Muswada wa mchakato wa Katiba Mpya: Hakuna mbunge alyechangia hoja ya maana!

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Ndugu wanaJF, leo nilikuwa nafuatilia kwa makini vikao vya Bunge tangu asubuhi hadi jioni. Baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa Kamati na Mwakilishi wa Kambi ya Ushindani Tundu Lisu kuwasilisha hotuba zao, walifuatia wachangia watatu mmoja kutoka CCM, CUF na Augustine Mrema. Kwa wote hawa sikuona hoja yoyote waliyochangia kwenye huo muswada badala yake niliona kama wamapiga vijembe Tundu Lisu. Hii inasikitisha au tuamini kuwa baada ya wabunge wa Chadema kutoka nje hapakubakia wabunge wenye hoja? Nilitegemea wabunge wangekuwa kitu kimoja katika kuhakikisha mchakato wa kupata Katiba Mpya unaenda vizuri na hasa kuhakikisha madaraka ya Rais yanapunguzwa na siyo kama serikali ilivyofanya kukataa mapendekezo ya wadau kuhusu kumpunguzia Rais madaraka.
 
Wenye akili walisoma alama za nyakati wakamtonya Bi. Kiroboto. Ndiyo sababu kamaliza mjadala dakika 30 kabla.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hawa CCM hawasomi alama za nyakati na kuona yaliyotokea Kenya hadi ikabidi katiba mpya itungwe! Kweli jamani Watanzania wa sasa siyo wa mwaka 47. Katiba mpya lazima by ANY MEANS NECESSARY.
 
Kawaida huwa kukosoa kwa hoja ya wengine hasa kambi rasmi ya upinzani ndo wanachojua,wazembe wakufikiri.
 
Back
Top Bottom