi sana wakati wake mwafaka ni sasa angekuwa na vichwa vilivoko bungeni kwa sasa utamu wa kutazama bunge ungekuwa unalipiwa kupitia Super Spot.
 
Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.

Ilikuwa 1994 na livutwa na jamaa wa FoE wakati huo
 
Malima classmate wangu pale FOE. nakumbuka baada ya kubonyea kwa mkwara wa prof Masenge , FOE walikuwa hawampend kabisa, akigombea uongozi wowote hapewi. Baadayelijiunga na NCCR mageuzi akapiga siasa...juzi juzi alikuwa mkurugenzi wa RITA, japo naambiwa nako wamemtimua.

Maswi alitembelea kazini wangu juzi nikampa tour na maelezo ya tunachofanya...lakini nilikuwa naiuliza huyu mbona yuko familiar hivi! Kumbe mzee wa kunji! JF ni kiboko hata kuliko google.

TzPride yaani umenikumusha mbali sana maana ilo tukio nalikumbuka sanaaa la Nkrumah.Vipi kuna jamaa mmoja alikuwa Bcom anaitwa Mwesiga anaye yupo wapi?
 
Nakumbuka kuweka no yake ya cm. Vp mr royal umempigia cm?kama mmeisahau no ni 0782486177. Ni juu yetu kuongea nae kwa cm ili ushawishi wetu auone kuwa ni muhimu.
 
Ukimuhitaji anakaa Jet ingawa sijui kama ni Mchimbo, Kwa Alli Mboa, Kwa Gude lakini mara nyingi nimekutana naye maeneo hayo. Kwa kweli maisha ni mzunguko huyu bwana amepungua sana ila kichwa bado kina mawazo ya kimapinduzi, kama kuna anayetaka mawasiliano yake nitampa namba yake ya simu maweze kukumbushana yaliyopita na mustakabali wa nchi yetu.

Mleteni anaweza akawa amabadilika kwani akiwa bungeni alikuwa ananikoga sana haswa style ya zile Kaunda Suti zake ambazo zilikuwa unique
 
Ilikuwa 1994 na livutwa na jamaa wa FoE wakati huo

Ilikuwa ni October 1994 ndipo Mutungirehi alipogaragazwa pale Nkrumah Hall. Soma headline ifuatayo: [UDSM wanaamriwa kuondoka kurudi makwao: {UHURU: November 07, 1994, pg. 1}].

Walioongoza kumtwanga Mutungirehi pale Jukwaani ni kweli mmemtaja Harold Mushi alikuwa Engineering. Mwingine ni Gasper Tracers aliyekuwa 3rd year Electrical Engineering. Huyu ninajua kuwa hadi 1998 alikuwa ni Engineer pale ITV ingawa sasa sijui yuko wapi.

Ila kuna moja wengi mnalisahau na hamlisemi. Wakati Mutungirehi anasulubiwa katibu wake wa DARUSO alikuwa Godwin Ngwilimi. Godwin alipoona Mutungirehi kaparamiwa na kuangushwa chini akachukua kiti na kumponda Harold Mushi ndipo fujo ikazidi.

Msiomjua Godwin Ngwilimi ni yule ambaye hadi mwaka jana alikuwa mwanasheria wa Vodacom ambaye sasa ni mwanasheria au Company Secretary wa TANESCO.

Kumbuka kabla ya Mutungirehi hajavamiwa kuna mtu nilimjua kwa jina moja la Mushi ndiye alikuwa anaongea kumlaumu Mutungirehi. Usichanganye na yule Harold Mushi.

Huyu alipoongea ndipo fujo zikaanza na kwa hakika ndiye aliamsha hisia ili fujo zile zianze. Ile headline hapo juu utaona kwamba Chuo kilifungwa Saturday, November 05, 1994.

Lakini kuna mtu ambaye wana JF mtashtuka kumjua habari zake. Naye ni huyu ambaye sasa ni mbunge wa viti maalum wa CHADEMA yaani Suzan Lyimo (Suzy). Wakati huo yeye alikuwa ofisi ya Dean of Students. Je, Suzy anahusikaje na fujo zile za Mutungirehi.

Ukweli ilikuwa ni vigumu hata leo kujua. Ila mimi kwa sababu ni mpenzi wa mpira, siku mbili baada ya Mutungirehi kugaragazwa kukawa na mpira pale Uwanja wa Taifa. Mimi nikapata nafasi jukwaa la kijani.

Kabla ya kuanza mechi chini kabisa nikaona kikundi cha watu watatu. Mmoja alikuwa ni Mushi yaani yule aliyetoa hotuba ya kumuondoa Mutungirehi, wa pili alikuwa ni jamaa mmoja mkurya ambaye ndiye aliwekwa kwa nguvu na wanafunzi ili kurithi nafasi ya Mutungirehi na wa tatu ni huyu Suzan Lyimo.

Leo ndiyo kwa mara ya kwanza ninalisema hili kwa watu naamini Suzy hawezi kulikana. Cha ajabu kwangu ama udogo wa mawazo yangu wakati ule ni kwamba wale vijana wawili wote ni wahusika katika kuuong'oa uongozi halali wa Mutungirehi. Nilitarajia management ya Chuo isiwe nao kokote kule.

Je, uwepo wa Suzan Lyimo na wale vijana wawili ulimaanisha kwamba kulikuwa na baraka za baadhi kwenye management ya Chuo? Nilitegemea ofisi inayohusu nidhamu kama Dean of Students wawe mbali kabisa na waliohusika na fujo zile.

Nimekutana ana kwa ana na Suzan Lyimo July 2009 kanisani Dodoma ndipo nikajua kuwa naye ni mkatoliki. Sikuwa najua kuwa ni mbunge na ndipo siku hiyo nikamjua ni mbunge.

Pamoja na kumkumbuka kama msaada wetu kwenye Ofisi ya Dean sikupata nafasi ya kumwuliza alikuwa na ushusiano gani na wale vijana waliomng'oa Mutungirehi pale jukwaani.

Ni hayo tu kwa post hii.
 
Hafai hata kwa dawa. Porojo nyingi utekelezaji hamna. Imagine kalimuahidi mtoto daftari kakipata Ubunge, hakakumplekea mpaka kanaondoka. Kumbe ka traitor, kapotee tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom